Na Erick Evarist
Ishu ya mastaa wawili wa kike Bongo, Judith Wambura ‘Jide’ na Jacqueline Patric ‘Jack’ kujipanga namna mazishi yao wanavyotaka yawe watakapoaga dunia, imezua kizaazaa ikielezwa kuwa wana pepo mbaya wa kifo.
Mbali na watu wa kawaida kwenye jamii kulaani kitendo hicho, mtumishi wa Mungu aliyejitambulisha kwa jina la Faustine Mwijage Kamugisha wa jijini Dar aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa amesikitishwa na wanadada hao akidai kuwa ni kinyume na matakwa ya Mungu hivyo wanaongozwa na pepo wa kishetani.
“Huku ni kumkufuru Mungu, wameingiwa na pepo wa shetani, kujipangia mazishi maana yake unajiwekea mipango ya kitu ambacho huna uwezo nacho, huko ni kutenda dhambi bila kujua.
“Kifo ni lazima kwa mwanadamu, lakini huwezi kujipangia kifo wala mazishi yako hata siku moja,” alisema mchungaji huyo na kuongeza:
“Wasome Yeremia 17:9, maandiko yanasema, Moyo huwa mdanganyifu. Hapo ina maana hao wameshadanganywa na shetani na ni vigumu wao kugundua kwani shetani naye ana nguvu zake hivyo wanahitaji maombi.”
Hivi karibuni Jide ambaye ni mwanamuziki mkubwa Bongo na Jack (modo maarufu), waliweka bayana namna na ratiba ya mazishi yao pindi watakapokufa ambapo gazeti hili limesheheni maoni ya watu mbalimbali waliokosoa na kulaani ishu hiyo.

Views: 3395

Tags: ijumaawikienda11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by abdullah Nassor on April 22, 2012 at 3:59pm

hawana lolote ila wanachotaka labda walikuwa wamesahaulika na magazeti ndio maana wanataka kujitokeza

hovyo kama kanda mbili za msalani

 

Comment by Mamy Shaluathu on March 30, 2012 at 2:10pm

Labda wameoteshwa siku ya kufa kwao.

Comment by Chidy Bizzy on March 30, 2012 at 12:05pm
Yeremia 17..9
Comment by Edwina Edwin on March 30, 2012 at 11:18am

kama una uwezo wa kupanga mazishi yako panga tu, watu wanapanga harusi na mchumba hawana sasa tofauti hiko wapi..  tatizo tunaogopa vifo kweli.. nunua jeneza utakalo ,ukifa hata ukiwa na pesa nyingi, ndugu wenye tamaa wanaweza wakakuchongea jeneza la mbao za mti bei ndogo. ili wabanie pesa.. wana sababu zao hao ambao sisi hatujui na hata hao walioandika hawajui.. pengine ni wagonjwa tayari wanaona mauti inasogelea..pengine waliuza roho zao kwa shetani in return of u star na muda wa kulipa roho zao umefika.. hawa mastar wana siri nyingi sana na umaarufu wao... sisi ni kuomba tu ..

Comment by ridhiwani gambalela on March 27, 2012 at 5:04pm

huko kote ni kuta futa umaruufu

Comment by meggie impostra on March 27, 2012 at 1:31pm

sijaona ubaya mtu kupanga mazishi yake jmnii ni jambo la kawaida tu

Comment by TZ on March 27, 2012 at 6:51am

HAWANA PEPO MCHUNGAJI ILA TU KAMA NA WEWE UNATAKA UPATE KITITA CHAKO KWAO SAWA. HAWA NI WATU WASIO NA AKILI AU KWA LUGHA NYENGINE NI WENDAWAZIMU WASIO NA TIBA. HUWEZI KUJIPANGIA MZIKO KAMA VILE ULIVYOKUWA HUWEZI KUPANGIA KIZAZI KIWEJE NA KIJE VP KATIKA DUNIA.

Comment by Simoma on March 27, 2012 at 1:47am

Sioni kosa walilolifanya hawa kina dada hadi walaniwe kiasi hicho, kwanini tunakwepa ukweli usiokwepeka, ila tu ninacho waomba hawa kina dada haya wanayoyafanya yasiwe ya kutaka kujiongezea umarufu tu, lakini kama kweli wamefanya haya kwa moyo haswaa na kuyatekeleza, basi mimi nawapongeza kwa hilo, na hii inaonyesha kiasi gani hawa kina dada wanavyojijali na kukumbuka kwamba iko siku watakuja kufa, na hivi sasa wanapesa kwanini wasijiandae na maisha yao ya mwisho. wangapi walikua na uwezo hawakua na malengo ya baadae wakaja kusumbua ndugu zao.

Comment by john bosco on March 27, 2012 at 1:40am

kifo ni haki ya mtu kama wanataka kufa mtawazuia kama nani? wengine wananunua makaburi hata kabla ya vifo vyao. ulizeni western countries

Comment by Mawazo Katota on March 26, 2012 at 9:22pm

Hawa ni wagonjwa wanatumia mihadarati. Na ni kweli mtu anayetumia madawa ya kulevya hafikiri vizuri. Mchungaji endelea kuwaombea mapepo yawatoke

ADVERTISEMENT


Advertisement

 

Forum

KIPIGO CHA BAO 2-1 KWA MAN UTD, KOSA LA MWAMUZI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Mohammed Mar 26. 6 Replies

JE, NI KWELI KWAMBA KIPIGO CHA BAO 2-1 ILICHOKIPATA MAN UTD KUTOKA KWA REAL MADRID USIKU WA KUAMKIA LEO LAWAMA ZOTE ZIMWENDEE MWAMUZI WA MCHEZO AU MAN UTD WAJILAUMU WENYEWE? TUPE MAONI YAKO!!!

HALI INAYOENDELEA BUNGENI, SPIKA NA NAIBU WAKE WAMESHINDWA KUONGOZA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Ali Abdalla Ali Apr 22. 20 Replies

Tumeshuhudia kwa siku za hivi karibuni hali halisi iliyokuwa inatokea katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, kwa hali hii ni ishara kuwa Spika na Naibu wake washindwa kuliongoza bunge hilo?

VURUGU ZA CCM NA CHADEMA KUGOMBEA MLINGOTI WA BENDERA DODOMA, NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Phinehas Rishiansia Kileo May 3. 6 Replies

Wafuasi wa CCM wakimshambulia mfuasi wa Chadema mkoani Dodoma…

Tags: BENDERA, WA, DODOMA, NANI, KULAUMIWA?

VURUGU ZINAZOENDELEA HAPA NCHINI NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by NELSON UVAMBE on Monday. 27 Replies

HIVI KARIBUNI KUMEKUWEPO UPOTEVU WA AMANI HAPA NCHINI PAMOJA NA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI. MKOANI KAGERA WANANCHI WENYE HASIRA WALIWAUA POLISI, IJUMAA ILIYOPITA WAKULIMA NA WAFUGAJI HUKO WILAYANI KILOSA WALIZUA VURUGU NA KUFUNGA BARABARA,…

MRISHO NGASSA KUPELEKWA SIMBA SC BILA RIDHAA YAKE, JE NI HALALI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Domino Bagambisa Jan 21. 17 Replies

Kiungo hatari wa Azam FC, Mrisho Ngassa leo amepelekwa Simba SC kwa mkopo na timu yake…

Tags: SOKA

hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Started by Gysper in Siasa. Last reply by Jamal amor May 9. 24 Replies

 hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Kauli Ya JK kuwa Mauaji ya Arusha ni "Bahati Mbaya"

Started by Kulikoni Ughaibuni in Siasa. Last reply by richardngeze Feb 12. 12 Replies

Tanzania tuna tatizo kubwa.Hakuna haja ya kunyoosheana vidole as to nani amechangia tatizo hilo bali cha muhimu na haraka ni namna tutakavyoweza kutatua tatizo hili.Nisimung'unye maneno: tatizo kubwa linaloikabili ni kuwa na Rais ambaye takriban…

© 2013   Created by Global Publishers.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service