HEART ATTACK (SHAMBULIO LA MOYO) - 12

ILIPOISHIA:
WAKAKUBALIANA kuwa Brighton akatoe posa nyumbani kwa akina Zainab ili taratibu za kufunga ndoa zianze kufanyika mara moja. Wakiwa katika mazungumzo hayo, simu ya Brighton iliita mfululizo, akaichukua na kupokea.
“Haloo, nani mwenzangu?”
“Ni mimi Matilda, nakupa taarifa kuwa nina mimba yako,” ulijibu upande wa pili kisha simu ikakatwa.
 SASA ENDELEA…

“WHAAAT!” Brighton alisema kwa sauti ya juu kiasi cha kumshtua Zainab, akamsogelea na kuanza kumuuliza kwa upole. Kutokana na suala lenyewe kukaa vibaya, huku Brighton akiwa na hasira kali juu ya msichana huyo kwa alichomfanyia, alishindwa kumueleza ukweli Zainab.
“Kuna nini tena mpenzi wangu?” aliuliza Zainab huku akijisogeza kifuani kwa Brighton ili amkumbatie, akafanya kama alivyokuwa anataka lakini akawa anashindwa kueleza moja kwa moja nini kilichotokea, akadanganya:
“Unajua huyu mwenzangu hayupo makini na kazi sasa amesababisha shoti kwenye mahesabu, hata sijui kama bosi atatuelewa. Tunaweza hata kusimamishwa kazi.”
“Ooh! Pole mpenzi wangu lakini wala usijali, nina akiba ya kutosha benki kwa sababu mshahara wangu huwa siutumii kwani napata kila kitu kutoka kwa wazazi wangu. Nitakupa fedha kwa ajili ya kufidia hiyo shoti mliyoisababisha,” alisema Zainab akitegemea kuwa taarifa hiyo itamfurahisha Brighton na kumrudisha kwenye hali yake ya kawaida lakini haikuwa hivyo.
Bado alionekana kuzama kwenye dimbwi la mawazo huku mapigo ya moyo wake yakienda mbio mpaka Zainab aliyekuwa amejiegemiza kifuani kwake akawa anayasikia. Aliendelea kumliwaza kwa muda mrefu huku akimtaka kutokuwa na wasiwasi kwani kila kitu kingekuwa sawa lakini bado Brighton hakurudi kwenye hali yake ya kawaida.
Kutokana na hali hiyo, ilibidi Zainab aage na kuondoka kwani maelewano hayakuwepo tena, Brighton alionekana kuwa na wasiwasi, hofu na hasira kwa wakati mmoja, ikabidi aondoke na kumuacha peke yake mpaka atakapotulia.
Tofauti na siku zote, siku hiyo Brighton hakumsindikiza Zainab kama ilivyokuwa kawaida yake, akamuacha aondoke peke yake huku yeye akiendelea kukaa palepale kwenye sofa.
“Haiwezekani!  Haiwezekani nasema,” alisema Brighton huku akijipigapiga kifuani. Taarifa kwamba Matilda alikuwa na ujauzito, zilikuwa sawa na kushindilia msumari wa moto kwenye kidonda ambacho bado hakijapona. Kumbukumbu zake zikamrudisha nyuma kuanzia siku ya kwanza walipokutana na yote yaliyoendelea baada ya hapo.
Alikumbuka jinsi msichana huyo chakaramu alivyomuingiza kwenye mtego na kujikuta akifanya naye tendo la ndoa, tena bila kinga. Alikumbuka pia jinsi alivyomuibia kila kitu ndani na jinsi alivyompigia mayowe ya mwizi siku aliyojaribu kutumia shuruti ili aeleze mahali alikoficha vitu vyake alivyomuibia.
Akiwa katika hali hiyo, Brighton alishindwa kuyazuia machozi yasiulowanishe uso wake, akainama kwa huzuni huku mawazo machungu yakiendelea kupita ndani ya kichwa chake. Mapenzi na Matilda yaligeuka shubiri na sasa alikuwa akitamani ardhi ipasuke na kummeza.
“Lakini simpendi kabisa Matilda!  Moyo wangu upo kwa Zainab kwa sababu ameonyesha upendo wa dhati kwangu na ni mwanamke mwenye vigezo vyote ninavyovihitaji, siyo huyu gumegume wa…,” alisema Brighton lakini kabla hajamaliza, alishtuliwa na mlio wa simu yake iliyokuwa inaita.
Alipotazama namba ya mpigaji, alikuwa ni Matilda, hakutaka kupokea simu, akaiacha iite mpaka ilipokata. Mpigaji hakuchoka wala kukata tamaa, akaendelea kupiga kwa fujo kiasi cha kumfanya Brighton atamani kuizima simu yake. Hata hivyo, alipiga moyo konde na kuamua kumsikiliza.
“Unasemaje?” alihoji kwa ukali Brighton, Matilda akajibu kwa jeuri:
“Si nimekwambia nina mimba yako? Ina maana hujasikia au?”
“Mimba gani acha kunichanganya kichwa malaya wewe?”
“Haaa! Unajifanya jeuri siyo? Hivi hujui kwamba mimi ni mwanafunzi? Au unataka ukaozee jela?”
“Wewe ni mwanafunzi? Matilda kwa nini unataka kuniharibia maisha yangu? Kwa nini hukuniambia mapema?” aliuliza Brighton huku kwikwi ya kilio ikimkaba shingoni. Taarifa kwamba kumbe Matilda alikuwa ni mwanafunzi zilizidi kumchanganya, akawa anaiona jela mbele yake.
“Sasa kama wewe ni mwanafunzi kwa nini uliniingiza kwenye ushawishi wa mapenzi? Au ulitumwa kuja kuyavuruga maisha yangu?”
“Nani alikuingiza kwenye ushawishi? Nilikulazimisha? Si tamaa zako ndiyo zilikuponza?” Matilda alizidi kutoa maneno ya karaha kwa Brighton kiasi cha kumfanya kijana huyo aishiwe la kusema.
“Na vipi kuhusu vitu vyangu ulivyoniibia?”
“We bwege nini? Kwa hiyo unaona hivyo vitakataka vyako vina thamani kuliko huu ujauzito wako ulionipa? Kwanza jiandae, itabidi ulipe fedha nyingi sana ili usipelekwe polisi vinginevyo miaka thelathini inakuhusu, hivi niko njiani nakuja nyumbani kwako,” alisema Matilda kisha simu ikakatwa.
Brighton alijihisi kuchanganyikiwa, akajiona kama amebeba gunia la misumari kwenye kichwa chake. Katika maisha yake, hakuwahi kunywa pombe hata mara moja lakini kutokana na jinsi alivyokuwa anajisikia, aliamini pombe inaweza kumpunguzia mawazo kama alivyokuwa akiwasikia baadhi ya watu wakisema.
Hakutaka Matilda akija amkute ndani kwake, harakaharaka akavaa na kutoka, akafunga mlango vizuri na kwenda kwenye baa iliyokuwa jirani na anapoishi. Alipofika, aliagiza bia na kuanza kunywa lakini kila alipopeleka chupa mdomoni, alikunja sura kutokana na uchungu ambao hakuwa ameuzoea.
Hata hivyo, kwa kuwa alikuwa anataka kulewa, alijikaza na kugida hivyohivyo huku akiwa amekunja sura. Alipomaliza chupa moja, tayari alikuwa amelewa kisawasawa kwani hiyo ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kunywa pombe. Akatoka huku akipepesuka mpaka nyumbani kwake. Alipofika, alipigwa na butwaa baada ya kuona kuna mtu amekaa pembeni ya mlango wake.
Alipomtazama vizuri, aligundua ni Matilda ambaye alipomuona alisimama, tumbo lake ambalo sasa lilikuwa limeongezeka ukubwa likaonekana vizuri na kumfanya Brighton aamini kuwa ni kweli alikuwa mjamzito.
Je, nini kitafuatia? Usikose wiki ijayo.

