Rehema Chalamila 'Ray C' akimshukuru Rais Kikwete kwa msaada wa matibabu. (Picha na Ikulu)

-RAIS KIKWETE, WALIKUBALI RAY C AFE, MAGAZETI PENDWA YAKAGOMA
ASSALAM aleykum mheshimiwa. Pamoja na majukumu mengi yanayokukabili, nimeona ni nafasi yangu nzuri kuwasiliana nawe na ninajua utaisoma barua hii kwa sababu kadhaa ambazo nitazieleza hapa chini.

Najua sina haja ya kukuambia nipo salama na nina hofu na wewe uliye mbali na upeo wangu, lakini acha niende moja kwa moja kuanza kukigusa kilichonifanya niandike barua hii.

Wiki iliyopita wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania, nilikusikia ukiwaambia Watanzania maneno haya, “mwenye macho haambiwi tazama”, nakubaliana nawe kwa kuwa angalau namshukuru Mwenyezi Mungu amenipa macho yanayoweza kuona.

Serikali yako haiwezi kuwa malaika kama ilivyo kwako wewe ambaye pia si malaika. Ndiyo maana unakosea, una upungufu na hiyo ni sifa ya uanadamu. Lakini kwa macho yangu bila ya kujali au kusubiri niambiwe nitazame, naona vitu vingi sana ambavyo serikali yako imejitahidi kuvifanya.

Kikubwa ambacho kinatakiwa mheshimiwa, lazima ukubali una kundi la watu wengi ambao umewaamini lakini wao wameamua kuendesha matumbo yao na familia zao na si wananchi wa Tanzania. Nakukumbusha tu kwa kuwa najua unaelewa “mwenye macho, haambiwi tazama!”

Dhumuni la barua hii ni kukueleza kuhusiana na mwanadada Rehema Chalamila ‘Ray C’, hakika umeonyesha unajali na umeonyesha wewe ni rais wa watu. Angekuwa mwingine angeamua kunyamaza na mwanadada huyo angepotea, hakuna ambaye angejali.

Lakini najua leo, wapo watakaokulaumu na kutaka kulalama kwamba mbona wengine haujawasaidia? Wala usijali kwa kuwa hauwezi kuwafurahisha watu wote, ingawa mimi nataka kutumia nafasi hii kukukumbusha angalau kidogo.

Nakukumbusha mheshimiwa kwamba, umeyasahau magazeti pendwa, hasa yanayochapishwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd, ambayo ndiyo yalifanya kazi kubwa ya kumfikisha Ray C mikononi mwako hadi ukagundua ukubwa wa tatizo lake.

Lakini hata wakati wa utoaji shukurani, nilifikiri Ray C na mama yake wangeweza kuyashukuru magazeti pendwa ya Global Publishers ambayo ndiyo yalikuwa ya kwanza kuanika matatizo hayo makubwa ya Ray C hadi wewe ukachukua hatua.

Wakati unachukua hatua, nilifurahi sana. Unajua nini kilinifurahisha mheshimiwa? Baada ya kugundua nawe ni msomaji wa magazeti pendwa ya Global Publishers. Wapo wanaoyadharau, sasa kama hadi wewe unasoma, huyo mwenye jeuri ya dharau ni nani? Hapo nakupa tano.

Sitaki kulazimisha magazeti pendwa yapewe tuzo, ila nakumbusha tu ili kuonyesha kazi ya Watanzania halisi kama hawa waliomo Global Publishers inathaminiwa. Maana nakumbuka mara baada ya stori na picha za kwanza za Ray C akiwa amelala kwenye bajaji, wapo watangazaji wa redio ya Clouds walishambulia magazeti ya Global, eti yametumwa.

Ajabu nao leo kila siku wanazungumzia hali ya Ray C! Nahisi baada ya mwanadada huyo kufika kwako, watakuwa hawana la kusema na kama ni aibu wanayo na wameihifadhi, wanaitumia taratibu kwa faida zao. Walikuwa wanajua matatizo yake, wakaona kuyaficha ndiyo kitu kizuri, walikubali afe. Magazeti pendwa yakakataa na kumfikisha mikononi mwako.

Wapo watu wa Clouds walielewa hilo lakini hata niliposikia wanazungumza na kupongeza, pia walitaja magazeti bila ya kusema ni ya Global Publishers ambayo ni maarufu kama udaku.

Mheshimiwa, picha za Ray C akiwa teja kamili kwenye bajaji, sisi vijana huku mtaani tunaita kubembea, hakika zilikuwa zinatia huzuni sana. Naamini ndiyo maana zilikugusa, ila nikuambie mchezo ulikuwa mgumu hadi kuzipata na ilikuwa kazi ya zaidi ya miezi kadhaa hadi kumvizia akiwa vile.

Ndiyo maana wengine wakashindwa kwa kuwa taarifa zao ni za kwenye vikaratasi maarufu kama ‘press realize’, au mkiwaalika kwenye ‘press conference’ ambako mara nyingi wanatoka na ‘lead story’ halafu wanapewa sifa za kuwa ‘serious’.

Mnaowaamini wako ‘siriaz’ hawafanyi kazi ya habari za uchunguzi, lakini kuna taarifa nyingi zinaanzia Global Publishers na baada ya hapo mnaowaona wako makini wanazidakia lakini nao kwa ujanja hawataki kuipongeza au hata kuitaja GPL.

Wasaidizi wako nao kama umewaita waandishi, hata siku moja hawataki kuwaalika waandishi au wahariri kutoka GPL, lakini nashangaa ilikuwaje safari hii hadi ‘newspaper’ likapenya na kukufikia halafu ukamuona Ray C alivyokuwa akiteketea.

Silazimishi mualiko, sina haja ya kusisitiza kuhusiana na tuzo kwa kuwa niliamua kujitoa baada ya kugundua hadi wale wanaozitoa wanaangalia waandishi kutoka serikalini, redio na magazeti ya chama au yale yanayoitwa yako ‘siriaz’ kwa habari za press conference!

Hapa tuna Championi, hili unalolisoma sasa. ‘Linakimbiza’ (kwa kuwa ni mwanampira wa kikapu najua unaelewa neno hili) vibaya, yapo yanayojiita magazeti kongwe, yamepotezwa kabisa na inafikia tunauza hadi magazeti mara tatu yao, lakini wanajaribu kutufunika kwa kisingizio cha ‘siriaz’.

Nimefanya kazi Habari Corporation (Dimba-halafu nikawa mmoja wa waanzilishi wa Bingwa), nikahamia Mwananchi (nilikuwa Mwanaspoti), acha mheshimiwa, kule nilikimbiza vibaya, wasomaji ni mashahidi wangu.

Ila hakuna sehemu niliyofanya kazi na watu wanaojituma, wabunifu na wenye uwezo kama hapa Championi, ndiyo maana unaona habari kama za Ray C zinatokea hapa nilipo.

Najua siku moja tutakutana (Mungu akipenda), sina haja ya kumueleza kitu Ridhwani ambaye nakutana naye mara kibao, pia ni mshikaji wangu, ila nikikuona nitakuhadithia zaidi ili ujue Global Publishers wanayolazimika kuibeza ni zaidi ya unavyoifahamu na imefanya mengi makubwa. Hilo la Ray C ni asilimia moja tu.

Natamani kuendelea kuandika, lakini najua una majukumu mengi kwa kuwa Tanzania ni kubwa. Acha nikupe nafasi, ila nakukumbusha mheshimiwa na najua utakubaliana nami kwamba kazi ya Global Publishers ingekuwa inafanywa na kampuni ya Wazungu kutoka Ulaya au Wakenya, basi Watanzania wenzangu wangesifia na kujikomba kweli.
Tukionana, tutachambua zaidi.
Heshima na salamu,

SALEH ALLY ‘Jembe’.

Views: 2585

Tags: championi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by anna msuya on January 2, 2013 at 11:47am

ubarikiwe Mheshimiwa una roho ya huruma sana jitahidi kuwafikia na wengine kwani wako wengi kama huyo binti pia wazazi wao wanauchungu sana kama mama wa Rey c ila uwezo hawana sijui utawasaidiaje hawa vijana

Comment by gueen on December 23, 2012 at 4:00pm

yani baba kikwete nakupa tano

Comment by gueen on December 23, 2012 at 3:59pm

Nakufagilia kikwete.

Comment by gueen on December 23, 2012 at 3:56pm

nakufagilia baba kikwete

Comment by mnasa mohd on December 16, 2012 at 8:52pm

sasa achana na hayo madude siunaana umetoka mbali na kama hujafahamu basi tena

Comment by Abdallah said on December 16, 2012 at 10:11am

Mwenye macho hambiwi soma naamini wamesoma na kukuelewa sisi tunakukubali

Comment by Focus Kunambi on December 15, 2012 at 9:36pm

JK kamuona RC tu, wagonjwa wengine mahututi, na wabwia unga hakuwaona????????

Comment by Jodat King on December 15, 2012 at 6:19pm
Ni kweli kuuza na kubwia madawa ya kulevya yote ni makosa ni sawa na kusema mtoa rushwa na mpokeaji rushwa wote wanamakosa!!
Comment by Hashim Yahya Settembo on December 15, 2012 at 6:11pm

Nakupa tano Bro

Comment by Hashim Yahya Settembo on December 15, 2012 at 6:10pm

Nakupa tano Bro

ADVERTISEMENT


Advertisement

 

Forum

KIPIGO CHA BAO 2-1 KWA MAN UTD, KOSA LA MWAMUZI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Mohammed Mar 26. 6 Replies

JE, NI KWELI KWAMBA KIPIGO CHA BAO 2-1 ILICHOKIPATA MAN UTD KUTOKA KWA REAL MADRID USIKU WA KUAMKIA LEO LAWAMA ZOTE ZIMWENDEE MWAMUZI WA MCHEZO AU MAN UTD WAJILAUMU WENYEWE? TUPE MAONI YAKO!!!

HALI INAYOENDELEA BUNGENI, SPIKA NA NAIBU WAKE WAMESHINDWA KUONGOZA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Ali Abdalla Ali Apr 22. 20 Replies

Tumeshuhudia kwa siku za hivi karibuni hali halisi iliyokuwa inatokea katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, kwa hali hii ni ishara kuwa Spika na Naibu wake washindwa kuliongoza bunge hilo?

VURUGU ZA CCM NA CHADEMA KUGOMBEA MLINGOTI WA BENDERA DODOMA, NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Phinehas Rishiansia Kileo May 3. 6 Replies

Wafuasi wa CCM wakimshambulia mfuasi wa Chadema mkoani Dodoma…

Tags: BENDERA, WA, DODOMA, NANI, KULAUMIWA?

VURUGU ZINAZOENDELEA HAPA NCHINI NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by NELSON UVAMBE on Monday. 27 Replies

HIVI KARIBUNI KUMEKUWEPO UPOTEVU WA AMANI HAPA NCHINI PAMOJA NA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI. MKOANI KAGERA WANANCHI WENYE HASIRA WALIWAUA POLISI, IJUMAA ILIYOPITA WAKULIMA NA WAFUGAJI HUKO WILAYANI KILOSA WALIZUA VURUGU NA KUFUNGA BARABARA,…

MRISHO NGASSA KUPELEKWA SIMBA SC BILA RIDHAA YAKE, JE NI HALALI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Domino Bagambisa Jan 21. 17 Replies

Kiungo hatari wa Azam FC, Mrisho Ngassa leo amepelekwa Simba SC kwa mkopo na timu yake…

Tags: SOKA

hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Started by Gysper in Siasa. Last reply by Jamal amor May 9. 24 Replies

 hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Kauli Ya JK kuwa Mauaji ya Arusha ni "Bahati Mbaya"

Started by Kulikoni Ughaibuni in Siasa. Last reply by richardngeze Feb 12. 12 Replies

Tanzania tuna tatizo kubwa.Hakuna haja ya kunyoosheana vidole as to nani amechangia tatizo hilo bali cha muhimu na haraka ni namna tutakavyoweza kutatua tatizo hili.Nisimung'unye maneno: tatizo kubwa linaloikabili ni kuwa na Rais ambaye takriban…

© 2013   Created by Global Publishers.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service