MADAWA YA KULEVYA... BINTI KIZIWI JELA MIAKA 5

Na Mwandishi Wetu
MTANDAO wa wauza madawa ya kulevya unazidi kupukutika Bongo kufuatia madai ya kukamatwa kwa watu wanaodaiwa kujishughulisha na ubebaji ‘punda’ wa biashara hiyo haramu, Ijumaa Wikienda lina mtiririko wote.

Mrembo aliyehukumiwa miaka mitano Sandra Khan 'Binti Kiziwi'.

Hivi karibuni, Video Queen wa Wimbo wa Masogange, Agnes Gerald ‘Masogange’ amedaiwa kunaswa nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ akiwa na kilo mia moja na hamsini za unga unaoaminika ni sehemu ya madawa ya kulevya. Ameshapanda kortini mara moja Ijumaa iliyopita.
Wakati Masogange akisota Sauzi kwa madai hayo mazito, habari ya mjini kwa sasa ni ya mtalaka wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ally Mohammed ’Z-Anto’, Sandra Khan au Binti Kiziwi kudaiwa kutupwa jela miaka mitano kwa sakata la ‘unga’.

HABARI YA MJINI KWA SASA NI BINTI KIZIWI
Kuanzia Alhamisi iliyopita, habari zilizoligubika Jiji la Dar ni kuwa Binti Kiziwi amenyongwa nchini China baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na madawa ya kulevya.
Kwa mujibu wa mitandao, Binti Kiziwi alinyongwa wiki mbili zilizopita.
Hata hivyo, mitandao hiyo haikusema kama mrembo huyo alinyongwa hadi kufa au la! Sheria za hukumu hiyo, mwenye hatia anatakiwa kunyongwa hadi kufa.

Agnes Gerald ‘Masogange’.

UKWELI WA BINTI KIZIWI NI HUU
Baada ya kusambaa kwa manenomaneno hayo, Ijumaa Wikienda liliingia mtaani kuisaka familia ya Binti Kiziwi lakini bila mafanikio.
Kwenye makazi ya mama yake, Buguruni, Dar, majirani walisema mzazi huyo amehama baada ya kufunga ndoa siku chache kabla ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

IJUMAA WIKIENDA LAZIDI KUCHIMBA
Ijumaa Wikienda lilizidi kuzama ndani katika kuchimbua tetesi hizo ambapo lilifanikiwa kumpata ndugu wa kiume wa Binti Kiziwi na kufanya naye mazungumzo kama ifuatavyo:
Wikienda: Samahani, nimeambiwa wewe ni ndugu wa Binti Kiziwi, ni kweli?
Ndugu: (huku akitaja uhusiano wao) Ni kweli, nikusaidie nini?
Wikienda: Kuna manenomaneno kwamba Binti Kiziwi amenyongwa nchini China baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na madawa ya kulevya, ni kweli?
Ndugu: Sijui hizo habari watu wanazipatia wapi?! Watanzania wana maneno sana. Si kweli ndugu mwandishi.
Wikienda: Ukweli ni upi?
Ndugu: Kwanza kabisa Binti Kiziwi hakukamatiwa China, alikamatiwa Hong Kong, kwa sheria za kule mtu akipatikana na hatia ya kukutwa na ‘unga’ anahukumiwa jela tu.
“Binti Kiziwi amehukumiwa miaka mitano jela Hong Kong, na si China. Watu wajue hilo na miaka mitano si mingi, atatoka.”
Wikienda: Nashukuru sana kwa ushirikiano ndugu yangu.
Ndugu: Asante, waambie Watanzania waache kuongeaongea sana.

Saada Ally Kilongo (26), maarufu kama ‘Demu wa Kanumba’.

DEMU WA KANUMBA NAYE ASOTA RUMANDE
Msichana anayejulikana kwa jina la Saada Ally Kilongo (26), maarufu kama ‘Demu wa Kanumba’ yeye bado anasota kwenye Gereza la Segerea, Dar kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya yanayokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 170.
Saada alidakwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar Juni 24, mwaka huu.
Kesi yake ilisikilizwa kwa mara ya kwanza, Juni 29, mwaka huu kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, Dar es Salaam.
Mdada huyo mkazi wa Mbezi Beach, Dar aliwahi kutoka kwenye Gazeti la Ijumaa la Desemba 9, 2011 ukurasa wa mbele kwa kichwa cha habari kisemacho: SAA 7 USIKU KANUMBA AGANDANA NA DEMU.
Demu huyo ambaye wakati huo alikuwa mwanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama, Dar (alimaliza mwaka jana), picha yake akiwa na marehemu Kanumba ilipigwa Desemba 2, 2011 ndani ya Ukumbi wa Mlimani City, Dar ambapo kulirindima Tamasha la Usiku wa Kiafrika lililopambwa na mkali wa dansi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ipupa Nsimba ‘Fally Ipupa’.

Sharifa Mahamoud (27).

MSANII BONGO MUVI ‘ASUBIRI KITANZI’ MISRI
Wakati mlolongo wote ukiwa hivyo, mrembo aliyewahi kushiriki filamu Bongo, Sharifa Mahamoud (27) naye anashikiliwa katika gereza moja nchini Misri wakati kesi yake ya kukamatwa na madawa ya kulevya ikirindima nchini humo.

BALOZI WA TANZANIA -MISRI AZUNGUMZA
Kwa mujibu wa Balozi wa Tanzania nchini Misri, Mohammed Haji, Mei 18, mwaka huu, Sharifa na nduguye, Abdallah Salum (28), wote wakazi wa Magomeni, Dar, walinaswa na unga jijini Cairo wakitokea Dar.
Mei 26, walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza. Madawa waliokutwa nayo ni heroine kilo saba (gharama ya fedha haikutajwa).  
Kwa sheria za Misri, kosa la kukutwa na madawa ya kulevya ni kunyongwa hadi kufa. Lakini kwa mujibu wa Balozi Salum, hana kumbukumbu za raia wa kigeni aliyewahi kuhukumiwa kunyongwa nchini humo kwa kosa hilo.
Balozi alisema: “Endapo watapatikana na hatia kwamba kweli dawa hizo zilikuwa zao, hili litakuwa doa la kwanza kwa nchi yetu (Tanzania) hapa Misri.
Kwa mujibu wa Sharifa wakati akihojiwa na TV ya Misri, alishangaa kuona begi lake likiwa na madawa ya kulevya baada ya kukamatwa na kwamba aliingia nchini humo kumtafuta binamu yake.

SOMA HABARI ZOTE ZA GAZETI LA IJUMAA WIKIENDA HAPA: IJUMAA WIKIENDA

Views: 9765

Tags: ijumaawikienda11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by hope on July 16, 2013 at 2:12pm

Watafute biashara nyingine hii imeshachina

Comment by steven emmanuel on July 15, 2013 at 9:35pm

bonge la dili ukifanikiwa lakin risk sana sana!!

Comment by LJH_3 on July 15, 2013 at 4:58pm
Disminder SY unachosems nakubaliana nacho kabisaaaa...yaani zamani km hujaolewa hata uwe na miaka 40 hutoki kwenu lkn siku hizi mapemaaa unasepa...na hao wasichana ni wengi sana wamekamatwa huko nje ila hapa mnaona hao wachache sbb ni watu waliokuwa wanajulikana na jamii ukiingia huko mitaani uliza utaambiwa..mie nafahamu baadhi ya waliokamatwa hong Kong yaani inauma sana ukiona wasichana wadogo sasa hivi ndio wanatumika kubeba mizigo ya madawa sbb wanajua wasichana ni nadra sana kupekuliwa lkn sasa kimenuka nao pia wanachekiwa km kawa...
Comment by hope on July 15, 2013 at 2:00pm

Ni sawa hawa punda wamekamatwa sijui watanyongwa au la lakini na waliowabebesha mizigo hawa punda nao wajulikane pia

Comment by Catherine Masaki on July 15, 2013 at 11:58am

hii inaonyesha kuwa ni kiasi gani mabinti wa bongo tunapenda shortcut..laiti kama tungekuwa tunajituma hata kwa kuuza maandazi nina imani wasingeshawishika na hili jambo,tuzishinde tamaa zetu tuseme na shida zetu tusiishi kwa kucopy maisha ya watu wengni...

Comment by lumi mwandelile on July 15, 2013 at 10:25am

HUYO BINTI KIZIWI ANGENYONGWA TU, KWANI NI SAWA NA MUUAJI

Comment by disminder on July 15, 2013 at 10:21am

NINI KIINI CHA HAYA YOTE?

UKAPA MJINI!!

WATU WANA ELIMU LAKINI HAKUNA KAZI MPAKA UWE NA MTU SERIKALINI, MAOFISINI.

TAMAAA KWA WATOTO WA MJINI KUTAKA KUISHI MAISHA MAKUBWA.

WAZAZI KUSHINDWA KULEA WATOTO KATIKA MAADILI.

Nakumbuka zamani sisi, huwezi toka kwenu hata uwe umemaliza vyuo vikuu vyote duniani kabla ya kuolewa.

siku hizi tunajitegemea tu mjini, muhimu umeshafikia umri fulani. (Sayansi na teke hiloooooooo linalotujia tekenolojia)

Kuna watoto ukikutana nao wako field mahotelini au maofisi mengine hata huamini kama huyo karuhusiwa nawazazi wake hasaaa kwenda kukaa mji mwingine peke yake!!

sasa na ile Freee Mandela tukishaipata wengine tunadanganya, tumepata na ajira ili usirudi home, kumbe unaSWAMPA TU KUHANGAIKA NA MJI KUTWA KUCHA!!!

JAMIII PIA IRUDIE MAADILI.

Comment by Faridi Mohamed on July 15, 2013 at 9:22am

Huyo unaemsema kuwa Fatma Saleh au Sharifa Mahamoud yeye amesema katika TV interview hajui kosa alokamatiwa dada yake, lakini ni wazi hatosema katika  kwamba dada yake amekamatwa kwa kosa la madawa ya kulevya ila mtangazaji na security walisema katika hiyo interview kuwa dada yake amekamatwa na madawa ya kulevya.

Tanzania inahusika kutokana huyu amesema ametokea Tanzania na watanzania wengi wamekamatwa misri na madawa ya kulevya Misri kwahiyo lazima aelezwe kuhusu udaifu uliopo katika Uwanja wetu wa ndege walikotokea hawa watu.  

Hawa siyo mapunda tu wanahusika kama vile Vigogo na wauzaji  wanahitaji adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine

Comment by amanda adam on July 15, 2013 at 9:21am

Siku zote wahalifu hujichongea makaburi yao wenyewe.

Comment by Jodat King on July 15, 2013 at 9:00am

Punda akikamatwa na mwenye Punda je?!

 

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by hiepelines Jul 4. 6 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Aug 15. 7 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Aug 15. 6 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by Joe reggan Apr 24. 2 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }