Mtoto aliyelelewa na jini... maajabu saba-2

ILIPOISHIA IJUMAA ILIYOPITA:

Yule aliyepokea begi na kumpa yule aliyekaa kitandani, naye akakaa karibu na mwenzake huku akionesha anayetabasamu japo uso ulikataa kwa jinsi alivyokuwa mbaya.
SASA ENDELEA…

Walichofanya walimbadili nguo mtoto wangu huku wakiimba.
Niliwauliza wanaimba nini, hakuna aliyenijibu. Kwanza sijui wangenijibu nini?
Wakati wanafanya tendo hilo walikuwa wakiimba nyimbo kama za kikabila lakini naweza kusema sijawahi kusikia lugha ile toka nimezaliwa kwa mama yangu.

Walipomaliza kumbadili nguo, mmoja alitoa chupa yenye pafyumu ndani yake, wakampulizia sehemu mbalimbali za mwili huku wakiendelea kumwimbia.
Walipomaliza, walisimama, wakanikabidhi. Na kwa mara ya kwanza, mmoja akasema kwa Kiswahili.
“Unasalimiwa sana, amesema ipo siku atakuja kwani alipo sasa ni mbali huwezi kufika hata iweje?”
“Nasalimiwa na nani?” niliwauliza kwa sauti iliyojaa ujasiri.
“Na Ally.”

“Ally! Ally gani?”
Mmoja akamchukua tena mtoto wangu na kumwinua juu huku akisema:
“Baba wa huyu mtoto, umemsahau mumeo?”
Mwili ulisisimka, damu zilinienda mbio huku nikihema kwa kasi ya ajabu.
“Kwani bado yuko hai?”
“Si tumekwambia yuko mbali kuna siku atakuja.”

“Mimi sitaki kumwona.”
Niliposema hivyo tu, mi sitaki kumwona, upepo mkali ulitikisa chumba kiasi kwamba, nguo zilizokuwa kwenye misumari nyuma ya mlango zilipeperuka, shuka kitandani likawa kama linataka kutanduka lenyewe huku nguo zangu zikivuka.
“Kwa nini hutaki kumwona baba wa mtoto wako ambaye pia ni mumeo?” mmoja aliniuliza.
“Namuogopa sana.”

“Unamuogopa kwa lipi?”
“Si mtu yule.”
“Ni nani sasa?”
“Ni jini.”
Niliposema ni jini, nikasikia kishindo chini tii! Kuangalia hivi, Mungu wangu.

Je, nini kiliendelea? Usikose kwenye gazeti hili Ijumaa ijayo. Ushauri tuma SMS kwenda namba hiyo hapo juu

Views: 1435

Tags: mikasa11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by msichoke mlugu on June 9, 2012 at 5:33pm

mbona stori hii imesizi vipi? ilikuwa nzuri au mmeishiwa madesa?

Comment by Kulthum Salum on May 2, 2012 at 3:16pm

jamaan hadi nimeogopa

Comment by Real De' Dear on April 30, 2012 at 1:02pm

jaman mbona imenoga alafu mmefupisha.

Comment by DORAH FREDY on April 24, 2012 at 12:56pm
jamani fupi sana
Comment by maryann on April 20, 2012 at 5:41pm

Mbona fupi hivi jamani Aah

NI SUPERMARKET GANI BORA KULIKO ZOTE KATI YA HIZI? NA KWA NINI? TOA MAONI YAKO!
  

Forum

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by TZ on Tuesday. 1 Reply

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson 5 hours ago. 13 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by maleka sakeha yesterday. 30 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

JUAN MATA KUTUA MANCHESTER UNITED ATASIADIA KULETA MATOKEO BORA BAADA YA TIMU KUSUASUA?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson Nov 21. 88 Replies

Juan Mata anataraji kutua Manchester United akitokea klabu ya Chelsea ya…

KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KILA MARA, TATIZO NI NINI?

Started by GLOBAL in Habari. Last reply by mark gibson Nov 28. 46 Replies

VITENDO VYA KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KWA SASA VIMEZOELEKA. KATIKA NCHI MBALIMBALI WATANZANIA WAMEKUWA WAKIKAMATWA KWA UBEBAJI WA MADAWA HAYO. JE, TATIZO NI NINI? NA NINI KIFANYIKE?

Tags: MARA, TATIZO, NI, NINI?, KILA

JESHI LA POLISI KUTOA MILIONI 100 KWA ATAKAYEWEZESHA KUPATIKANA WAHALIFU WANAOMWAGIA WATU TINDIKALI NI KWAMBA LIMESHINDWA KAZI?

Started by GLOBAL in Maisha. Last reply by mark gibson Nov 30. 84 Replies

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.Jeshi la Polisi…

SIMBA SC WAMTUPIA VIRAGO JUMA KASEJA

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson 4 hours ago. 13 Replies

TIMU ya Simba SC leo imetangaza rasmi kuachana na mlinda mlango wake mahiri, Juma…

JE, NI SAHII KWA JESHI LA POLISI KULIPUA MABOMU WAKATI WANANCHI WAKIAGA MIILI YA WENZAO?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson 5 hours ago. 38 Replies

Juzi (Jumanne) polisi walilipua mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa wamekusanyika katika Viwanja vya Soweto jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili ya wenzao watatu waliopoteza maisha katika…

TOP NEWS WEEK HII

© 2014   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }