Kajala Masanja na mumewe Faraji Agustino siku ya harusi yao.

Stori: Musa Mateja

STAA wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja amewaacha midomo wazi marafiki zake waliomtembelea katika Gereza la Segerea, Dar es Salaam hivi karibuni baada ya kufunguka kuwa, anataka talaka yake kutoka kwa mumewe Faraji Agustino.
Chanzo cha kuaminika cha Ijumaa Wikienda kilichokuwa miongoni mwa mashosti zake waliofika gerezani kumtembelea mwishoni mwa wiki iliyopita (jina kapuni) kilitonya kuwa, wakiwa hapo Kajala alidai akifanikiwa kushinda kesi inayomkabili hatahitaji tena kurudi kwa mumewe huyo ambaye wameshitakiwa pamoja.
“Mwenyewe alieleza kuwa, ndoa ndiyo iliyomfikisha hapo alipo kiasi kwamba anajuta kuolewa, akasema bora apewe talaka yake.
“Tulijaribu kumsihi asiwe na mawazo hayo kwa kuwa kila kinachotokea ni mipango ya Mungu lakini alionekana kushupalia hilo la talaka akidai isingekuwa kuolewa na mwanaume huyo, sasa hivi angekuwa anakula bata mtaani,” alidai mtoa habari huyo.
Kilieleza kuwa, siku hiyo Kajala aliwatoa watu machozi baada ya kueleza kuwa, ndoa yake imemuingiza kwenye matatizo ambayo yamemfanya ashindwe kwenda kushuhudia mazishi ya Kanumba, msanii aliyemfanya asimame kwenye filamu.
Kajala na mumewe wanaendelea kusota kwenye Gereza la Segerea wakikabiliwa na kesi ya kutakatisha fedha haramu.

Views: 9090

Tags: ijumaawikienda11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by neema molleli on June 11, 2012 at 4:37pm

pole sana dadangu hayo ni mapito tu ya katika maisha

Comment by meggie impostra on May 26, 2012 at 12:28pm

WE JISHAUE TU UMUACHE HANDSOME KAMA HUYOOO WENZIO WAJE MWAMCHUKUE BADAE UJE ULIEEEE SHAURI YAKOOO

Comment by meggie impostra on May 26, 2012 at 12:27pm

MATATIZO KTIKA NDOA NI KAWAIDA BI DADA KUWA MVUMILIVU HIYO MITIHANI LAZIMA ITAKUWEPO TU HATA KAMA USINGEKUWA GEREZANIII POLENI SN YATAISHAA TU WALA MSIJALII

Comment by Focus Kunambi on May 23, 2012 at 5:16pm

UNADAI TALAKA YA NINI WAKATI KESI YA KUTAKATISHA FEDHA SI CHINI YA MVUA 10????

Comment by saddam george on May 23, 2012 at 12:05am

umekomaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa eeeeeeeeeeeeeeeh

Comment by Rogers Mwachali on May 22, 2012 at 8:36am
Kumbuka ulikula kiapo ndoa huwa haitenganishwi na kitu chochote isipokuwa kifo pekee vumilia mama.
Comment by lumi mwandelile on May 21, 2012 at 3:43pm

“Mimi, KAJALA  na kuchukua wewe, FARAJI  kuwa MUME wangu naahidi KUISHI na wewe katika hali zote, SHIDA AU RAHA katika magonjwa na afya. Nikupende na kukuheshimu siku zote za maisha yangu HADI KIFO KITUTENGANISHE”

Comment by Mija Mihayo on May 21, 2012 at 3:36pm

talaka sio solution ina maana hukumpenda mumeo kwa dhati

Comment by Man KKK on May 21, 2012 at 3:14pm

yah sio mnaona wanaume wana ela mnashoboka tu hujui zinapotokea, ila kwa kua mlitumia wote basi lipia kwa jasho pia...pole dada

Comment by DORAH FREDY on May 21, 2012 at 3:14pm

Pole dada kajala hayo ni maisha tu wala usivunje ndoa yako endelea na ndoa ni mapito tu

UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

Latest Activity

jus ctobeli posted a status
5 minutes ago
Ruth D. Fay posted a status
10 minutes ago
vanhelsing posted a status
23 minutes ago
vanhelsing posted a status
23 minutes ago
vanhelsing posted a status
24 minutes ago
vanhelsing posted a status
24 minutes ago
vanhelsing posted a status
25 minutes ago
vanhelsing posted a status
25 minutes ago
vanhelsing posted a status
26 minutes ago
jus ctobeli posted a status
27 minutes ago
vanhelsing posted a status
27 minutes ago
vanhelsing posted a status
27 minutes ago

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }