Diamond akisalimiana na mtasha kwa ishara ya Kifreemason.

Stori: Shakoor Jongo na Erick Evarist

SIRI imefichukua kuwa madai kwamba ‘kichaa’ wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ ni memba wa jamii ya siri inayodaiwa kumwabudu shetani, Freemason a.k.a Wajenzi Huru zilianza kitambo lakini sasa zimeshika kasi baada ya kunaswa kwa picha inayomuonesha akisalimiana na mtasha kwa ishara ya Kifreemason, Ijumaa Wikienda linaibumburua.
Kwa mujibu picha hiyo, tukio hilo lilijiri nchini Uingereza, mwaka jana, Diamond alipokwenda huko kwa ajili ya shoo.

MAVAZI
Ilidaiwa pia kuwa mavazi ya Diamond (meusi) yalishabihiana sawia na yale ya mtasha huyo yanayoelezwa kuwa sehemu ya mavazi ya jamii ya Freemason.

ISHARA
Kingine kilichoibua maswali ni ishara ya salamu ya wawili hao ambayo ilitengeneza nembo ya Freemason ya ‘V’ au bikari kwa namna walivyogusana kwa vidole.
Kwa mujibu wa wadau walioiona picha hiyo iliyonaswa kwenye mtandao wa Twitter, Diamond amekuwa na ishara nyingine nyingi za aina hiyo hivyo kuzidi kuzua utata kama ni memba wa jamii hiyo.
“Lakini inawezekana kwa sababu nasikia ukishajiunga unapata mafanikio ya ghafla. ‘So’ kuhusu hili, sina upande wa kusimamia,” ilisomeka sehemu ya maoni kwenye mtandao huo baada ya kuibuka mjadala mzito juu ya ishu hiyo inayozidi kushika kasi mithili ya moto wa kifuu.
“Tungeshukuru kama Diamond mwenyewe angejitokeza aseme ukweli kwani akinyamaza anazidi kutuweka njia panda,” ilisomeka sehemu nyingine ya maoni hayo huku ikiungwa mkono na wengi.

UNATAKA KUMSIKIA DIAMOND? SOMA HAPA
Ili kumaliza utata wa je, Diamond ni Freemason au la, Ijumaa Wikienda lilibeba jukumu la kumtafuta ili aanike ukweli wake ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Unajua mwanzoni nilikuwa sikumbuki ni lini na wapi nilipiga picha ya dizaini hiyo. ‘Anyway’, isiwe kesi, nakumbuka ilikuwa Uingereza kipindi kile nilikuwa na shoo nchini humo.
“Nakumbuka walinifuata watasha wengi tofauti lakini huyo mmoja alining’ang’ania sana nipige naye picha.
“Kwa kweli alinilazimisha sana kwa sababu mwanzo nilikataa lakini baadaye nikaona isiwe ishu nikampa ushirikiano alioutaka.
“Mimi sikuona matatizo alivyotaka tusalimiane kwa kugusisha vidole kwa sababu nilikuwa sijui chochote kuhusu Freemason. Nimeijua baada ya mambo haya kuyasikia kwa sana hivi karibuni.
“Kwa hiyo inawezekana siku hiyo waliniunganisha bila mimi kujua (kicheko).”

SASA UKWELI NI UPI?
Mara kadhaa Diamond amekuwa akihusishwa na Freemason kutokana na mafanikio ya ghafla aliyoyapata na mvuto alionao kwa mashabiki wake ndani na nje ya Bongo.
Ijumaa Wikienda lilipotaka kupata ukweli kutoka kwake, Diamond alifunguka:
“Si kweli bwana, mimi nazisikia tu hizi habari kama wengine. Nasikia tu ipo hapa Bongo na kiongozi wake ni Sir Andy Chande, zaidi ya hapo sijui chochote.
“Mimi ni mtu wa swala tano na mafanikio yangu naamini Mungu ndiyo kila kitu.”

KUNA MSANII MWINGINE
Mbali na mwigizaji Jacqueline Wolper na marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’ ambao wamekuwa wakitajwatajwa na mambo ya Ufreemason, Ijumaa Wikienda limetajiwa msanii mwingine ambaye yupo mbioni kujiunga akidai anakwenda kufuata utajiri.

AANZA KUPATA MAFANIKIO
Msanii huyo ambaye ni mwigizaji mwenye jina (tunalihifadhi kwa sasa) anadaiwa kuanza kupata mafanikio ya ghafla hivyo Ijumaa Wikienda lipo mzigoni na litakapomuweka kati litamrusha hewani.

Views: 26976

Tags: ijumaawikienda11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by julius moses nnko on July 12, 2012 at 3:39pm

tanzania ya freemanson itakuwa tajiri

Comment by Khalid Japhary GOMEKA on July 2, 2012 at 4:21pm

Aisee na mimi ngoja nikachukue form

Comment by Tematema Jeremia on June 16, 2012 at 4:48pm

Angalia kijana usije ukamaliza ukoo wako kwa kutoa sadaka kwa mashetani

Comment by FIKRA PEVU on June 15, 2012 at 9:46am

aah EDWINA UMENIKONGA MOYO NDUGU YANAKILI YANGU WAJANJA NA MATAJIRI WA AKILI KAMA MIMI NA WEWE TUPO WACHACHE SANA HAPA TZZ

Comment by FIKRA PEVU on June 15, 2012 at 9:45am

aah EDWINA UMENIKONGA MOYO NDUGU YANAKILI YANGU WAJANJA NA MATAJIRI WA AKILI KAMA MIMI NA WEWE TUPO WACHACHE SANA HAPA TZZ

Comment by FIKRA PEVU on June 15, 2012 at 9:40am

hakuna cha freemason hapo mnampa misifa tuu huyo mshirikina wa uchochoroni hana lolotee..

Comment by msichoke mlugu on June 14, 2012 at 9:50pm

acheni majungu bwana kila anayefanikiwa ni freemason mnashangaza

Comment by Mamy Shaluathu on June 14, 2012 at 3:50pm

Diamond kaza buti kashfa za ufreemason kama hazikuhusu zisisumbue kichwa chako.

 

Comment by Bryso Wilson on June 14, 2012 at 10:03am

Watanzania mara ningi tunakalia majungu bila sababu mtu akijituma anaitwa freemason tuache majungu jitume na wewe utafanikiwa siyo kusema ya mtu wakati ya kwako yamekushinda unafuatilia ya watu siyo vivuri tubadilikinen bwana

Comment by judith jonathan on June 13, 2012 at 9:30pm

Bro....acha waseme una lako moyoni, kama kweli ama la..! mnabishana mpaka mchomane visu bure kisa  Diamond ni freemason...binadamu hamna dogo, kwani ukijifunguia kwako ukala dagaa wako na ugali, hutaishi? kwanza hivi yanawahusu nini? kila m2 na moyo wake hata ww ukipenda unaingia..MNANIKERA SANA MIMI..Diamond Baba kaza buti na mwakani tena Tuzooooooooooooooo, mpaka watajinyonge na bg G

ADVERTISEMENT


Advertisement

 

Forum

KIPIGO CHA BAO 2-1 KWA MAN UTD, KOSA LA MWAMUZI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Mohammed Mar 26. 6 Replies

JE, NI KWELI KWAMBA KIPIGO CHA BAO 2-1 ILICHOKIPATA MAN UTD KUTOKA KWA REAL MADRID USIKU WA KUAMKIA LEO LAWAMA ZOTE ZIMWENDEE MWAMUZI WA MCHEZO AU MAN UTD WAJILAUMU WENYEWE? TUPE MAONI YAKO!!!

HALI INAYOENDELEA BUNGENI, SPIKA NA NAIBU WAKE WAMESHINDWA KUONGOZA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Ali Abdalla Ali Apr 22. 20 Replies

Tumeshuhudia kwa siku za hivi karibuni hali halisi iliyokuwa inatokea katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, kwa hali hii ni ishara kuwa Spika na Naibu wake washindwa kuliongoza bunge hilo?

VURUGU ZA CCM NA CHADEMA KUGOMBEA MLINGOTI WA BENDERA DODOMA, NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Phinehas Rishiansia Kileo May 3. 6 Replies

Wafuasi wa CCM wakimshambulia mfuasi wa Chadema mkoani Dodoma…

Tags: BENDERA, WA, DODOMA, NANI, KULAUMIWA?

VURUGU ZINAZOENDELEA HAPA NCHINI NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mayalilwa Mar 8. 26 Replies

HIVI KARIBUNI KUMEKUWEPO UPOTEVU WA AMANI HAPA NCHINI PAMOJA NA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI. MKOANI KAGERA WANANCHI WENYE HASIRA WALIWAUA POLISI, IJUMAA ILIYOPITA WAKULIMA NA WAFUGAJI HUKO WILAYANI KILOSA WALIZUA VURUGU NA KUFUNGA BARABARA,…

MRISHO NGASSA KUPELEKWA SIMBA SC BILA RIDHAA YAKE, JE NI HALALI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Domino Bagambisa Jan 21. 17 Replies

Kiungo hatari wa Azam FC, Mrisho Ngassa leo amepelekwa Simba SC kwa mkopo na timu yake…

Tags: SOKA

hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Started by Gysper in Siasa. Last reply by Jamal amor May 9. 24 Replies

 hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Kauli Ya JK kuwa Mauaji ya Arusha ni "Bahati Mbaya"

Started by Kulikoni Ughaibuni in Siasa. Last reply by richardngeze Feb 12. 12 Replies

Tanzania tuna tatizo kubwa.Hakuna haja ya kunyoosheana vidole as to nani amechangia tatizo hilo bali cha muhimu na haraka ni namna tutakavyoweza kutatua tatizo hili.Nisimung'unye maneno: tatizo kubwa linaloikabili ni kuwa na Rais ambaye takriban…

© 2013   Created by Global Publishers.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service