Fomu ya kujiunga na Freemason.

Kiongozi wa Freemasons Bongo, Sir Ande Chande.

Pete ya Freemasons.

Alama za Freemasons.

Jacqueline Wolper.

Marehemu Steven Kanumba.

Na Mwandishi Wetu
HATIMAYE fomu zenye maelekezo ya binadamu aliye tayari kujiunga na imani inayodaiwa ni ya kishetani ya Freemason inapatikana kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii huku ikizua kizaazaaa Bongo hasa kwa vijana wanaoamini ni njia ya kupata utajiri wa ghafla.
Ufukunyuku wa Ijumaa Wikienda umeiibua fomu hiyo yenye maelekezo kwa lugha ya Kiingereza ikimtaka mjazaji kuikabidhi ndani ya mtandao husika baada ya kuijaza.

MWONEKANO WA FOMU
Fomu hiyo nyeupe, juu ina rangi ya njano yenye maandishi ya utukufu kwa Mungu na ukamilifu wa kibinadamu (To the Glory of God and Perfection of Humanity).
Kushoto mwa fomu hiyo kuna picha ya mwanamke aliyesimama akiwa amenyoosha mkono ulioshika kitu chenye ncha kali kwa mwanaume aliyepiga magoti.
Inaonekana mwanaume huyo anaapishwa ili kuingia kwenye imani hiyo na pembeni kuna watu wamesimama wakishuhudia tukio hilo.

KUNA SIFA?
Sifa na masharti ambayo mwombaji anatakiwa kuwa nayo vinashangaza watu kwani baada ya mwombaji kuijaza, kuna mtu atampigia simu kwa ajili ya kujibu maswali ya mjazaji.
Kuhusu hilo kuna maelezo yanayosomeka:
If you are interested joining or just getting some more information, please fill out the form below and some one from order will contact you for your preference to answer any question you may have.
(Kama unapenda kujiunga au kupata maelezo zaidi, tafadhali jaza fomu hii chini na kuna mtu atawasiliana na wewe kwa ajili ya kujibu maswali yako yoyote uliyonayo).

KINACHOTAKIWA KUJAZWA
Hakuna makeke mengi kwenye fomu hiyo kama zilivyo za kugombea ubunge hivyo kufanya watu kumiminika mitandaoni kwa ajili ya kuijaza.
Fomu yenyewe inatakiwa kujazwa jina la kwanza na la pili. Mji anaoishi muombaji, mkoa na nchi.
Baada ya hapo, kuna sehemu inatakiwa kujazwa baruapepe (e-mail) na simu.
Aidha, kuna sehemu ya kuandika maoni kisha mwombaji anabonyeza mahali palipoandikwa submit (wasilisha).

FOMU YAZUA KIZAAZAA BONGO
Tangu kuibuka kwa wimbi la watu kudaiwa kujiunga na imani hiyo nchini, wasomaji wengi wa magazeti wamekuwa wakitaka kuwa wanachama.
Baadhi ya wasomaji hao wamekuwa wakipiga simu kwa namba za wahariri zinazopatikana magazetini wakiuliza wapi wanaweza kujiunga na Freemason.
Mfano mzuri juzi Jumamosi, msomaji mmoja ambaye hakuwa tayari kutaja jina, alipiga simu kwa wahiriri watatu wa Global, uhitaji wake ukiwa kuelekezwa sehemu ambayo ataweza kujiunga na imani hiyo yenye utata.

WACHUNGAJI MUWE MACHO
Kutokana na hali hiyo, iko sababu kwa watumishi wa Mungu (wachungaji) kufuatilia kwa makini imani hii na kuwafundisha waumini wao kama inakubalika kwa Mungu au la!
Wapo wanaodai Freemason si imani ya kishetani bali ni mahali ambapo mtu akijiunga anakuwa na maisha mazuri.
Hata hivyo, kuna madai kwamba ni imani ya kishetani ambapo ibada zake huambatana na kafara ya damu za wanyama, hususan mbuzi.

NINI KINAFUATWA FREEMASON?
Dalili zote zinaonesha kuwa wengi wanatamani kujiunga na imani hii si kwa sababu ya kuitafuta njia ya kweli na sahihi ya kufika kwa Mungu, bali tetesi ni kwamba ukiwa mwanachama wa Freemason utajiri njenje kama inavyodaiwa kuwatokea mastaa wa Kibongo, marehemu Steven Kanumba, Naseeb Abdul ‘Diamond’ na Jacqueline Wolper.
Utafiti wa Ijumaa Wikienda umebaini kuwa, Wabongo wengi wanatamani kuwa na maisha mazuri, nyumba na magari ya kifahari, hivyo wanaamini ni Freemason tu ndiyo itakayowakomboa.

Views: 250480

Tags: ijumaawikienda11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by Hellen Attarsingh Gupta on February 20, 2013 at 5:17pm

Hizi ni siku za mwisho wa mfumo huu wa mambo. Kila mtu ajipime imani yake, kupitia Neno la Mungu Biblia (Kwa Wakristo). Kama watu wanajiunga kwa sababu ya utajiri na si kwa sababu ya upendo wao kwa Mungu, iko wazi, kwamba wako tayari kwa lolote, ili wawe matajiri. TAHADHARI: Yesu kristo, Mwana wa Mungu, alishawishiwa na Shetani amsujudie ili apewe utajiri, akakataa. Mathayo4:8-11. Unadhani kwa nini Yesu alikataa utajiri wa kupewa ki hivyo? Tafakari. Hata ukipata kila unachokihitaji hapa duniani, kama uhusiano wako na Mungu wa Kweli Yehova hauko vizuri, hutakuwa na tumaini la uzima wa milele. Kwa sababu Biblia inasema, uzima wa mtu haupo katika wingi wa mali alizonazo.Luka 12:15. Tumwombe Mungu akiokoe kizazi chetu kutoka katika tamaa mbaya ya utajiri wa haraka-haraka. Wafanye kazi kwa bidii, ili wapate maisha mazuri kihalali. Pia wakumbuke, maisha ya sasa yanapita kasi, si ya kudumu. Katika Ulimwengu Mpya chini ya utawala wa Yesu Kristo, ndipo tutapata uzima ulio kweli kweli, bila magonjwa, uzee, uhalifu wala kifo. Ufunuo 21:3-5.

Comment by Mgisha Jackson on February 20, 2013 at 10:59am

kweli acha mambo ya ajabu basi tutafute njia ya kuepuka haya mambo

Comment by Emmie Saitoti on December 17, 2012 at 2:17pm

Subhana llaw dunia imekwisha bora tufe masikini kuliko kutoa kafara za wale tuwapendao mungu atulinde na kutupa muongozo mwema na si kupita njia fupi zenye tamaa na majaribu mengi ya kumwaga damuuu...

Comment by richardngeze on November 19, 2012 at 10:13am

Hajiungi mtu hapo!

Comment by Edwina Edwin on June 23, 2012 at 4:49pm

Huyo chande afukuzwe tanzania kwani atatumalizia vijana wetu wenye tamaa kwa hiyo imani yake ya kishetani..huko nje wanaiponda na wameona waelekeze nguvu zao Africa.. ni kipindi cha watanzania kukemea vitendo vyao vya kishetani.. wanatufanya sisi ni jalala la kutumia ujinga wao.. wao ndio mashoga, devil worshippers , vita na kila kitu.. watuache kwa jina la Yesu.

Comment by Fauster H. Lasway. on June 20, 2012 at 12:50pm

Mungu na atusaidie,, maanaa!!!!

Comment by Bakari Mchila on June 18, 2012 at 3:33pm

Kama ni dini ya kishetani, kafara haitakuwa ya kuku au mbuzi bali binadam. Na ukishidwa kutoa mtu inaonekana wanakuchukua wewe mwenye then inkua the END of ur life. Watu waache ushirikina jamani ni mbaya sana. Hata huu ufreemason mdogo wa kwenda kwa waganga, umeshawaliza wengi. Kama mtu hujui bora uache.

Comment by Leons Freedom on June 12, 2012 at 3:54pm
Hakuna Zawadi ya Shetani iliyo ya Bure, Atakupa na mkono wakulia atachukua na wa kushoto kitu ambacho ni muhimu sana maishani mwako, Ndugu Zangu mwombeni MUNGU aliye Juu sana nae atawapa kwa wakati wake na sio wakati mnaotaka ninyi.LORD JESUS CHRIST SAVE US FROM THE HANDS OF OUR ENEMIES AMEN!
Comment by Astely kapinga on June 12, 2012 at 2:32pm

tusisahau kuna usemi usemao kwamba ''UKIONA CHA ELEA UJUE KIMEUNDWA'' hii imani ya freemason imundwa na shetani,ni njia ya shetani tu kuwanasa binadamu wapendao vya dezo na kama kweli members wake wanapata utajiri basi hao members  wajue kabisa huo utajiri wataulipia kwa gharama kubwa zaidi,,embu tumuogope Mungu jamani,,duniani tunapita tu,,kuna faida ghani ya kuwa na utajiri ambao utagharimu maisha yako na ya ndugu zako,,tusidanganyike na hawa jamaa

Comment by neema molleli on June 11, 2012 at 4:23pm

JESUS CHRIST rufunike kwa damu yako taamaa za mali za kifreemason zishindwe kwa jina la YESU

UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

Latest Activity

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }