Mfanyabiashara, Anetty Ngulu maarufu kwa jina la Mama Mbilinyi akiokolewa na polisi asishambuliwe na wananchi.

Na Mwandishi Wetu
LILE sakata la mwanamke mmoja mkazi wa Kitongoji cha Frelimo, Manispaa ya Iringa, Anetty Ngulu maarufu kwa jina la Mama Mbilinyi kudaiwa kufuga misukule na habari zake kuandikwa kwenye vyombo vya habari nchini, mapya matano yameibuka kuhusiana na sekeseke hilo.

...baadhi ya majeruhi katika vurugu hizo.

Habari kutoka kwa vyanzo vyetu zimebainisha mambo matano mapya ambayo yamejitokeza mara baada ya tukio la awali.


             LA KWANZA
Inadaiwa baada ya sakata la mama Mbilinyi ambalo mpaka sasa halijathibitishwa, baadhi ya watu wanaofuga misukule kwenye eneo hilo waliwachukua na kwenda kuwahifadhi jirani na Makaburi ya Makanyagio. Eneo hilo limepakana na Frelimo.

Habari kutoka kwa baadhi ya majirani zinasema kuwa wafuga misukule hao walilazimika kuchukua hatua hiyo baada ya vurugu za nyumbani kwa mama Mbilinyi wakiamini aibu hiyo inaweza kuwakuta na wao.


...gari la mfanyabiashara huyo likiwa yamevunjwa vioo kwa mawe.
                  

  LA PILI
Baadhi ya wakazi wa Frelimo ambao waliomba hifadhi ya majina yao, waliliambia gazeti hili kuwa ukiachilia mbali tukio la mama Mbilinyi kudaiwa kuwa misukule ilitoka nyumbani kwake, baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wanaoishi kwenye kitongoji hicho wanafuga misukule kwa ajili ya kusimamia biashara zao.

“Hiki kitongoji ni kichafu tangu zamani, kwani tukiziacha tuhuma za mama Mbilinyi, baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wanaoishi huku wamekuwa wakituhumiwa kuua ndugu zao na kuwafanya misukule ili kuimarisha biashara zao,” alisema mkazi mmoja.

                 LA TATU
Wafanyabishara wenye asili ya kabila moja maarufu mkoani humu ndiyo wanaoaminiwa kujishughulisha na mambo ya kufuga misukule.
Inadaiwa kuwa, wafanyabiashara hao huua ndugu mmoja kila mwaka na kumfanya msukule au ndondocha katika biashara zao, hali inayowaongozea utajiri (kwa mujibu wa imani yao).


...nyumba ya mama huyo baada ya kuvamiwa na wananchi wenye hasira.

 

Kwa sasa Mkoa wa Iringa wenye wilaya 6 ambazo ni Iringa Mjini, Ludewa, Njombe, Makete, Kilolo na Mufindi una makabila makubwa matatu, Wahehe, Wabena na Wakinga.

                LA NNE
Wapo wanaodai kwamba Mama Mbilinyi alikutwa na mkasa huo kufuatia kisasi kutoka kwa mwanamke mwenzake aliyetofautiana naye kibiashara.

Inasemekana kuwa mwanamke huyo ambaye jina halijapatikana, ‘alitengeneza’ watu watatu ambao aliwavisha mashuka meupe na kuwaweka nje ya geti la nyumba ya Mama Mbilinyi na baadaye watu hao walitoka mbio kwenye geti hilo na kwenda kuingia kwenye gari, hali iliyowafanya baadhi ya majirani kuamini ni misukule iliyotoka kwenye nyumba hiyo.

               LA TANO
Watu saba (majina yamehifadhiwa) wanashikiliwa mpaka sasa kufuatia kasheshe hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Evarist Mangala alisema watu hao wanashikiliwa na maafande wake huku uchunguzi ukiendelea.


...wananchi wakiishambulia nyumba ya mama huyo.


     HARUFU YA DAMU
Katika sakata hilo, waandishi wa habari 10 na Mama Mbilinyi mwenyewe walinusurika kujeruhiwa kufuatia mashambulizi ya silaha mbalimbali yaliyokuwa yakifanywa na baadhi ya wananchi.

Aidha, watu wanaokadiriwa kufikia 200 walidaiwa kuizingira nyumba ya Mama Mbilinyi wakitaraji kuiona misukule mingine ikitokea humo.  Mama huyo alilala selo kwa siku nne kabla ya kuachiwa kwa dhamana.

     IMANI ILIYOSAMBAA
Imani ya misukule imekuwa ikichukua nafasi kubwa katika imani za kishirikina nchini ambapo miaka ya hivi karibuni, baadhi ya makanisa yamekuwa yakidai kuirudisha misukule katika maisha ya kawaida.


...askari polisi aliyejeruhiwa katika vurugu hizo akipelekwa wodini.


Mchungaji wa Kanisa la Assemblies of God ‘Mikocheni B’, Dk. Getrude Pangalile Rwakatare amewahi kuwaonesha misukule (angalia picha kubwa mbele) kwa waumini wake akisema walirudia hali ya awali baada ya maombi yake yenye nguvu.

Msukule mmoja alipata ajira kanisani hapo huku mzee mmoja aliyedaiwa kumchukua msukule mtu huyo, akikata shauri na kuokoka.

Views: 8335

Tags: uwazi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by nurdin mkelemi on December 10, 2011 at 9:59pm

dah! huyo mama naamfahamu kabis na kweli atakuwa mchaw kama ndo stail zenyewe ndo hizo du

Comment by Dongonyo Juniour on December 3, 2011 at 3:59pm

Hujui kusoma hata picha huoni; nani asyejua sifa za hilo kabila

Comment by Joseph Mwasha on December 3, 2011 at 2:34am

ukiwa na mihela wanasema unatumia nguvu za giza,ukiwa maskini unadharaulika.mama wa watu usikute wanamzushia kisa ana mihela.wanaacha kwenda kwenye maduka ya wahindi huko wakutane na matukio noma

 

Comment by Mamy Shaluathu on December 2, 2011 at 10:59am

Wanaouwa binadamu wenzao na kuwafanya misukule, wanastahili kupatiwa adhabu ya kifo kabisa.  Huyu mama Mbilinyi  kama ni kweli anahusika Mungu atamuangaza naye siku moja atageuka msukule.

Comment by KINKONGO SERUPYIPYINYURAIMPYISI on December 1, 2011 at 2:30pm

Hapa Dar hilo kabila ndilo linaongoza kwa maduka kariakoo, mtu hajasoma lakini ana pesa balaa za kichawi tena wanaua ndugu bila huruma,

Comment by Ukweli100 on December 1, 2011 at 2:51am

hii kali! wa-iringa mna nini vichwani? khaaa..mnaabisha taifa!

Comment by Rogers Mwachali on November 30, 2011 at 2:49pm
Duh kweli binadam hatuna hofu ya mungu kabisa ni hatari sana hii.
Comment by Zakayo Phillyx on November 30, 2011 at 1:29am
Pole sana ila kweli iyo ipo
Comment by sol on November 29, 2011 at 8:29pm

makanisa yamejaa Dar wakati watu wenye matatizo wapo mikoani makanisa yapelekwe huko mikoani sio Dar

Comment by Mawazo Katota on November 29, 2011 at 6:47pm

Kwanza poleni watu wa Iringa maana hii sio sifa ya kujivunia. Dunia hii ya sayansi na teknolojia bado watu wanafuga misukule kwa matumaini ya kutajirika kweli viongozi wa dini mbali mbali sasa mnayo special assignment iringa kwasaidia kondoo wa bwana.

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by hiepelines Jul 4. 6 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Aug 15. 7 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Aug 15. 6 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by Joe reggan Apr 24. 2 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

Latest Activity

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }