‘DIAMOND’ AKABIDHI MISAADA HOSPITALI YA LIGULA, MTWARA

Mwanamuziki Diamond (katikati) akipena mikono na Dk. Mdoe wakati wa zoezi la kutoa misaada Hospitali ya Ligula.  Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Safari Radio Foundation, Haroun Maarifa.  Wengine ni wafanyakazi wa hospitali hiyo.

Na Sijawa Omary, Mtwara
MSANII anayetamba katika muziki wa kizazi kipya (Bongo Flava), Naseeb Abdul ‘Diamond’,  ametoa misaada mbalimbali yenye thamani ya sh. 3,500,000 na laki tano katika wodi ya wazazi ya  Hospitali ya Ligula Mkoa Mtwara.

Akikabidhi msaada huo, Diamond alisema  yeye kama msanii amevutiwa kutoa msaada katika wodi ya wazazi kwa kuwa watoto wanaozaliwa watakuwa mashabiki wake na watapenda kazi zake hapo baadaye.  Msaada msaada huo umefadhiliwa na Safari Radio Foundation.

Alisema pia hufanya hivyo ni kuwa karibu na jamii katika kujenga upendo na mshikamano ili kupata ushauri ambao utakuwa tija katika utendaji wa kazi zake  kwani yeye pekee hawezi kupanga jambo pasipo kupata mwongozo kutoka kwa wadau wake.

“Wazazi ni watu wa kuwaheshimu na kuwaenzi  kwani kazi wanazotufanyia ni kubwa na nzito katika hatua zote hadi kufikia hapa tulipo,” alisema.
Aidha aliushukuru uongozi wa Safari Radio Foundation kwa kumpa fursa hiyo ya pekee kwani amepata faraja na heshima kubwa katika jamii sambamba na mashabiki wake kwa jumla.

Naye Mkurugenzi wa Safari Radio Foundation  ambaye pia ni Mkurugenzi wa Safari Radio FM, Haroun Maarifa,  alisema  taasisi yake imelenga katika kudumisha umoja na mshikamano.
Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Mdoe Mhuza, ameushukuru uongozi huo kwa msaada uliotolewa ambapo umeonyesha moyo wa kusaidia wagonjwa.

Mhuza aliwataka watu wengine kuiga mfano huo kwani siyo lazima kuitegemea serikali kwa kila kitu, na kwamba kutoa ni moyo siyo utajiri.

  






Views: 777

Tags: AKABIDHI, HOSPITALI, LIGULA, MISAADA, MTWARA, YA, ‘DIAMOND’

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by samora rajab albert on October 17, 2011 at 7:25pm
hongera Diamond
Comment by DINA FLAMINGO on October 17, 2011 at 6:26pm
Mungu akubariki
Comment by Glady-Cathy on October 17, 2011 at 4:41pm
VIZURI SANA DIAMOND NA MUNGU AZIDI KUKUZIDISHIA, KUKULINDA NA KUKU BARIKI
Comment by hadija abdallha on October 17, 2011 at 3:47pm
mungu akubariki kwa kutoa msaada sasa unaendana na kioo cha jamii, hayo ndo mambo ya kufanya na kuandikwa katika gazeti ili tukupe heshima unayostahili. big up kaka sasa umekua kiakili.
Comment by FURAHA TAUSI on October 17, 2011 at 3:31pm
HAPO UPO SAWA
Comment by simpo makoye on October 17, 2011 at 3:10pm
hapo sawa kijana ,bigup sana mungu akuzidishie.
Comment by lumi mwandelile on October 17, 2011 at 2:38pm
kazi nzuri, hivyo ndo inavyotakiwa
Comment by lawrence joseph mwonyonyi on October 17, 2011 at 2:24pm

KEEP ON DIMOND NOW YOUR GROWN UP.

BIG UP.

 

Comment by Muni Nassir Tawil on October 17, 2011 at 1:55pm

mungu akubarik

 

Comment by VJAY on October 17, 2011 at 1:41pm
kidogo sasa naona umeanza kuwa na nidhamu na ukiendelea na tabia hiyo utafika mbali mana kwa kufanya hivyo utakua umemkopesha  MUNGU..


ADVERTISEMENT


TANGAZA HAPA

ADVERTISEMENTS

Latest Activity

GUNZ TRUVADA posted a status
"KUMPA ASIYE KUPA NI SAWA SAWA NA KUTUPA"
4 minutes ago
othman Ochu posted a status
"SCENE 1 WAHUSIKA: AMIDU , SHARIFA MAHALI: ZANZIBAR MUDA : JIONI ( WAKIWA WANASHUKA TOKA KATKA BOTI YA JION KUINGIA KATKA MJI WA ZANZI"
9 hours ago
Priscus Adelard shared GLOBAL's blog post on Facebook
9 hours ago
mrembo commented on julius manning's photo
Thumbnail

Mtanzania huru

"pole sana usijali iko siku mungu atakujaalia mungu hamtupi mja wake"
10 hours ago
mrembo commented on Sili Silali's photo
Thumbnail

Duh!

"mama mzima hayawani mavazi gani hayo takupa mfano chungwa likiwa halijamenywa unatamani ulile…"
10 hours ago
kaka commented on Ali Amur Ali's video
Thumbnail

AZIMIO LA KUANGAMIZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE

"hapo ni kina dada kutua comment zao"
10 hours ago
Gaston Kayombo commented on Ali Amur Ali's video
12 hours ago
roylicious and Jackson Jacob are now friends
12 hours ago
babu wa loliondo (cup) updated their profile
12 hours ago
julius manning commented on julius manning's photo
Thumbnail

vijana 2016 itakuwa hivi

"@furaha mimi ni kikongwe hayo ni kazi kwako."
13 hours ago
Masalu Mayeji Many'hasimha shared GLOBAL's blog post on Facebook
13 hours ago
kheri zewe commented on Sili Silali's photo
Thumbnail

Duh!

"minyama uzembe"
13 hours ago

© 2012  

Designed & Developed by
G5 CLICK COMPANY.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

How to make a Website