‘Kumshika’ mpenzi wako siyo mpaka umpe mapenzi kinyume na maumbile!

NAMSHUKURU Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia uhai kiasi cha kuweza kuiona siku hii ya leo nikiwa salama salmin. Nimshukuru pia kwa kunipa uwezo wa kuandika haya ninayowaandikia kila wiki kupitia safu hii nikiamini ni yenye manufaa katika maisha yenu ya kimapenzi.

Mpenzi msomaji wangu, leo nataka kuzungumzia mada ambayo inawagusa wote walio katika ulingo wa mapenzi, wawe wamo ndani ya ndoa au wapenzi wa kawaida. Nazungumzia mapenzi kinyume na maumbile, tabia ambayo nahisi nikinyamaza bila kuzungumza chochote haitakuwa sahihi.
Hivi karibuni nilikatiza maeneo ya Tandale kwa Mtogole, nikakutana na vurugu kati ya mwanaume na mwanamke. Katika kufuatilia nikabaini yule mwanamke alimfumania mumewe. Kilichoniumiza pale si kile kitendo cha mwanaume kutoka nje ya ndoa yake bali ilikuwa maneno aliyokuwa akitoa yule mke wa mtu.
“Mwanaume gani usiyeridhika na mapenzi ninayokupa…? Nimefikia hatua ya kukupa hata mapenzi kinyume na maumbile ili usitoke nje lakini bado, hivi ni kipi ulichokikosa kwangu?” alisika akipayuka mwanamke huyo.
Maneno aliyokuwa akiyatoa yule mwanamke yalinichoma sana. Nikabaini siri moja ambayo nahisi ipo kwa wanawake wengi walio kwenye ndoa na hata wale walio kwenye uhusiano wa kawaida kwamba, wanafikia hatua ya kutoa aina hiyo ya penzi eti ili wapenzi wao wasiwasaliti. Jamani hii inaingia akilini kweli?
Unafikia hatua ya kuhatarisha maisha yako kisa unataka kukamilisha ile sentesi ya kwamba unampa mumeo kila anachokitaka? Huo ni ulimbukeni na kama wapo wanaoendelea kufanya hivyo, wanajitafutia matatizo yatakayowafanya waje kujuta baadaye.
Ni kweli washauri wa masuala ya mapenzi wanaeleza kuwa, ili uweze kumshika vilivyo mpenzi wako unatakiwa kuhakikisha unampatiliza katika kila anachokitaka lakini hawakuzungumzia ishu ya wewe kukubali mapenzi kinyume na maumbile. Hawakurusu hilo kwa kuwa wanajua madhara ya kufanya hivyo. Sasa iweje leo ukubali kufanya dhambi hiyo eti kwa kuwa mpenzi wako kataka na unampenda?
Katika ulimwengu wa sasa wapo wanaume wa ajabu sana. Hawa ni wale ambao si wastaarabu. Wao hawaangalii madhara yanayoweza kuwapata wenzao bali wanaangalia kujifurahisha wao tu. Mbaya zaidi baadhi ya wanawake nao wamekuwa mbumbumbu.
Eti kwa kuogopa kuachwa au kusalitiwa wanasema bora wafanye hivyo. Jamani, ifike wakati tufikirie kila tunalolifanya katika maisha yetu ya kila siku. Zipo mbinu nyingi za kumridhisha mpenzi wako na wala asifikirie kukuacha wala kukusaliti bila hata kumkubalia afanye hivyo.
Pia unatakiwa kufahamu kwamba, unaweza kumpa mpenzi/mume wako mapenzi hayo lakini bado akakusaliti tu. Sasa kwa nini ujidhalilishe?

Ni kamchezo ka’ nyumba ndogo
Ukijaribu kuchunguza utabaini kuwa wanaoongoza kwa mchezo huo mchafu ni wale wezi wa mapenzi ambao hufahamika kwa jina la nyumba ndogo.
Hawa eti wanatumia mbinu hiyo kuwashika waume za watu. Kimsingi hii ni aibu na wanaokubali kufanyiwa hivyo wanajidhalilisha na hawawezi kudumu na wanaume wao.

Usithubutu kabisa
Mapenzi kinyume na maumbile licha ya kwamba yamekatazwa hata na vitabu vitakatifu, madhara yake kiafya pia ni makubwa. Wapo wengi ambao sasa wanajuta kwa kufanya mchezo huo kutokana na kupata matatizo wakati wa kujifungua lakini pia wengi wao imekuwa ni rahisi kuambukizwa magonjwa mbalimbali ya zinaa ukiwemo Ukimwi.

Ni laana
Wanaofanya hivyo wamelaaniwa na wanaweza kushangaa uhusiano wao unakumbwa na matatizo kisha kusambaratika kwani Mungu hawezi kuubariki  ule unaokwenda kinyume na maagizo yake.
Ni suala tu la kukaa na kujiuliza, wewe mwanamke unapata raha gani kufanya mapenzi kwa njia ambayo haijaruhusiwa? Wakati mwingine nashindwa hata kuwaelewa hawa wanaofikia hatua ya kujisifia kuwa eti wanawaachia waume zao ‘wajisevie’ wanachotaka kwa kuwa wanawapenda.
Hivi watakuwa na akili timamu? Kumpenda mtu ndiyo uwe tayari kuhatarisha maisha yako kiasi hicho? Tena kwa taarifa yako wale wanaowakubalia wapenzi wao mapenzi kunyume na maumbile wanaonekana wajinga na wanadharaulika. Hakuna mwanaume anayeweza kumheshimu mwanamke anayeweza kuuweka rehani mwili wake kwa njia hiyo.
Nimalizie makala haya kwa kusema kuwa, kanuni ya kwamba unatakiwa kuhakikisha unampatia mpenzi wako kile anachokipenda inabaki palepale lakini umkubalie katika yake yasiyo na madhara kwako. Yale ambayo unaona yatakuletea matatizo, mkatalie kwa kumpa sababu za msingi. Kama ni muelewa atakuelewa, asipokuelewa kuwa tayari akuache lakini usihatarishe maisha yako.

Views: 2584

Tags: mahaba11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by bongo on March 15, 2012 at 7:52pm

Huo ni udhaifu tu ambao mtu unakua hujiamini na maisha yako.Lakini kwa yeyote mwenye kujiamini basi hawezi kukubali kufanya dhambi kwa kumridhisha mwanaume.Na mwanaume akikuona kama ni dhaifu wa moyo basi lazima akujaribu kwasababu anakuwa na jeuri yakuwa mwanamke anampenda sana na atapata chochote kile atakacho.Lakini akijua upo makini hatothubutu kukudhalilisha hata siku moja.Na hasa pale utakapomuonyesha kwamba "siku nikigundua umenisaliti nakupiga na chini kwani mwanaume ni wewe tu hapa duniani mbona wengi wananitamani wapo waliotangulia na hutokuwa wamwisho ikibidi"Acheni kujidhalilisha dada zangu hebu rudini kwa mungu huu sio wakati wa kumridhisha mtu huu ni wakati wa yarabbi nafsi.

Comment by Mohamed Idd on March 15, 2012 at 5:56pm
Hiyo ni laana na wote wanaofanya mapenzi wamelaaniwa duniani na mbinguni.
Comment by AJMAL MAHIR on March 15, 2012 at 12:46pm

sisi waislam mume wa ndoa akitamka kutaka kinyume na maumbile ni talaka yako tayari hivo ukiendelea kukaa nae unakua munazini

Comment by bianca kingu on March 15, 2012 at 11:12am

mapenzi kinyume na maumbile hata shetani mwenyewe hataki kushuhudia watu wanapofanya hivyo.

Comment by julius manning on March 15, 2012 at 9:55am

he, kumbe ndivyo wanavyofanya !!!!!

UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

Latest Activity

jancikop posted a status
17 seconds ago
Alan Munk posted a status
1 minute ago
Alan Munk posted a status
1 minute ago
Alan Munk posted a status
2 minutes ago
Alan Munk posted a status
2 minutes ago
Alan Munk posted a status
3 minutes ago
Alan Munk posted a status
3 minutes ago
Alan Munk posted a status
4 minutes ago
Alan Munk posted a status
5 minutes ago
Alan Munk posted a status
5 minutes ago
Alan Munk posted a status
6 minutes ago
Ruth D. Fay posted a status
6 minutes ago

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }