Maulidi Kitenge aoa mke wa tatu

Prizenta anayekimbiza kwenye habari za michezo na burudani Bongo, Maulidi Baraka Kitenge amevuta mke wa tatu, Ijumaa limepenyezewa.

Kwa mujibu wa sosi wa habari hii ambaye jina lake linawekwa kibindoni kwa sasa, Maulidi ‘Namba Tisa Mgongoni’, amefunga ndoa na Mwanaidi Yatery Juni 17, 2010 kwenye Msikiti wa Kichangani, Magomeni Mapipa jijini Dar.
Ikazidi kuanikwa kwamba, baada ya ndoa hiyo, cherekochereko na vifijo vilihamia nyumbani kwa wazazi wa Bibiharusi, Mabibo, Dar.

Aidha, Juni 20, 2010 kukafanyika Maulidi kwenye ukumbi uliopo jengo la May Fair, Mikocheni, Jijini Dar kabla ya kufunga pazia kwa Pati ya ‘kuvunja na shoka’ iliyotwaa nafasi yake Jumamosi ya Juni 26, 2010 ndani ya hoteli ya Paradise, iliyopo Jengo la Benjamin Mkapa, Barabara ya Azikiwe, jijini Dar.


Wakati huo huo habari zisizo na chenga zinasema kuwa, mtangazaji huyo ameamua kufunga ndoa na Mwanaidi baada ya kumpiga chini kwa talaka aliyekuwa mkewe wa pili Januari mwaka huu.

“Unajua kwanini jamaa kaamua kuoa mke mwingine? Yule aliyemuoa mwaka 2007 alimpa talaka Januari mwaka huu, kwa hiyo nafasi ikabaki tupu,” kilisema chanzo chetu.
Juhudi za kumpata Maulidi ziligonga mwamba baada ya simu yake ya mkononi kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa hata pale iliporudiwa.

Hata hivyo, mtu wake wa karibu alipopatika na kuulizwa alithibitisha kuwepo kwa ndoa hiyo na pia alikiri kuwepo kwa talaka kwa mke wa pili, Rehema Kayugwa, hivyo kumfanya mtangazaji huyo kuendelea kuwa na wake wawili licha ya kufunga ndoa ya tatu. Mke mkubwa wa Maulidi anaitwa Eshe Muhidin ambaye pia ni mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha TBC1.

Gazeti hili linamtakia maisha mema ndani ya ndoa mpya huku akikumbuka kuwa, mke ndani ya nyumba hapigwi kwa fimbo au makofi, hupigwa kwa upande wa khanga.

Views: 7091

Tags: ijumaa11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by hajimakame on February 3, 2011 at 10:49am
 nyinyi akina dada hivi upi ni umalaya  kati ya nyumba ndogo au kuoa wake watatu tambueni idadi ya wasichana  mara tano zaidi ya wavulana. sasa nani atakayewaoa hawa dada zetu katika idadi kama hiyo .kuoa mke mmoja ni kujiweka katika risk ya kupata maambukizo ya virusi vya ukimwi, maana ukiwa na wake zaidi ya mmoja ni kuwasitiriana . mwachieni aoe 1,2,3, mpaka 4 sasa kuoa uzeeni ndio atakua hawamudu sasa ndio anawamudu kwa sababu ana nguvu uwezo wa kuwahudumia  akioa wakatiwa uzeeni hataweza kutekeleza majukumu ya wake hao.hatakua fataki kwa sababu wake watatu wanatosha. kuondosha kiu aliyokua nayo.unajua ukiwa na wake 3 ndio ushamba wa kumuona kila mwanamke mzuri unaisha kuoa wake watatu sio ujinga ndugu yangu acha jazba  mwanasheria wewe ndio tunakutegemea utetee haki za wanawake waolewe lakini unatetea wabaki mitaani kazi hawana  wakajiuze  aa mimi naona mweye busara na kama wewe ni mwanamke basi kubali ukewenza ingawa una changamoto zake   ahsanteni
Comment by neema molleli on February 1, 2011 at 1:20pm
mmmh wewe inaelekea unapenda wanawake sana,,,, sasa wazuri ndio hao wanazaliwa kila siku na wewe unaelekea uzeeeni,, si utakua fataki wewe jamani??
Comment by h.k.th on January 17, 2011 at 12:13pm

aah hongera bwana jitahidi na kulinganisha penzi lako lisiwe hafifu kwa mmoja

 

 

Comment by Mambo Jambo on January 14, 2011 at 5:00pm

Kweli ujinga umetawala ktk jamii za watu waishio dunia ya tatu,!! Adui mkubwa wa Tanzania ni Ujinga na Umasikini, Sasa mtu kama huyu alieshindwa kumiliki tamaa zake za kimalaya eti anasifiwa? 1)Ninahakika hana uwezo wa kuakamilishia mahitaji yao haswa elimu kwa watoto watakao zaliwa humo, 2) Watoto wanao zaliwa ktk family kama hii hua na mvutano chuki ambayo wakati mwingini husababisha kurogana na uana 3) Tasisi za kijamii nyingi zipo wapo wapi kuzungumzia tatizo kama hili ?? Wa Tanzania amkeni kupinga vitendo viovu ktk jamii yenu watoto wa mtaani hawata isha kwa mtindo huu.  

Comment by RAJAN HUSSEIN on January 13, 2011 at 9:44am
Congrats wa kitenge ila ningependa kushauri uwe mwenye jitihada za kuweka wakawa kitu kimoja kama wake zako na pia kushirikiana kwa kila hali.....basi utakuwa wa amani ktk ndoa zako kwani Fitna hazitokuwepo za kupitiliza...
Comment by Lucy Samwel on January 10, 2011 at 11:14am
Mmh! siyo sifa tena hata kama dini inaruhusu ndiyo ufanye hivyo
Comment by Mohamed Abdulaziz on September 19, 2010 at 8:23am
Safi sana Maulid, bado wawili mtu wangu! hadi nakuonea wivu mwana!
Comment by Joyce on July 12, 2010 at 8:53am
yaani we maulid ni mzuri ila unapenda sana wanawake acha hizo utakufa na ngoma
Comment by meggie impostra on July 11, 2010 at 7:40pm
hamna lolote tamaa zake na umalaya wake ndio wamfanya aoe kila kukichaaa ew mtt mdogo unakuwa na tabia kama za mababu zetu bwana ambazo siku hz wachache wanaozfuata kuoa wake wa 3 wa tano hata kama unawaudumia lkn kwa mtu kama wewe na ujana wako wala haipendezii kbsaaaa lol
Comment by Dinna on July 6, 2010 at 9:07am
Mh! hakuna cha udini wala nini kwa karne hii kijana mdogo kama wewe unaoa oa hovyo hata haipendezi kwani huyo mmoja umeshaweza kumtimizia haja zake? kwanza ni kumdhalilisha mkeo wa kwanza acha ushamba maulid unakuwa kama hujaenda hata darasa. Dini dini mbona viongozi wapo waislam na uwezo wao hawana zaidi ya mmoja acha kusingizieni dini ni tabia ya kutotulia na kupenda chini.
UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }