Na Imelda Mtema
Mzazi mwenza wa prodyuza mwenye jina kubwa Bongo, Paul Matthysse ‘P.Funk’, Kajala Masanja (pichani) amesema kuwa ndoa yake ni mateso kwa sababu alipoolewa alifaidi ‘kiduchu’ raha ya kuwa na mume.

Kajala baada ya kuachana na P .Funk mwaka juzi, alidondokea kwa mwanaume anayeitwa, Faraja Augustine ambaye kwa sasa yupo mahabusu kwenye Gereza la Segerea akikabiliwa na mashtaka ya kula njama na kupora fedha.
Katika mahojiano yake na gazeti hili katikati ya wiki iliyopita, Kajala alisema kuwa hivi sasa hana amani na inamuuma kumkosa mume wake muda mfupi baada ya kufunga naye ndoa.

“Nahisi sina bahati, yaani kuolewa tu na haya mambo yanatokea. Nimefaidi ndoa kwa miezi minne tu, baada ya hapo ni misukosuko mpaka na mimi nikalazwa Segerea kwa mashtaka hayo ya mume wangu,” alisema Kajala na kuongeza:
“Ukweli maisha ya upweke yananitesa sana na yanazidi kuwa magumu. Namhitaji sana mume wangu, furaha ya nyumba siyo kukimbizana na polisi.”

Hata hivyo, mama huyo wa mtoto mmoja aliyezaa na P .Funk alisema: “Hivi sasa simfikirii mwanaume yeyote mpaka nijue kwanza hatma ya mume wangu, wala siwezi kukurupuka kwa maana ndoa yangu ni ya kanisani.”

Views: 2608

Tags: ijumaawikienda11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by lilian mosha on February 25, 2011 at 7:22pm
pole sana dada yote maisha vumilia 2
Comment by Janeth Jr on February 18, 2011 at 10:40pm
Pole sana dada,mkabidhi Mungu maisha yako..kwani hashindwi na kitu. mwambie pia mmeo aombe sana kwani Paulo na Sila waliomba hadi milango ya gereza ikafunguliwa.. shikilia ndoa yako kwani kuwagerezani siyo kufa!!huwezi kufungandoa wakati mmeo yu hai. Kuwa mumilivu siku moja utakuwa mwenye furaha..
Comment by mama imu on February 17, 2011 at 4:10am
Pole mamii,vumilia tu mungu ndo ajuaye kila kitu,muombee kheri tu,inshallah mtakuwa pamoja tena
Comment by chain Dyamwalle on February 14, 2011 at 3:38pm
Pole sana kajala mume bora utoka kwa mungu  nina amini huyo mumeo umepewa na mungu na ndio maana umefunga ndoa halali ya kidini(kanisani) kwani uliishi miaka mingapi na p funk na mpaka mkapata mtoto bila ndoa huyo ndiye mumeo uliopewa na mungu vumulia omba mungu, usiache kwenda kumtembelea mumeo jela yote hayo ni mitihani ya kimaisha tu na atatoka epukana na vishawishi watanzania hatuna dogo ukiteleza kidogo tu basi habari zote zitamfikia mumeo jela.sasa si afadhali wewe mumeo kafungiwa jela za hapa kwetu unayo nafasi ya kwenda kumtembelea.mm nilikaa mwezi mmoja tu tangia harusi yangu mume akaniacha na mimba kenda tafuta maisha ugaibuni na alipofika uko kakumbwa na balaa mpaka leo hii yuko jela mtoto hamjuhi babaye na anamiaka sita sasa lakini naamini ya kwamba mungu yupo ipo siku atarudi tu as long as napata salamu zake yupo hai.vumilia ndugu yangu kama kweli unampenda mumeo. 
Comment by KUU LA MAADUI on February 14, 2011 at 2:47pm
Katika maisha matatizo ni jambo la kawaida jela sio kifo ni sehemu ya maisha ambayo wanaume wengi tumeyapitia kwa mtu yeyote anaye elewa maisha hawezi kukulaumu kwa hili zaidi ya kukupa moyo wa uvumilivu, kwa uzoefu wangu nilishagudua hasa sisi wanaume jela inaweza kukuta wakati wowote sio lazima uwe jambazi unacho takiwa muombe mungu mumeo atatoka na maisha yataendelea,nikupe mifano nani alijua kama iko siku  mh Dito, liyumba,kombe,na wengineo wengi kama wangeweza kufungwa ni sehemu ya maisha siku zote tumuombe mungu atuepushie na mabalaa ,sasa wewe subiri akijatoka huko atakuwa mwema mpaka utashanga.
Comment by Glady-Cathy on February 14, 2011 at 2:29pm
mhu!!!!!! pole sana dada
Comment by Sebastian Salatiel Shemhilu on February 14, 2011 at 2:24pm
Pole sana dada vumulia yanamwisho
Comment by Josephine Beneth on February 14, 2011 at 12:43pm
Pole sanaa mpenzi yote mapito amini yatakwisha
Comment by MRS Willy(good mother) on February 14, 2011 at 12:38pm

POLE

Comment by Sarah Anuary on February 14, 2011 at 12:05pm
Pole sana dada vumilia tu ndo mambo ya kidunia hayo, na mungu atakupa kilicho rizki kwako.

NI SUPERMARKET GANI BORA KULIKO ZOTE KATI YA HIZI? NA KWA NINI? TOA MAONI YAKO!
  

Forum

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by TZ on Tuesday. 1 Reply

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson Nov 22. 11 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by mark gibson Nov 25. 29 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

JUAN MATA KUTUA MANCHESTER UNITED ATASIADIA KULETA MATOKEO BORA BAADA YA TIMU KUSUASUA?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson Nov 21. 88 Replies

Juan Mata anataraji kutua Manchester United akitokea klabu ya Chelsea ya…

KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KILA MARA, TATIZO NI NINI?

Started by GLOBAL in Habari. Last reply by mark gibson Nov 28. 46 Replies

VITENDO VYA KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KWA SASA VIMEZOELEKA. KATIKA NCHI MBALIMBALI WATANZANIA WAMEKUWA WAKIKAMATWA KWA UBEBAJI WA MADAWA HAYO. JE, TATIZO NI NINI? NA NINI KIFANYIKE?

Tags: MARA, TATIZO, NI, NINI?, KILA

JESHI LA POLISI KUTOA MILIONI 100 KWA ATAKAYEWEZESHA KUPATIKANA WAHALIFU WANAOMWAGIA WATU TINDIKALI NI KWAMBA LIMESHINDWA KAZI?

Started by GLOBAL in Maisha. Last reply by mark gibson Nov 30. 84 Replies

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.Jeshi la Polisi…

SIMBA SC WAMTUPIA VIRAGO JUMA KASEJA

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson Nov 22. 12 Replies

TIMU ya Simba SC leo imetangaza rasmi kuachana na mlinda mlango wake mahiri, Juma…

JE, NI SAHII KWA JESHI LA POLISI KULIPUA MABOMU WAKATI WANANCHI WAKIAGA MIILI YA WENZAO?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson Nov 23. 36 Replies

Juzi (Jumanne) polisi walilipua mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa wamekusanyika katika Viwanja vya Soweto jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili ya wenzao watatu waliopoteza maisha katika…

TOP NEWS WEEK HII

© 2014   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }