Na Mwandishi wetu
HEKAHEKA ya wimbi la mastaa wa Bongo kutumika kwenye imani inayodaiwa kuwa ni ya kishetani duniani maarufu kwa jina la Freemason a.k.a Wajenzi Huru inazidi kuchukua nafasi kwa kasi baada ya hivi karibuni kudaiwa kuwa, staa wa sinema za Bongo, Jacqueline Wolper Massawe naye ametumbukia humo, Risasi Jumamosi limesheheni.
NI NCHINI AFRIKA KUSINI
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, Wolper ameinamisha kichwa na kumwagiwa maji ya imani hiyo kama ishara ya kujiunga nchini Afrika Kusini, mapema mwaka huu.
NANI SHAHIDI?
Mmoja wa marafiki wa Wolper aliliambia gazeti hili kwamba, Wolper alishawishiwa na msanii mwingine wa kiume wa filamu Bongo ambaye hana jina kubwa kuwa ndiye aliyempa namba za mawasiliano za wahusika nchini Afrika Kusini.
“Wolper ameingia Freemason na aliyemshawishi ni msanii ….(anataja jina), yeye alimwambia akiwa huko anaona matunda yake kwani ni imani ambayo binadamu unaishi kama peponi,” alisema rafiki huyo.
UTAJIRI WA HARAKA WATAJWA
Kwa mujibu wa chanzo hicho, tangu Wolper amejiunga na imani hiyo inayosambaa kwa kasi nchini Tanzania amekuwa akipata mafanikio makubwa tena kwa haraka.
“Wee kama unataka kuamini, angalia tangu mwaka huu (2012) umeanza, Wolper mambo yanamyookea tu. Awali alikuwa akiishi eneo ambalo halimfai kama staa, sasa amehamia Mbezi, tena kwenye jumba zuri sana,” alisema mtoa habari huyo.
Aliendelea kuweka wazi kuwa, magari na miradi mingine aliyonayo si ofa kutoka kwa mchumba wake aitwaye Abdallah Mtoro ‘Dallas’ kama anavyodai mwenyewe Wolper bali ni ‘baraka’ ya Freemason.
Akasema: “Mmekuwa mkiandika eti kanunuliwa magari na mchumba wake, nani kasema? Ile ni kama njia ya kukwepea tu, lakini ukweli ni kwamba Freemason ndiyo wanambeba kwa sasa.”
Akaongeza: “Wazazi wa Wolper wapo katika wakati mgumu, mama yake amepata fununu za mwanaye kujiunga na Freemason na ndugu wakamweka chini kumwonya kama ni kweli ajitoe mara moja.”

KANUMBA ALIJIUNGIA NIGERIA
Hivi karibuni, mtu mmoja aliyejitaja kuwa ni mchungaji wa kanisa moja la kiroho jijini Dar, George Kariuki alizungumza kupitia Kituo cha Radio Times FM na kudai kuwa marehemu Steven Kanumba alijiunga na u-Freemason nchini Nigeria, nchi ambayo iko mbali kidogo kutoka Tanzania kuliko ilivyo Afrika Kusini anakodaiwa kwenda Wolper.
Hata hivyo, matokeo ya Kanumba kujiunga yalionekana, kupata mali kwa kasi ya ajabu, nyota yake kung’ara lakini mwisho wa yote ilifika mahali imani hiyo inatajwa na baadhi ya watu kuwa ndiyo chanzo kikuu cha kifo chake (Mungu amlaze pema peponi-amina).

BOFYA HAPA UMSIKIE WOLPER
Baada ya madai hayo, Risasi Jumamosi lilimsaka Wolper kwa nguvu zote na kubahatika kukutana naye siku ya Jumatano maeneo ya Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Baada ya salamu, msanii huyo mwenye aibu kwa mbali, alisomewa ‘mashitaka’ yake yote huku akiwa amemkazia macho paparazi.
Wolper: “Mh! jamani, mnajua haya mambo bwana yana siri kubwa ndani yake. Wako watu wanatajwa ni Freemason, wengine wapo lakini hawatajwi, ni kwa nini?”

WOLPER JIBU SWALI
Paparazi: “Labda kikubwa ungetuambia ni kweli upo huko au si kweli?”
Wolper: “Unajua bwana, mimi sina hela kama wanavyosema watu. Na haya yote yametokana na nilivyomsaidia Sajuki (Juma Kilowoko). Yule nilimsaidia kwa sababu niliguswa kutoka moyoni, lakini familia yangu yenyewe ina uhitaji mkubwa sana.
“Tena naomba jamii ielewe kuwa, sina ‘minoti’ ya kumwaga. Napata tabu watu wananifuata wakilia shida zao wakiamini nina fedha kibao, si kweli jamani.”

WOLPER VIPI?
Paparazi: “Umezungumza vizuri, lakini hujajibu suala la kujiunga na Freemason kama ni kweli au si kweli?”
Wolper: “Mimi gari si alininunulia Dallas, mbona nilishasema jamani au?”
Paparazi: “Sawa, ulishasema, vipi kuhusu Freemason sasa?”
Wolper: “Ni kwa sababu ya hizi nguo au? Maana nguo navaa bila kujua alama zake, sasa kama kuna za Freemason mimi nitajuaje jamani, ee?”

HAYA SASA
“Ila labda nikiri kitu kimoja, ni kweli niliwahi kuitwa na watu wakaniambia nijiunge kwenye imani hiyo, waliniahidi kwamba nikikubali maisha yangu yatakuwa mazuri na ulinzi wa afya yangu.”
Paparazi: “Ina maana hujajiunga unafikiria kwanza?”
Wolper: “We unaonaje, nijiunge au? Mimi sitaki nasikia wengi wameingia wanafanikiwa kwa kasi.”

MASWALI YA MHARIRI
Kama kweli Wolper si Freemason, amejuaje mavazi yake yana alama ya imani hiyo? Kwa nini anaomba ushauri huku anasema haitaki imani hiyo?  Risasi Jumamosi linaendelea kumfuatilia kwa karibu kuhusu shughuli zake za mchana kutwa.

Views: 20346

Tags: risasi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by CHRISS PATY on June 25, 2012 at 12:12pm

hivi nyie waandishi mna uhakika gani

Comment by IL-YA on June 15, 2012 at 5:59pm

Fidodido@ taratibu bwana,utanifanyiaje mipango kunipeleka kwenye ushetani bwana!! Ushindwe na ulegee kwa nguvu za Mwenyeezi Mungu Muumba aliyeumba Mbingu na Ardhi,akaweka humo viumbe vyake ili waishi humo,kisha viumbe hivyo vikaanza kumuasi Mola aliyeviumba na kuviweka humo kupitia kujiunga na Shetani rais wa waasi,ambae kajaza wafuasi wake katika dunia hii wenye kumsaidia kufanya kazi yake ya kishetani,ana mawakala kila kona,na wengine ni wasaidizi wa mawakala hao,na wengine ni wasaidi wa wasaidizi wa mawakala ambao kazi yao kubwa ni kufanya intimation  itoayo  wito wa kuelekea motoni na hakuna zaidi ya hilo.

Basi na wajue wanaomuasi Mwenyeezi Mungu Muumba kwa kukimbilia utajiri wa dunia kuwa hakima watapa utajiri utakaodumu kwa muda wa miaka 60,au 70 au 80,lakini adhabu inayowangojea baada yake itakuwa ni nzito mno,na itakuwa ni yenye kudumu milele.watadumu katika kuadhibiwa milele na milele.

Na hiyo ni Promise ya Mwenyeezi Mungu kwa viumbe wake watakaochagua kuwa wafuasi wa Shetani (katika maisha yao ya duniani) aliyelaaniwa na Mola.

Comment by Fidodido on June 14, 2012 at 7:42pm

Noti hutolewa  hata kwa weye  msukuma Rikwama  ila  Muhimu uwe na Ushuzi mkubwa ukiwa tayari wewe nambie tu nitakufanyia mipango@IL-YA.

Comment by Elisha J. Mwankundile on June 11, 2012 at 7:34pm

mbona raha....mtahangaika daima,MWACHENI MUNGU ABAKI KUWA MUNGU. aala

Comment by IL-YA on June 9, 2012 at 10:41pm

Si mbaya nikauliza sehemu hii: Ina maana hawa watu (Freemasons) hawataki watu maskini katika chama hicho au! maana naona kila wakati wanadili na watu mastaa au watu maarufu ,ama wale watu kabwela sioni wakiwaelekea,ina maana dini hiyo itakuwa ni ya watu matajiri tu,hebu tuweke wazi nyie mliokwisha jiunga huko na kupata minoti kimiujiza!?

Comment by young platnium on June 8, 2012 at 6:59pm

kwani jamani lazima mtu maarufu kujiunga na mason?

Comment by Ediclad Ansgary Kihinja on June 8, 2012 at 1:18am
Nawaomba waandishi muwe makini mnapo andika habari, Nimefuatilia mambo mbalimbali kuhusu Freemansory;na wanao jiunga ni wanaume tu na si wanawake. Si pingi moja kwa moja kuwa JACQULINE hayupo kwenye chama cha waabudu mashetani ila kama yumo basi yumo kwenye kile cha waumini wa kike tu nacho kina jina lake. kwa msaada hebu GOOGLE neno FREEMANSORY halafu nenda origin of freemansory kisha soma how a man become a freemansory
Comment by msichoke mlugu on June 7, 2012 at 8:49pm

watajeni na wengine sio hao tu

Comment by Elisha J. Mwankundile on June 7, 2012 at 4:05pm

''''the announcement for the new word order"""""

Comment by penina mwailunda on June 7, 2012 at 11:53am

Roho wa Mungu atupiganie na kutuonyesha nuru

UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

Latest Activity

kemeya posted a status
1 minute ago
ketrina1liono posted a status
2 minutes ago
suny suriyan posted a status
5 minutes ago
Polat Salla posted a status
6 minutes ago
skysports24 posted a status
11 minutes ago
skysports24 posted a status
11 minutes ago
suny suriyan posted a status
12 minutes ago
skysports24 posted a status
13 minutes ago
begumnurjahan posted a status
14 minutes ago
begumnurjahan posted a status
14 minutes ago
K Nagr posted a status
14 minutes ago
Shakil Hasan posted a status
15 minutes ago

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }