HEART ATTACK (SHAMBULIO LA MOYO) - 2

ILIPOISHIA:
Aliendelea kupatiwa matibabu na baada ya saa sita tangu afikishwe hospitalini hapo, Brighton alizinduka na kujikuta yupo sehemu tofauti.
“Unajisikiaje Brighton,” sauti ya muuguzi wa kike ilisikika masikioni mwa Brighton lakini badala ya kujibu, alianza kububujikwa na machozi kwa uchungu. Kwa jinsi ilivyoonesha, alikuwa na tatizo kubwa lililokuwa linautesa moyo wake.
SASA ENDELEA…

“Mbona unalia kaka, kwani kuna tatizo?”
“Nesi we niache tu, acha nilie ili kupunguza uchungu uliomo ndani ya mtima wangu.”
“Jikaze usilie kwani hali yako bado siyo nzuri, utajizidishia matatizo,” nesi alimwambia Brighton kwa upole huku akiwa amemuinamia pale kitandani. Brighton aliendelea kuugulia ndani kwa ndani mpaka usingizi ulipompitia. Alipozinduka, alimkuta Matilda, msichana aliyekuwa na ujauzito wake akiwa amekaa pembeni ya kitanda chake, uso akiwa ameukunja kwa hasira.
“Umeona faida za ulevi? Mwanaume huna haya wewe… najuta kukubebea ujauzito,” alisema Matilda kwa jazba na kuamsha uchungu uliokuwa umeanza kupoa kwenye mtima wa Brighton.
“Kwa nini usiniulize ninavyoendelea kwanza ndiyo mengine yafuate? Huu siyo muda wa kulaumiana.”
“Huna lolote, starehe uponde na wanawake zako halafu mimi naambulia kazi ya kukuuguza, mwanaume huna shukrani wewe… najuta!” Matilda aliendelea kumnanga Brighton bila kujali hali aliyokuwa nayo, ikabidi nesi aliyekuwa anamhudumia aingilie kati na kumtaka Matilda kutoka nje ya wodi. Aliondoka huku akiendelea kuporomosha mvua ya matusi, hali iliyofanya kila mmoja amshangae.
“Hivi huko nyumbani kwenu mnaishije kaka? Amani ipo kweli? Mbona mwenzio anaonekana mkali sana,” aliuliza nesi kwa upole mara baada ya Matilda kutoka, Brighton hakujibu kitu zaidi ya kuendelea kutokwa machozi.
Licha ya kusikia watu wa rika mbalimbali wakisifia utamu wa mapenzi kila kukicha, kwa Brighton hali ilikuwa tofauti, aliishia kusimuliwa tu. Hakuwahi kufurahia mapenzi hata siku moja tangu alipokutana na Matilda, kila siku ilikuwa ni maumivu, mateso, vilio na uchungu ndani ya mtima wake, hali iliyomfanya Brighton abadilike sana kitabia.
Hakuwa Brighton yule ambaye watu walikuwa wanamfahamu, kijana mpole, mstaarabu, mtanashati na mtiifu kwa watu wa rika zote. Hakuwa Brighton ambaye kila mtu alikuwa anapenda kukaa karibu naye kutokana na ucheshi, uchapa kazi na tabia njema aliyokuwa nayo! Alibadilika kabisa na kuwa mtu mwingine tofauti.
Ghafla alianza tabia ya ulevi wa kupindukia, akawa anatumia muda mwingi kwenye vilabu vya pombe za kienyeji na mara mojamoja alipopata fedha, alikuwa akikesha baa. Mara kwa mara alikuwa mtu wa mwisho kuondoka vilabuni, akiwa amelewa tilalila.
Kulala kwenye mitaro ya maji machafu halikuwa jambo geni tena kwake, uso wake ulichakaa kwa pombe, kila sehemu akawa na makovu ya michubuko na majeraha aliyokuwa anayapata baada ya kulewa. Kwa watu waliokuwa wanamfahamu, walikuwa wakimuonea huruma sana kwani alionesha kupoteza dira ya maisha akiwa bado kijana mdogo sana.
Hata muda wa kumpa ushauri wa nini cha kufanya haukupatikana tena kwani muda wote alikuwa amelewa, si asubuhi, mchana wala usiku. Aligeuza pombe kuwa starehe yake kubwa, akaharibu kazi na kila kitu kwenye maisha yake! Alitia huruma.
Akiwa amelala juu ya kitanda kilichotandikwa mashuka meupe, dripu ikitiririka taratibu kuingia mishipani mwake, machozi yakilowanisha kichwa chake na mashuka, kumbukumbu zake zilimrudisha nyuma, siku aliyokutana kwa mara ya kwanza na Matilda.
***  
April 8, 2012
Dar es Salaam
Jua kali lilikuwa likiwaka katikati ya Jiji la Dar es Salaam, Mtaa wa Posta hali iliyofanya kila mtu aliyekuwa anatembea kushika kitambaa cha kujifutia jasho. Kila mtu alionekana kuwa katika pilikapilika za kusaka tonge, watu wakawa wanapishana kwa kasi huku daladala nazo zikipakia na kushusha abiria.
“Kaka samahani, naomba kuuliza.”
“Uliza tu dada’angu.”
“Eti jengo la kitega uchumi liko wapi?”
“Wewe ni mwenyeji hapa mjini? Maana hata sijui nikuelekezeje kwa hapa tulipo.”
“Hapana, mimi ni mgeni, nimekuja leo kutoka Mlalo, Tanga, kuna ndugu yangu nasikia anafanya kazi huku mjini ndiyo nimekuja kumtafuta.”
“Ok pole, kama ungekuwa huna haraka ningekwambia tuongozane nikanunue wino wa kompyuta hapo dukani kisha tutarudi wote maana na mimi nafanya kazi kwenye steshenari moja jirani na hapo.”
“Hamna shida kaka’angu, nitakusubiri tu. Umesema unaitwa nani?”
“Brighton au kwa kifupi Bright. Wewe je?”
“Mi naitwa Matilda.”
“Ok, nashukuru kukufahamu,” hivyo ndivyo Brighton na Matilda walivyokutana. Baada ya Brighton kununua catridge za wino wa kompyuta kwenye duka kubwa la jumla, aliongozana na Matilda mpaka kwenye steshenari aliyokuwa anafanyia kazi. Hakukaa, akatoka na kumpeleka Matilda mpaka kwenye jengo la kitega uchumi. Alipomfikisha, alimuaga na kurudi kuendelea na kazi.
Muda ulizidi kuyoyoma, kutokana na kuzongwa na wateja wengi waliokuwa wanahitaji huduma mbalimbali kwenye steshenari aliyokuwa anafanyia kazi, Brighton hakupata muda wa kumfikiria Matilda tena mpaka muda wa kufunga ofisi ulipowadia. Wakati anajiandaa kufunga, alishtuka kumuona Matilda mbele yake, safari hii akiwa amejitwisha begi lake.
“Vipi? Umefanikiwa kumpata huyo ndugu yako?”
“Nimemkosa kaka yangu, hapa nilipo nimechanganyikiwa hata sijui pa kuanzia, naomba msaada wako tafadhali nipate sehemu ya kulala kesho nitajua cha kufanya,” alisema Matilda huku akitua begi lake mbele ya Brighton.

Je, nini kitafuatia? Usikose wiki ijayo.

Views: 1738

Tags: hadithi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by florence masilila on April 15, 2013 at 3:07pm

Mh pole

Comment by florence masilila on April 15, 2013 at 2:49pm

Sio mwanzo wa kuraumia matlida msikilize mwenzio kwanza ndio umhukumu

Comment by kulthum mattar on April 14, 2013 at 1:12pm

heee yamekua hayo

Comment by DORAH FREDY on April 13, 2013 at 10:44am

Mmhhhh

UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }