Mshahara sasa kwenda kwa mke
Maafisa katika jimbo la Gorontalo nchini Indonesia wamepata njia mpya ya kuhakikisha wake wa wafanyakazi wa serikali wanapata mgao wa kutosha wa mshahara wa waume zao.
Mpango huo ni kuweka fedha za mishahara katika akaunti za benki za wake wa wafanyakazi wa serikali. Mpango huo unatazamiwa kuanza mwezi Machi na unatarajiwa kuweka familia pamoja, kutokana na kongezeka kwa vitendo vya wanaume kutumia fedha za ziada kwa wanawake wa nje.
Ni mpango rahisi lakini wa aina yake. Kuanzia mwezi Machi, kila mwanaume aliye na mke na anayefanya kazi katika serikali katika jimbo la Gorontalo atashuhudia mshahara wake ukiingia kwanza katika akaunti yake na mara moja fedha hizo kuhamishwa kwenye akaunti ya mke wake.
Hatua hiyo ni ya kuzuia matumizi "mabaya" ya fedha. Maafisa wanasema wamepokea malalamiko mengi mwezi uliopita kutoka kwa wake wa wafanyakazi wa serikali, ambao wanasema hwapati fedha za kutosha kutoka kwa waume zao kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Msemaji wa jimbo la Gorontalo Rudy Iriawan amesema kanuni hiyo mpya ina lengo la kulinda familia zisimeguke. "Tuna wasiwasi kwa kuwa mwanaume ndio anadhibiti fedha za familia.
Na tunataka kuhakikisha mishahara ya wafanyakazi wa serikali inatumika kujenga familia na sio kwa ajili ya mambo mengine hasa wanawake wa nje".
Hata hivyo maafisa hao pia wameonya kuwa wake wa wafanyakazi hao wa serikali wasitumie fedha kujinunulia vitu vya kifahari.
Wametakiwa kuzingatia hatua hiyo kama kazi, zimesema mamlaka, katika kutazama fedha za familia za nyumba zao.
chanzo na bbcswahili
Comment
Comment by Babu Lao on February 14, 2012 at 1:37pm SAFI SANA, VERY NICE IDEA!!!
Comment by samora rajab albert on February 11, 2012 at 7:19pm ikifika TZ iyo am sure wanawake watazidi kukoma, mana ukishapata mgao tu mume hakujui tana itoshe isitoshe utajijua mwenywewe
Kwa jinsi tunavyopenda kuiga sasa hivi tutaanza kusikia kelele za wanaharakati wa haki za mwanamke. Wakianzisha hilo nitakuwa mvuvi na samaki nitauzia baharini
Ikija bongo ndoa zitavunjika balaa, wanawake full kujiachia Dar live na watoto hata socks za shule hawatapata, kitchen part na michiriku kila leo. Kila mtu ashike kile anachokichuma na asiyeweza kuhudumia watoto akafie mbali na Mungu amlaani.
Comment by Isalia on February 10, 2012 at 6:16pm
Comment by kibabaa on February 10, 2012 at 5:41pm Huu ndio mwisho wa watu kuoa, zinaa itakomaa, je mume akisema kuwa hakuweza kuja kazini kwakuwa hana nauli nani awajibike. mimi sikudhani watu wa karne hii wanaweza kuwa na mawazo ya kipumbavu kama hayo. ina maana kuzaliwa mwanamke ndio ufunguo wa kuwa tajiri, ndio maana ndo za jinsi moja zinapamba moto, mwisho wa dunia, walioshangilia hapa utakuta hawaelewi madhara yake. je na wanawake waofanya kazi mishahara yao iende wapi?
Comment by Suleiman Abdalla Salim. on February 10, 2012 at 4:53pm Hili kidogo lina utata!
Comment by julius manning on February 10, 2012 at 4:49pm ha ha ha hao hawajafanya lolote zaidi ya kuwapelekea wanawake wabadilishe Serengeti boys kila kukicha.
Comment by marimar ethan on February 10, 2012 at 3:26pm HEHEHEEEEEE kumbe hata uko yapo yanii gud job nimeipend sn aisee hata uku wafanyiwe hivyo hvyo maana wanawk tunapata tabu uwiiiiiii
Comment by kaka on February 10, 2012 at 2:30pm NA BONGO LETA TUMALIZE VIBANDA VYA NYUMA NIPO NAWE DADA LUMI MWANDELILE NA BONGO TUFANYE KAMA WAO
| 1 |
GLOBAL |
| 2 |
julius manning |
| 3 |
Man KKK |
| 4 |
Sili Silali |
| 5 |
IL-YA |
| 6 |
chama baby |
| 7 |
msichoke mlugu |
| 8 |
kaka |
| 9 |
Maji Marefu |
| 10 |
Kelvin Luhala Eto'o |
othman Ochu posted a status
mrembo commented on Sili Silali's photo

You need to be a member of Global Publishers to add comments!
Join Global Publishers