Views: 2343

Tags: hadithi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by FURAHA TAUSI on June 11, 2013 at 9:59am

dah huo ni mtihani kwako

Comment by Anna Andrew Mwakasita on June 10, 2013 at 7:02pm

dah

Comment by neema erasto on June 10, 2013 at 2:52pm

mmmmhh! pole sana  brighton

Comment by penina mwailunda on June 10, 2013 at 2:29pm

Brighton Kazi unayo

Comment by robert ludger nyagali on June 10, 2013 at 2:27pm

Hata mimi Nachanganyikiwa

Comment by Mishy chunga on June 10, 2013 at 12:50pm

we ungemweleza ukweli zainab angekupa msaada wa mawazo, unaona sasa umejiingiza kwenye ulevi bila kutegemea?

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by hiepelines Jul 4. 6 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Aug 15. 7 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Aug 15. 6 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by Joe reggan Apr 24. 2 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

Latest Activity

mulailagibro posted a status
45 seconds ago
misu babu posted a status
"HDTV Geelong Cats vs Collingwood Live AFL Fox Telecast http://alturl.com/dvqza"
1 minute ago
misu babu posted a status
"HDTV Geelong Cats vs Collingwood Live AFL Fox Telecast http://alturl.com/dvqza"
1 minute ago
Profile IconGlobal Publishers via Facebook
Facebook1 minute ago · Reply
misu babu posted a status
"HDTV Geelong Cats vs Collingwood Live AFL Fox Telecast http://alturl.com/dvqza"
1 minute ago
misu babu posted a status
"HDTV Geelong Cats vs Collingwood Live AFL Fox Telecast http://alturl.com/dvqza"
2 minutes ago
misu babu posted a status
"HDTV Geelong Cats vs Collingwood Live AFL Fox Telecast http://alturl.com/dvqza"
2 minutes ago
misu babu posted a status
"HDTV Geelong Cats vs Collingwood Live AFL Fox Telecast http://alturl.com/dvqza"
2 minutes ago
Mrs. Mathilda Kayagambe commented on GLOBAL's blog post SIRI 4 MATUSI YA DIAMOND KWA DIVA
"Kuna kijiukweli flani hivi kuwa Diva anamtamani Diamond. Mbona watu wengi wanaalikwa studio na huwa…"
2 minutes ago
mulailagibro posted a status
3 minutes ago
makhon lal posted a status
4 minutes ago
Asif Sujon posted a status
5 minutes ago

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }