Issa Mnally na Richard Bukos
Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Saidi amefanya tukio ambalo halijawahi kutokea baada ya kuandaa sherehe kubwa ya harusi akisema anakwenda kumwoa mwanaume mwenzake kwa madai kwamba, amezidi umbea, Risasi Mchanganyiko lina kila kitu kibindoni.

Baikoko kutoka Tanga.
Tukio hilo la aina yake lilitokea Septemba 17, 2010 Sinza ya Kumekucha jijini Dar es Salaam jirani kabisa na hoteli ya Lion ambako mwanaume aliyedaiwa kufanyiwa kitendo hicho (jina tunalo) anaishi.

Msafara wa magari ya kifahari yapatayo kumi na tano yaliwasili nyumbani kwa mwanaume huyo ndani yake kukiwa na waalikwa walioonekana kuwa na furaha za shamrashamra hizo.


Msafara huo ulipofika nje ya nyumba ya mwaname huyo mwenye mke ulisimama huku matarumbeta yakipulizwa na watu wakiserebuka kwa ngoma ya Baikoko iliyokodishwa toka jijini Tanga.

Hata hivyo, ilidaiwa kwamba mwanaume huyo ambaye bado kijana alipochungulia nje na kuona wageni akiwemo ‘bwanaharusi’ aliingia mitini kwa kutumia mlango wa nyuma kwani toka jana yake alishanyetishiwa kuwepo kwa ‘ndoa’ hiyo ya aina yake.

Mpambe wa 'bwana harusi'.
“Jamaa alichungulia dirishani, alipoona msafara ukifika nyumbani kwao akatimua mbio kwa kupitia mlango wa nyuma, ikabidi tumueke bibi harusi wa bandia ili kumwakilisha.” kilisema chanzo.

Akiongea na waandishi wetu eneo la tukio, mmoja wa wageni waalikwa (hakupenda kutaja jina lake) alisema kuwa, wamealikwa katika sherehe ya ‘ndoa’ ya kijana huyo kwa lengo la kumshikisha adabu na kuachana na tabia yake ya ambea mtaani anakoishi.

“Ndiyo, tumekuja kusherehekea harusi ya rafiki yetu Saidi, ni kweli anaoa leo, hii itampunguzia jamaa tabia ya umbea si unaona hata zawadi za Bi harusi tunazo,” alisema mwalikwa huyo ambaye alikuwa ameshikilia sidiria na pete mkononi.

Akifafanua zaidi, alidai kuwa, kijana huyo ana tabia mbaya sana, kwani kila akimkuta mwanaume mume wa mtu amekaa na mwanamke yeye humpigia simu mke na kumnyetishia ishu nzima.

Akasema: “Dawa ya wambea kama hawa ni kuolewa tu, aende akaishi ndani ya nyumba kama mke.”

Hata hivyo, pamoja na ‘mwolewaji’ huyo kuingia mitini sherehe ziliendelea nje ya nyumba kwa ngoma huku ratiba za chakula zikifanyika kama kawaida.

‘Bwanaharusi’ aliyetarajiwa ‘kumuoa’ kijana huyo alipoulizwa kama kweli alikuwa na nia hiyo alikiri na kuongeza kuwa, ndiyo maana aliamua kufanya sherehe kubwa kama ile.

“Ndiyo nimekuja kuoa leo, nataka nikiondoka hapa niwe na mke wangu, nimekamilisha mipango yote ya harusi,” alisema.

Alisema kuwa, amekuwa akigombana na mkewe kila mara akimshutumu kwamba, alikuwa mahali na mwanamke lakini alipofuatilia kwa undani, wasamaria wema kwake wakamtonya kuwa, kijana huyo ambaye awali walikuwa marafiki na hukaa naye beneti ndiye anayemwambia mkewe kuwa mumewe yupo na ‘nyumba ndogo’ mahali.

Aliongeza kuwa, alipania kufanya hivyo na alishakusanya michango ya watu wakiwemo marafiki ili kufanikisha sherehe hiyo ambayo alidai kuwa, kama angemkuta ‘mkewe’ huyo ingekuwa ya kifahari.

Naye Shehe ambaye alitegemewa ‘kuunganisha’ wawili hao, Abdallah Mohamed alisema kuwa, alifika eneo hilo kwa nia ya kufungisha ndoa hiyo ya wanaume kwa sababu ya mabadiliko ya maendeleo ya kisasa duniani.

Habari zaidi katika eneo la tukio zinapasha kuwa, Pedeshee maarufu jijini Dar, Kizaizai yeye alichangia shilingi Laki tano ili kufanikisha sherehe hiyo ambayo Bajeti yake iligonga Shilingi milioni moja za Kibongo.

Pete ya uchumba na ndoa.
Ili kusikia toka upande wa pili, Risasi Mchanganyiko, Jumatatu mchana lilimpandia hewani mwanaume huyo ambaye mkewe inasemekana aliangua kilio kwa tukio hilo, lakini simu yake ya mkononi iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

Baadaye alipopigiwa tena, hakuwa hewani tena hali iliyotafsiriwa kuwa, huenda simu yake iliishiwa chaji au aliizima kwa sababu zake mwenyewe.

Kutoka mezani kwa Mhariri: Tunaamini kuwa, njia zilizotumika kukomesha tabia inayodaiwa kuwa inafanywa na kijana huyo si sahihi, kwani mitaani kuna Wajumbe wa Nyumba Kumi na Serikali za Mitaa, Saidi alitakiwa kwenda huko kutoa malalamiko yake kama kweli ana ushahidi wa ndoa yake kuvurugwa na kijana huyo.

Views: 285

Tags: mchanganyiko11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by hamza salum on April 11, 2011 at 5:22pm
mambo ya kiswahili,yaani mnaharibu hela kwa kwenda kufanya kitendo kama hichi,aise kama ni huyo jama anaweza kuwafungulia mashitaka,ila nadhani naye atakua amekoma na umbea wake
Comment by ashura mohamed ally on October 8, 2010 at 3:16pm
sasa huyo bwana saidi angemuoa huyo mwanaume angemfanya nini wakati mwanaume mwenyewe amekamilika?wanaume na wanawake tuache mambo ya umbea jamani,hausaidii chochote sana sana unaharibu ndoa za watu jamani
Comment by ManChandE on October 5, 2010 at 10:58am
kuelimika kazi!!!
Comment by vita wilbards on October 3, 2010 at 8:24pm
KWA UTARATIBU HUU WATAOLEWA WENGI WANAUME KAMA MABINTI
Comment by moizze g simba on October 2, 2010 at 5:47am
ahahahhah mambo ya fwedha na kutiana adabu hap mjini
Comment by jabal kiss on September 28, 2010 at 12:46pm
DAH HII NIMEIPENDA JAMAA KAFANYA DAWA NZURI SANA NA MIMI KUNA MTU NITAFANYIA MAANA KZIDI UMBEA
Comment by Salum S Esry on September 25, 2010 at 11:04pm
huyo shekhe akamatwe akapimwe akili anaonekana alikua ameshapiga viroba vya konyagi , shenz type .
Comment by adanse nkombe on September 23, 2010 at 9:13am
Hakika hakika busara, hekima pia na ubinadamu haujatumika hata kidogo kwa weye muoaji mshenzi, pia waaalikwa na wachangaji ikiwa ni pamoja na Shekhe.Hivi kweli inaingia akilini kuhusu ndoa ya jinsia moja inavyopigiwa kelele duniani kote eti weye wajidai waenda kuoa, Hivi mwanao angekuuliza baba waenda kumuoa nani tena na mama yupo? What was the answer? Nadhani ile dhana ya kuweza kufanya upembuzi yakinifu kwako ni ZERO, Sasa elewa unavyoendelea kuishi hapa duniani utapata matjaribu mengi sana, so tafuta njia za kutatua diplomatically!! Kwa maana hiyo unawafundisha wanao siku wakiongopewa nao wakaolewe au wakaoe wakiwa under age??? Bulshitttttt
Comment by Anselm on September 23, 2010 at 7:31am
Hivi harusi za kiwango cha kusimulika za kiislamu huwa zina budget ya Tshs 1,000,000/= enh?
Comment by TZ on September 23, 2010 at 6:45am
Mlijuwaje kama yu mmbeya kama na wewe si mmbeya?


ADVERTISEMENT


TANGAZA HAPA

ADVERTISEMENTS

Latest Activity

GUNZ TRUVADA posted a status
"KUMPA ASIYE KUPA NI SAWA SAWA NA KUTUPA"
4 minutes ago
othman Ochu posted a status
"SCENE 1 WAHUSIKA: AMIDU , SHARIFA MAHALI: ZANZIBAR MUDA : JIONI ( WAKIWA WANASHUKA TOKA KATKA BOTI YA JION KUINGIA KATKA MJI WA ZANZI"
9 hours ago
Priscus Adelard shared GLOBAL's blog post on Facebook
9 hours ago
mrembo commented on julius manning's photo
Thumbnail

Mtanzania huru

"pole sana usijali iko siku mungu atakujaalia mungu hamtupi mja wake"
10 hours ago
mrembo commented on Sili Silali's photo
Thumbnail

Duh!

"mama mzima hayawani mavazi gani hayo takupa mfano chungwa likiwa halijamenywa unatamani ulile…"
10 hours ago
kaka commented on Ali Amur Ali's video
Thumbnail

AZIMIO LA KUANGAMIZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE

"hapo ni kina dada kutua comment zao"
10 hours ago
Gaston Kayombo commented on Ali Amur Ali's video
12 hours ago
roylicious and Jackson Jacob are now friends
12 hours ago
babu wa loliondo (cup) updated their profile
12 hours ago
julius manning commented on julius manning's photo
Thumbnail

vijana 2016 itakuwa hivi

"@furaha mimi ni kikongwe hayo ni kazi kwako."
13 hours ago
Masalu Mayeji Many'hasimha shared GLOBAL's blog post on Facebook
13 hours ago
kheri zewe commented on Sili Silali's photo
Thumbnail

Duh!

"minyama uzembe"
13 hours ago

© 2012  

Designed & Developed by
G5 CLICK COMPANY.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

How to make a Website