KWA NINI PADRI APIGWE RISASI, OFISA TAKUKURU AUAWE KINYAMA?

>> Polisi, Takukuru wajichanganya, risasi yakaa mwilini siku nne
WIKI iliyopita watu wawili walipigwa risasi katika matukio mawili tofauti, moja ni Bara jijini Dar es Salaam ambapo mwanamke aliuawa  na lingine ni Zanzibar ambako padri alijeruhiwa kwa risasi.

Tuanze na hili la Zanzibar ambapo Padri  Ambrose Mkenda  alipigwa risasi siku ya Krismasi na watu wasiojulikana lakini polisi wakaeleza ndivyo sivyo hata kusababisha mchungaji huyo wa roho za watu kukana maelezo ya awali waliyoyatoa kwamba yeye ni Mhasibu wa Kanisa Katoliki, Zanzibar.
Gazeti hili lilikuwa miongoni mwa wanahabari waliozungumza na padri huyo mwishoni mwa wiki iliyopita katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako amelazwa na alianza kwa kufafanua wadhifa wake kuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Uchungaji anayeshughulikia masuala yote ya Kanisa Katoliki visiwani humo.
Alikana kwamba yeye si mhasibu wa kanisa hilo kama ilivyoelezwa na polisi na kwamba taarifa hizo siyo za kweli.Hata hivyo, Padri Mkenda alisema alikuwa akimsaidia mhasibu kwa kipindi cha miezi mitatu.
“Mimi sikuwa mhasibu wa kanisa kama inavyoelezwa na watu. Napinga vikali taarifa hizo kwani mimi nilikuwa namsaidia mhasibu kwa muda tu kwani hakuwepo,” alisema.
Imeelezwa kwamba washambuliaji hawakuchukua kitu chochote baada ya shambulio hilo na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Saidi Mwema ametuma makachero watano Zanzibar ili kuongeza nguvu ya upelelezi ambao umezaa matunda kwani tayari watu watano wamekamatwa.
Lakini vipi hali yake kiafya kwa sasa? Padri Mkenda aliliambia gazeti hili kuwa anaendelea vizuri lakini bado ana maumivu makali katika sehemu za mwili wake ikiwa ni pamoja na kichwani. Hata hivyo maumivu hayo yalitokana na risasi kukaa mwilini kwa siku nne kwani zilitolewa Ijumaa.
Afisa uhusiano wa Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (Moi), Almasi Jumaa alipoulizwa na gazeti hili idadi ya risasi alizopigwa padri huyo alisema hilo ni suala la kipolisi wanaofanya uchunguzi, lakini alithibitisha Mkenda kuingizwa chumba cha upasuaji ili kutolewa risasi mwilini mwake.

UWAZI NA WAZIRI WA SMZ
Swali  ambalo watu wengi wanajiuliza ni kwa nini amepigwa risasi kiongozi huyu wa kiroho?  Gazeti hili lilifanikiwa kuzungumza ana kwa ana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mohamed Aboud aliyekwenda kumjulia hali Padri Mkenda.
Waziri alisema serikali inafanya uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo cha tukio hilo huku akisisitiza kuwa kwa sasa ni mapema kujua chanzo kwani tayari vyombo vinavyohusika ikiwa ni pamoja na Jeshi la Polisi vimeshapewa jukumu la kufanya uchunguzi.
“Tukio hili ni kubwa na limetuhuzunisha. Kwa kutambua umuhimu wa watumishi wa dini nchini, serikali inafanya uchunguzi wa kina ili kutambua chanzo cha tukio hilo haraka. Kwa sasa ni vyema tukawaachia madaktari ili wandelee na uchunguzi wa afya yake lakini ifahamike wazi kwamba serikali ipo makini na pindi wahusika watakapopatikana watachukuliwa hatua kali za kisheria.”

MAUAJI YA AFISA TAKUKURU
Katika tukio la pili la kuuawa kwa risasi aliyekuwa Afisa Uchunguzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), marehemu Bhoke Ryoba nako kulikuwa na utata wa kauli kwani wafanyakazi wenzake walidai kuwa aliuawa na majambazi waliowavamia.
Lakini Charles Gibore ambaye ni mume wa marehemu, kabla ya kuanza safari kwenda kuzika mwili wa marehemu alisema:
“Mke wangu aliuawa na mfanyakazi mwenzake na tukio hilo limegubikwa na utata ambao Takukuru na polisi ndiyo pekee wanaoweza kutupa ukweli,” alisema Gibore nje ya chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam.
Gibore alieleza kuwa mkewe huyo aliuawa usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita katika tafrija ya kuagana na kupongezana na baadhi ya wafanyakazi wenzake wa Takukuru waliokuwa wamepandishwa vyeo, tafrija ambayo Bhoke alipewa zabuni ya kupika chakula.
Alisema pia mkewe aliombwa awapatie kwenye sherehe hiyo, vijana wawili wa kuwachomea nyama.
“Wale vijana walinieleza kwamba baadaye saa 8:30 mchana, Bhoke na wenzake walifika ukumbini na kuwakuta vijana wawili wanaofanya nao kazi wakinywa pombe, huku wakichezea silaha aina ya bastola wakishindana kulenga shabaha.Vijana hao walifyatua risasi juu na ndipo muuaji alipompiga kichwani marehemu na mauti kumfika muda mfupi baadaye,” alisema.
Alisema baada ya hapo muuaji huyo alitoweka kisha kujisalimisha mwenyewe katika Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Temeke, Chang’ombe. Swali la kujiuliza ni je ni haki kuchezea bastola tena kwa kufyatua risasi mbele ya kadamnasi?
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Engelbert Kiondo alithibitisha mtuhumiwa huyo kujisalimisha na kisha kushikiliwa kituoni hapo. “Tunaendelea kumshikilia hapa na uchunguzi utakapokamilika tutamfikisha mahakamani kwa taratibu nyingine za kisheria,” alisema Kiondo.
Marehemu Bhoke Ryoba alizaliwa Juni 18, 1978 katika Kijiji cha Kiterere, Wilaya ya Tarime mkoani Mara na amezikwa huko. Ameacha watoto watatu; Doloresy (10), Dolrisy (4) na Dolrick Gibore ambaye ana mwaka mmoja.

Views: 1393

Tags: uwazi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by Mama Wawili Jr. on January 2, 2013 at 11:01am

Wauwaji wanajua kuwa hatuna vyombo thabiti vya sheria na usalama nchi ndio maana wanafanya mauaji haya hadharani bila woga wala wasiwasi.

Comment by julius manning on January 1, 2013 at 6:41pm

hii ndo bongo

ADVERTISEMENT


Advertisement

 

Forum

KIPIGO CHA BAO 2-1 KWA MAN UTD, KOSA LA MWAMUZI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Mohammed Mar 26. 6 Replies

JE, NI KWELI KWAMBA KIPIGO CHA BAO 2-1 ILICHOKIPATA MAN UTD KUTOKA KWA REAL MADRID USIKU WA KUAMKIA LEO LAWAMA ZOTE ZIMWENDEE MWAMUZI WA MCHEZO AU MAN UTD WAJILAUMU WENYEWE? TUPE MAONI YAKO!!!

HALI INAYOENDELEA BUNGENI, SPIKA NA NAIBU WAKE WAMESHINDWA KUONGOZA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Ali Abdalla Ali Apr 22. 20 Replies

Tumeshuhudia kwa siku za hivi karibuni hali halisi iliyokuwa inatokea katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, kwa hali hii ni ishara kuwa Spika na Naibu wake washindwa kuliongoza bunge hilo?

VURUGU ZA CCM NA CHADEMA KUGOMBEA MLINGOTI WA BENDERA DODOMA, NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Phinehas Rishiansia Kileo May 3. 6 Replies

Wafuasi wa CCM wakimshambulia mfuasi wa Chadema mkoani Dodoma…

Tags: BENDERA, WA, DODOMA, NANI, KULAUMIWA?

VURUGU ZINAZOENDELEA HAPA NCHINI NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by NELSON UVAMBE 6 hours ago. 27 Replies

HIVI KARIBUNI KUMEKUWEPO UPOTEVU WA AMANI HAPA NCHINI PAMOJA NA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI. MKOANI KAGERA WANANCHI WENYE HASIRA WALIWAUA POLISI, IJUMAA ILIYOPITA WAKULIMA NA WAFUGAJI HUKO WILAYANI KILOSA WALIZUA VURUGU NA KUFUNGA BARABARA,…

MRISHO NGASSA KUPELEKWA SIMBA SC BILA RIDHAA YAKE, JE NI HALALI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Domino Bagambisa Jan 21. 17 Replies

Kiungo hatari wa Azam FC, Mrisho Ngassa leo amepelekwa Simba SC kwa mkopo na timu yake…

Tags: SOKA

hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Started by Gysper in Siasa. Last reply by Jamal amor May 9. 24 Replies

 hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Kauli Ya JK kuwa Mauaji ya Arusha ni "Bahati Mbaya"

Started by Kulikoni Ughaibuni in Siasa. Last reply by richardngeze Feb 12. 12 Replies

Tanzania tuna tatizo kubwa.Hakuna haja ya kunyoosheana vidole as to nani amechangia tatizo hilo bali cha muhimu na haraka ni namna tutakavyoweza kutatua tatizo hili.Nisimung'unye maneno: tatizo kubwa linaloikabili ni kuwa na Rais ambaye takriban…

Latest Activity

GLOBAL's 6 blog posts were featured
8 seconds ago
Boyd Slagle posted a status
1 minute ago
tina babi left a comment for seleman yahaya sombe
"tinalutunku@yahoo.comHello,My name is Miss tina lutunku.i saw your profile today and become…"
1 minute ago
tina babi left a comment for Ponsino TT
"tinalutunku@yahoo.comHello,My name is Miss tina lutunku.i saw your profile today and become…"
1 minute ago
Boyd Slagle posted a status
1 minute ago
tina babi left a comment for Alfredy Wilson Kakili
"tinalutunku@yahoo.comHello,My name is Miss tina lutunku.i saw your profile today and become…"
1 minute ago
Boyd Slagle posted a status
2 minutes ago
Boyd Slagle posted a status
2 minutes ago
Boyd Slagle posted a status
2 minutes ago
Boyd Slagle posted a status
3 minutes ago
Boyd Slagle posted a status
3 minutes ago
tina babi left a comment for Lucas Michael
"tinalutunku@yahoo.comHello,My name is Miss tina lutunku.i saw your profile today and become…"
3 minutes ago

© 2013   Created by Global Publishers.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service