Na Mwandishi Wetu
Zimebaki siku saba kumalizika kwa mwaka 2010, tukielekea kufunga wiki ya 51, orodha ya mastaa wa Bongo waliotia fora kwa skendo wanaanikwa.
The Udaku Master, Ijumaa linaanika staa mmoja baada ya mwingine na jinsi walivyovuma na skandali zao;

ELIZABETH MICHAEL ‘Lulu’
Ni staa mwenye umri mdogo ambaye alitikisa zaidi mwaka 2010. Aliandikwa kwa matukio yake ya kulewa kupita kiasi kwenye kumbi za starehe na kuvaa nusu uchi.

Lulu ambaye umri wake una utata, ikidaiwa yupo chini ya miaka 18, pia alihusishwa na matukio ya kimapenzi, kubwa zaidi likiwa lile la kutoka kimapenzi na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba.

Kama hiyo haitoshi, aliripotiwa mwaka huu kugombana na ‘sidanganyiki’ mwenzake, wakidaiwa kurushiana makonde kisa kikiwa ni penzi la ‘janki flani’ hivi.


JACQUELINE WOLPER
Kati ya mastaa waliofanya vizuri kwenye soko la filamu Bongo mwaka 2010 ni Jacqueline Wolper lakini alitikisa kwa kuandikwa mara kwa mara akihusishwa na skandali mbalimbali.

Moja ya matukio hayo ni ile ya kudaiwa kutoka kimapenzi na chipukizi wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’.

Tukio lingine ni lile alilodai kutaka kubakwa na mtu aliyemsema ni mjomba wake anayeitwa Exaud Macha.

Hata hivyo, baadaye Macha alidai kuwa Wolper ni mpenzi wake na hakuwa na lengo la kumbaka, isipokuwa msanii huyo alitaka kujimilikisha gari lake ndiyo maana alimdai.

Wolper alinaswa na skendo nyingine ambayo ilielezwa kwamba ‘alibondana’ na chipukizi wa filamu, Zuwena Mohammed Yusuf ‘Shilole’, ingawa baadaye walirekebisha tofauti zao.

REHEMA CHALAMILA ‘RAY C’
Staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ alinaswa na skendo kadhaa, moja ikiwa ile ya kudai kulazimishwa penzi na promota wa Kenya, Sadat Muhindi.

Hata hivyo, Sadat alikanusha skendo hiyo lakini Ray C hakurudi nyuma, kwani siku chache zilizofuata alitangaza kuachana na mchumba wake aliyedumu naye kwa zaidi ya miaka mitatu, Isaac Waziri Makuto ‘Lord Eyez’.

Ray C a.k.a Kiuno Bila Mfupa pia mwaka huu aliandamwa na mzimu wa kuhama hama makazi kabla ya kuuza nyumba yake na kufungua duka, kisha ikaripotiwa kwamba amerudi nyumbani kwa mama yake, Bunju, Dar es Salaam.

AUNT EZEKIEL ‘GWANTWA’
Super Character wa Kiwanda cha Filamu Bongo, Aunt Ezekiel ‘Gwantwa’ aliandika historia mwaka huu kwa kuripotiwa kuhusika na skendo mbalimbali.

Moja ya matukio hayo ni lile la kugombana na msanii mwenzake wa filamu, Jennifer Mwaipaja ‘Shumileta’.
 

SYLVIA SHALLY
Miss Ilala 2009-2010, Sylvia Shally aliandikwa sana kupitia uhusiano wake wa kimapenzi na staa wa filamu Bongo, Steven Kanumba.

MIRIAM JOLWA ‘KABULA’
Super-tall wa Kiwanda cha Filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Kabula’, aliandikwa kwa skendo zake za kuvaa nguo ambazo zilimuacha wazi karibu asilimia 80 ya mwili wake.

Kabula ambaye aliitwa Jini kutokana na jinsi alivyomudu kucheza Igizo la Jumba la Dhahabu kwa nafasi ya jini, alivuma mwaka huu kwa uhusiano wake na Mfalme wa TAKEU, Nice Lucas Mkenda ‘Mr. Nice’ ambaye baadaye waliachana kwa kukashifiana.


MR. NICE
Mbali na skendo ya Kabula, Mr. Nice aliripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini baada ya kikundi cha watu fulani kumteka na kumpiga picha chafu ambazo walizisambaza.


KHALEED MOHAMED ‘TID’
Mkurugenzi wa Top Band, Khaleed Mohamed Salum ‘TID’ kwa mara nyingine, mwaka huu aliingia kwenye ‘kashkash’ za kupigana, mojawapo akiripotiwa kumtwanga mrembo mmoja jijini Dar.

HASHEEM THABEET
The 7.3 ft, Hasheem Thabeet Manka, alivuma na skendo yake moja ya ‘kumzibua’ TID mpaka staa huyo wa Bongo Fleva akazimia.

Hasheem anayevaa jezi namba 34 akiwa na Klabu ya Basketball ya Memphis Grizzlies inayocheza Ligi ya NBA, Marekani alipoulizwa kuhusu kumpiga TID alisema kuwa staa huyo wa Zeze alimchokoza.

BONIFACE AMBANI
Aliwika akiwa na Klabu ya Yanga kwa misimu miwili mfululizo, 2008-09 na 2009-2010 kabla ya kuondoka, akiwa nchini alivuma kwa uhusiano wake wa kimapenzi na msanii wa filamu nchini, Flora Mvungi.

NELLY KAMWELU
Ni Miss Ilala namba 2 2008-09, pia alifanikiwa kutinga 10 Bora ya Miss Tanzania mwaka huo, skendo zake mwaka huu zilikuwa nyingi, akiripotiwa kuchapa kilevi ‘kwa sana’ mpaka kupoteza ‘network’.

NASEEB ABDUL ‘DIAMOND’
Mwaka huu alitoka vema kimuziki lakini baada ya kulamba tuzo tatu za KTMA Mei 14, 2010 pamoja na ‘dili’ la ubalozi wa malaria, alianza kuchangamkia skendo akianza na kutoka kimapenzi na Wolper.

Diamond pia alihusishwa na ‘kashkash’ za mapenzi na warembo, Rehema Fabian ‘Balozi wa Kiswahili’, mshiriki wa Miss Tanzania, Amisuu Maliki na Upendo Mushi aliyeshiriki Maisha Plus.

JOSEPH SHAMBA ‘VENGU’
Hivi sasa amesimamishwa kwenye kundi lake la Orijino Komedi na sababu ya kupigwa ‘suspensheni’ ni skendo mfululizo lakini zote zikiambatana na ulevi wa kupitiliza.

Views: 1383

Tags: ijumaa11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by Omary Muhidin on December 28, 2010 at 6:01pm
Acheni sifa mbaya jamani kumbukeni kuwa ninyi ni kioo cha jamii so mnapokuwa unaonyesha sifa mbaya sisi pia tutaiga zaidi yenu sawa ila huo ni ushauri
Comment by Christina on December 28, 2010 at 10:04am

mhm!

 

Comment by marimar ethan on December 26, 2010 at 10:31am
ndio maana hawaolewi
Comment by vita wilbards on December 25, 2010 at 4:28pm
bwana MSEMI MGONZA KIRUNGI UMENENA
Comment by MSEMI MGONZA KIRUNGI on December 25, 2010 at 5:16am
ni hivi kwa nini mzee jongo akuitwa staa au mbaraka mwinshehe,mzee morisi,akina sembuli na watu mashuhuri wakati wote na tena walikuwa wanasifika sio nchini peke yake ata nje ya nchi hivi sasa mtu akipigwa picha mara tatu au akisika kwenye vyombo vya habari lokali basi ashakuwa staa  hivi mnajua maana ya ustaa ebu fikirieni mtu kama bluce lee akujiamini kuitwa star ata bob marley alikuwa  akikanusha habari sio eti walikuwa awafiti la asha ila kukimbilia sifa siyo ufumbuzi leo hii msanii ata soko ana ashaitwa staa sasa serikali ikitaka kodi ya kazi zenu mnaweza kutoa kulingana majina yenu?na mnapotaka kupewa mialiko ya nje ya nchi munaweza kuzitaja hizo fani zenu kwa viwango?na kama mtafanya maonyesho munaweza kufikia kama akina mbaraka,molisi,afro sabini walivyokuwa wanatingisha bila ivyo vijina visivyo na maana tunachojua huwa mnasafiri kama watu wa kawaida na huko uraya mnapokewa kienyeji na hao wenyeji wenu ndio huwa wanawatafutia vikumbi vya chini hili wajifurahishe na sio kama akina mwaruka jiji lolote wakitua lilikuwa linawaka moto na huwa wanawacha kumbukumbu ugenini.
Comment by Bena Mushi on December 25, 2010 at 1:26am
Ustaa ni upi haswa.
Comment by moses sarai on December 24, 2010 at 11:53pm
hakuna star bongo wanajifurahisha tuu
Comment by Mustapha Hanya on December 24, 2010 at 5:56pm

Hivi ustar kibongo bongo maana yake ni nini hasa....??!!!

Kuwa player ama....??

Kama ni mwanadada kukaa nusu uchi ama....??

Wapi maana ya kioo cha jamii kuandikwa sana magazetini kwa kufanya mautumbo....??

Mwaka unaishia huu kama vipi jipangeni upya 2011 mjisafishe maana mtaishia kuwa big G....!!

Mustapha maDish

Comment by Sarah Anuary on December 24, 2010 at 2:03pm
Jamani nyie mnaoitwa kioo cha jamii acheni upuuzi, mwafkiri mwafundisha kitu gani kwa vizazi vipya vikuaavyo na taifa kwa ujumla? Acheni ujinga fanyeni ya maana ili watu waweze kuproud kwa muyatendayo sio kuwachukia......tieni akili sasa za kiutuzima acheni akili za kipumbaaaa.
Comment by KIRIMENI on December 24, 2010 at 1:02pm


ADVERTISEMENT


TANGAZA HAPA

ADVERTISEMENTS

Latest Activity

GUNZ TRUVADA posted a status
"KUMPA ASIYE KUPA NI SAWA SAWA NA KUTUPA"
5 minutes ago
GUNZ TRUVADA posted a status
"KUMPA ASIYE KUPA NI SAWA SAWA NA KUTUPA"
5 minutes ago
othman Ochu posted a status
"SCENE 1 WAHUSIKA: AMIDU , SHARIFA MAHALI: ZANZIBAR MUDA : JIONI ( WAKIWA WANASHUKA TOKA KATKA BOTI YA JION KUINGIA KATKA MJI WA ZANZI"
9 hours ago
Priscus Adelard shared GLOBAL's blog post on Facebook
9 hours ago
mrembo commented on julius manning's photo
Thumbnail

Mtanzania huru

"pole sana usijali iko siku mungu atakujaalia mungu hamtupi mja wake"
10 hours ago
mrembo commented on Sili Silali's photo
Thumbnail

Duh!

"mama mzima hayawani mavazi gani hayo takupa mfano chungwa likiwa halijamenywa unatamani ulile…"
10 hours ago
kaka commented on Ali Amur Ali's video
Thumbnail

AZIMIO LA KUANGAMIZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE

"hapo ni kina dada kutua comment zao"
10 hours ago
Gaston Kayombo commented on Ali Amur Ali's video
12 hours ago
roylicious and Jackson Jacob are now friends
12 hours ago
babu wa loliondo (cup) updated their profile
12 hours ago
julius manning commented on julius manning's photo
Thumbnail

vijana 2016 itakuwa hivi

"@furaha mimi ni kikongwe hayo ni kazi kwako."
13 hours ago
Masalu Mayeji Many'hasimha shared GLOBAL's blog post on Facebook
13 hours ago

© 2012  

Designed & Developed by
G5 CLICK COMPANY.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

How to make a Website