-Ijumaa lashuhudia mmoja akifariki dunia mapokezi.
KUFUATIA mgomo wa madaktari unaoendelea, athari zimezidi kuwa kubwa kwa wagonjwa, Ijumaa limebaini.
Waandishi wetu walikuwepo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili juzi Jumatano na kushuhudia kifo cha Jonson Aseno (picha ya kulia) aliyefia mapokezi baada ya kukaa muda mrefu bila kupata huduma.
Akizungumzia tukio hilo, ndugu wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Philip alisema kifo hicho kimewahuzunisha sana kwani kama kusingekuwa na mgomo kisingetokea.
Philip aliongeza kuwa, Johnson alipata masaibu hayo baada ya kuanguka ghafla eneo la Kariakoo ndipo walimkimbiza hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu.
“Tukiwa Kariakoo pamoja na marehemu tukijiandaa kwenda Uwanja wa Taifa kuangalia mpira kati ya Yanga na Mtibwa alianguka ghafla ndipo tulipokodi gari na kumleta hapa,” alisema Philip na kuongeza;
“Tumekaa muda mrefu mapokezi bila kupata huduma na ndipo kaka yangu akafariki dunia.”
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa tangu madaktari bingwa nao waingie kwenye mgomo, wagonjwa wamekuwa wakiondoka hospitalini hapo na kwenda kufia kwao.
Aidha, wakati gazeti hili linakwenda mtamboni baadhi ya wagonjwa wa akili walichukuliwa na ndugu zao na waliobaki mpango wa kuwarudisha makwao ulikuwa unafanywa.
Comment
Nani wa kulaumiwa? baada ya serikali? mimi naona na madaktari wamekwenda kinyume cha taaaluma yao ya kuacha wagonjwa kufa kwa sababu ya maslahi. Unapopanga mgomo kama huu lazima uangalie huduma za dharura kama za wagonjwa kama hawa. kugoma moja kwa moja ni kukiuka maadili na hili sioni haya kulisema Inelekea siku moja Tanzania itakuwa nchi ya kwanza kwa vifo utakapotokea mgomo wa mdaktari wa nchi nzima. Endeleeni kuwa support.
Comment by Gerrardinho Robert on February 11, 2012 at 12:01am
Comment by Gerrardinho Robert on February 10, 2012 at 11:58pm
Comment by kaka on February 10, 2012 at 2:19pm HAPO KAZI SASA
| 1 |
GLOBAL |
| 2 |
julius manning |
| 3 |
Man KKK |
| 4 |
Sili Silali |
| 5 |
IL-YA |
| 6 |
chama baby |
| 7 |
msichoke mlugu |
| 8 |
kaka |
| 9 |
Maji Marefu |
| 10 |
Kelvin Luhala Eto'o |
othman Ochu posted a status
mrembo commented on Sili Silali's photo

You need to be a member of Global Publishers to add comments!
Join Global Publishers