FAIDA YA INATIBU NINI?
Ni dawa ya kikohozi, inasaidia kuondoa baridi mwilini, inasaidia kuondoa gesi ndani ya tumbo, inatibu mtu mwenye matatizo ya tumbo hasa likiwa linasokota, ukitumia tangawizi iliyopikwa kwa sukari, kuchanganywa na maji ya moto kisha mwenye tatizo akinywa glasi 3 za maji hayo kwa siku inasaidia kuchangamsha mzunguko wa damu mwilini.
Mbali na hayo tangawizi husaidia kuondosha ute wa mdomo.

JAM YA TANGAWIZI
Jinsi ya kuitengeneza
Kamua tangawizi mbichi, kisha changanya maji yake (juisi) na sukari. Chemsha mpaka mchanganyiko huo uwe mzito. Ongeza zafarani iliyosagwa, iliki iliyosagwa, kungumanga zilizosagwa na karafuu iliyosagwa.
Iweke dawa hii vizuri na tumia inapohitajika kwa kutumia, unapoitumia jamu hii unakuwa umeongeza kitu mwilini.

Kuvumbiwa na kukosa hamu ya chakula
changanya vipimo vilivyo sawasawa vya juisi ya tangawizi na sukari mawe. Koroga vizuri, kunywa kabla ya kula.
Changanya juisi ya tangawizi, juisi ya limao na chumvi mawe kwa vipimo vilivyo sawa. Hakikisha umechanganya vizuri. Kunywa dawa hii kabla ya kula.
 Dawa hii husafisha ulimi na koo na hukuongeza hamu ya kula na kukufanya mchangamfu.

MAUMIVU YA KOO NA KUKAUKA SAUTI
Tafuna vipande vidogo vya tangawizi.

KWA KUHARISHA
Chua sehemu zinazozunguka kitovu kwa juisi ya tangawizi.

KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA
Kunywa mchanganyiko wa juisi ya tangawizi na juisi ya kitunguu.

BARIDI YABISI SUGU
Changanya kijiko kimoja cha tangawizi ya unga na vijiko 24 vya maji ya kunywa, mchanganyiko huu ukiwa wa vuguvugu. Ulale na ujifukize mpaka utoe jasho.

MAUMIVU YA JINO NA KICHWA
Chukua tangawizi ya unga koroga na maji kidogo iwe nzito kama tope. Jipake na uchue kwenye paji la uso kabla ya kulala. Kwa jino lipake na uchue kwenye shavu.
Tangawizi si tu hutibu magonjwa mbalimbali bali pia ni kiburudisho. Mathalani unapokuwa na mafua makali na kikohozi, osha kisha twanga tangawizi na uichemshe katika maji kwa muda mrefu.
Unaweza kuweka majani ya chai au maziwa na kisha kunywa taratibu ikiwa ya moto. Fanya hivyo kwa siku mbili, mafua na homa hushuka.
Faida nyingine ni kurekebisha siku za hedhi kwa akina mama. (GINGER)

Views: 3088

Tags: makala11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

NI SUPERMARKET GANI BORA KULIKO ZOTE KATI YA HIZI? NA KWA NINI? TOA MAONI YAKO!
  

Forum

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson on Friday. 11 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by mark gibson on Friday. 28 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

JUAN MATA KUTUA MANCHESTER UNITED ATASIADIA KULETA MATOKEO BORA BAADA YA TIMU KUSUASUA?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson on Thursday. 88 Replies

Juan Mata anataraji kutua Manchester United akitokea klabu ya Chelsea ya…

KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KILA MARA, TATIZO NI NINI?

Started by GLOBAL in Habari. Last reply by mark gibson on Friday. 45 Replies

VITENDO VYA KUKAMATWA WATANZANIA NA MADAWA YA KULEVYA KWA SASA VIMEZOELEKA. KATIKA NCHI MBALIMBALI WATANZANIA WAMEKUWA WAKIKAMATWA KWA UBEBAJI WA MADAWA HAYO. JE, TATIZO NI NINI? NA NINI KIFANYIKE?

Tags: MARA, TATIZO, NI, NINI?, KILA

JESHI LA POLISI KUTOA MILIONI 100 KWA ATAKAYEWEZESHA KUPATIKANA WAHALIFU WANAOMWAGIA WATU TINDIKALI NI KWAMBA LIMESHINDWA KAZI?

Started by GLOBAL in Maisha. Last reply by mark gibson on Friday. 74 Replies

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.Jeshi la Polisi…

SIMBA SC WAMTUPIA VIRAGO JUMA KASEJA

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by mark gibson yesterday. 12 Replies

TIMU ya Simba SC leo imetangaza rasmi kuachana na mlinda mlango wake mahiri, Juma…

JE, NI SAHII KWA JESHI LA POLISI KULIPUA MABOMU WAKATI WANANCHI WAKIAGA MIILI YA WENZAO?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mark gibson 23 hours ago. 36 Replies

Juzi (Jumanne) polisi walilipua mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokuwa wamekusanyika katika Viwanja vya Soweto jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili ya wenzao watatu waliopoteza maisha katika…

UKIMYA WA VYOMBO VYA DOLA KUTOA TAARIFA ZA MATUKIO YA MAUAJI NA UTEKAJI NI ISHARA KUWA WANAHUSIKA?

Started by GLOBAL in Habari. Last reply by mark gibson 5 hours ago. 21 Replies

Absalom Kibanda akiwa ICU.USIKU wa Jumanne ya Machi 5 kuamkia Machi…

Tags: UTEKAJI, NA, MAUAJI, NI, ISHARA

TOP NEWS WEEK HII

Loading… Loading feed

© 2014   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service