MADHARA YA KURUKWA UKUTA KWA WANAWAKE

KAMA ilivyoa ada, wanadamu tunatakiwa kumtanguliza mbele Muumba kwa kila jambo kwani ndiye aliye tegemeo letu sote.
Nimekuwa nikiandika mada nyingi ambazo zimewasaidia watu wengi kurudisha tumaini lililopotea na wengine kujijua wao ni kina nani na wapo hapo walipo kwa ajili gani.

Kuna mada ambazo zimekuwa zikiwashtua wengi kiasi cha wengine kuchanganyikiwa kutokana na kufanya mambo kimazoea, kitu ambacho kimewafanya wafanye makosa bila kujua au wengine kufanya kitu wakijua madhara yake juujuu na kuendelea kufanya bila kujua madhara yake kiundani.
Baada wa wiki jana kuandika mada kuhusu mtu kumpenda mkewe kwa kipi hasa, nimekuwa nikipata simu nyingi na ujumbe mfupi wa simu ‘SMS’.
Wengi walishtuka sana, wengine wakaeleza waliingia kwenye mchezo ule bila kujua madhara yake. Wengi waliomba ushauri wafanye nini kutokana na kuzoea mchezo ule wenye madhara makubwa kiafya.
Si hao tu, wapo waliotaka kujua madhara yake kiundani kwa mtu kuingiliwa kinyume na maumbile au mtu kumwingilia mwenzake kinyume na maumbile.
Leo nataka kumzungumzia kwanza mwanamke ambaye ndiye amekuwa kwenye wakati mgumu kuliko mwanaume.
Tumeona wanaume ndiyo chanzo cha mchezo huu mchafu ambao umetambaa kama moto kwenye majani makavu na kuwaambukiza wanawake, ambao nao wameugua ugonjwa huo wa kuwashwa sehemu za haja kubwa na kuwatafuta wanaume kufanya nao mapenzi ili kuondoa muwasho huo unaotokana na mtu kuufanya mchezo ule kwa muda mrefu.
Kwako inaweza kuwa ni starehe usiyojua hasara yake, lakini madhara yake ni makubwa kuliko hiyo starehe ya dakika chache unayopata na matibabu yake ni ya gharama yanayoweza kukusababisha uishi kwenye mateso makubwa au kusababisha kifo.
Wengi hawapendi kufanya mchezo huo lakini wamejikuta wameingia kwa ajili ya shinikizo, nao hukubali ili kuokoa penzi bila kujua madhara yake.
Madhara ya mwanamke kuingiliwa kinyume na maumbile:
Mwanamke anayefanyiwa mchezo huu hupata matatizo makubwa wakati wa kujifungua ikiwa ni pamoja na kutokwa na haja kubwa mfululizo wakati akijaribu kumsukuma mtoto.
Tukio hili humsababishia aibu kubwa mwanamke, kiasi cha kumshushia hadhi yake mbele ya jamii.
Pili, pia anaweza kumuua mtoto kwa vile kila akimsukuma atoke, pumzi hukata kutokana na misuli inayofahamika kwa jina la ‘sphincter’ kulegea na kusababisha ambane mtoto.
Tatu, umri unaposonga, haja kubwa hutoka bila kizuizi kutokana na misuli ya sphincter inayobana njia ya haja kubwa kulegea.
Nne, inaweza kusababisha saratani ya eneo hilo ‘cancer of colon’.
Tano, ugonjwa wa UTI, yaani uambukizi kwa njia ya mkojo, huwa sugu, maana akitokea mwanaume alifanya kitendo hicho kisha akafanya ngono kama kawaida, bakteria wanaoishi sehemu hiyo wanaingia na kuwa na madhara makubwa.
Sita, hasara yake kubwa mwanaume anayekufanyia mchezo huwa hawezi kukuoa, pia ni rahisi kukutangaza kwa jamaa zake na kuonekana kituko mbele za watu, kama umeolewa heshima yako hupungua ndani ya ndoa.
Mwisho kabisa baada ya kuharibiwa ni kuwa na msongo wa mawazo na kuilaumu nafsi yako.
Nina imani umeona baadhi ya madhara hatari kwa mwanamke kuingiliwa kinyume cha maumbile. Mchezo huo ni mbaya, najua aliyeuanza muda mrefu utamsumbua kuuacha kutokana na hali anayokutana nayo. Lakini ukiivumilia kwa muda lazima itakata na kurudi kwenye hali yako ya zamani.

Tukutane wiki ijayo kwa mada ya madhara kwa wanaume.

Views: 3920

Tags: mahaba11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by sunday urassa on March 18, 2013 at 10:27am

Safi sana waambie wao

Comment by zide on March 15, 2013 at 9:31pm

good

Comment by julius manning on March 15, 2013 at 2:56pm

NIMEKUBALI

Comment by Shema Idrisa on March 15, 2013 at 12:49pm

MWENYEZIMU AMEHARAMISHA KWA DINI ZOTE IMEKATAZWA KWA NGUVU.

MFANYAJI NA MFANYWAJI WAMELAANIWA NA MWENYEZIMUNGU.

Comment by tatu said on March 15, 2013 at 12:20pm

Yan katika mada zote mada ya leo ni kiboko nimeipenda sana,wenye tabia hzo muache.

Comment by mayalilwa on March 15, 2013 at 11:21am

Ni ukweli mtupu

Comment by Sudi Mkwara on March 15, 2013 at 11:12am
wengi tumeshafahamu madhara ya kuingia kuingiliwa kimaumbile, ahsante kwa kutuelimisha
Comment by Tatu Kiondo on March 15, 2013 at 11:11am

wameelimika katika ili safi sana

Comment by Asia abdillahi on March 15, 2013 at 10:06am

somo zuri sana!

NI SUPERMARKET GANI BORA KULIKO ZOTE KATI YA HIZI? NA KWA NINI? TOA MAONI YAKO!
  

Forum

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by TZ Dec 16. 1 Reply

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson on Sunday. 13 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by maleka sakeha on Saturday. 30 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

JUAN MATA KUTUA MANCHESTER UNITED ATASIADIA KULETA MATOKEO BORA BAADA YA TIMU KUSUASUA?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson Nov 21. 88 Replies

Juan Mata anataraji kutua Manchester United akitokea klabu ya Chelsea ya…

KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KILA MARA, TATIZO NI NINI?

Started by GLOBAL in Habari. Last reply by mark gibson Nov 28. 46 Replies

VITENDO VYA KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KWA SASA VIMEZOELEKA. KATIKA NCHI MBALIMBALI WATANZANIA WAMEKUWA WAKIKAMATWA KWA UBEBAJI WA MADAWA HAYO. JE, TATIZO NI NINI? NA NINI KIFANYIKE?

Tags: MARA, TATIZO, NI, NINI?, KILA

JESHI LA POLISI KUTOA MILIONI 100 KWA ATAKAYEWEZESHA KUPATIKANA WAHALIFU WANAOMWAGIA WATU TINDIKALI NI KWAMBA LIMESHINDWA KAZI?

Started by GLOBAL in Maisha. Last reply by mark gibson Nov 30. 84 Replies

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.Jeshi la Polisi…

SIMBA SC WAMTUPIA VIRAGO JUMA KASEJA

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson on Sunday. 13 Replies

TIMU ya Simba SC leo imetangaza rasmi kuachana na mlinda mlango wake mahiri, Juma…

JE, NI SAHII KWA JESHI LA POLISI KULIPUA MABOMU WAKATI WANANCHI WAKIAGA MIILI YA WENZAO?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson on Sunday. 38 Replies

Juzi (Jumanne) polisi walilipua mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa wamekusanyika katika Viwanja vya Soweto jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili ya wenzao watatu waliopoteza maisha katika…

TOP NEWS WEEK HII

Loading… Loading feed

Latest Activity

marychristan posted a status
4 minutes ago
marychristan posted a status
5 minutes ago
hapee posted a status
5 minutes ago
marychristan posted a status
5 minutes ago
robinrubby posted a status
6 minutes ago
panditpronthey posted a status
10 minutes ago
Shailene Woodley posted a status
10 minutes ago
robinrubby posted a status
11 minutes ago
vGrooves posted a status
13 minutes ago
panditpronthey posted a status
14 minutes ago
hope liked GLOBAL's blog post MAMA KANUMBA: KRISMASI KWANGU NI MBAYA
21 minutes ago
marychristan posted a status
24 minutes ago

© 2014   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }