KHADIJA KOPA: SHAROBARO NI TUSI KUBWA

Na Shakoor Jongo
MalkIA wa Mipasho Bongo, Khadija Omary Kopa, ameibuka na kusema kuwa, neno sharobaro ambalo limeenea mitaani ni tusi kubwa lenye maana ya mwanaume aliyelegea anayefanyiwa kila kitu.

Mwanamipasho huyo alifunguka hivi karibuni jijini Dar es Salaam kuwa, anashangazwa na vijana wa kiume wanaojiita masharobaro huku wakiwa hawajui maana na asili ya neno hilo.

“Siku hizi eti kijana wa kiume anajigamba kuwa yeye ni sharobaro huku akiwa hajui maana halisi ya neno hilo. Ukimuuliza maana yake atakwambia ni mtu mtanashati anayejua kupangilia ‘pamba’.

“Ukweli ni kwamba, neno hilo linatumika Uarabuni kwa mwanaume ambaye hajishughulishi na kazi yoyote,  badala yake huzurura kutwa na watoto wa kike akisubiri afanyiwe kila kitu na dada au mama yake.

“Hata sauti yake akiongea utamuonea huruma jinsi alivyolegea,” alisema malkia huyo na kuwataka vijana kuacha kujiita jina hilo.

Hivi karibuni kumeibuka rundo la wanaume, hasa vijana kujiita masharobaro huku wakishindwa kujua maana halisi ya jina hilo.

Safu hii inafanya jitihada ya kujua ni kweli jina hilo lina maana aliyosema Hadija Kopa? Fuatilia matoleo yajayo.


Views: 5120

Tags: amani11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by Bob Fern on June 19, 2011 at 1:17pm
mhl
Comment by Akram on April 14, 2011 at 9:23pm

Duh noma masharabaro umeumbuka kujita majina hamjui maana yake.

Comment by Ashagrace on April 13, 2011 at 8:59am
haa haaa A town inakuwa vp! "SHARUBARU"
Comment by dinah kimz on April 13, 2011 at 8:39am
bora 2 uwaambie hao wa2 waache kujiiita hayo majina koz wanaona cfa kwly kumbe wanaji2kana wenyewe !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! xx je cku 2kiwaita maana ya jina halic watakacrika au????
Comment by Khalid Japhary GOMEKA on April 11, 2011 at 12:12pm

Tatizo vijana siku hizi hawataki kutafuta elimu kwanza wanaona kuwa msanii ndio kila kitu matokeo yake wanakuwa wapo nyuma kiufahamu wa mambo...ona sasa mngekuwa weledi wa mambo msingejiita masharobaro...aibu yenu.

Comment by Focus Kunambi on April 10, 2011 at 4:25pm
BIG UP BI MKUBWA KUWAFUMBUA WATU MACHO. KISERENGETI BOY CHAKO KINAENDELEAJE BI MKUBWA?????
Comment by Gerald Mlyomi on April 10, 2011 at 12:46pm

laha tupu kumbe wanao jiita masharobaro ni mazoba yacyo jua mbele wala nyuma ya maisha yao

Comment by William Jotham on April 10, 2011 at 10:15am
Tatizo la kukopi vitu vya wengine!!!ndo maana unakuta vijana wengi wana vaa suruali makalio nje.Hawajui maana yake.Huko kwa wenzetu ukivaa hivyo unakuwa unajitangaza kuwa wewe unaingiliwa kinyume na maumbile!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Comment by Anselm on April 8, 2011 at 9:22am
Masharo u'haro!
Comment by Ney Reno on April 8, 2011 at 9:00am
SHOLOBALO

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by hiepelines Jul 4. 6 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Aug 15. 7 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Aug 15. 6 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by Joe reggan Apr 24. 2 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }