Kheri ya Krismasi mpenzi msomaji, natumaini umekula, umekunywa na umefurahia maisha, sasa ni wakati wa kuutibu mwili wako kama baada ya kula na kunywa kwenye sikukuu hii vimekuletea ‘mgogoro’ tumboni.
Bila shaka kila mtu anafahamu umuhimu wa maji, lakini si watu wote wanafahamu kuwa maji ni dawa pia, licha ya kutumika kwa ajili ya kunywa ili kukata kiu.

Nchini Japan na nchi nyingine nyingi za Bara la Asia, ni jambo la kawaida kwa watu wake kunywa maji kwanza asubuhi kabla ya kula kitu chochote.

Tabia hii ina faida kubwa kwa afya ya binadamu na hata utafiti wa kisayansi uliofanywa, umethibitisha thamani ya maji katika kuponya, kuzuia au kudhibiti magonjwa kadhaa yanayosumbua watu wengi.

Chama Cha Madaktari wa Japan (Japanese Medical Society) kimethibitisha kuwa maji yana uwezo wa kutibu, kwa asilimia 100, magonjwa sugu na maarufu yafuatayo, iwapo mtu atafuata kanuni na taratibu za kunywa maji hayo kama tiba:

Kuumwa kichwa, maumivu ya mwili, mfumo wa moyo, moyo kwenda mbio, kifafa, uzito mkubwa, pumu, kifua kikuu, uti wa mgongo, ugonjwa wa figo, magonjwa ya mkojo, kutapika, vidonda vya tumbo, kuharisha, kisukari, saratani, ukosefu wa choo, matatizo ya macho, tumbo, hedhi, sikio, pua, nk.

JINSI YA KUTUMIA MAJI KAMA TIBA
Ili maji yatumike kama tiba, kunywa kiasi cha lita moja na robo (glasi nne kubwa) za maji safi na salama (yasiwe maji baridi) asubuhi na mapema kabla ya jua kuchomoza na kabla ya kupiga mswaki.

Baada ya kunywa kiasi hicho cha maji, usile wala kunywa kitu kingine hadi baada ya dakika 45 au saa moja. Baada ya muda huo, sasa unaweza kusafisha kinywa na kula mlo wako wa asubuhi kama kawaida.

Aidha, mara baada ya kula mlo wako wa asubuhi, usile wala kunywa kitu chochote hadi baada ya muda wa saa mbili kupita. Hivyo hivyo utafanya baada ya mlo wako wa mchana au jioni.

Kwa wale wagonjwa ambao hawawezi kunywa kiasi cha maji cha lita 1 na robo kwa wakati mmoja, wanaweza kuanza kwa kunywa na kiasi kidogo watakachoweza na kuongeza taratibu hadi kufikia kiwango hicho cha glasi nne kwa siku.

Utaratibu huu wa kunywa maji ulioelezwa hapo juu, una uwezo wa kutibu maradhi yaliyotajwa hapo awali na kwa wale ambao hawana maradhi yoyote, basi wataimarisha afya zao zaidi na kujipa kinga itakayowafanya waishi maisha yenye afya bora zaidi.

UNAWEZA KUPONA BAADA YA MUDA GANI?
Yafuatayo ni baadhi ya magonjwa na idadi ya siku zake za kupona zikiwa kwenye mabano kama ilivyothibitishwa na watafiti:

Shinikizo la damu (High Blood Pressure) (siku 30), vidonda vya tumbo (siku 10), kisukari (siku 30), saratani (siku 180) na kifua kikuu (siku 90).

Kwa mujibu wa watafiti, tiba hii haina madhara yoyote, hata hivyo katika siku za mwanzo utalazimika kukojoa mara kwa mara. Ni bora kila mtu akajiwekea mazoea ya kunywa maji kwa utaratibu huu kila siku katika maisha yake yote ili kujikinga na maradhi mbalimbali.
KUNYWA MAJI ILI UWE NA AFYA NJEMA NA UBAKI MCHANGAMFU SIKU ZOTE!

Views: 5611

Tags: uwazi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by Gaston Kayombo on December 31, 2011 at 7:25pm

Ahsante kwa mada nzuri ambayo imelenga kuokoa maisha yetu lakini upatikanaji wa maji safi ni tatizo kwa mji wetu wa Musoma -Mara, maji ambayo yanayotoka katika mabomba ni ya asili toka ziwa Victoria yaani hayachujwi wala dawa hayawekwi inafikia hatua magonjwa ya typhoid,Amiba na kichocho ni ka huku kawaida huku kwetu da! heri yaop wanaopata maji safi katika miji yao

Comment by Gaston Kayombo on December 31, 2011 at 7:25pm

Ahsante kwa mada nzuri ambayo imelenga kuokoa maisha yetu lakini upatikanaji wa maji safi ni tatizo kwa mji wetu wa Musoma -Mara, maji ambayo yanayotoka katika mabomba ni ya asili toka ziwa Victoria yaani hayachujwi wala dawa hayawekwi inafikia hatua magonjwa ya typhoid,Amiba na kichocho ni ka huku kawaida huku kwetu da! heri yaop wanaopata maji safi katika miji yao

Comment by pjoan audes on December 30, 2011 at 6:07pm

Kunywa maji hakuna formula yoyote cha muhimu ni kunywa maji mengi kulingana na body volium yako mtu. Ni kwelli watu wengi hawana tabia ya kkunywa maji utakuta mtu anakojoa mkojo wa njano iliyokolea kwelikweli na mwingine unatoka kama sylup! hii ina maanisha huna maji kabisa au una kiwango kidogo sana cha maji mwilini ( to be precise sitataja kwa percenatge mpaka ni refer) lakini mwili wa binadamu una kiwango kkikubwa cha maji kuliko vitu vingine na maji yanatusaidia kkusafisha mwili kusafirisha oygen vizuri mwilini na kuweka fluid balance mwilini. Kwa sababu hizi chache kati ya nyingi ni vyema mtu akanywa maji kwa kiasi cha kutosha kwa siku. hesabu kwa lita sio vikombe au glasi

Comment by Bob side on December 30, 2011 at 4:37pm
asnate sana ,,,,,,,,,,,,,kwa elimu yenu pia mungu ameshaa wahi kutuambia kila kitu maji yanafanya uahi
Comment by issa m moshi on December 27, 2011 at 8:41pm

mgekuwa siku zote mnaandika habari nzuri kama hizi nadhani pangekuwa hapatoshi

Comment by Mawazo Katota on December 27, 2011 at 4:33pm

Elimu haina mwisho wadau Kunyweni maji kwa afya zenu

Comment by Isalia on December 27, 2011 at 4:18pm
Ahsanteni kwa elimu yenu nzuri sana
Comment by julius manning on December 27, 2011 at 3:56pm

nimekubali ,mi mwenyewe yamenisaidia mara kibaao

Comment by aljahdhami ahmed humaid on December 27, 2011 at 12:52pm

gpl hizi ndio habari za kuandika katika magazeti sio wema kaenda bafuni anti kala ugali bila mboga hiyo havitusaidii kitu sana sana vinawafundisha mabinti zetu maadili mabovu wanaona kumbe kuandikwa ndio unakuwa maarufu ina huuuuuuuuuu!

Comment by ROSE on December 27, 2011 at 10:41am

Asante sana sana kwa somo nzuri.

NI SUPERMARKET GANI BORA KULIKO ZOTE KATI YA HIZI? NA KWA NINI? TOA MAONI YAKO!
  

Forum

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by TZ Dec 16. 1 Reply

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson 8 hours ago. 13 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by maleka sakeha yesterday. 30 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

JUAN MATA KUTUA MANCHESTER UNITED ATASIADIA KULETA MATOKEO BORA BAADA YA TIMU KUSUASUA?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson Nov 21. 88 Replies

Juan Mata anataraji kutua Manchester United akitokea klabu ya Chelsea ya…

KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KILA MARA, TATIZO NI NINI?

Started by GLOBAL in Habari. Last reply by mark gibson Nov 28. 46 Replies

VITENDO VYA KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KWA SASA VIMEZOELEKA. KATIKA NCHI MBALIMBALI WATANZANIA WAMEKUWA WAKIKAMATWA KWA UBEBAJI WA MADAWA HAYO. JE, TATIZO NI NINI? NA NINI KIFANYIKE?

Tags: MARA, TATIZO, NI, NINI?, KILA

JESHI LA POLISI KUTOA MILIONI 100 KWA ATAKAYEWEZESHA KUPATIKANA WAHALIFU WANAOMWAGIA WATU TINDIKALI NI KWAMBA LIMESHINDWA KAZI?

Started by GLOBAL in Maisha. Last reply by mark gibson Nov 30. 84 Replies

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.Jeshi la Polisi…

SIMBA SC WAMTUPIA VIRAGO JUMA KASEJA

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson 7 hours ago. 13 Replies

TIMU ya Simba SC leo imetangaza rasmi kuachana na mlinda mlango wake mahiri, Juma…

JE, NI SAHII KWA JESHI LA POLISI KULIPUA MABOMU WAKATI WANANCHI WAKIAGA MIILI YA WENZAO?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson 9 hours ago. 38 Replies

Juzi (Jumanne) polisi walilipua mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa wamekusanyika katika Viwanja vya Soweto jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili ya wenzao watatu waliopoteza maisha katika…

TOP NEWS WEEK HII

© 2014   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }