MATOKEO MABOVU YA KIDATO CHA NNE, WAZIRI WA ELIMU NA NAIBU WAKE WAWAJIBIKE - ZITTO KABWE

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa.

Matokeo ya Kidato cha Nne ya namna hii (zaidi ya nusu ya wahitimu kupata sifuri) na takribani asilimia 90 kufeli kwa kupata daraja la nne na daraja la sifuri ni mwaka tatu sasa mfululizo. Matokeo yakitoka tunasema weeee mpaka povu linatoka. Baada ya wiki tumeshasahau na hakuna hatua yeyote. Lazima Uwajibikaji utokee.

Kwanza Waziri lazima awajibike na Naibu wake na Katibu Mkuu na Kamishna. Najua kuwa haina uhusiano wa moja kwa moja maana matatizo ya elimu ni makubwa sana nchini. Lakini ni lazima kitu fulani kitokee ili kufanya mabadiliko. Uwajibikaji ni njia mojawapo inayoleta nidhamu na 'urgency' katika utendaji kazi.

Tumwambie Rais aichukue Wizara ya Elimu, yaani Waziri wa Elimu awe yeye (kuwe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Elimu). Tumwambie matokeo yakibaki hivi mwakani na yeye atatoka. Najua wa mwakani ndio wapo kidato cha nne sasa na wana msingi mbaya tayari lakini sio jukumu letu kujipa majibu bali ni jukumu letu kuiambia Serikali hapana. Tuwape Masharti. Vinginevyo haya yatakwisha na mwakani itakuja nk.

Hawa watoto wanakwenda wapi? Mwaka jana tulisema mpango wa kujenga vyuo vya ufundi kila Halmashauri ya Wilaya uanze mara moja. Katika Bajeti Kivuli mwaka 2011 tulipiga hesabu kwamba tunahitaji tshs 720 bilioni katika kipindi cha miaka 5 ijayo kujenga vyuo vya ufundi vya VETA kila Wilaya. Tukawaambia badala ya kukopa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kulipana posho ni vema tukope kuwekeza kwenye elimu maana Elimu ni Hifadhi ya Jamii. Elimu yetu ya sasa inazalisha matabaka kwneye jamii na ni hatari sana kwa uhai wa Taifa.

Tunaweza kujidai kujenga madaraja na miji mipya. Tunaweza kujidai kujenga mabomba ya gesi na kusambaza umeme kila kijiji mpaka kwenye vyoo. Kama hakuna Elimu haya yote ni bure kabisa. Hata kukosa uvumilivu wa kiimani sasa hali itakuwa mbaya zaidi unapokuwa na Taifa la mambumbumbu. Waziri Kawambwa na wenzake watoke. Watoke SASA! - HIVI NDIVYO ALIVYOANDIKA MH. ZITTO KABWE KATIKA UKURASA WAKE WA FACEBOOK

CHANZO: Zitto Kabwe

Views: 654

Tags: Kabwe, Zitto

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by sabbo sabbo on February 20, 2013 at 3:06pm

nani alaumiwe? matatizo ya elimu ni mengi hayajapembuliwa katika kile wanachodai wachambuzi na wapembuzi 'kwa upembuzi yakinifu'. Nchi yangu Tanzania na dunia ya Utandawizi! mbona hata viwango vya ufaulu kwa watoto wa nchi za magharibi vimeshuka na watu kudanganya ktk mitihani inawapa ma-professor wa UK na Amerika kutolala katika miaka ya hivi karibuni?.

Comment by samora rajab albert on February 19, 2013 at 5:01pm

watoke kweli, hakuna peace hapa watt wamefeli kupindukia

Comment by Zamda Misemo on February 19, 2013 at 4:19pm

Kwanza mi nashangaa huko msingi eti kila shule tena ya serikali wanajiamulia ni vitabu gani watumie. Kuna wanaotumia Oxford, wengine MacMillan, wengine Jadida nk. Ubora wa vitabu unatofautiana na wote hao wameidhinishwa na serikali. Halafu hesabu za kuzidisha na kugawa wanaanza kufundisha darasa la tano. Sasa hao wakiingia sekondari ni kuambulia sifuri na hakuna cha ajabu. Wajibikeni waheshimiwa kazi imewashinda wajaribu wengine.

Comment by Zamda Misemo on February 19, 2013 at 4:10pm

Elimu ya msingi imeoza, kumbe na sekondari hakuna kitu. Naunga mkono hoja ya Mh Zitto, yafaa Mh Dr Kawambwa awajibike kiungwana atakuwa ametutendea haki Watanzania.

Comment by tatu said on February 19, 2013 at 2:45pm

hzo za kata ndo uozo kabisa,mwanafunz hajui kusoma atafauru vp?

 

NI SUPERMARKET GANI BORA KULIKO ZOTE KATI YA HIZI? NA KWA NINI? TOA MAONI YAKO!
  

Forum

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson on Friday. 11 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by mark gibson on Friday. 28 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

JUAN MATA KUTUA MANCHESTER UNITED ATASIADIA KULETA MATOKEO BORA BAADA YA TIMU KUSUASUA?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson on Thursday. 88 Replies

Juan Mata anataraji kutua Manchester United akitokea klabu ya Chelsea ya…

KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KILA MARA, TATIZO NI NINI?

Started by GLOBAL in Habari. Last reply by mark gibson on Friday. 45 Replies

VITENDO VYA KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KWA SASA VIMEZOELEKA. KATIKA NCHI MBALIMBALI WATANZANIA WAMEKUWA WAKIKAMATWA KWA UBEBAJI WA MADAWA HAYO. JE, TATIZO NI NINI? NA NINI KIFANYIKE?

Tags: MARA, TATIZO, NI, NINI?, KILA

JESHI LA POLISI KUTOA MILIONI 100 KWA ATAKAYEWEZESHA KUPATIKANA WAHALIFU WANAOMWAGIA WATU TINDIKALI NI KWAMBA LIMESHINDWA KAZI?

Started by GLOBAL in Maisha. Last reply by mark gibson on Friday. 74 Replies

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.Jeshi la Polisi…

SIMBA SC WAMTUPIA VIRAGO JUMA KASEJA

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson on Saturday. 12 Replies

TIMU ya Simba SC leo imetangaza rasmi kuachana na mlinda mlango wake mahiri, Juma…

JE, NI SAHII KWA JESHI LA POLISI KULIPUA MABOMU WAKATI WANANCHI WAKIAGA MIILI YA WENZAO?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson yesterday. 36 Replies

Juzi (Jumanne) polisi walilipua mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa wamekusanyika katika Viwanja vya Soweto jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili ya wenzao watatu waliopoteza maisha katika…

UKIMYA WA VYOMBO VYA DOLA KUTOA TAARIFA ZA MATUKIO YA MAUAJI NA UTEKAJI NI ISHARA KUWA WANAHUSIKA?

Started by GLOBAL in Habari. Last reply by mark gibson 20 hours ago. 21 Replies

Absalom Kibanda akiwa ICU.USIKU wa Jumanne ya Machi 5 kuamkia Machi…

Tags: UTEKAJI, NA, MAUAJI, NI, ISHARA

TOP NEWS WEEK HII

© 2014   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service