I Want My Dady Back (Nataka Baba Yangu Arudi-53)

MZEE Mwandambo akiwa ofisini kwake akiwaza namna ya kumpata Arthur, anapokea ujumbe kwa namba asiyoijua ukimueleza kila anachokifanya. Cha kushangaza, ulimwambia kuwa Arthur alikuwa amejificha Lindi.
Alihisi kuchanganyikiwa kabisa. Kitu cha kwanza kufanya ilikuwa ni kumpigia simu Ben na kumwuliza kama kuna mtu aliyewaona wakati wakiwatosa Zanzan na Peter majini. Alipomhakikishia kuwa hakuna, alimwambia kwamba aangalie wenzake wanaweza kuwa wamevujisha siri hiyo.

Baada ya kumaliza na Ben, akampigia simu Tino na kumweleza kila kitu kuhusu ujumbe aliotumiwa na mtu asiyemfahamu. Pamoja na kwamba walikuwa na mambo mengi ya kuhisi, walikubaliana vijana wao wagawane, wengine waende Lindi na wengine wabaki Dar es Salaam.
Siku iliyofuata tu, asubuhi na mapema. Kazi ikaanza. Kweli vijana waligawanyika, wengine Dar wengine Lindi. Msako wa Arthur ukaanza.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO...

ULIKUWa usiku mgumu kutoka kawaida, usingizi ulikataa kabisa kumjia mzee Mwandambo. Aliishia kugalagala kitandani. Pamoja na fedha zake, fumbo la wapi alipo Arthur lilimchanganya sana.
Alitamani sana kukutana na kijana huyo, hakutaka kuamini kirahisi kuwa alishindwa kabisa kumtia mikononi mwake. Siku zote aliamini kuwa fedha ni kila kitu katika maisha, lakini siku hiyo kwa mara ya kwanza alianza kuhisi kuwa kumbe si chochote!

Mkewe alishuhudia kila kitu, aliumia sana kumuona mumewe akikesha wakati yeye akiishia katika usingizi mzito. Aliamka na kukaa kitako kitandani, kisha akamgusa mumewe.
“Unasemaje?” mzee Mwandambo akauliza.
“Vipi mume wangu, kuna tatizo?”
“Hapana, nipo sawa.”

“Si kweli baba Nicole, mimi si mgeni kwako. Nakufahamu vizuri sana. Ukiwa haupo sawa ni rahisi sana kujua. Tafadhali naomba uniambie, nini shida yako?”
“Mke wangu, nipo sawa.”
“Najua unachowaza, lakini hupaswi kufikiria sana.”

“Wewe unaona madogo siyo?”
“Lakini yameshatokea.”
“Sikia wewe mwanamke, nakuambia uwe makini na ninakuomba sana, sana, sana, zungumza na mwanao. Mimi sitaki haya mambo yaendelee kwenye familia yangu.”
“Nitaongea naye mume wangu, basi pumzika, kesho una majukumu makubwa sana ofisini.”

“Hata kama, kumbuka zile ni kampuni zangu, hakuna aliye juu yangu, ninaweza kuamua kwenda au nisiende na kazi zikaendelea kama kawaida.”
“Ni kweli baba, lakini kesho una kikao na Bodi ya Wakurugenzi...najua utakuwa umesahau!”
“Daaah! Sikuwa na wazo hilo kabisa. Ahsante sana kwa kunikumbusha mke wangu. Ni kesho saa nne kamili asubuhi, makao makuu.”
“Ndiyo!”
“Basi tulale mama, lakini tafadhali sana zungumza na mwanao.”

“Sawa nimekuelewa mume wangu. Nitahakikisha nazungumza naye, naamini atanielewa.”
“Iwe hivyo, mtoto wa kike ni wa mama, angekuwa mvulana ningejua cha kumfanya.”
“Sawa mume wangu, nakuahidi kuzungumza naye.”
Wakazima taa na kulala.

***
Woga dhidi ya baba yake uliongezeka siku hadi siku, siku hiyo aliamka mapema sana kwa ajili ya kuwahi shuleni, pamoja na wazo lake la kuwahi, alitaka kumkwepa baba yake. Hakutaka kukutanisha naye uso.
Baada ya kujiandaa kikamilifu, akatoka akiwa na begi lake. Alipofika sebuleni, akakutana na mama yake.
“Shikamoo mama.”
“Marhaba, habari za asubuhi binti yangu?”

“Njema mama, acha niwahi shule.”
“Huna lolote mtoto wa kike. Tangu lini ukawahi shuleni kiasi hiki? Najua unamkimbia baba yako. Sikia nikuambie kumkimbia hakuna maana yoyote kama hutajirekebisha. Hebu rudi chumbani kwako tuzungumze kidogo, nahitaji kuongea na wewe.”
“Kweli mama nawahi.”

“Rudi chumbani kwako,” mama yake akasema kwa sauti ya amri kidogo.
Nicole akarudi, mama yake akamfuata nyuma. Walikuwa wawili tu chumbani, mama yake akionekana kuwa na jambo la muhimu sana la kuzungumza naye.
“Hali si nzuri, nadhani unafahamu kwamba Zanzan na Peter wamejinyonga na juzi usiku wametoshwa baharini. Kama hiyo haitoshi baba yako bado anamfuatilia Arthur, matatizo yote haya unayasababisha wewe.

“Kuna wengine hawana makosa, lakini kwa sababu yako unawababishia matatizo. Mwanangu achana na dunia, haya mambo utayakuta tu. Haraka ya nini?”
“Sawa mama nimekuelewa.”
“Naomba uwe makini, sasa hivi hakuna amani hapa nyumbani, yote ni kwa sababu yako. Wewe mwenyewe umekuwa ukirukaruka tu, kila wakati unaishi kwa mashaka, kwa nini iwe hivyo? Hebu jitahidi kuwa na nidhamu mwanangu.”
“Mama nimekuelewa mama yangu, sitarudia tena.”

“Kwa hiyo ni kweli kuhusu huyo Arthur wako?”
“Ni kweli mama, lakini nimekoma. Sina sababu ya kukuficha mama yangu.”
“Ahsante kwa kuniambia ukweli, lakini nataka uachane kabisa na hii tabia, wewe bado mdogo, muda bado sana. Hata hivyo muda ukifika unataka kuwa makini kufanya uchaguzi, achana na watu wasio na dira.
“Baba yako ana utajiri, familia ina heshima na fedha nyingi, lazima uolewe na mtu anayefanana na hadhi yako, si kukurupukia wapuuzi ambao hawana maana. Umenielewa mama?”

“Nimekuelewa mama.”
“Unaweza kuwahi shule sasa.”
“Ahsante sana.”
Nicole akatoka nje, alipokutana na mfanyakazi mpya aitwaye Binamu, wakaongozana hadi kwenye boti, safari ya kuvuka ikaanza. Walipotia nanga, walishuka na kuingia kwenye gari kuelekea shuleni, kama kawaida dereva alikuwa ni Nicole.

***
Shuleni, muda wa mapumziko ulipofika, Nicole alikuwa akizungumza na rafiki yake kipenzi Naomi. Yeye ndiye anayemfundisha mambo yote hayo ya mapenzi. Ndiye rafiki waliyeshibana ambaye anaweza kumweleza kila kitu.
“Hivi Zanzan na Peter waliishia wapi?” Naomi akamwuliza Nicole.
“Mwenzangu we acha tu, una kifua nikupe mchapo?”
“Sana.”

“Walijinyonga bwana.”
“Ilikuwaje?”
“Walifungiwa kwenye chumba cha mateso, huko ndipo walipoamua kujiua kwa mashati yao.”
“Mh! Sasa walitolewaje?”
“Walitoswa baharini usiku.”

“Mh! Nicole umewasababishia wenzio matatizo. Vipi kuhusu Arthur.”
“Hili ndiyo unatakuwa kufanya siri ya ndani ya moyo wako kabisa.”
“Usijali niambie.”
“Ametorokea Lindi.”

“Kazi ipo...”
“Kwa nini?” Nicole akauliza, lakini kabla hajajibu kengelea ya kurudi darasani ikalia.
Wakakatisha mazungumzo.

Je, nini kitatokea? Usikose kufuatilia katika Gazeti la Championi Jumatatu.

Views: 1934

Tags: hadithi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by Real De' Dear on February 24, 2012 at 9:27am

mh! wht next

Comment by lumi mwandelile on February 13, 2012 at 9:50am

nzuri sana

Comment by faisalone on February 12, 2012 at 8:30pm

da ila haina mvuto kivile, ki2 deadly treasure

Comment by Anna Andrew Mwakasita on February 11, 2012 at 12:53pm

naomi atakuwa ndo mnafki

Comment by Jamal Aadamu on February 11, 2012 at 9:11am
Hawa watoto wawenye nazo taabu tupu
Comment by Kakytee The Director on February 11, 2012 at 8:34am
Nyie kweli akili zenu hazina akili, mwamuona naomi ndio kwanza apewa izo taarifa hapo na nicole, sasa atawezaje kugundua? Na anawezaje kujua km zanzan wametoswa baharini? Tisizinguane bhanaa, hamjui kutabiri yakhee, msinione mie natabiri halafu napatia, mkaona ni kazi rahisi hua naumiza kichwa sana tu.
Comment by Mawazo Katota on February 11, 2012 at 12:50am

Naomi mnoko

Comment by Yohana Joseph on February 10, 2012 at 9:40pm
kazi kwelkweli da!.
Comment by HAPPINESS MARCEL MASSAWE on February 10, 2012 at 9:04pm

Weee mtoto wewe unahatari kubwa sana

Comment by Daudi on February 10, 2012 at 8:56pm

Ni fupi sana


ADVERTISEMENT


TANGAZA HAPA

ADVERTISEMENTS

Latest Activity

GUNZ TRUVADA posted a status
"KUMPA ASIYE KUPA NI SAWA SAWA NA KUTUPA"
4 minutes ago
GUNZ TRUVADA posted a status
"KUMPA ASIYE KUPA NI SAWA SAWA NA KUTUPA"
4 minutes ago
othman Ochu posted a status
"SCENE 1 WAHUSIKA: AMIDU , SHARIFA MAHALI: ZANZIBAR MUDA : JIONI ( WAKIWA WANASHUKA TOKA KATKA BOTI YA JION KUINGIA KATKA MJI WA ZANZI"
9 hours ago
Priscus Adelard shared GLOBAL's blog post on Facebook
9 hours ago
mrembo commented on julius manning's photo
Thumbnail

Mtanzania huru

"pole sana usijali iko siku mungu atakujaalia mungu hamtupi mja wake"
10 hours ago
mrembo commented on Sili Silali's photo
Thumbnail

Duh!

"mama mzima hayawani mavazi gani hayo takupa mfano chungwa likiwa halijamenywa unatamani ulile…"
10 hours ago
kaka commented on Ali Amur Ali's video
Thumbnail

AZIMIO LA KUANGAMIZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE

"hapo ni kina dada kutua comment zao"
10 hours ago
Gaston Kayombo commented on Ali Amur Ali's video
12 hours ago
roylicious and Jackson Jacob are now friends
12 hours ago
babu wa loliondo (cup) updated their profile
12 hours ago
julius manning commented on julius manning's photo
Thumbnail

vijana 2016 itakuwa hivi

"@furaha mimi ni kikongwe hayo ni kazi kwako."
13 hours ago
Masalu Mayeji Many'hasimha shared GLOBAL's blog post on Facebook
13 hours ago

© 2012  

Designed & Developed by
G5 CLICK COMPANY.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

How to make a Website