Na Gladness Mallya
WIKI chache baada ya kujifungua, mtangazaji maarufu wa zamani wa Kituo cha Runinga cha EATV na TBC 1, Maimartha Jesse a.k.a Mai (pichani) amedai kuwa, mtoto huyo ni zaidi ya mumewe kwani furaha aliyonayo hajawahi kuipata maishani mwake.
Akichonga na Motomoto Newz juzikati jijini Dar, Mai alisema wakati akiwa mjamzito alikuwa anamuomba Mungu ajifungue salama na kweli amesikia dua yake na kitendo cha kumpata mtoto huyo anaona raha kuliko starehe zote alizowahi kupitia.
“Asikwambie mtu bana, kuna wakati najikuta nataka kumsahau mume wangu kutokana na huyu mwanangu, kila nikimuangalia anaipagawisha akili yangu, kwangu huyu naona kama ni zaidi ya Shaa (mumewe),” alisema Mai.
Mai alimaliza kwa kusema; “Muda mwingi nilitamani kupata mtoto na hii ilitokana na misukosuko niliyopitia na kitendo cha Mungu kutimiza ndoto yangu kwangu ni raha isiyokifani.”
Comment
Comment by Misana on March 20, 2012 at 2:45pm Hongera dada,Mungu akupe nguvu na busara ili umlee vema mwanao.
Comment by Dongonyo Juniour on March 3, 2012 at 12:30pm Haya wee!!!
Comment by kaka on February 26, 2012 at 8:35am MAI JE MTOTO NI WA SHAA?
||||\Hongera kwa kupata mtoto lakini usimsahau baba yake na mtoto. Very important
Comment by samora rajab albert on February 24, 2012 at 6:47pm hongera kwa kupata mtt
naomba utambue kuwa mume ni zaidi ya mtoto maana ndiye aliyesababisha mtoto awepo
Comment by Rogers Mwachali on February 24, 2012 at 8:18am mi nafikiri mtoto si zaidi ya mume kwani aliefanya huyo mtoto awepo ni mume na anaweza kufanya tena na tena. Unajua watu wameshindwa kutambua ndoa na kuwa na watoto.Kama mtu aliingia katioka ndoa ili wazae watoto wakishapata tu watoto hakuna ndoa tena kwa ni lengo lipo at climax success so what next ni kuvunjika kwa ndoa,Mai mpende mtoto kwa nafasi yake na mume kwa nafasi yake
Comment by Theddy Jacob on February 23, 2012 at 3:47pm Kawaida wamama wengi wakishapata watoto mapenzi hupungua kwa mume na huo ndio mwanzo wa mume kuanza kutoka nje ya ndoa jitahidi kugawa mapenzi pande zote yani kwa baba na mwanao. Ongera sana dada.
Comment by lumi mwandelile on February 23, 2012 at 3:27pm kuitwa mama raha iliyoje jamani, hongera dada
| 1 |
GLOBAL |
| 2 |
julius manning |
| 3 |
Man KKK |
| 4 |
Sili Silali |
| 5 |
IL-YA |
| 6 |
chama baby |
| 7 |
msichoke mlugu |
| 8 |
kaka |
| 9 |
Maji Marefu |
| 10 |
Kelvin Luhala Eto'o |
othman Ochu posted a status
mrembo commented on Sili Silali's photo

You need to be a member of Global Publishers to add comments!
Join Global Publishers