Na Dustan Shekidele, Morogoro
GUMZO wikiendi iliyopita ya shamrashamra za Sikukuu ya Pasaka mjini hapa, ni lile la bosi wa kiwanda cha maturubai aliyetajwa kwa jina la Daudi, kufumwa gesti akiwa na mfanyakazi wake ambaye ni mke wa mtu aliyetajwa kwa jina la Aisha.
Tukio hilo la aibu kwa bosi huyo lililoshuhudiwa na paparazi wetu, lilitokea muda mfupi kabla ya Pasaka majira ya saa 1:00 usiku ndani ya gesti maarufu iliyopo maeneo ya Sabasaba mjini hapa.
Habari zilizopatika eneo la tukio zilidai kuwa mzee huyo ana mazoea ya kufika mahali hapo na mwanamke huyo anayefanya kazi chini ya usimamizi wake ambapo huwa wanajiachia sehemu ya baa kabla ya kuingia ndani.
Siku ya tukio, 40 yao ilitimia baada ya wawili hao kutinga kwenye gesti hiyo na kujianika wakiponda raha.
Ilidaiwa kuwa wakiwa mahali hapo, kuna mtu alimuona Aisha ‘akidendeka’ na mzee huyo hivyo akamjulisha mumewe aliyetajwa kwa jina la Mwinshehe.
Ilisemekana kuwa, baada ya kupokea taarifa hizo, Mwinshehe alipanga mikakati ya fumanizi ambapo alitinga kwenye gesti hiyo na kuhakikishiwa kuwa mkewe yupo ndani katika chumba chenye jina la Uganda ndipo alipoingia vitani.
Akiwa kwenye mvutano na wenye gesti waliomkataza kuingia, ghafla alimuona mkewe akitokea msalani akiingia ndani na ndipo alipovamia kwenye chumba na kumkuta mgoni wake ameshamaliza mchezo.
Baada ya kumuona mumewe, mwanamke huyo alianza kuangua kilio huku akisikika akisema, ‘Baba Nassoro nisamehe, makosa wamewekewa binadamu, sitarudia tena’.
Hata hivyo, Mwinshehe ambaye alikuwa na hasira hakumsikiliza zaidi ya kuwashushia kipigo ambapo yule mzee alishindwa kumudu mashambulizi baada ya kuzidiwa na kujikuta akichanika paji la uso, wenye gesti waliingilia kati na kuwatoa nje kisha wakafunga geti.
Baada ya hapo, timbwili zito lilihamia kwenye kituo kidogo cha polisi cha Kiwanja Cha Ndege ambapo baada ya kufika, Mwinshehe aliangua kilio alipowaona wakwe zake (baba na mama wa mkewe Aisha).
Aidha, wawili hao walitoa maelezo yao kituoni lakini hawakuelewana hivyo polisi waliingilia kati, wakaita gari la kuwapeleka kituo kikuu.
Katika hali ya kushangaza, wakiwa njiani, wahusika hao walielewana na kurudi tena kituoni hapo ambapo Mwinshehe aliwaeleza polisi hao kuwa ameamua kumsamehe mkewe hivyo ametaka mgoni wake, Daudi alipe faini ya shilingi elfu 70.
Mzee Daudi aligoma kulipa kiasi hicho akidai kuwa ni kikubwa na alipoulizwa ana uwezo wa kulipa fidia ya kiasi gani alidai atalipa elefu 50. Mwishehe alichukua kiasi hicho cha fedha na kuondoka na mkewe nyumbani.

Views: 5592

Tags: ijumaawikienda11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by Gervas Daniel Nyalusi on April 30, 2012 at 8:48am

mmeyataka

Comment by Sagana on April 13, 2012 at 1:18pm

lol

Comment by DORAH FREDY on April 13, 2012 at 9:31am
Huu umaskini balaa yaani mpaka mtu anadiriki kujidhalilisha kisa pesa wewe Manshehe aibu kubwa sana duh hii hatari sana
Comment by lumi mwandelile on April 12, 2012 at 2:33pm

hayaaa

Comment by Elly Maduhu on April 12, 2012 at 10:22am

ningekuwa mimi namwachia mke, kuna wanawake wengi sana wanashida ya kuolewa wanakunywa mpaka madawa ili wapatte wachumba yeye anaenda kumdhalilisha mumewe. yaani kamvua nguo mbele ya mwanaume mwingine.

let me tell you a thing. watu hawajua maana ya kugawa unyumba nje ya ndoa. kama wewe mwanamke unatoka nje basi wewe huna uaminifu kwa mumeo maana unaweza hata kutoa pesa ndani ukaenda kuhonga  na kuacha familia na njaa, unaweza hata kumuua mumeo ili uolewe na bbaradhuli mwenzako. so mimi sina msamaha kabiisa kwa mke mzinzi dawa ni kumtupilia mbali

Comment by saleh gumbo on April 11, 2012 at 8:42am

chamtu sumu

Comment by john bosco on April 10, 2012 at 3:01am

bosi kaangukia kwenye mtego!!! mke na mme wamepanga ili wapate matumizi ya pasaka!!!

Comment by kilos on April 10, 2012 at 12:05am

sijaona mtu bwege na mpumbavu kama huyo mwinshehe, inamaana  unauza heshima yako na afya yako kwa sababu ya elfu 50? inamaana njaa  ya watanzania imefikia hapa? mimi siamini zaidi ya kuendekeza kupewa vya bure tu.

kinacho takikana ni huyo  mwinshehe kukamatwa na kufunguliwa mashtaka, kwa kuidhalilisha ndoa, na kuwadhalilisha wanaume.

Comment by haji shehe (ustadh on April 9, 2012 at 9:24pm

Duhhh huyu mwanamme ana roho ngomu kweli inamaana mkewe ndio ameshafanya biashara mapata amepokea looooo massalaleee Ama hii ndio duniaa! LAKINI pengine ndio kawaida yao mara na mume ameshawahi kufumaniwa TIT 4 TAT

Comment by Ukweli100 on April 9, 2012 at 9:14pm

duuh! njaa! mpaka unapokea 50 elfu toka kwa bosi na mkeo kesha jichnaa!..wanawake mbona baadhi yetu tunajishusha thamna kweli, ina mana wew mwanamke na kuma yako ina thamani ya 50 elfu ama penzi na kuheshimiana na mumewe?? hii saasa ni kinyaa!

huyo mwanaume nna mashaka ishu kama hizi hazisamehewi kirahsi , ukiona hivyo naye anapo pakupumzikia, hapo anamzalizia njaa to, afu hata hivyo 50  itaitumia kwa masaa mangap kabla haijaisha!??  upuuz tu!

wenye gesti waliingilia kati na kuwatoa nje kisha wakafunga geti. safi sana wenyew, inatalkuwa kuwa hivi always. 

UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }