Na Shakoor Jongo
ULE uhasama usioisha kati ya mke mkubwa na mdogo wa mwimbaji na Mkurugenzi wa Kundi la Jahazi Modern Taarab Mzee Yusuf, umemtoa chozi mama mzazi (jina hatunalo) wa mfalme huyo wa mipasho nchini, aliyekwenda kutazama shoo ya mwanaye ukumbini.

Leyla Rashid (mke mkubwa) na Chiku Salum mke mdogo wa Mzee Yusuf, juzikati walizua timbwili la nguvu ndani ya ukumbi wa Travertine uliopo Magomeni jijini Dar es Salaam, huku sababu zikitajwa kuwa ni kupigana vijembe.

Simulizi ya shuhuda inaanzia kwa binti mmoja anayetajwa kuwa ni ‘hausigeli’ wa zamani wa Leyla kuingia ukumbini humo wakati wa maandalizi ya shoo ya Jahazi na kuketi karibu na Chiku kisha kuanza kuimba nyimbo zilizotafsiriwa kuwa za kejeri kama sio vijembe.

Uvumilivu ulipozidi kipimo, mke mdogo wa Mzee Yusuf alifura, ambapo alimuita mumewe na kumshtakia ‘ushambenga’ wa msichana huyo aliyedaiwa kuwa katumwa kumpaka shombo ya maneno machafu.

Inaelezwa kwamba kabla mumewe hajatafakari kwa kina maelezo hayo, Chiku na yule msichana walianza kurushiana matusi ya nguoni na kutambiana kidume.

Mzee Yusuf alipoona hewa inazidi kuchafuka alipanda jukwaani kuteta na Leyla ili ashuke kwenda kumuondoa yule msichana aliyedaiwa kuwa ni mpambe wake, ili aibu isitokee mbele ya mkwewe.

Hata hivyo hatua hiyo ilishindwa kuuzima mtiti huo kwani, Leyla na yule msichana waliendelea kupiga vijembe vilivyompandisha jazba Chiku ambaye aliamua kutaka kuzipiga na mke mwenziye.

Ndipo Mfalme Mzee Yusuf alipoingilia kati na kuanza kuzuia mapigano hayo, hali hiyo ilifanya kutawala kwa matusi ambayo yalimfadhaisha mama Mzee na kujikuta akiangua kilio kama mtoto.

“Uwiii…iiiiii…jamani ..jamanii” alisikia mama huyo akilia huku akijipigapiga kifuani kuashiria uchungu usiokuwa na kifani juu ya tukio hilo.

Shetani wa machafuko hakuishia hapo, alimuingia Mzee Yusuf ambaye alijikuta akimpiga makofi yasiyokuwa na idadi mke wake mdogo kwa utovu wa nidhamu mbele ya mkwe wake.

Habari zaidi zinaeleza, mtifuano ulipozidi Mkurugenzi wa Fedha wa Jahazi aitwaye Seif Magwalu aliingilia na kufanikiwa kutuliza mambo.

Hadi tunakwenda mtamboni Mzee Yusuf hakupatika kuelezea kilichojitokeza baada ya tukio hilo la aibu la wakeze kumvunjia heshima mama mkwe wao ukumbini.

Views: 5172

Tags: mchanganyiko11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by lion on October 12, 2010 at 2:41pm
MAMA YUSUFU NAWE UMEZIDI LIP SHINE LOTE HILO WAKWE ZAKO NAO WANAJUA NAWE BADO WAMO
Comment by lion on October 12, 2010 at 2:38pm
POLE SANA MZEE YUSUFU LAKINI LITAFUTIE UFUMBUZI
Comment by moses sarai on October 7, 2010 at 2:10am
KUNA WATU WANA WAKE WANNE NA HAKUNA NGUMI WALA KELELE,NA KUNA WATU WANA MKE MMOJA TUU FULL VURUGU NA KUPIGANA,KINACHOONEKANA HAPA NI KWAMBA HUYU MZEE YUSUPH HANA UWEZO WA WAKE WAWILI HIVYO INABIDI AKAE CHINI AFIKIRI TENA KWANZA KIUMRI HAJATULIA, NA HUYO MAMA WA MZEE YUSUPH PIA HAJATULIA WE USHAKUWA MTU MZIMA NINI KILICHOKUFANYA UMKIMBIE MUMEO NA KWENDA KUANGALIA NGOMA,HUU MAMA NI WAKATI WA KUFANYA SANA IBADA NA KUACHANA NA HIZI NGOMA ZILIZOJAA IBILISI,UTAKUJAFIA KWENYE NGOMA BURE NI BORA UFIE MSIKITINI MAMA KWA UMRI HUO?NAKUSHAURI MAMA USIENDE TENA KWENYE NGOMA HIZI SIO TAARAB KAMA ZILE ZA WAKATI WENU HIZI NI NGOMA ZA MASHETANI KWANI HAPO NI MAMBO MACHAFU TUU HAKUNA ZURI HAPO WAACHIE VIJANA MAMA,
Comment by isack solomon on October 7, 2010 at 12:34am
mzee na wewe uwe unajua utaratibu bana,aliepaswa kuhudhuria ilo onyesho ni yule mwenye zamu yake ya wewe kulala ambae hana zamu angebakia tu kwake na yeye angoje siku yake.sasa si unaona balaaa?
Comment by kibabaa on October 6, 2010 at 8:45pm
Sebastian unakosea, hakuna dini inaruhusu mke mmoja, ila maamuzi ya watu baada ya kuondoka Yesu, ukiangalia wapi mitume imetoka, utagundua maeneo hayo yote hakukuwa na sheria hiyo ya mke mmoja, hii ilianzishwa na nchi za Ulaya na wafalme wao, ndio maana ukiangalia madhehebu mengi yanafuata maamuzi ya wafalme wa siku hizo, kama CEO - Anglican ilianza baada ya mfalme kukataliwa kuoa mke wa pili na kanisa Katoliki, vivyo hivyo ndio unaona sasa ndoa za jinsi mmoja zinaruhusiwa kanisani je hapo unasemaje? mtume Abraham alioa wake wawili je unasema?
Comment by vita wilbards on October 6, 2010 at 6:28pm
MZEE WAKE WAWILI WANAKUSHINDA NA NGUZO ZA MTUME ZINASEMA WAKE WANNE ITAKUWAJE SHEIKH
JIFUNZE KWA MSWATI NA JACOB ZUMA
Comment by khamis H Haji on October 6, 2010 at 4:54pm
Huyu mzee mtazameni tu...sisi huku zanzibar tunamjuwa malezi yake from A-Z, hatushangazwi na vituko vyake na mama yake seuze wake zake
Comment by nasser on October 6, 2010 at 4:13pm
unajua siyo sababu wake hao wa wawili ni mume kashindwa kuwamudu.Unaona yupo mzee mmoja sehemu za Kenya alikuwa ameoa wake 135 lakini aliwamudu.
Comment by SANDIA John on October 6, 2010 at 3:16pm
pole mama
Comment by Kaiser Kailembo on October 6, 2010 at 3:02pm
NI MAKOSA YA MAMA MTU KUTOKANA NA MALEZI MABOVU ALIYOMPA MWANAE, NDIYO MAANA MTOTO ANASHINDWA KUWA MUDU WAKEZE TAMAA YA NGONO HIYOO!!!

NI SUPERMARKET GANI BORA KULIKO ZOTE KATI YA HIZI? NA KWA NINI? TOA MAONI YAKO!
  

Forum

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by TZ on Tuesday. 1 Reply

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson 18 hours ago. 12 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by maleka sakeha 19 hours ago. 30 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

JUAN MATA KUTUA MANCHESTER UNITED ATASIADIA KULETA MATOKEO BORA BAADA YA TIMU KUSUASUA?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson Nov 21. 88 Replies

Juan Mata anataraji kutua Manchester United akitokea klabu ya Chelsea ya…

KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KILA MARA, TATIZO NI NINI?

Started by GLOBAL in Habari. Last reply by mark gibson Nov 28. 46 Replies

VITENDO VYA KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KWA SASA VIMEZOELEKA. KATIKA NCHI MBALIMBALI WATANZANIA WAMEKUWA WAKIKAMATWA KWA UBEBAJI WA MADAWA HAYO. JE, TATIZO NI NINI? NA NINI KIFANYIKE?

Tags: MARA, TATIZO, NI, NINI?, KILA

JESHI LA POLISI KUTOA MILIONI 100 KWA ATAKAYEWEZESHA KUPATIKANA WAHALIFU WANAOMWAGIA WATU TINDIKALI NI KWAMBA LIMESHINDWA KAZI?

Started by GLOBAL in Maisha. Last reply by mark gibson Nov 30. 84 Replies

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.Jeshi la Polisi…

SIMBA SC WAMTUPIA VIRAGO JUMA KASEJA

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson Nov 22. 12 Replies

TIMU ya Simba SC leo imetangaza rasmi kuachana na mlinda mlango wake mahiri, Juma…

JE, NI SAHII KWA JESHI LA POLISI KULIPUA MABOMU WAKATI WANANCHI WAKIAGA MIILI YA WENZAO?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson Nov 23. 36 Replies

Juzi (Jumanne) polisi walilipua mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa wamekusanyika katika Viwanja vya Soweto jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili ya wenzao watatu waliopoteza maisha katika…

TOP NEWS WEEK HII

© 2014   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }