Fomu ya kujiunga na Freemason.

Kiongozi wa Freemasons Bongo, Sir Ande Chande.

Pete ya Freemasons.

Alama za Freemasons.

Jacqueline Wolper.

Marehemu Steven Kanumba.

Na Mwandishi Wetu
HATIMAYE fomu zenye maelekezo ya binadamu aliye tayari kujiunga na imani inayodaiwa ni ya kishetani ya Freemason inapatikana kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii huku ikizua kizaazaaa Bongo hasa kwa vijana wanaoamini ni njia ya kupata utajiri wa ghafla.
Ufukunyuku wa Ijumaa Wikienda umeiibua fomu hiyo yenye maelekezo kwa lugha ya Kiingereza ikimtaka mjazaji kuikabidhi ndani ya mtandao husika baada ya kuijaza.

MWONEKANO WA FOMU
Fomu hiyo nyeupe, juu ina rangi ya njano yenye maandishi ya utukufu kwa Mungu na ukamilifu wa kibinadamu (To the Glory of God and Perfection of Humanity).
Kushoto mwa fomu hiyo kuna picha ya mwanamke aliyesimama akiwa amenyoosha mkono ulioshika kitu chenye ncha kali kwa mwanaume aliyepiga magoti.
Inaonekana mwanaume huyo anaapishwa ili kuingia kwenye imani hiyo na pembeni kuna watu wamesimama wakishuhudia tukio hilo.

KUNA SIFA?
Sifa na masharti ambayo mwombaji anatakiwa kuwa nayo vinashangaza watu kwani baada ya mwombaji kuijaza, kuna mtu atampigia simu kwa ajili ya kujibu maswali ya mjazaji.
Kuhusu hilo kuna maelezo yanayosomeka:
If you are interested joining or just getting some more information, please fill out the form below and some one from order will contact you for your preference to answer any question you may have.
(Kama unapenda kujiunga au kupata maelezo zaidi, tafadhali jaza fomu hii chini na kuna mtu atawasiliana na wewe kwa ajili ya kujibu maswali yako yoyote uliyonayo).

KINACHOTAKIWA KUJAZWA
Hakuna makeke mengi kwenye fomu hiyo kama zilivyo za kugombea ubunge hivyo kufanya watu kumiminika mitandaoni kwa ajili ya kuijaza.
Fomu yenyewe inatakiwa kujazwa jina la kwanza na la pili. Mji anaoishi muombaji, mkoa na nchi.
Baada ya hapo, kuna sehemu inatakiwa kujazwa baruapepe (e-mail) na simu.
Aidha, kuna sehemu ya kuandika maoni kisha mwombaji anabonyeza mahali palipoandikwa submit (wasilisha).

FOMU YAZUA KIZAAZAA BONGO
Tangu kuibuka kwa wimbi la watu kudaiwa kujiunga na imani hiyo nchini, wasomaji wengi wa magazeti wamekuwa wakitaka kuwa wanachama.
Baadhi ya wasomaji hao wamekuwa wakipiga simu kwa namba za wahariri zinazopatikana magazetini wakiuliza wapi wanaweza kujiunga na Freemason.
Mfano mzuri juzi Jumamosi, msomaji mmoja ambaye hakuwa tayari kutaja jina, alipiga simu kwa wahiriri watatu wa Global, uhitaji wake ukiwa kuelekezwa sehemu ambayo ataweza kujiunga na imani hiyo yenye utata.

WACHUNGAJI MUWE MACHO
Kutokana na hali hiyo, iko sababu kwa watumishi wa Mungu (wachungaji) kufuatilia kwa makini imani hii na kuwafundisha waumini wao kama inakubalika kwa Mungu au la!
Wapo wanaodai Freemason si imani ya kishetani bali ni mahali ambapo mtu akijiunga anakuwa na maisha mazuri.
Hata hivyo, kuna madai kwamba ni imani ya kishetani ambapo ibada zake huambatana na kafara ya damu za wanyama, hususan mbuzi.

NINI KINAFUATWA FREEMASON?
Dalili zote zinaonesha kuwa wengi wanatamani kujiunga na imani hii si kwa sababu ya kuitafuta njia ya kweli na sahihi ya kufika kwa Mungu, bali tetesi ni kwamba ukiwa mwanachama wa Freemason utajiri njenje kama inavyodaiwa kuwatokea mastaa wa Kibongo, marehemu Steven Kanumba, Naseeb Abdul ‘Diamond’ na Jacqueline Wolper.
Utafiti wa Ijumaa Wikienda umebaini kuwa, Wabongo wengi wanatamani kuwa na maisha mazuri, nyumba na magari ya kifahari, hivyo wanaamini ni Freemason tu ndiyo itakayowakomboa.

Views: 251978

Tags: ijumaawikienda11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by john bosco on June 10, 2012 at 10:26am

hata wolper !!!!! msanii wa kik ambae nilikuwa nadhani kwamba ana  akili!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Comment by Hellen Attarsingh Gupta on June 10, 2012 at 9:42am

Hakika, Unabii wa Biblia unatimia mbele ya macho yetu. Mwenye macho haambiwi TAZAMA! Kwanza hata kama elimu ya mtu si kubwa, anaweza kujiuliza tu maswali ya kawaida kama:- 1. Kwa nini mambo haya yanafanywa siri?  Kama sio siri, kwa nini hayafundishwi darasani kama masomo mengine ya muhimu kwa binadamu? 2. Kama Freemason si wa Shetani, kwa nini wanadai makafara ya damu? 3. Kama mtu alijiunga kwa hiari yake, kwa nini kujitoa isiwe hiari? 4. Kama ni jambo jema, lina kibali cha nani? Naye kapewa na nani Mamlaka hayo? TAHADHARI:- Mtu anayetaka kujua zaidi, hasa wale wanaovutiwa kujiunga, waende kwenye mtandao, wafungue google , waandike Freemasonry, kisha wasome kwa makini, polepole, bila haraka yoyote, hata kama itachukua mwezi mzima kumaliza kusoma, waelewe picha ya tengenezo hili. Kisha mtu atafute muda mzuri wa utulivu, asali kwa bidii, amwombe Mwenyezi Mungu (Yehova) amfunulie ukweli.

Hakika, Mungu hataacha kukuonyesha ukweli, kama nia yako ni kuujua ukweli. 2Wakorintho 11:14 ; 2 Wakorintho 6:17 ; Zaburi 91:14 ; Mithali 19:22 ; Waebrania 10:39 ; Zaburi 111:10 ; Methali 3:5 ; (Methali 8:17-21. Tafakari kwa uzito zaidi andiko hili) . Mungu wa Pekee wa Kweli, awabariki sana mnaoutafuta ukweli.

Comment by IL-YA on June 9, 2012 at 10:17pm

Dini gani hii inayomtaka mtukutuma maombi anapotaka kujiunga?! utadhani chama cha siasa!!

Comment by Shukuru costantine on June 9, 2012 at 9:04pm
Muda mfupi tu unakula batta kwenda mbele
Comment by young platnium on June 8, 2012 at 6:57pm

mmmmmmmmmmmmhhhhhhhhh lakini sijui kammmmmmmaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!?

Comment by Paschal John on June 8, 2012 at 3:44pm

bora misha mafupi, lakini matamu, kuliko kuwa na maisha marefu lakini machungu.

Comment by neema erasto on June 8, 2012 at 2:33pm

INAFAIDA GANI UKAUPATA ULIMWENGU WOTE ALAFU UKAUKOSA UFALME WA MBINGUNI? FUNGUA MACHO

Comment by leonard de caprio on June 7, 2012 at 11:10pm

Ninasoma sanaa sanaa hasa mtandaoni na kwa kua muda mwingi nautumia kusoma ninachimba mambo mengi sana nimefurai kuona kaka na wewe ni mmoja wao kama mimi unapenda kujua mambo hasa kwa reference mbalimbali watanzania walio wengi ni wepesi wa kukubali jambo bila ya tafakari za kina...habari za U_ freemason c za leo kwa Marekani ni miaka zadi ya 300 , nakusudia kusema kuanzaia kupata uhuru wao taree 04 JULY 1776 chini ya Rais wa kwanza John Hanson ambapo baadae walianza kuujenga mji wa Washintong DC na majengo mengo mengine ya serikali kama Capitol alipoapishwa OBAMA jengo hili huonekana nyuma ya moja ya note zao , pia White House nk , mji huo umejenjwa ki freemason kwa alama ambazo wewe huwezi jua na kuona ila wao wanaoana na wanajua maana ake zimejengwa ktk pembe kama nyota na ikihusisha jengo moja na jingine hizi ni alama za ...shetani ambayo kama katk nyota huuita PENTAGRAM ambayo kila pembe according to the docrine of occultics..hizi pembe humaanisha mambo makuu matano hapa duniani..ikiwa ni MAJI , MOTO, NCHI, HEWA, na pembe ya tano ni ROHO YA SHETANI..ambayo katk raman ya Washington ikulu ndio pembe ya tano sasa kwa wewe ambae huna hili wala lile unaoana ni kama raman tuu kumbe watu wanaabudu hapo na ni imani zao wanajua zinavo wasaidia wenyewe kwanini wazi ni ushetani...ogopa sana hii watu hawa vivuli vyao vikuu ni misaada utaskia cc ni tunakaa kwa u friendship, fellowship au mara nyingi hizi Rotary kama lion , YMCA, WMCA, na nyingine nyingi ni ngumu sabna kujua hii mambo ila ipoo.Kingereza neno OCCULT lina maana hide from view...sasa sign zao zotee zimefichwa na huwezi ona ila wao tuu..anaglia pia note ya dola moja ya marekani utaoana kuna piramid haijaisha na juu ina jichoo....ushetani na freemason waliwai sema kweli ni lama zetu ila kwa sasa haina maana huon wamekubali afu tena wanabisha kwanini wasiitoe inajulikana kama ALL SEEING EYE..kwa kila anaeliona jichoo unaingia katk ibada zao hata kama huendii haina ubishi kila mtu anapenda pesa na hiyhiyo peasa inaigia kila mahali yaani bila ya MUNGU tumekwishaa..ukizidi fafanua kuhusuu hii piramid inaonesha kipindi cha kale OLD AGE na ikiisha kuanza na kutangwazwa kwa NEW WOLRD ORDER...Hivo hata maneno ya kirumi yaliyoandikwa pale kwene hilo jicho..yanasema ANNUIT COEPTIS...god c MUNGU huyuu huyoo wao TUSAIDIE KTK MARIKA YETUU(VIZAZI) god favor us through our ages , pia inamaanisha kwa tafsri nyingne tanagaza kuzaliwa kwa NEW WORLD ORDER..Hvo badoo hatujafika ndo mana hiyo piramida haijaisha unaweza soma katka mtandao na ukaona nini maana ya unfinished pyramid..Kwanini undahani wanataka mimi na wewe tuwe washiriki hata kama c moja kwa moja? Dunia ya leo imejionda ktk utegemezi na MUNGU na wanataka kukufanya uone kila kitu kinawezaekan bila uwepo wa MUNGU..NA KUFANYA KILA TUNACHOWAZA NAKUONA INAFAA una ushaidi wa kutosha sasa , mambo machafu kama ushoga, ulawiti, kuingiliana kinyume cha maumbile kwa wanawake imekua fashen leo , kusagana na mengine machafuu..afuu wanasubutu kusema hazarani bila ya woga BLATANT acts ni aibu , kila kilicho kichafu leo ndio kinachopendwa na wengi jiadhari sana ndg yangu..hata...Naomba niseme wazi mi nafatilia sana hivi vituu na napenda pia anaeviibua ila japo tusizidi potea Nimeona katk mazishi ya nyota wa TZ ktk filamu moja ya picha zilizotumika kumwakilisha na kuwekwa nyumbani mbele ya kitabu cha wageni ktk rambi rambi na pia ilitumika kuwekwa pembeni jeneza lake ktk kumwaaga..HAIKUA NZR..moja ina kama alama ya fuvu la kichwa binadamu na ina namba 13 , Alama hizi ni za kishetani na freemaso hutumia sanaa...ujue pia wa2 hawaeshimu ibada kuna watu wanajua maana ake ila wamekaa kimya..ipo picha ingine akiwa anatoa msaada ktk moja ya vituo vya watoto yatima mbele kuna majina ya waliowahi kufika hapo..picha kwa nyuma ina alama ambayo pia c nzr na hakupiga aonekane ila ionekane alama yenyewe..ni nyingi mi huwa hazi nivutii ndo mana naweka wazii hapa..ujue pia watu sasa hawana hofu ya MUNGU kwa imani zao watu wamebaki majina tuu umeona ktk msiba kumekua kma KLABU TUU..mtu umevaa hereni mwanaume umechoma nywele hapana hapo wewe sii MKRISTO wala ISLAM nguo mbaya mbayaaaa kifupii mi ckupenda maengii kwani ndo hayoo tunapelekwa na dunia hii..Staki niseme mengii mimi ila kwa wene akili wamejua nasema nini na nakusudia nini usiwe sahabiki tuu jua pia athari zake kwa kufikiriii.....

Comment by leonard de caprio on June 7, 2012 at 11:08pm
Januari 2005 nchini Isarel ‘walipata’ kiongozi mpya wa Freemasons, Chaim Henry Gehl, ambapo sherehe yao ilifanywa katika Hoteli ya Sheraton iliyopo Herzlia.
Wageni walitokana Uingereza, Ujerumani,Uholanzi, Austria, Luxemborg,Romania,Italia,Bulgaria na China. Kiongozi huyo alikuwa akikabidhiwa madaraka kutoka kwa Sami Raphaeli, mhasibu mstaafu wa benki mstaafu wa hekalu la Caspi lenye namba 56 lililopo mjini Haifa. Huyu cheo chake cha utendaji mkubwa katika freemasons ni 33rd degree alichotunukiwa mwaka 2003.
Naam katika kuselebuka huko ndipo wakajigamba kwamba mnamo Oktoba 9, 2004 kulifanywa sherehe ya kutimiza miaka 100 ya Freemasons katika eneo la afrika mashariki.
Hapa kwetu Tanzania haikusemwa sana, ingawaje Jayantilal Kashavji Chande , au Sir Andy Chande katika mahojiano yake na mwandishi wa Ernest C. Ambali(The Guardian, Oktoba 8, 2004) haikuelezwa mahali patakapofanyiwa sherehe hizo.
Katika mahojiano yale Sir Andy Chande alieleza kuwa mgeni rasmi alikuwa Rais Benjamini Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa. Pia kulikuwapo na wafanyabiashara wakubwa,wanadiplomasia,mawaziri n.k
Sir Andy Chande akiwa nchini India katika mji wa Chennai kuzindia hekalu lao East Star alieleza  kwamba ‘marais wawili wa kwanza wa Tanzania (hawakuwa freemasons) lakini walifahamu ni nini’. Je unahitaji akili gani kuwatambua marais wako? Unahitaji Mungu akuongezee ubongo gani ili utambue kuwa ni akina nani wanaozungumziwa? Ndiyo maana nasema tatizo siyo kasi uliyonayo bali kule uendako!
Tukubaliane, kuwa kwa kiasi Fulani inajionyesha ikulu zetu zimezingirwa na Freemasons. Na katika mahojiano hayo hakusemwi ni Dar es Salaam eneo gani ambao sherehe hiyo ilifanywa, lakini katika kumsimika Chaim Henry Gehl (kule Israel)ilitajwa Hoteli ya Royal Palm ambapo wageni 350 walihudhuria.
Katika miaka hii 100(108) ikaelezwa kuwa Freemasons walianza kujenga hekalu lao la kwanza la Harmony namba 3084 mwaka 1904 mjini Zanzibar.
Katika uzinduzi wa jengo hilo Zanzibar inaelezwa Rais Theodore Roosecelt alikuwapo, Duke of York(ambaye baadaye alikuja kufahamika kama Mfalme George VI)na Duke of Connaugh na Strathean walikuwepo pia.
Ukimsoma mwanahistoria Robert Muchembled(katika; A History of the Devil) ameorodhesha majina yenye kuabudiwa kwa ibada za kishetani lakini tunayathamini na kupofushwa nayo. Nami kwa matendo wanayoyatenda hapa duniani sina soni kusimamia hoja yangu kuwa ni ubatili mtupu waufanyao).
Naweka orodha ya mambo wanayojigamba Freemasons kujinasibu kwa miaka yao 100(108) ndani ya afrika mashariki huku wakibainisha kuwa makao makuu ya eneo zima ni barabara ya Nyerere, jijini Nairobi(soma;The Guardian, 0ktoba 8, 2004). Katika mahojiano hayo ndipo kukaorodheshwa ‘misaada’(ibilisi?), eti Kindwitwi Leprosy Centre(Utete), Mama Theresa Home for the children, shule ya vipofu(Pongwe, jijini Tanga), na Leprosy Projects (jijini Arusha).
Montessori School (jijini Mwanza), Mnazi Mmoja Hospitali (iliyopo Zanzibar), Missionaries of Charity, shule ya walemavu (Buguruni, jijini Dar es salaam), wamejenga madarasa shule ya msingi Kinondoni(Dar es salaam) na kutoa pauni za Uingereza 15,000 mnamo mwaka 1996 katika ajali ya Mv Bukoba. Ukiangalia ‘misaada’ yao unapumbazika kuwa ni hisani ya hali juu
Na tatizo kubwa linalotukabili, ni utegemezi ambao huzaa utumwa na kukengeuka akili zetu. Tunaishi huru mitaani lakini tupo gerezani, tunakwenda kasi sana lakini hatuangalii tunakokwenda, hatutaki kujua nini hiki tunachosaidiwa?
Ni mungu gani aliruhusu mashoga na wasagaji wasimame madhabauni/altareni? Naam ndivyo tunavyouvaa uovu, ndivyo yanakotakiwa Uganda Museven aliruhusu hali hiyo. Na wenyewe husingizia haki za kiraia au dini za kiraia, inaeleweka kuwa Marekani imejngwa na Freemasons kwani wanajieleza kwa mengi tu. Je nasi tuwe na akina Jack Straw wetu bungeni? Tuvuje jasho kwa kupitisha sheria za kuruhusu mashoga, wasagaji halafu tuseme mungu anaruhusu hayo?
VIGOGO  WA FREEMASONS  KATIKA  UKANDA  WA AFRIKA MASHARIKI  NA AFRIKA  KWA UJUMLA
Sir.Andy chande ajitokeza na kusema kuwa yeye ni mmoja wa freemason afrika mashariki .Pia hakuwa nyuma kuwataja viongozi wanaohusika kwenye chama hicho akiwemo rais mstaafu wa awamu ya tatu Mh.Benjamin Mkapa .
Pia alimtaja steven kanumba, msanii nguli hapa Tanzania,Baba Riz raisi wa Tz,lowassa,AY,Mr. Blue,na wengineo wengi. Pia hakusita kumtaja yoweri museveni raisi wa uganda,Obama raisi wa marekani,George Bush,Bill Clinton,George washington,Elizabeth malkia wa uingereza na wengineo wengi.
Sir.Andy Chande alitaja yeye kwenye chama hicho ni Grand District Master akiwa amebobea kwa miaka 18 iliyopita.
Alipoulizwa makao yao makuu hapa Tanzania yapo wapi alijibu bila kusita "we are located at sokoine Drive behind kilimanjaro hotel here in Dar es salaam" (tunapatikana barabara ya sokoine nyuma ya hoteli ya kilimanjaro).
Pia Sir. Andy alisema wananyaraka zote za kumiliki jengo hilo toka serikalini. Aliongezea kuwa vikao vyao hufanyika kwa siri nyakati za usiku na mtu akishaingia kwenye chama hiko hatotoka tena
TUKUTANE  KATIKA SEHEMU YA TATU  AMBAPO   TUTAZUNGUMZIA  JUU YA MALENGO YA FREEMASONS NA UJIO WA "NEW WORLD ORDER".......,
ASANTENI
Comment by leonard de caprio on June 7, 2012 at 11:07pm

Watanzania wenzangu tutahadhari na hali hii, vyombo vya habari na nyie natoa angalizo kwenu!!!! kama mmetumwa na hawa madhalim wa ulimwengu huu kuwafanyia promo ili u-masonia uonekane wa kawaida tu na iwe rahisi watanzania kujiunga basi hiyo kalamu mnayoitumia kuandika itawagharimu......Watanzania wenzangu, kwa moyo wa upendo na uzalendo wa mchi yetu na tunu nyingi tulizojaaliwa na aliye mkuu wa ulimwengu huu ni wazi kabisa kuwa hawa maadui wanazitamani neema hizi na wanaingia uchu wakuzinyakua na ikiwezekana hata kufanya dhulma kubwa ili kupata hicho wanachokitaka, sasahivi mawakala wao wameanza kujitokeza waziwazi bila aibu wala hofu kama ilivyokuwa mwanzo....sasa tujue kabisa wameshajipanga hivyo ndugu zangu amkeni na tupige vita kwa nguvu zetu zote imani hii ikiwezekana wananchi wapenda amani tuombe idhini ya Serikali yetu tupoteze kabisa haya Makazi ya mashetani katika nchi yetu, nasi tunayajua yote na majina ya taasisi zao.

UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }