Kupenda sawa lakini usiwe mtumwa wa mapenzi

KWA mara nyingine tumekutana kwenye kona yetu ya mahaba ili kujuzana machache kuhusiana na maisha yetu ya kila siku ambayo yametawaliwa na mapenzi.
Kutokana na uwezo wa Mungu nina imani wote mu wazima wa afya njema, yangu hali namshukuru Mungu. Leo nataka nizungumzie kuhusu kupenda kulikopitiliza na hatimaye kuwa utumwa katika mapenzi.

Kila kiumbe kina utashi wa kupenda kwa vile upendo ndiyo tuliohimizwa wanadamu, lakini ukizidi unakuwa ugonjwa ambao huenda usipate dawa na kuendelea kuumia. Hii inakuja baada ya kupata swali kutoka kwa dada yangu mmoja ambaye alitokea kumpenda kaka mmoja kufikia kushindwa hata kuzungumza pale anapomuona.

Amejikuta amekosa kujiamini vkujieleza kwa yule kaka na kuona hawezi kuzungumza chochote kitakachoeleweka kwa vile amepoteza kujiamini kutokana na kumpenda kupita kiasi. Ni kweli kupenda bila kujielewa sawa na wendawazimu hata unapokuwa ndani ya penzi hilo lililokutia wendawazimu unapoteza kujiamini kwa kuogopa kulipoteza penzi ulilolitafuta kwa muda mrefu.

Nimekuwa nikielezea kujiamini kwa mwanadamu mbele ya mapenzi na kutojishusha thamani hata kama umempenda mtu kupindukia. Kupenda ni haki yako ya msingi lakini usiwe mtumwa wa mapenzi kwa kushindwa kujitambua wewe ni nani na kwa nini upo pale.

Kupenda sawa, lakini ukizidisha inakuwa sumu inayokutafuna taratibu kwa vile huna maamuzi yoyote ya moyo wako kuogopa kumuuzi umpendaye. Hii si kwa wanawake pekee, bali kwa watu wote. Wapo wanaofanyiwa vituko vya makusudi na wapenzi wao kwa vile tu wanatambua wanapendwa na kukaa kimya kiasi cha kuwashangaza watu.

Kwa vile hujiamini na mapenzi ndiyo yaliyochukua nafasi kubwa kwako na kuziba mishipa ya ufahamu na kuamini hakuna mpenzi mzuri kama uliyenae na kuona kumpata kwako ni bahati. Unakuwa huna maamuzi juu yako kila utakaloambiwa kwako sawa liwe zuri au baya.

Hapa kidogo napenda mnisikilize kwa makini kila kiumbe kina haki ya kupenda, lakini lazima ujue unayempenda kweli ana mapenzi ya dhati kwako. Kwa vile unampenda anajitoa kwake kama kafara ya mapenzi na kuwa radhi kufanyiwa chochote lakini usiachwe.

Tumeshuhudia wanawake kwa wanaume wakiteseka ndani ya mapenzi yao kwa penzi la upande mmoja, unalazimisha mapenzi kwa vile tu unampenda na kuona hakuna kiumbe chochote mbele yako. Acha kuwa kipofu wa mapenzi, siku zote mbegu ya upendo huota katika moyo wenye rutuba ya upendo.

Usihadaike na rangi tamu ya chai sukari, matendo mema ndiyo yanayojenga upendo ndani ya nyumba. Usiitupe ovyo mbegu yako kwa vile tu umetokea kumpenda kila ukimuona unachanganyikiwa. Je, unajua historia yake? Ana mapenzi ya kweli kwako?

Jiepushe kuutoa mwili wako ovyo kwa vile umependa tu, bila kujua kama mwenzako naye anakupenda. Hata unayempenda ukimpata basi usikubali kuwa mtumwa wa mapenzi, kwa penzi kukuongoza wewe na si wewe kuliongoza penzi.

Siku zote wewe ndiye uliongoze penzi kufikia kutoa maamuzi pale litakapokwenda kinyume. Hii itakufanya uonekane mwenye msimamo na siyo mtu wa kuburuzwa.
Kwa hayo machache tukutane wiki ijayo.

Na Ally Mbetu
Simu: +225 713 646500 E-mail:ambedkt@yahoo.com

Views: 1017

Tags: mahaba11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

NI SUPERMARKET GANI BORA KULIKO ZOTE KATI YA HIZI? NA KWA NINI? TOA MAONI YAKO!
  

Forum

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by TZ on Tuesday. 1 Reply

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson Nov 22. 11 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by mark gibson Nov 25. 29 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

JUAN MATA KUTUA MANCHESTER UNITED ATASIADIA KULETA MATOKEO BORA BAADA YA TIMU KUSUASUA?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson Nov 21. 88 Replies

Juan Mata anataraji kutua Manchester United akitokea klabu ya Chelsea ya…

KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KILA MARA, TATIZO NI NINI?

Started by GLOBAL in Habari. Last reply by mark gibson Nov 28. 46 Replies

VITENDO VYA KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KWA SASA VIMEZOELEKA. KATIKA NCHI MBALIMBALI WATANZANIA WAMEKUWA WAKIKAMATWA KWA UBEBAJI WA MADAWA HAYO. JE, TATIZO NI NINI? NA NINI KIFANYIKE?

Tags: MARA, TATIZO, NI, NINI?, KILA

JESHI LA POLISI KUTOA MILIONI 100 KWA ATAKAYEWEZESHA KUPATIKANA WAHALIFU WANAOMWAGIA WATU TINDIKALI NI KWAMBA LIMESHINDWA KAZI?

Started by GLOBAL in Maisha. Last reply by mark gibson Nov 30. 84 Replies

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.Jeshi la Polisi…

SIMBA SC WAMTUPIA VIRAGO JUMA KASEJA

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson Nov 22. 12 Replies

TIMU ya Simba SC leo imetangaza rasmi kuachana na mlinda mlango wake mahiri, Juma…

JE, NI SAHII KWA JESHI LA POLISI KULIPUA MABOMU WAKATI WANANCHI WAKIAGA MIILI YA WENZAO?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson Nov 23. 36 Replies

Juzi (Jumanne) polisi walilipua mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa wamekusanyika katika Viwanja vya Soweto jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili ya wenzao watatu waliopoteza maisha katika…

TOP NEWS WEEK HII

© 2014   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }