Na Brighton Masalu
STAA mkubwa katika tasnia ya filamu za Kibongo, Steven Kanumba Charles ‘The Great’ ameweka wazi siri za maisha yake ya utotoni na kumfumua baba yake mzazi aliyemwacha ateswe na mama wa kambo na kukataa kumsomesha, Ijumaa linakushushia vesi za ukweli.
Akizungumza kwa majonzi ndani ya Kipindi cha Take One, kinachorushwa na Runinga ya Clouds ya jijini Dar, Kanumba amemtupia zigo la lawama baba yake, Mzee Charles Kusekwa kwa kuchangia mateso yake.
“Maisha yangu ya utotoni yalikuwa ya mateso baada ya wazazi wangu kutengana, nilionja joto ya jiwe kwa kwenda kuishi kwa baba aliyekuwa ameoa mke mwingine, jambo hilo lilinikosesha furaha na amani ya utotoni,” alisema Kanumba.
Kanumba ambaye hadi sasa amejinyakulia umaarufu mkubwa kutokana na filamu zake, alisema wazazi wake walitengana akiwa anasoma darasa la nne.
“Nilikuwa naishi na mama, nilitamani sana kumjua baba yangu, nilimsumbua mama mpaka akanionesha baba yangu, nikaenda kuishi naye, nilikuwa nampenda sana baba yangu,” alisema Kanumba.
Akazidi kutupa madongo kupitia kipindi hicho kinachoongozwa na Zamarad Mketema kwamba, siku za mwanzo waliishi kwa furaha na baba yake pamoja na mama wa kambo lakini kadiri siku zilivyozidi kusonga mbele ndipo kibao kilivyoanza kumgeukia.
Ukurasa wa mateso
“Nilianza kuamshwa na kutakiwa kuchota maji asubuhi na kwenda kufunga mbuzi kwenye malisho kisha niliporudi nilitakiwa kuosha vyombo.
“Nikitoka hapo, nilitakiwa kwenda shule, sisi tumesoma kipindi cha viboko, ukifika shule unakutana na mwalimu wa zamu, unachapwa bakora, mwalimu wa darasa naye anakupa adhabu kwa kuchelewa kipindi chake…,” alisema Kanumba na kuongeza;
“Unajua Shinyanga kuna shida kubwa sana ya maji, niliporudi nyumbani kutoka shuleni nilitakiwa kwenda kuchota tena maji. Nilipewa tolori na madumu sita ya kwenda kuchota maji.”
Staa huyo alisema kuwa baba yake alikuwa akiyajua mateso aliyokuwa akiyapata lakini hakuchukua hatua zozote ili kumnusuru.
“Kule Shinyanga huwa tunachimba mashimo ya taka, hakuna ‘ma-dastibin’ kama huku, siku moja mama alinitaka kuwapelekea mbuzi maganda ya viazi lakini kwa kuona kuwa mbuzi wale walikuwa wameshiba na ilikuwa usiku niliona bora niyatupe kwenye shimo la taka.
“Mama alipogundua nimefanya hivyo, hakujali kama ni usiku, akanitaka niingie shimoni na kuyatoa yale maganda na kuwapelekea mbuzi, niliingia kwenye shimo kukiwa na giza na kuanza kuyakusanya ingawa nilikuwa sioni kutokana na giza.
“Baba alipita, alidhani ni paka, kabla ya kurusha jiwe, aliwasha tochi na kuniona, aliniuliza nilikuwa nafanya nini, nikamweleza,” alisema Kanumba na kusema kuwa hiyo ilikuwa sababu tosha ya baba yake kuona mateso yake na kuweza kumnusuru.
Kanumba alisema mama yake mzazi, Flora alimchukua baada ya kusikia mateso aliyokuwa akiyapata.
“Mama akiwa anakwenda harusini na wenzake aliniona nikichunga mbuzi mchana wa jua kali. Alijisikia vibaya sana, akaamua kunisaidia bila ya aibu na akanichukua kabisa pale alipoyaona mateso yangu,” alisema Kanumba.
Kanumba aliongeza kuwa alijitahidi sana kumshawishi mama yake awasiliane na mzazi mwenzake huyo ili wasaidiane kumsomesha.
Mama yake alimfikisha mzazi mwanzake huyo Ustawi wa Jamii, lakini siku ya mashauri, mama yake alirudi na hakutaka kumwambia Kanumba kilichotokea.
“Nilijitahidi kutaka kujua lakini mama aliniambia kuwa atanisomesha yeye mwenyewe, nilishindwa kuelewa lakini nikiwa nacheza nje nilimsikia mama kupitia dirishani alipokuwa akiongea na wanawake wenzake kwamba baba yangu amesema kuwa hawezi kumsomesha jambazi.
“Eti baba alisema kuwa nilikuwa nikimuibia mama yangu wa kambo fedha,” alisema Kanumba kwa majonzi.
Akiri kumpenda Mama kuliko Baba
Bila aibu wala simile, Kanumba alisema kuwa anakiri nafsi yake inampenda mama yake mzazi kuliko baba yake.
“Samahani sana najua hata baba anaweza kuwa anaangalia kipindi hiki lakini ukweli ni kwamba nampenda mama kuliko baba yangu,” alisema kwa unyonge na kuongeza:
“Kusema kweli baba yangu alianza kunitafuta baada ya kuwa maarufu, lakini mimi nilishawasamehe yeye pamoja na mama yangu wa kambo, kwani hadi sasa huwa nawasiliana nao kwa simu, nawasaidia panapowezekana.”
Comment
Comment by Frank Fungamenza on February 18, 2012 at 8:04pm Peter d.Mwaimu,unaishi wapi? nataka nipange chumba jirani na ww,kwa mawazo haya juu ya huyu Kanumba ww ni mtu wa kuombwa ushauri kabisa!!...ukitaka kuona uchungu wa maisha hapa duniani anza na starehe utotoni na umalizie na shida ukubwani,wee!!....huyu kanumba wa sasa angekuwa aliaza na starehe mwazoni leo huyu angejulikana kama yupo duniani kwa kuangalia tathmini ya vizazi na vifo serikalini,asingekuwa na maisha hayo....enzi za utoto wetu nasi tuliteseka sana tena hata zaidi yake na tumeishi na akina mama wa kambo zaidi ya wa 2,ye anaongelea mmoja??...sema hatujafanikiwa tu kama yeye lakini tunaelewa sasa hv kuwa malezi yale yalikuwa mazuri maana yaliondoa uvivu na kujenga moyo wa kujituma katika kazi....ninaamini wale waliotoka kijijini kama mm wataniunga mkono!...jamani Bony Mwaitege kaimba sana "mama ni mama" hakumaanisha umuheshimu mama na kumchukia baba hapana!!
Mama alitajwa kwa kuwakilisha Wazazi....kama ni hivo je,Kanumba unapata wapi ujasiri wa kumsema baba kwene vyombo vya habari?....alafu kuna msanii mwingine kaimba..."Kusamehe bure"..au Kanumba hafuatilii kazi za wasanii wezake?....Kanumba naomba uende ukatubu kwa mzee na usamehe kabisa!.
Comment by THE SEC_BORN on February 17, 2012 at 8:06pm Hayo ndo maisha katika utengano wa wazazi wetu hasa pale unapoishi na mama wakambo so chukulia kama ilikuwa ndo chanzo cha mafanikio yako kwani kusinge kuwa hivyo pengine leo tusinge kujua kuna mtu anaitwa KANUMBA....
Comment by REBECA ZAMBI on February 17, 2012 at 12:24pm
Comment by sophia suleiman mohamed on February 17, 2012 at 3:06am kaka kanumba pole kwa ulivyojisikia ktk malezi ambayo ukuyapenda dhidi ya mzazi wako wa kiume lkn nakupa ushauri usmlaumu na wala kumdharau baba ako kuna wenzako wanatafuta kama huyo hawampati ktk maisha kukutana na mambo kama hayo ni vitu vya kawaida cc ktk uislam tunaambiwa mzazi hakuna wa kulinganisha naye nakama amejirudi kuwa pamoja nawewe usimtangaze kwa mabaya yameshapita sameheaneni tafadhali ili mpate baraka zake mungu kama anavyosema ktk amri kumi za mungu
@Grace kwa upande wa wazazi here you have a point.
Comment by pjoan audes on February 16, 2012 at 6:38pm
Comment by grace abel on February 16, 2012 at 11:28am nimekaa kimya but mmh! kanumba hizo kazi ni za kawaida kwa watoto tuliolelewa kijijini kama sisi, ila baba yako anamakosa kwa kujiweka mbali na wewe wakati wa utoto jamani kina baba hamuoni jinsi mnavyowafanya watoto wenu wawadharau? kwanini usiwe na mtoto, kumsikiliza matatizo yake, kumdadisi, kumtia moyo panapotakikana? mfano baba yake kanumba angekuwa karibu naye na kupanga shughuli za familia pamoja yasingekuwa haya. mfano wangekuwa wote yaani baba mama yake huyu wa kambo na kanumba akamwambia mwanaye, unaona shughuli za hapa nyumbani? sasa wewe utafanya hichi na hichi na hichi, na akampa strategy ili kufanikisha hilo mwanangu, ina bidi uuamke mida flani uanze na hichi na umalize na hichi. na siku hakufanikisha zote angekuwa huru kuongea na wazazi wake na kutoa sababu na wazazi wangemsikiliza coz washajenga ule ukaribu. jamani asilimia 92% ya watoto wa kiafrica hasa tanzania hawana mapenzi na baba zao kwa sababu yamfumo dume na ubabe wa mababa zetu kwamba hata kukaa anaongea na baba, unauliza maswali hakuna yaani unaongea na baba wakati unashida ya hela tu, labda daftari zimeisha vingine nenda kakae huko na mama yako sasa kwa nini mtotomama ambaye yuko naye karibu zaidi na anamjali zaidi ? akiugua mama, akikosa ujue wewe mama, kula mama, wengine hata kuvaa mama, unatatizo brnza kwa mama yaani every thing mama mama. 2 bad we have to change.
Comment by peter d. mwaimu on February 15, 2012 at 1:19pm Kanumba kama ulikuwa unachungishwa mbuzi wakati wa masomo na ulikuwa unachunga wewe pekee na watoto wa mama yako wa kambo hawachungi kweli hayo yalikuwa mateso, lakini kama mlikuwa mnasaidiana hizo zilikuwa kazi za kawaida, wenzako tuliishi na mama na baba wa kutuzaa lakini tulishika jembe kabla ya shule na kufanya kazi zote hizo lakini hatukuona ni mateso na tulizoea na ndio zimetupa msingi mzuri wa kujitegemea tofauti na watoto wa siku hizi anamaliza mpaka darasa la saba na wengine kidato cha nne lakini hawajui kufua hata nguo zao za ndani. Hivyo mama yako huyo kama alikuwa unaona anakutesa badili mawazo jua alikuwa anakukomaza na ndio maana leo wewe sio goigoi na unapiga mzigo na umepata mafanikio uliyo nayo. Kuokoteshwa maganda ya viazi kwenye shimo usiku ilikuwa halali yako, wewe umetumwa uwape mbuzi ukadai uliwaona wameshiba ulikuwa na kipimo gani cha kupima shibe ya mbuzi, hivyo ulikuwa kiburi ningekuwa mimi ndio mzazi wako ungeyaokota na bakora juu ili siku nyingine ufuate maagizo ya wakubwa. wewe ulikuwa na infiriority kwa kuwa si mama yako mzazi, lakini mshukuru sana asingekulea hivyo Kanumba leo si ajabu tungesema mengine, unaona kuna vijana wa kiume tunawaita sio riziki kwa kuwa hawataki kazi wanataka vya bure lakini wewe unapiga mzigo kutokana na malezi uliyoyapata ya kuchapa kazi. Mshukuru sana mama yako huyo na uusomapo ujumbe wangu huu ukamnunulie tenge la waxla Nigeria sio la urafiki mapande matatu umpelekee na umwambie asante mama kwa malezi uliyonipa leo silali njaa.
Ninyi hamjamuelewa huyu Kanumba, anadai kuwa kazi alizokuwa anapewa nyumbani ni mateso. Kuchunga mbuzi kwa watoto wa vijijini ni jambo la kawaida, kwa kuwa yeye ni mtoto wa kiume kwake yeye anaona hakustahili kuosha vyombo wala kuchota maji. Ukisikia mtoto mwenye kasumba ya mfumo dume, huu ndio mfano halisi. Hivi ni nani aliyelelewa katika familia za kawaida za kitanzania ambaye hakufanya kazi hizi. Kwa akili yake aliona nani anastahili kwa mujibu wa mila za kitanzania kufanyia kazi hizo? Baba yake au mama yake wa kufikia. Halafu kwa kuwa hana adabu anamtangaza baba yake hadharani. Bwana mdogo hakuna radhi ya mtoto lakini baba yako akikutolea radhi itakupata usihadaike na mafanikio kiduchu uliyoyapata. Mzazi wako anavyokuthamini kwa kweli unanisikitisha kumsema kwa kiasi hicho. Kanumba usidhani umejificha tunakujua Dar hadi Shinyanga.
Comment by Mzalendo on February 14, 2012 at 10:20am | 1 |
GLOBAL |
| 2 |
julius manning |
| 3 |
Man KKK |
| 4 |
Sili Silali |
| 5 |
IL-YA |
| 6 |
chama baby |
| 7 |
msichoke mlugu |
| 8 |
kaka |
| 9 |
Maji Marefu |
| 10 |
Kelvin Luhala Eto'o |
othman Ochu posted a status
mrembo commented on Sili Silali's photo

You need to be a member of Global Publishers to add comments!
Join Global Publishers