HEART ATTACK (SHAMBULIO LA MOYO) - 3

ILIPOISHIA:
“Vipi? Umefanikiwa kumpata ndugu yako?”
“Nimemkosa kaka yangu, hapa nilipo nimechanganyikiwa hata sijui pa kuanzia, naomba msaada wako tafadhali nipate sehemu ya kulala kesho nitajua cha kufanya,” alisema Matilda huku akitua begi lake mbele ya Brighton.
SASA ENDELEA…

Brighton alifikiria kwa kina ombi la Matilda, akajikuta akishindwa kuamua nini cha kufanya. Alifikiria kuwa endapo atamchukua msichana huyo na kumpeleka nyumbani kwake, nini kitatokea? Alipofikiria kuwa atafute gesti na kumpangishia chumba mpaka asubuhi pia alikwama kwani hakuwa na fedha za kutosha na siku hiyo alitoa sehemu kubwa ya fedha za mauzo na kununua wino wa kompyuta.
“Mbona umeduwaa,” Matilda alimuuliza Brighton swali lililomshtua na kumtoa kwenye dimbwi la mawazo alilokuwa amezama ndani yake, akashtuka na kufikicha macho yake vizuri.
“Vipi, uko sawa?”
“Nipo sawa, nimeduwaa kwa sababu sijui hata nikusaidieje,” alisema Brighton kwa kubabaika. Kazi ya kufunga ofisi aliisitisha kwa muda, Matilda akamuuliza swali alilolijibu bila kujiuliza mara mbilimbili.
“Kwani wewe unasihi na nani?”
“Peke yangu,” alijibu Brigthon.
“Basi nitalala hata chini, mi nataka sehemu ya kujisitiri tu,” alisema Matilda, safari hii akiwa amemsogelea sana Brighton, akawa anaongea kwa sauti ya upole kuwa asimfikirie vibaya kwani anachotaka yeye ni sehemu ya kujihifadhi tu, kukishapambazuka atajua nini cha kufanya.
Brighton alishusha pumzi ndefu na kuamua kupiga moyo konde, akamwambia Matilda kuwa amsubiri amalizie kufunga ofisi halafu atajua nini cha kufanya. Msichana huyo akakaa pembeni huku akimtazama sana Brighton. Alipomaliza kufunga ofisi na kukabidhi funguo kwa mlinzi, Brighton alimsaidia Matilda kubeba begi lake mpaka kwenye kituo cha daladala, Posta.
Muda mfupi baadaye, walipanda kwenye daladala inayoelekea Mwenge. Wakiwa njiani, Matilda alianza kumuuliza Brighton maswali mbalimbali huku akionesha kama tayari alishaanza kumzoea kijana huyo mpole.
“Makumbushoooo,” konda wa daladala aliita kwa sauti kubwa akiwataarifu abiria wake kuwa tayari wamefika makumbusho.
“Shushaaa,” aliitikia Brighton wakati akiingiza mkono mfukoni na kutoa nauli ya watu wawili, akalipa. Gari liliposimama, alimsaidia Matilda kushusha begi lake na wakaanza kutembea taratibu kuelekea kwenye nyumba aliyokuwa anaishi Brighton.
“Karibu sana, hapa ndiyo nyumbani kwangu, naishi kigetogeto,” alisema Brighton huku akiona hata kwani hakuwa ametegemea kupata mgeni nyumbani kwake hapo hivyo hakufanya usafi wa kutosha wala kutandika kitanda chake.
“Whaooo! Pazuri,” alisema Matilda wakati akivua viatu na kuingia ambapo alienda kukaa kwenye sofa moja lililokuwa ndani ya chumba hicho.
Japokuwa Brighton alikuwa akifanya kazi ya kawaida, kwa kiasi fulani alikuwa amejijenga kimaisha kwani alikuwa na kitanda kikubwa na godoro lake, alikuwa pia na kabati la kisasa la nguo, dressing table, runinga, deki na ‘music system’ pamoja na sofa moja, vitu vilivyokifanya chumba chake kionekane cha kisasa.
Matilda alikuwa akigeuza kichwa huku na kule kukiangalia chumba hicho cha kisasa, baada ya kumuwekea mzigo wake sehemu nzuri, alirudia kumkaribisha tena na kumuuliza anatumia kinywaji gani. Alipomjibu, alitoka nje na kwenda kwenye duka lililokuwa jirani kununua soda.
Huku nyuma, Matilda alionesha kuchanganywa kabisa na maisha aliyokuwa anaishi Brighton, akaanza kutamani awe mpenzi wake ili apatesehemu ya kuishi kwani kiukweli alishachoka kuishi kijijini ukizingatia bado alikuwa msichana mwenye uzuri wa kawaida.
“Nitamtega mpaka tufanye naye mapenzi na akikubali tu, sitaondoka hapa ng’o, nataka anioe ili na mimi nifaidi maisha haya,” alijisemea Matilda huku akijiapiza. Baada ya muda, Brighton alirejea dukani akiwa amebeba soda mbili, akazifungua na kumkaribisha mgeni wake, wakaanza kunywa huku Matilda akionesha uchangamfu sana.
Baada ya muda, Matilda aliomba aoneshwe bafu akidai kwamba anataka kuoga ili apunguze uchovu wa safari. Brighton hakuwa na hiyana, alimpelekea maji bafuni na kumpisha ili abadili nguo na kwenda kuoga kwa uhuru.
Yeye akatoka na kwenda kununua chakula cha usiku kwani tayari ilishafikia saa mbili za usiku. Baada ya takribani dakika kumi, Brighton alirejea akiwa na mifuko miwili ya chipsi, akabisha hodi mlangoni ili kama Matilda hajamaliza kuvaa, amjulishe.
“Karibu, pita ndani,” aliitikia Matilda kwa sauti iliyotokea puani. Alipoingia, alipigwa na butwaa baada ya kumkuta Matilda akiwa amevaa khanga moja tu mwilini mwake, hali iliyosababisha maungo yake yaonekane sawia.
“Yaani huku kwenu joto mpaka naona kero kubaki na nguo,” alisema Matilda huku akiinua mguu mmoja na kuubebesha juu ya mwingine, hali iliyosababisha maeneo yake muhimu kuonekana.
“Mungu wangu,” Brighton alijisemea kimoyomoyo huku mapigo ya moyo yakianza kumwenda kasi. Awali alipania kujikaza kiume na kuhakikisha hakuna chochote kibaya kinachotokea kati yake na Matilda mpaka asubuhi lakini kwa hali aliyoikuta, alijikuta akiwa katika mtihani mgumu.
Usoni hakuonesha kushtuka, akaanza kuandaa chakula ili wale pamoja na mgeni wake. Alipomaliza, Matilda alimtaka wakae pamoja kwenye sofa na kula, tofauti na Brighton alivyofikiria kwani alipanga yeye akae juu ya ndoo na mgeni wake kwenye sofa ili kuepusha kugusana kusiko kwa lazima.
Walipoanza kula, Matilda alikuwa akimtazama Brighton na kumrembulia macho yake meupe, hali iliyozidisha mfadhaiko kwa kijana huyo. Walipomaliza, Matilda aliinuka haraka na kujifanya anatoa vyombo, akawa anatembea kwa kujitingisha makusudi mbele ya Brighton. Alipomaliza, alirudi na kukaa palepale kwenye sofa, safari hii akiwa amemsogelea mwilini kiasi cha Brighton kuanza kulihisi joto la msichana huyo.
Wakazungumza mambo kadhaa kisha Brighton akatoka na kwenda kuoga kisha akarudi, alipoingia ndani, alizidi kuwa katika wakati mgumu baada ya kumuona Matilda amelala kitandani kihasara, tena akiwa kama alivyozaliwa.

Je, nini kitafuatia? Usikose wiki ijayo.

Views: 2036

Tags: hadithi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by kulthum mattar on April 14, 2013 at 1:30pm

mhhh jamanii hebu tujiheshimu tusubiri tuombwe kwanza sio twato atuuu hata mtu humjui kama ana ukimwi jee

Comment by RUKHAIYA ISSA on April 13, 2013 at 3:59pm

ndio maana siku hizi wanawake hatuna thamani hata kidogo maana mtu wala haombi anapewa tu akitakacho. dah inatia aibu sanaaaaaaaaaa.

Comment by katalinafrank on April 13, 2013 at 11:13am

mmh!

Comment by DORAH FREDY on April 13, 2013 at 11:06am
Wanawake bwana mmh wewe umepewa hifadhi unakuja kufanya mambo ya ajabu ajabu
Comment by neema erasto on April 13, 2013 at 10:20am

mmmmmmmh!!!jamani na ss wanawake tuna matatizo eeeh!!!pole sana bright

UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

Latest Activity

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }