GEA HABIB: Siko tayari kuishi uke wenza, bora niachwe


Gea Habibu alizaliwa 1981 katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam na kuanza shule ya msingi 1989 katika Shule ya Kurasini Temeke jijini Dar es Salaam na kuhitimu mwaka 1995 ambapo alifanikiwa kujiunga Kidato cha Kwanza kwenye Shule ya Sekondari Jitegemee hadi alipohitimu Kidato cha Sita 1999 kisha kujiunga na Chuo cha Uandishi wa Habari cha Times kilichopo Ilala jijini Dar, kwa muda wa mwaka mmoja.

Hayo ni kwa uchache tu, zaidi ungana nami uweze kujua yale ambayo huenda ulikuwa huyajui kuhusu mwanadada huyu.
TQ:Kwanini uliamua kuwa mtangazaji na si kazi nyingine? Je,kuna aliyekushawishi?

GEA:Hakuna mtu aliyenishawishi kuwa mtangazaji ila mimi mwenyewe nilikuwa napenda sana kusaidia jamii kutokana na hilo njia pekee niliamua kusomea fani hii.
TQ:Ni matatizo gani ambayo umekuwa ukikumbana nayo kupitia fani yako?

GEA:Aah! Kusema kweli kutokana na ugumu wa kazi ya uandishi wa habari matatizo nakutanayo mengi tu ingawa mara nyingi nayachukulia kama changamoto za kazi.

TQ:Wanawake wengi wamekuwa wakikumbwa na skendo ya kutoa rushwa ya ngono ili kufanikisha mambo yao na inadaiwa hata wewe ulipitia njia hiyo kupata kazi yako je, unalizungumzia vipi hilo?

GEA:Kwa upande wangu sijawahi kutoa rushwa ya ngono kwakuwa najiamini,nina uwezo mkubwa wa kufanya kazi. Wanaoitanguliza hiyo bora waiache kwani madhara yake ni makubwa kuliko wanavyofikiri.
TQ:Sawa! Turudi kwenye maisha yako ya kimapenzi najua umeolewa je,unaifurahia ndoa yako?

GEA:Yah! Naifurahia sana ndoa yangu maana naamini mume wangu ananipenda kuliko kitu chochote kile.
TQ: Je, ni kitu gani kinachokuvutia zaidi kwa mumeo?

GEA:Duh! We naye, naweza kusema kila kitu cha mume wangu kinanivutia.
TQ:Katika familia yako umejaaliwa kupata watoto? Na je ungependa kuzaa watoto wangapi?

GEA: Nina watoto wawili hadi sasa na malengo yangu ni kuwa na familia ya watoto watatu tu.
TQ:Najua wewe ni muumini wa dini ya Kiislamu ambayo inaruhusu mume kuwa na mke zaidi ya mmoja, je akitaka kuongeza mke wa pili utakuwa tayari kwa hilo?

GEA: Siku zote kwa hilo siko tayari labda aoe bila taarifa yangu na asiniambie ukweli.
TQ:Unadhani ni kipi kilichomfanya mumeo akuoe wewe na si mwanamke mwingine?

GEA:Naweza kusema ilikuwa imeishapangwa na Mungu anioe mimi.
TQ:Ni jambo gani la huzuni lililokuumiza sana katika maishani yako?
GEA: Siku nilipofiwa na baba yangu mzazi na siku mdogo wangu, mtoto wa mama mdogo aliponifia mikononi mwangu hospitalini. Nikikumbuka matukio hayo mawili hadi leo huwa nakosa raha.
TQ:Nini malengo yako ya baadaye?

GEA: Ni kujiendeleza zaidi katika kazi yangu ya utangazaji.
TQ: Unawashauri nini mastaa wenzako wa kike?
GEA: Wajiheshimu wawapo mbele za watu. Waache majivuno yasiyo na msingi na kwamba wanapopata kazi wafanye kwa bidii bila kusubiri kusukumwa.

Views: 4663

Tags: ijumaa11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by Sarah Anuary on October 19, 2010 at 12:22pm
Vizuri mwaya kuwa na msimamo tabu ya nini ya kumizana roho bure?
Comment by zuleya rashid on October 13, 2010 at 6:12pm
We, misana acha kumuonea wivu mtoto wa watu gea anaubaya gani?ni tamaa 2 za kimwili za wanaume wanaopenda kuowa wake 2 pia mwandishi acha kutuongopea 1995-1999 amesomaje kufika six au inawezekana hakufika kidato cha sita alimaliza form 4 akakimbilia kusomea uwandishi, pili wanaume wa kiislam mnaboa sana m/mungu amesema unatakiwa uwoe wake 4 kama unauwezo na kwa kuwafanyia uwadilifu lakini nyinyi mnataka mpendelee upande 1 kama si kujitafutia dhambi kwa m/mungu kaza buti dada usikubali nakuunga mkono.
Comment by Renatus Rwezahura on October 9, 2010 at 3:24pm
Hii siyo kweli 1995-1999 kidato cha sita bali kidato nne au labda alisoma 2in 1.
Comment by lion on October 9, 2010 at 6:31am
sura mbaya hivo mumeo asioe mke wa pili? bc kazi anayo
Comment by Habibu Kissio on October 8, 2010 at 11:07pm
Ina bidi ubadili Dini bidada kwani hapo unapingana na maandiko matakatifu ya kile kitabu kisicho badilika,lakini usijali sie wenye majina kama la mumeo huwa ni waungwana na hatuna pepo la ngono,kaza moyo Bi dada bado umchanga maisha ya ndoa yanachanga moto nyingi,kiitajikacho ni uvumilivu na kumtanguliza Rabbana.
Comment by vita wilbards on October 8, 2010 at 6:53pm
mtoto hujakomaa kidini utamkatazaje mumeo kuongeza mke wa pili, tatu au nne kama ilivyo aja katika uislamu

badilika mtoto wa kiislamu
Comment by Maiza on October 8, 2010 at 5:15pm
Nakupenda dada Gea, Unatangaza vizuri na huwa siikosi leo tena,,,,,, Big up
Comment by disminder on October 8, 2010 at 3:21pm
Siyo lazima kila mwanaume wa kiislamu kuowa wake wengi lakini dada Gea hapo rudi kwa Muumba na uombe msamaha. Hakuna mja mwenye haki ya kupinga maandiko ya Allah, imepita wanaume waowe wake kuanzia wawili hiyo haina kipingamizi.
Kumbuka duniani wanawake tuko wengi kuliko wanaume, na Allah aliyajua haya kabla na ndiyo maana aliweka hiyo sheria ili wanawake wengine pia wapate kustirika na kuishi katika misingi ya haki. kwa hiyo hapo unasema bora mumeo azini kuliko kuowa mke wa halali.

Hukumu ni yake Allah lakini mrudie Allah kwa hiyo kauli yako.
Comment by Estar on October 8, 2010 at 2:16pm
Mh!!!!!! waislam tena lazima ataowa tu wake wengine so suburia wake senza mamy
Comment by Habibu Shaaban on October 8, 2010 at 2:01pm
Hivi mtu akimaliza la saba 1995 atamaliza form six mwaka 1999? au ni form four? We Gea acha kudharau dini yako suala la kuolewa au kuoa ni mipango ya Mungu usitukane Mamba kabla hujavuka mto hujui hatma ya maisha yako mbele ikoje kwani wote walioolewa ukewenza wamependa?
UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }