Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi’- 2

WIKI iliyopita tulianza makala haya kwa kueleza ukweli kuhusu juisi ya boksi ambayo huandikwa asilimia 100 ‘pure fruit juice’ na kusema kwamba haya ni maneno ya kibiashara ambayo hayana ukweli wowote.  Sasa endelea...

Aidha, Hamilton anaendelea kueleza mchezo mchafu unaochezwa na watengeneza juisi viwandani kwamba ladha ya juisi hiyo ya machungwa hutofautiana pia kati ya nchi na nchi, kwani viwanda huweka aina ya ladha kwenye chungwa kulingana na vile ambavyo wanapenda watu wa eneo inakokwenda.

Juisi inayotengenezwa kwa ajili ya nchi za Amerika Kaskazini huwa na kiwango kikibuwa cha kirutubisho aina ya ‘ethyl butyrate’, ambacho ni moja ya kemikali inayotumika sana kwenye utengenezaji wa manukato na ladha. Mbali ya kirutubisho hicho kuwa na uwezo wa kutengeneza aina mbalimbali za ladha za matunda, lakini pia hakina gharama (cheap).

HATUA GANI ZA KUCHUKUA SASA?
Kama makala haya yatakuwa yamekushitua na kukushangaza, jua hauko peke yako. Hata hivyo, lengo kubwa la makala haya ni kukufumbua macho  ujue juisi unayokunywa siyo salama kiasi gani na uwe na uamuzi wa kuicha au kuendelea kuitumia kwa hiyari yako mwenyewe, lakini siyo kwa kudanganywa na maelezo ya uongo ya kibiashara yanayowekwa juu yake.

Kama ambavyo mwandishi wa kitabu hicho Bi. Hamilton anavyosema: “Lengo la kitabu changu siyo kukataza watu kunywa juisi, isipokuwa kuwafanya wakijue vizuri wanachokinywa. Watu wana haki ya kujua ni kwa kiasi gani utengenezaji wa juisi hivi sasa umekuwa wa kibiashara zaidi, hii itawafanya wawe na maamuzi sahihi kuhusu afya zao.”

Ingawa ni vigumu sana kuepuka ‘kuingizwa mkenge’, lakini unaweza kujiepusha na madhara ya kiafya yatokanayo na unywaji wa juisi hizi ‘feki’ kwa kupendelea kunywa juisi uliyoitayarisha mwenywe nyumbani na kuacha kununua vyakula au vinywaji ‘ready made’, hasa kwa vile ambavyo vinapatikana kwa wingi sokoni.

TAHADHARI
Kwa ujumla matunda na juisi zake zina virutubisho vingi muhimu kwa ustawi wa afya ya binadamu, lakini tahadhari inatolewa kwa wanaopenda kunywa kiasi kingi cha juisi za matunda, hasa juisi ya machungwa ambayo inaelezwa kuwa na sukari nyingi.

Kiasi cha glasi moja ya juisi ya machungwa ina wastani wa gramu 25 za ‘fructose’, (sukari), kiwango ambacho ni cha mwisho kabisa anachotakiwa mtu kutumia kwa siku moja. Hii ina maana kama utakunywa zaidi ya glasi moja pamoja na vinywaji vingine vinavyotumia sukari, kama vile chai, tayari utakuwa umezidisha kiwango kinachopendekezwa kwa siku.

Iwapo utakuwa na tatizo la unene na unahitaji kupunguza uzito, ni vyema ukapunguza sana au ukajiepusha kabisa na uywaji wa juisi za matunda, kwa sababu kiwango cha sukari kilichomo ni zaidi ya wastani unaotakiwa.

Ili upate faida za virutubisho vinavyopatikana kwenye matunda, yakiwemo machungwa, unashauriwa kula matunda hayo kama yalivyo kuliko kukamua juisi na kutupa makapi yake. Inaelezwa kwamba sukari iliyomo kwenye chungwa inapoliwa pamoja na nyama zake (fibre), sukari hiyo huwa haina madhara kwani huweza kujichanganya kwenye mfumo wa damu bila kuleta athari zozote kwa mlaji.

Hivyo ushauri wa ujumla unatolewa kwamba pendelea zaidi kula matunda na mboga za majani kama zilivyo kuliko kunywa juisi zake. Kwa kufanya hivyo utajiepusha na uwezekano wa kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari. Iwapo utakunywa, basi kunywa nusu glasi au isizidi glasi moja kwa siku.  Asanteni.

Views: 864

Tags: makala11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by juliana adamu on November 17, 2011 at 1:40pm

asanteni kwa kutufumbua macho

Comment by Mary Stephen Makonda on September 6, 2011 at 4:27pm
 sasa hako kapicha inaonesha hautumii juisi ya aina yoyote ile ausiyo@Kijungujiko
Comment by Mary Stephen Makonda on September 6, 2011 at 4:25pm

Kuanzia leo si nunui tena juisi  ya  bokis staki

Comment by Ungujaukuu on September 6, 2011 at 1:03pm
thx kwa info bhanya
Comment by lumi mwandelile on September 6, 2011 at 10:10am
asante kwa elimu uliyotupa

ADVERTISEMENT


Advertisement

 

Forum

KIPIGO CHA BAO 2-1 KWA MAN UTD, KOSA LA MWAMUZI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Mohammed Mar 26. 6 Replies

JE, NI KWELI KWAMBA KIPIGO CHA BAO 2-1 ILICHOKIPATA MAN UTD KUTOKA KWA REAL MADRID USIKU WA KUAMKIA LEO LAWAMA ZOTE ZIMWENDEE MWAMUZI WA MCHEZO AU MAN UTD WAJILAUMU WENYEWE? TUPE MAONI YAKO!!!

HALI INAYOENDELEA BUNGENI, SPIKA NA NAIBU WAKE WAMESHINDWA KUONGOZA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Ali Abdalla Ali Apr 22. 20 Replies

Tumeshuhudia kwa siku za hivi karibuni hali halisi iliyokuwa inatokea katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, kwa hali hii ni ishara kuwa Spika na Naibu wake washindwa kuliongoza bunge hilo?

VURUGU ZA CCM NA CHADEMA KUGOMBEA MLINGOTI WA BENDERA DODOMA, NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Phinehas Rishiansia Kileo May 3. 6 Replies

Wafuasi wa CCM wakimshambulia mfuasi wa Chadema mkoani Dodoma…

Tags: BENDERA, WA, DODOMA, NANI, KULAUMIWA?

VURUGU ZINAZOENDELEA HAPA NCHINI NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by NELSON UVAMBE on Monday. 27 Replies

HIVI KARIBUNI KUMEKUWEPO UPOTEVU WA AMANI HAPA NCHINI PAMOJA NA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI. MKOANI KAGERA WANANCHI WENYE HASIRA WALIWAUA POLISI, IJUMAA ILIYOPITA WAKULIMA NA WAFUGAJI HUKO WILAYANI KILOSA WALIZUA VURUGU NA KUFUNGA BARABARA,…

MRISHO NGASSA KUPELEKWA SIMBA SC BILA RIDHAA YAKE, JE NI HALALI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Domino Bagambisa Jan 21. 17 Replies

Kiungo hatari wa Azam FC, Mrisho Ngassa leo amepelekwa Simba SC kwa mkopo na timu yake…

Tags: SOKA

hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Started by Gysper in Siasa. Last reply by Jamal amor May 9. 24 Replies

 hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Kauli Ya JK kuwa Mauaji ya Arusha ni "Bahati Mbaya"

Started by Kulikoni Ughaibuni in Siasa. Last reply by richardngeze Feb 12. 12 Replies

Tanzania tuna tatizo kubwa.Hakuna haja ya kunyoosheana vidole as to nani amechangia tatizo hilo bali cha muhimu na haraka ni namna tutakavyoweza kutatua tatizo hili.Nisimung'unye maneno: tatizo kubwa linaloikabili ni kuwa na Rais ambaye takriban…

© 2013   Created by Global Publishers.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service