“Mimi sasa naomba niende, Mungu akipenda tutaonana kama si hapa duniani basi huko mbinguni.”
“Martin! Martin! Martin!” Bibi Monica aliita, tayari alishatoka nje ya wodi na kutokomea.


Alitoka moja kwa moja  na kukielekea kituo cha basi, huko akapanda basi na safari ya kurejea nyumbani ikaanza. Akili  yake yote ikiwaza kitu kimoja tu; Kujinyonga.  Mara kadhaa alijilaumu lakini hakuwa na namna yoyote ya kufanya, tayari shetani alishamvaa.


Kwa sababu ya kutokuwa na foleni muda huo, gari walilopanda lilikwenda kwa mwendo wa kasi na kuwasili kituo alichotakiwa kushuka dakika saba tu baadaye,  akiwa na mawazo mengi akashuka na kuanza kutembea kuelekea nyumbani kwake, akafika na kuingia ndani.


Kwa dakika kumi nzima alizitumia kuzunguka huku na kule ndani ya ngome  kama vile alikuwa akitafuta kitu fulani na alipomaliza akaingia ndani, huko  nako aliingia chumba kimoja baada ya kingine na kutoka aliporidhika akatembea kuelekea sebuleni huko nako akapepesa macho yake huku na kule  ukutani akiziona picha nyingi za mtoto Theresia, machozi yakamtoka.


Alipohakikisha kwamba moyo wake ulikuwa umeridhika, Martin akavuta kipande cha karatasi  na kuanza kuandika kitu kilichoonekana kama ni ujumbe.


“Imetosha!” aliongea akiweka vyema karatasi hiyo juu ya meza ndogo iliyokuwepo eneo hilo.


Akatembea kuelekea nje ambako aliingia kwenye chumba kidogo kilichokuwa pembeni, alipotoka mkononi alikuwa ameshika kamba. Bila kupoteza muda  Martin akaangaza macho yake huku na kule akauona mti na kuusogelea.
Je, nini kitatokea? SONGA NAYO…

“Ngriii! Ngriii! Ngriii!”  ulikuwa ni mlio wa simu ikiita ndani ya Ofisi ya Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ocean Road.


“Mh! Mbona ni asubuhi sana na nani huyo?” alijiuliza akisimama kuifuata simu hiyo.
Taratibu bila kujiuliza mara mbili akanyoosha mkono wake na kunyanyua mkonga wa simu, moja kwa moja akaupeleka sikioni.
“Hallow!” aliita kwa sauti ya unyenyekevu.
“Naongea na Mganga Mkuu, Hospitali ya Ocean Road?”
“Ndiyo!”
“Habari za  kazi?”
“Salama kabisa ndugu yangu, naweza kukusaidia tafadhali?”
“Napiga simu kutoka Geneva, Uswizi, Kitengo cha Union For Internatinal Cancer Control (UICC) mimi ni mjumbe, ninayo maagizo machache kutoka kwa rais wa kitengo hiki.”
Baada ya kusikia  ujumbe huo, jasho jingi likamtiririka kwani haikuwa kawaida ya watu hao kupiga simu mara kwa mara na ilipotokea hivyo, basi huenda kulikuwa na tatizo kubwa au  maelezo yaliyohitajika, akapumua kidogo kisha akamjibu.
“Ndiyo.”
“Naweza kuongea na Dk. Martin?” lilikuwa swali kutoka  upande wa pili wa simu.
“Martin?”
“Ndiyo.”
“Mh! Mh!” kigugumizi cha ghafla kikamshika mganga mkuu.
“Tafadhali sana ni vyema ukaniunganisha na mtu huyo moja kwa moja ni muhimu sana.”
Ukimya wa ajabu ukatawala kwa muda wa sekunde tatu alishindwa kuelewa atoe jibu gani kwa  mwakilishi huyo.


“Hallow! Hallow! Hallow!”
“Ah! Samahani kidogo bwana nimeenda mbali kidogo.”
“Pole, je tunaweza kuongea naye? Ninao ujumbe  muhimu kutoka huku.”
“Huyu mtu hatunaye kazini, ni muda mrefu kidogo.”
“Unasema?” lilikuwa swali jingine.
“Hayupo kazini.”
“Amefariki au?”
“Hapana aliacha kazi yeye mwenyewe kwa hiari yake.”
“Fyuuuu! Hebu subiri kidogo hapo  hapo kwenye simu yako,” aliongea mtu huyo na mkono wa simu ukasikika ukiwekwa chini.


Dakika mbili baadaye  maongezi yaliendelea.
“Tunaweza kumpata kwa njia gani?”
”Kwa kweli  hata sisi hatufahamu lakini tunaweza kumtafuta.”


“Basi ni vyema akatafutwa na kupewa ujumbe huu kwamba amechaguliwa kwa kura nyingi kushika nafasi ya urais katika shirika hili, tutapiga tena simu kesho kwa maongezi zaidi ni vyema akapatikana, ahsante na siku njema!” aliongea mjumbe huyo kwa kusisitiza.


Baada tu ya kuweka mkono wa simu chini mganga mkuu alirejea kwenye kiti chake na kuketi, akaiona hiyo kuwa ni bahati kwa Dk. Martin lakini wangempata wapi kwani  mpaka wakati huo hakuwa na makazi maalum, alishakuwa mtu wa kushinda kijiweni na kulala huko huko.


“Ni lazima apatikane, wamesisitiza mno,” aliongea mganga huyo, bila kuchelewa akausogelea mlango na kuufungua kisha kutoka nje. 
Haraka akatembea na kuingia kwenye ofisi ya wauguzi, huko akamtafuta sista Blandina, alifahamu kwamba  angekuwa na ufahamu kidogo ni wapi wangeweza kumpata Dk. Martin.
“Shikamoo daktari?”
“Marahaba, hamjambo?”
“Siye wazima kabisa hofu kwako.”
“Mimi mzima sijui naweza kumpata sista Blandina?” aliuliza.


“Unaweza kumpata ila kwa sasa ametoka kidogo.”
“Basi ni vyema akirejea tu afike ofisini kwangu mara moja.” aliongea mganga huyo akitoka nje ya ofisi.
Haikuchukua muda mrefu sana Sista Blandina akarejea na kupewa taarifa hizo naye bila kuchelewa alitoka mbio kuelekea  ofisini kwa bosi wake.  Alimkuta mganga mkuu akimsubiri.
“Jambo moja tu nataka kutoka kwako!”
”Ndiyo bosi!”
“Ni vipi tunaweza kumpata Martin bila kuchelewa.”
“Martin?” aliuliza.
“Ndiyo... kuna ujumbe umekuja hapa kutoka UICC unamhitaji sana yeye!”
“Mungu wangu!” aliongea Sista Blandina kwa mshangao huku akionyesha tabasamu kwa mbali, furaha ya ajabu ilikuwa imemwingia baada ya kusikia kwamba Martin alitafutwa  na shirika hilo kubwa duniani.


“Hakuna haja ya kushangaa sana ni vyema mtu huyu akatafutwa mara moja na kesho wameahidi kupiga simu ili waongee naye,” alimaliza mganga mkuu.


“Ni kwa muda mrefu sana sijapata taarifa za mtu huyu, pengine tujaribu kwenda hospitali ya Muhimbili tunaweza kumpata huko.”
“Wazo zuri sana, tunaweza kwenda sasa hivi?”
“Hakuna shida.”
Bila kuchelewa wakanyanyuka vitini na kutoka nje ya ofisi, huko waliwapitia madaktari wengine wawili zaidi ili kuunganisha nguvu zao.

Wakatembea kwa pamoja na kuingia ndani ya gari na safari ya kuelekea Hospitali ya Muhimbili ikaanza.


Dakika ishirini tu baadaye walishafika hospitalini hapo, wakashuka na kutembea kuelekea wodi ambayo alilazwa mkewe wakagonga mlango na kuingia ndani.


“Habari za hapa bibi?” walisalimia kwa pamoja.


“Tunamshukuru Mungu,” alijibu bibi Monica  kwa sauti ya chini.
“Vipi Martin ameonekana hapa leo?”
“Mh! Ndiyo...” alijibu lakini tayari mashavu yake yalishalowa machozi.
“Kuna nini bibi mbona unalia?”
“Mambo hayaendi sawa tena ninashukuru Mungu mmefika pengine mnaweza kunisaidia juu ya hili.”
“Nenda moja kwa moja kwenye pointi bibi.”
“Amekuja hapa lakini ameondoka, akiniachia maswali mengi kichwani mwangu.”
“Kama yapi?”
“Kwa inavyoonekana ni mtu aliyekata tamaa ya maisha na anaweza kufanya lolote lile, ameongea maneno yaliyonitia shaka sana moyoni mwangu.”
“Amesema anakwenda wapi?”
“Hajaniambia ila…” kwikwi ya kulia ikamkaba bibi Monica, hakuweza tena kuendelea kuzungumza.
“Nahisi atakuwa nyumbani hebu twendeni huko.”
“Mh! Sidhani awe nyumbani kweli?”
“Nashauri tuanzie huko kama atakosekana basi tutaingia mitaani,” aliongea mganga mkuu, wote kwa pamoja bila kupoteza wakati wakafungua mlango na kutoka.


Ni huko nje ndipo walipokutana  na mtoto Theresia, walisalimiana na kumwomba mtu aliyeongozana na mtoto huyo, haraka wageuze kuondoka eneo hilo.
“Kuna nini kwani?”
“Baba yake! Baba yake…” bibi Blandina aliongea akimshika mkono Theresia.


Wote kwa pamoja wakaingia ndani ya gari na kuondoka eneo hilo.

Safari ya kuelekea nyumbani kwa Dk. Martin ikaanza, watu wote ndani ya gari wakionekana wenye mawazo mengi kupindukia.
***
Taratibu huku akitetemeka na jasho jingi kummwangika, machozi mengi yakimbubujika, Dk. Martin alifanikiwa kupanda juu ya mtu na kuliendea tawi moja kubwa, hapo akatoa kamba aliyokuwa nayo lakini kabla hajafanya lolote taswira za mkewe Manka na mtoto Theresia zikamwijia, alikuwa akiwaacha duniani peke yao.


Akajipa moja akisema kwamba hata Manka naye hakuwa na muda mrefu angeungana naye ahera, tatizo pekee lilokuwa kwa mtoto Theresia ambaye angebaki duniani bila baba wala mama.


“Bibi Monica atamtuza vyema naamini hivyo, Mungu wangu nisamehe kwa kosa hili pengine linaweza kuwa kosa kubwa sana lakini sina jinsi, sipo tayari kushuhudia kifo cha mwanamke niliyempenda katika maisha yangu, hivyo mimi natangulia yeye atafuta baadaye…”aliongea Martin.


Tayari alishakamata sehemu ya kamba aliyokuwa nayo mikononi mwake. Akaifunga kwenye tawi la mti kisha akachukua upande mwingine na kutengeneza kitanzi, akakivaa shingoni mwake.


Akiwa juu ya mti akatupa macho yake huku na kule akaiona nyumba nzuri aliyokuwa akiishi yeye na familia yake lakini sasa alikuwa akiiacha bila kujua nini ingekuwa hatima yake. Akafumba macho yake na kuanza kuhesabu ili ajiachie kuelekea chini.
“Moja…mbili…taaaaat...”alihesabu akijiandaa kijiachia.

Je, nini kitaendelea? Fuatilia Jumatano ijayo katika Gazeti la Ris

Views: 2251

Tags: hadithi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by michael sammy on November 7, 2011 at 9:15am
ukipona hapo songa mbele usikate tamaa
Comment by Ediclad Ansgary Kihinja on November 5, 2011 at 11:38pm
acha upumbavu dogo
Comment by barick mtery on November 5, 2011 at 10:45pm
Mh..ya leo tamu mpaka kichogon japo fupi!
Comment by HAPPINESS MARCEL on November 5, 2011 at 7:17pm
Hafi wala , watamuokowa
Comment by vincent on November 5, 2011 at 12:41pm
jiachie haraka basi kabla hawajakukuta hai bana
Comment by apple on November 5, 2011 at 12:18pm
Angalau leo mwanga umeonekana.
Comment by Kyaruz Chris on November 5, 2011 at 12:02pm
Mbona inaishia kwenye utamu?but hafi watamkuta.
Comment by Glady-Cathy on November 5, 2011 at 10:54am
haiyaaaaaaaaa utam ila hatowahi kujinyonga
Comment by sugar s on November 5, 2011 at 10:49am
this story is more than a shit
Comment by Righteousness Mmasa on November 5, 2011 at 10:47am
Nikwel inauma na inatesa kuona kama dunia inakadhibu phillipo lakin sisahihi kujatiza uhai wako.Fikiria na atangalia nyuma ya kiganja chako ndipo ukatesha shauri na lenye manufaa kwa sasa na baadae.Piga moyo konde na songa mbele.
UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }