I Want My Dady Back (Nataka Baba Yangu Arudi-58)

ARTHUR akiwa mikononi mwa mzee Mwandambo, alijilaumu sana moyoni mwake, alijiona mpumbavu sana kuamua kurudi Dar badala ya kuendelea kujificha Lindi. Aliamini alishakifikia kifo chake.
Tofauti na matarajio yake, baada ya mzee Mwandambo kuondoka naye, alimuuliza mambo mengi kuhusu historia ya maisha yake, alipogundua kwamba alikuwa yatima, akaamua kumsaidia fedha.

Arthur bila kutegemea kabisa, alisalimika mkononi mwa mzee Mwandambo, akashuka garini akiwa na fedha zake kisha akatafuta usafiri mwingine. Safari ya kuelekea Chanika ikaendelea.
Mzee Mwandambo alikuwa na wasiwasi mwingi sana, alishangazwa na jinsi mwanaye Nicole alivyoonekana kukosa furaha baada ya Arthur kukamatwa. Alihisi kuna kitu kinaendelea ndiyo maana alipoteza furaha ghafla.


Alipomwuliza Nicole, hakuonekana kuwa na jibu lolote, zaidi ya kuonekana kuwa na kigugumuzi kikali huku macho yakiwa yamemkodolea baba yake.
Je, nini kitatokea? SONGA NAYO...

Mimi ni baba yako, tena unatakiwa kufahamu kwamba, nimetangulia kuiona dunia. Hebu niambie ni nini kinaendelea?” mzee Mwandambo akakazia msimamo wa swali lake huku akimwangalia mwanaye usoni.
Nicole alitakiwa kuwa makini sana, jibu la swali aliloulizwa lingeweza kuwa dawa au tatizo zaidi kwa baba yake. Ubongo wake ukafanya kazi kuliko kawaida, akajipa matumaini. Akapiga moyo konde na ghafla akavaa ujasiri.

“Baba sijakuelewa vizuri unachomaanisha.”
“Hivi ina maana hujanisikia au?”
“Baba unazungumzia kuhusu ajali?”
“Ndiyo.”

“Hata wewe naamini ulichanganyikiwa, ndiyo maana ulishuka kwa hasira na kumchukua yule kijana. Kama ilivyo kwako, kwangu pia ilikuwa hivyo hivyo. Sikuwa na amani baada ya kukaribia kumgonga yule kijana.
“Kwa kiasi kikubwa sana nilihisi ulikuwa unataka kumdhuru, ndiyo maana nikapatwa na simanzi ya ghafla moyoni mwangu na kuwa na wasiwasi mwingi, maana nilihisi kwamba ungeweza kumdhuru.”
“Hilo tu!”

“Ndiyo baba.”
“Si kweli.”
“Kama si kweli, sasa ukweli ni upi?”
Mzee Mwandambo alikaa kimya kwa muda, kilipita kimya cha zaidi ya dakika tatu, alipoanza kuzungumza baadaye alikuwa anaongelea kitu kingine kabisa.

“Lakini mwanangu, unaionaje hii shule?”
“Nzuri sana baba. Naona ni nzuri na inavutia sana.”
“Sasa kama ndivyo una sababu gani ya kuhangaika na wapuuzi wasio na maana?”
“Kwa kweli baba sina. Nimeona wazi makosa yangu.”

“Kuona makosa si tija Nicole.”
“...pia nimekubali kubadilika baba. Ni ahadi ambayo hata mama anaijua.”
“Nitafurahi sana ikiwa hivyo mwanangu.”
“Imeshakuwa baba, siwezi kuidhulumu nafsi yangu.”
“Vema. Naona turudi nyumbani sasa.”

“Sawa baba!”
“Vipi kuhusu mtoko wa kesho? Natamani sana niende nanyi mahali.”
“Ni wazo zuri baba.”
“Unapenda wapi?”

“Unanijua vizuri sana baba, ufukweni ni sehemu ambayo moyo wangu huridhika zaidi nikienda.”
“Sawa.”
Hawakukaa sana, walizungumza machache na mafundi, kisha wakaingia kwenye gari na kurejea nyumbani kwao, kisiwani Bongoyo.
***
Mpaka muda huo akiwa amesimama mapokezi, Arthur alikuwa hajaamini kama ni kweli alipona katika mkono wa mzee Mwandambo. Alihisi alipata bahati ya kipekee, maana kwa kiasi kikubwa alitarajia kuingia mikononi mwake.

Alijiandikisha kwenye Gesti hiyo, iliyokuwa ndani ndani kabisa, eneo la Manzese Tip Top. Alitamani sana kumpigia Nicole lakini alishindwa, maana walikubaliana kwamba hatakiwi kumpigia simu mpaka Nicole mwenyewe atakapoamua kufanya hivyo.
Aliingia ndani ya chumba chake na kuanza kutafakari tukio zima lilivyokuwa, akashindwa kuelewa kabisa, kitu pekee alichokifanya kwa wakati ule ilikuwa ni kumshukuru Mungu.

***
Zoezi la kumsaka Arthur mjini Lindi lilifanyika kwa kasi na kwa kutumia mbinu zote bila mafanikio. Ni kama Lindi ilifunikwa na kufunuliwa, lakini Arthur hakupatikana.
Baada ya wiki mbili, Tino na wenzake walirudi kwa mzee Mwandambo na kumweleza namna walivyohangaika lakini bila mafanikio yoyote.
“Umemtafuta vizuri Tino?”

“Sana Chief, kitu ninachotaka kukuambia ni kwamba, Arthur hayupo Lindi, kama angekuwepo lazima tungemtia mkononi.”
“Sawa, achaneni naye kabisa. Hili jalada nimelifunga rasmi.”
“Sawa Chief.”
Tangu hapo mzee Mwandambo aliamua kuacha kumfuatilia Arthur kwa uwazi, lakini kichwani mwake alipanga kumsaka kimya kimya. Ndicho kitu kilichokuwa kichwani mwake.

***
BAADA YA MIAKA MITATU
Arthur aliendelea kuishi katika Gesti ile kwa siri, msaada mkubwa akiwa anaupata kwa Nicole. Aliendelea kuwasiliana na Nicole kwa siri kubwa na mara kadhaa walikuwa wakikutana na kufanya mapenzi bila kugundulika.
Tayari Nicole alikuwa ameshafika kidato cha pili, muhula wa mwisho akikaribia kabisa kuanza kidato cha tatu. Pamoja na umri wake mdogo, alionekana msichana mkamilifu. Alikuwa na kila kitu kinachopaswa kuwa na mwanamke ambaye tayari ana mtoto!

Nicole alibadilika, alikuwa msichana anayejipenda, mwenye maringo na anayejua thamani yake kama msichana. Hata Arthur naye alikuwa na mabadiliko makubwa sana, alikuwa kijana anayevutia sana.
Alivaa vizuri na kula mlo safi, afya yake ikaimarika, pamoja na kwamba alikuwa akiishi katika hofu kuu. Akiwa katika Gesti hiyo anayoishi, alikutana na kijana mmoja aliyeitwa Emmanuel.

Emmanuel alionekana kuvutiwa sana na Arthur. Alikuwa mfanyabishara anayefanya shughuli zake katika nchi za China na Ujerumani. Alifika nchini Tanzania kwa shughuli zake za kibiashara.
Alitamani sana kushirikiana na Arthur. Akaamua kumweleza ukweli.

“Tangu nimekuona hapa, nakuona una kitu cha tofauti kabisa ambacho kama ukisaidiwa unaweza kubadili maisha yako,” Emmanuel akamwambia Arthur.
Arthur akashtuka. Hakutegemea kusikia maneno hayo kutoka kwa mfanyabiashara mkubwa kama Emmanuel. Akakaa sawa akimsikiliza kwa makini.
Je, nini kitaendelea? Usikose kufuatilia katika Gazeti la Championi Ijumaa. 

Views: 2094

Tags: hadithi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by vincent on March 2, 2012 at 2:11pm

haaaahhaaaa kama mimi vile miaka mitatu kwa siri kuu

Comment by Real De' Dear on February 27, 2012 at 1:50pm

wanasema ridhiki ya mbwa iko miguuni.

Comment by hamisi mohamed juma on February 24, 2012 at 5:43pm
Aisee arthur yupo mikononi mwa mpelelezi atakamatwa tu then pesa zitadhulumiwa daah inasikitisha!
Comment by Jamaldin A Issa on February 24, 2012 at 4:36pm
Safi umeokoka sasa
Comment by Emmanuel Mallewo on February 24, 2012 at 12:35am

EMMANUEL atampeleka Arthur nje atakuwa mfanya Biashara mkubwa na atakuja kumwoa Nikole kirahisi

Comment by DORAH FREDY on February 23, 2012 at 2:02pm
ooh Arthur emanuel sasa atakuplekeka pabaya maana utamwamini halafu utamwambia ukweli wako wote kuwa makini sana Arthur halafu usije kusema wewe ni Arthur maana utakufa
Comment by rosetarimo86 on February 23, 2012 at 11:35am

bg hap shigongo

Comment by Kidugwa Ramadhani on February 23, 2012 at 6:38am
Bro Bigg up upo juu
Ila kitu kimmoja Athur amekose ilibidi baada ya hapo amtafute mzee ili apate msaada mzuri na wala asingeweza kumpata. Ona anavyokamatwa kirahisi kwa asimia 90 Emmanuel ni mpelelezi wa mzee mwandambo aaaache ujinga anaenda kukamatwa kizembe saaaanaaaa
Comment by dorice damian nkane on February 23, 2012 at 12:14am

Hofu yangu ni kwa aina na biashara, we emma usimwaribu mkwe wa mwandambo huyo.

Comment by Mawazo Katota on February 22, 2012 at 8:51pm

Inafurahisha


ADVERTISEMENT


TANGAZA HAPA

ADVERTISEMENTS

Latest Activity

GUNZ TRUVADA posted a status
"KUMPA ASIYE KUPA NI SAWA SAWA NA KUTUPA"
12 minutes ago
GUNZ TRUVADA posted a status
"KUMPA ASIYE KUPA NI SAWA SAWA NA KUTUPA"
12 minutes ago
othman Ochu posted a status
"SCENE 1 WAHUSIKA: AMIDU , SHARIFA MAHALI: ZANZIBAR MUDA : JIONI ( WAKIWA WANASHUKA TOKA KATKA BOTI YA JION KUINGIA KATKA MJI WA ZANZI"
9 hours ago
Priscus Adelard shared GLOBAL's blog post on Facebook
9 hours ago
mrembo commented on julius manning's photo
Thumbnail

Mtanzania huru

"pole sana usijali iko siku mungu atakujaalia mungu hamtupi mja wake"
10 hours ago
mrembo commented on Sili Silali's photo
Thumbnail

Duh!

"mama mzima hayawani mavazi gani hayo takupa mfano chungwa likiwa halijamenywa unatamani ulile…"
10 hours ago
kaka commented on Ali Amur Ali's video
Thumbnail

AZIMIO LA KUANGAMIZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE

"hapo ni kina dada kutua comment zao"
10 hours ago
Gaston Kayombo commented on Ali Amur Ali's video
12 hours ago
roylicious and Jackson Jacob are now friends
12 hours ago
babu wa loliondo (cup) updated their profile
12 hours ago
julius manning commented on julius manning's photo
Thumbnail

vijana 2016 itakuwa hivi

"@furaha mimi ni kikongwe hayo ni kazi kwako."
13 hours ago
Masalu Mayeji Many'hasimha shared GLOBAL's blog post on Facebook
13 hours ago

© 2012  

Designed & Developed by
G5 CLICK COMPANY.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

How to make a Website