Lulu afunua kinywa kuhusu skendo ya picha za utupu, penzi na Alikiba

Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Wiki iliyopita tulimuweka staa wa sanaa za maigizo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, hii ilitokana na ombi maalum la wasomaji wetu. Tulitii ombi kumuweka kitini. SMS zote zilipokelewa na kufikishwa kwa mwenyewe ambaye alijibu zote.
Hivi ndivyo ambavyo ilikuwa, mechi kati ya Lulu na wasomaji.

Mtoto anafuatiliwa sana!
Upo juu Lulu ila punguza skendo za kipuuzi best, ila naomba kuwasiliana na wewe zaidi.

Albert, Dar, 0714035288
LULU ANAJIBU: Asante, siyo kwamba napenda skendo ila mimi ni star ndiyo maana nafuatiliwa sana.

Ni Alikiba na yeye!
Lulu unakaa pande gani na kuhusu Alikiba na una mchumba inakuaje?
Msomaji, 0657196400
LULU ANAJIBU: Naishi Tabata kuhusu Alikiba ni rafiki yangu wa kawaida na sina mchumba.

Eti skendo zinamzidi umri!
Lulu wewe ni mtoto mdogo sana kuandikwa magazetini tena kwa skendo za kugombea wanaume, huoni kama hiyo ni mbaya mdogo wangu? Halafu kingine hata kama wewe ni msanii usipende kuvaa nguo za aibu kwani kama wewe ni mzuri watu watakukubali tu, na kazi zako kama mimi nakupenda sana na napenda kazi zako tulia mdogo wangu. Big up kwa kazi zako natumai sitakuona tena magazetini.

Doreen, Dar, 0655767679
LULU ANAJIBU: Skendo zote siyo za ukweli, kuhusu mavazi huwa navaa sehemu husika na sehemu ambazo siyo husika siwezi kuvaa nguo fupi.

Ashauriwa kwenda shule!
Lulu nenda shule hayo mambo yatakupotezea malengo, wewe umri wako wa kujirusha bado.
Selemani Alifa, Dar, 0755363204
LULU ANAJIBU: Sawa.

Atakiwa kujiweka mbali na starehe!
Mdogo wangu napenda sana uigizaji wako lakini nakuomba usilewe na sifa wewe bado ni mwanafunzi, maliza shule starehe zipo kila siku, iga mfano wa kaka Cheni aliyegundua kipaji chako.
Wema Mwaipopo, 0654857882.
LULU ANAJIBU: Asante kwa ushauri wako nitaufanyia kazi.

Elimu na masomo muhimu!
Lulu nakuomba uwe serious na masomo elimu ni njia ya maisha japokuwa unaingiza fedha kwa filamu ila kaza buti pia na masomo, napenda kipaji chako.
Kakimi, Dar, 0715028832
LULU ANAJIBU: Asante kwa ushauri wako.

Ile pete ya uchumba yahojiwa!
Nilisikia Lulu umevalishwa pete ya uchumba kwa hiyo nilitaka kujua kama pete hiyo ulivalishwa na Ali Kiba maana nijuavyo mimi sasa hivi unatoka naye.
Sister K, Dar, 0656331515
LULU ANAJIBU: Sina pete ya uchumba, ila navaa kama urembo tu.

Aendelea kubanwa na skendo!
Lulu kama kipaji kweli unacho shukuru Mungu ila punguza skendo wewe bado mdogo sana unatia aibu wazazi na jamii, ustaa utaupata siyo mpaka uwe na skendo mbaya.
Msomaji, 0658081940
LULU ANAJIBU: Sawa.

Hee, Amani wa Kimara tena!
Napenda sana Lulu unavyoigiza ila nasikitika kwa kumuacha mpenzi wako Amani wa Kimara na kwenda kwa Ali Kiba.
Brayarn, Dar, 0657200020
LULU ANAJIBU: Sijawahi kuwa na mpenzi Kimara na wala Ali Kiba siyo mpenzi wangu ni rafiki tu.

Eliza ni mtoto wa shule jamani!
Elizabeth kwa umri uliokuwa nao ulitakiwa bado uwe shuleni, je bado unasoma au unajishughulisha na nini?
Ester Hyera, Dar, 0712144384
LULU ANAJIBU: Bado nasoma.

Eliza ni ‘miksa’ wa Kihaya, Kichaga!
Lulu umezaliwa mwaka gani, wapi na ni kabila gani na mko wangapi katika familia yenu?
Aziza, Dar, 0718498747
LULU ANAJIBU: Mwaka sipendi kuweka hadharani ila nimezaliwa Dar es Salaam, mimi ni mchanganyiko Mchaga na Mhaya.

Kanumba nA Ali kiba ni makaka!
Nasikia eti umetoka na Kanumba na Ali Kiba ni kweli? Na kama ni kweli achana na hiyo tabia mdogo wangu soma kwanza wewe bado ni mdogo sana.
Msomaji, 0715776637
LULU ANAJIBU: Hapana hao ni kaka zangu tu.

Jamani mueleweni akiwa kazini!
Eliza nimeiona shooting moja hivi nadhani umeshirikishwa huoni kuwa mavazi uliyoyatumia na umri wako unajiweka katika mazingira magumu?
Man Shilla, Dar, 0652031224
LULU ANAJIBU: Shooting ndiyo ilinitaka nifanye hivyo.

Vipi ujeuri shuleni pale Buguruni?
Nimjuavyo alisoma Shule ya Msingi Buguruni ambayo sasa hivi inaitwa Hekima alikuwa mjeuri kwa sababu ni msanii. Mama yake ni mfanyabiashara wa chakula Tabata.
Sara, Dar, 0787797074
LULU ANAJIBU: Ndiyo nilisoma darasa la 1-5 na sijawahi kuwa mjeuri.

Ile picha chafu jamani!
Mdogo wangu umeniboa kupiga picha za utupu, ninayo kwenye simu yangu badilika kuna watoto kama wewe wana vipaji wazazi wanahofia kuwaruhusu.
Thaby, Dar, 0717431337
LULU ANAJIBU: Ile picha siyo ya kwangu na kama unanijua vizuri iangalie, siwezi kufanya upuuzi kama huo.

mkakati wake wa kukuza vipaji!
Elizabeth ulianza sanaa zamani sana una mpango gani kwa hawa wasanii wadogo ambao hawajatoka? Innocent Mloka, Moshi, 0686774949
LULU ANAJIBU: Bado sijaweza kujitegemea ila baadaye nikimaliza masomo nitajitahidi kukuza vipaji vya wasanii hasa watoto kwani na mimi nimetokea huko.

Mapenzi, sanaa na shule vipi?
Unawezaje kuchanganya mapenzi, shule na sanaa kwa wakati mmoja?
Samad, Dar, 0713525288
LULU ANAJIBU: Mimi sichanganyi mapenzi ila nachanganya sanaa na shule kwa sababu nimekulia katika mfumo huo.

Jamani Lulu hajaacha shule!
Eti Lulu nasikia umeacha shule na unaendekeza starehe?
Calven, Dar, 0756443932
LULU ANAJIBU: Hapana.

Lulu ni mwanzo mzuri wa watoto!
Hongera Lulu kwa kuwa mwanzilishi wa wasanii wenye umri mdogo pia napenda nifahamu ya kuwa una mipango ya kusomea sanaa katika masomo yako?
Mama Swaumu, Dar, 0718261447
LULU ANAJIBU: Asante, baadaye ndiyo nitajua nitafanyaje nikimaliza masomo yangu.

Ni ushauri tu!
Nimependa kumshauri Lulu aangalie masomo na maisha yake ya baadaye kwanza kwani haya anayoyafanya sasa yapo tu, kwanini ukimbilie kutembea kabla hujatambaa kila kitu kina wakati wake na wazazi kuweni makini.
Msomaji, 0713524807
LULU ANAJIBU: Asante.

Penzi lake kwa Jely Rhymes na Ali kiba!
Ukiwa ni mwanafunzi unawezaje kuchanganya mapenzi na shule? Na je ni kweli una uhusiano wa mapenzi na Jely wa Rhymes na Ali Kiba?
Master G, Dar, 0766187302
LULU ANAJIBU: Wote hawa ni marafiki zangu na kuna kazi tunashirikiana.

Starehe usiku mtoto unasomaje?
Mara nyingi nimekuwa nikikuona viwanja tofauti hapa mjini usiku ukijiachia, je, unajisomea saa ngapi? Naomba kujua umri wako na kidato.
Daudi Sanga, Iringa, 0782947805.
LULU ANAJIBU: Huwa natoka siku nikijisikia na huwa ninapangilia muda wa kusoma.

Huyu kamfananisha!
Ninavyomfahamu mimi Lulu alikuwa anaishi Kirumba Mwanza baba yake alikuwa anafanya kazi UN, anaitwa Michael Lukas, napenda kukuuliza una miaka mingapi?
Frank, Mwanza, 0753911737
LULU ANAJIBU: Sijawahi kuishi Mwanza na baba yangu anaitwa Michael Edward.

Mama yake ni Mhaya
Ninavyomfahamu Lulu mama yake ni Mhaya, naomba uwe mdogo wangu chukua namba yangu tuwasiliane.
Rashidat, Dar, 0688236865
LULU ANAJIBU: Kweli mama ni Mhaya, usijali nitakutafuta.

ALIENDA CHINA NA FATAKI
Nilisikia ulienda China na mwanaume ‘fataki’.
Msomaji, 0788000921
LULU ANAJIBU: Hapana sijaenda na mwanaume, nilienda mwenyewe.

Kumbe Lulu first born!
Lulu wewe kwenu ni mtoto wa ngapi na mko wangapi? Nakupa big up unajua kuigiza.
Saada, Dar, 0714626862
LULU ANAJIBU: Mimi ni mtoto wa kwanza na tuko wawili.

Views: 14389

Tags: ijumaawikienda11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by lee lewis on April 14, 2011 at 4:17pm
siyo siri mrembo lyk u alaf.... Duh! Ucwe ivo best utavuruga @ki2 wangu.
Comment by Cleophas Ntakije on February 26, 2011 at 10:30pm
POA
Comment by dennis steven fulluge on November 16, 2010 at 4:34pm
lulu miminishabiki wako ila naomba utulie na uzingatie elimu kwani elimu ni ufunguo wa maisha yako.hiyo ni slaa ya maisha yako mdogo wangu.0715470379
Comment by allex katagira on September 27, 2010 at 4:58am
LULU ni kweli una kipaji lakini kipaji bila busara nibule!
badilika soma kwanza hayo mamboutayakuta.
lakini wewe bado mkali tuuuuuuuuuuuuuuu!!!
Comment by allex katagira on September 27, 2010 at 4:51am
LULU una kipaji lakini kipaji bila busara ni bule!
mimi kama mshabeki wako nakuomba ubadiliuke
lakini we mkali I REAL APPRECIATE.!
Comment by preety Hans on September 23, 2010 at 12:06pm
Hey ,Lulu is that really ur pict...? ur too young to act like dat, i really like u but ur behavior threatening me.
Behave ur self baby..,but all in all i appreciate ur work...do not allow bad scandals in ur life ,that is the one among of the way to success..Keep it up, we want to see ur work crossing boarder, go international so avoid these scandal my dear...4 ur own good..... preety--- am out"
Comment by david peter mkonyi on September 20, 2010 at 10:59am
upo juu lulu kaza buti,life lenyewe fupi.
Comment by moses sarai on September 17, 2010 at 11:03pm
UNALOLIONA ZURI KWAKO LIFANYE MAMA YAKO ANAKUJUA ZAIDI KULIKO SISI MSIKILIZE SANA YY NDIE ALIEKUZAA NA HAPO ULIPOFIKIA NI JUHUDI ZAKO WE MWENYEWE NA SIO WATU FANYA KWELI HUU NDIO WAKATI WAKO,NAAMINI UNAJUA UNALOLIFANYA,,,,,,,,,,,,,,,,
Comment by MASINDE JUSTINE on September 17, 2010 at 11:26am
kama kweli yote uliozungumza ni ya kweli basi mungu akusaidie milele na milele.NI JOVIN WA UKWELI
Comment by frederi on September 14, 2010 at 11:47am
thats my niece na she is Ok. Mambo mengine na picha za uigizaji tofautisheni na picha za maisha ya kawaida. every scene has an acting look. So stop wasting your efforts on minor things of her and work on your major problems. in the longrun maisha yangu ni yangu ya lulu ni ya Lulu na yako ni yako. So long us I dont interfere your daily income live your life, she live her life and I live my life
UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }