DAWA YA LOLIONDO: WALIOKUNYWA KUPUKUTIKA

Wagonjwa wote wa kisukari waliokunywa dawa kwa Mchungaji Ambilikile Masapile ‘Babu’ kijijini Samunge, Loliondo watakufa (au watapukutika) ikiwa wataacha kutumia dawa za hospitalini, Uwazi limegundua.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa gazeti hili, watu wengi waliokunywa dawa ya Babu ambao walikuwa na ugonjwa wa kisukari wamefariki dunia baada ya kuacha kutumia dawa za hospitalini.
Baadhi ya ndugu waliozungumza na gazeti hili walisema kuwa, mara baada ya ndugu zao kunywa dawa ya Babu, waliacha kunywa dawa za hospitali na matokeo yake sukari ilipanda au kushuka, hivyo wakaaga dunia.

Ndugu wa marehemu Juliani Lyasenga mkazi wa Arusha ambaye alibahatika kunywa dawa ya Babu kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari, alikufa baada ya kuacha kutumia dawa kama alivyoelekezwa na daktari wake.
Mwingine ambaye alikufa baada ya kunywa dawa ya Babu kutokana na kuugua kisukari ni John Piswa, mkazi wa Tandika, Rafael Kisijo mkazi wa Kijitonyama, Saidi Mohamed mkazi wa Buguruni na Hausi X. Hollo “HH”, mkazi wa Gongo la Mboto.

HAITIBU KISUKARI
Licha ya dawa hiyo ya Babu kuaminika kuwa inatibu magonjwa kadhaa sugu ukiwemo wa kisukari, imeelezwa kuwa hadi sasa hakuna dawa iliyothibitishwa kitaalam kuwa na uwezo wa kutibu maradhi hayo.

“Kwa kifupi, hii ni aibu. Serikali haipaswi kuogopa kusema ukweli kuwa dawa ya Babu haitibu kisukari. Wote wanaosumbuliwa na ugonjwa huo nawaomba wasiache kutumia dawa za hospitali.
Wakifanya hivyo watapoteza maisha, najua kwa kusema hivi sasa mawaziri wapo matumbo moto, lakini huo ni ukweli,” alisema daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambaye aliomba jina lake kuhifadhiwa kwa kuwa si msemaji.

Aliitaka serikali kusema ukweli juu ya hilo ili kuokoa maisha ya Watanzania wengi ambao wanaamini kisukari kinaponywa kwa kikombe cha Babu, hali inayofanya baadhi yao kuwa hoi kwa kuzidiwa na ugonjwa huo.

AINA MBILI ZA KISUKARI
Alifafanua kuwa, kuna aina kuu mbili za kisukari kama wataalam wa tiba walivyoweza kuzigawa. Aina ya kwanza ni kisukari ambacho mtu anakipata tangu wakati anazaliwa hadi anapofika umri wa miaka 35, ikamaanisha kuwa katika muda huo mtu anaweza akaugua kisukari.
Aina ya pili ni kile ambacho mtu hukipata anapofika umri wa miaka 40 na kwenda juu. Vile vile kuna kisukari humtokea mtu anapokuwa na mimba, akasema hicho huitwa kisukari cha mimba.

“Aina mbili za kisukari nilizoelezwa zina tiba zinazotofautiana. Mgonjwa anayepata kisukari cha kwanza hutakiwa kufuata miiko (kutokula vyakula vya sukari), kisha hutakiwa kuchoma sindano yenye dawa ya Insulin ambayo hufanya kazi ya kuiweka sukari ndani ya mwili katika kiwango kinachotakiwa.

“Mgonjwa wa kisukari wa aina hii hutakiwa kuchoma sindano ya Insulin mara mbili au tatu kila siku. Mara nyingi wagonjwa hufundishwa kujichoma wenyewe sindano au kwa watu walio karibu nao. Kutokana na hayo, sikuona sababu ya serikali kutongoja uchunguzi wa kisayansi kuhusu dawa ya Babu kabla ya kuiruhusu kutumika,” alisema daktari huyo.

MAJIBU YA WAZIRI BUNGENI
Akijibu swali bungeni katika kikao cha bunge kilichopita mjini Dodoma , Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya alisema kuwa, hadi sasa tafiti za kitaalam zilizofanywa nchini na duniani zimeonesha kuwa, dawa zote zilizopo pamoja na za asili zina uwezo wa kudhibiti ugonjwa usisababishe madhara zaidi lakini hazina uwezo wa kuponyesha kabisa.
“Katika mfumo wa tiba asilia, kuna dawa nyingi zinazotumika kudhibiti ugonjwa wa kisukari mwilini kama ilivyo katika mfumo wa tiba za kisasa. Wizara kupitia Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na Taasisi ya Tiba Asili ya Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba ya Jamii Muhimbili, hufanya tafiti mbalimbali za dawa asili zinazosadikiwa kutibu magonjwa mbalimbali ikiwemo kisukari.
 Matokeo ya tafiti hizo hayajaonesha dawa yoyote ya asili yenye uwezo wa kutibu kisukari,”alisema Dk. Nkya.

Dk.Nkya ambaye alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Kidawa Hamisi aliyetaka kujua tamko la serikali kuhusiana na wimbi la waganga wa tiba za asili wanaojitangaza kutibu ugonjwa wa kisukari, alisema kuwa dawa inapotangazwa kwenye vyombo vya habari lazima iwe imefanyiwa utafiti wa kitaalam na kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu, kinyume chake ni uvunjwaji wa sheria namba 23 ya mwaka 2002 kuhusu tiba mbadala na kanuni zake.

Alisema wataalam wa miti shamba kabla ya kutangaza hizo dawa zao kwa umma wanapaswa wawasiliane na waganga wakuu wa wilaya na mikoa ili taratibu za kuzifanyia dawa hizo utafiti wa kisayansi zifanyike.

Dk.Nkya aliitahadharisha jamii kuhusiana  na dawa hizo asili zinazotajwa kutibu ugonjwa wa kisukari kuwa hazitibu zaidi ya baadhi kuthibitika kuudhibiti ugonjwa na kwamba wananchi wajenge tabia ya kwenda kuchunguza hali ya afya zao mara kwa mara ili kuwezesha kudhibiti ugonjwa mapema.
Hata hivyo, uchunguzi wetu umebaini kuwa licha ya majibu hayo mazuri ya naibu waziri huyo, hivi sasa serikali imekuwa ikiacha watu, wakiwemo mawaziri na wafanyabiashara mbalimbali wakienda kwa Babu Loliondo na kunywa dawa ambayo bado haijathibitishwa kisayansi kama inatibu magonjwa yanayotajwa.

Wakati huo huo, viongozi mbalimbali wa serikali wamelaumiwa na wananchi kwa kitendo chao cha kwenda kwa Babu kwa ‘mgongo’ wa serikali kumbe wana nia ya kunywa dawa.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti walisema viongozi wa serikali wakiwemo mawaziri, wakuu wa mikoa, majaji, wakuu wa wilaya na hata makamanda wamekunywa dawa ya babu kwa kutokaa kwenye foleni.

“Mara baada ya kufika nyumbani kwa Mchungaji Masapila, huwa wanaandaliwa eneo maalum na hujifanya wana mazungumzo ya kiserikali lakini baadaye kila mmoja hupata kikombe cha dawa, na kuwaacha wananchi kwenye foleni. Hili ni kosa kubwa kabisa kiimani,” alisema mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Aloyce Ngongoa.

Baadhi ya mawaziri waliopata kikombe kwa Babu wa Loliondo ambao picha zao zipo ukurasa wa mbele wa gazeti hili ni William Lukuvi, Steven Wassira, John Magufuli, Teresya Hovisa na Wakuu wa Mikoa Abbas Kandoro, Yohana Balele, mtoto wa baba wa taifa, Rose Nyerere na Mbunge Nimrodi Mkono.
Wengine ni Augustino Mrema, mawaziri wakuu wa zamani, Edward Lowassa, (pichani)  Frederick Sumaye, Mkuu wa Wilaya, Edmund Mjengwa na viongozi wengine wa chama na serikali.

Raia  wa kigeni
Mamia ya raia wa kigeni kutoka nchi mbalimbali duniani nao wamekuwa wakimiminika katika Kijiji cha Samunge kupata tiba ya magonjwa mbalimbali.

Kwa mujibu wa takwimu zinazokusanywa katika eneo la utoaji wa dawa, raia hao wa  kigeni wametoka Kenya, Marekani, Finland, Uholanzi, Sri Lanka, Jumuiya ya Falme za Kiarabu (UAE), Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Uganda, Rwanda, Burundi na Comoro.

Nayo Idara ya Uhamiaji tayari imepeleka ofisa wake ambaye ameweka kambi Samunge kupitia nyaraka mbalimbali za wageni wanaoingia kijijini hapo kunywa dawa.

Views: 154

Tags: uwazi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by erick john on April 26, 2011 at 1:16pm

Hii inahusiana na imani. Kuwa na imani uishi/kosa imani ufe!!

Comment by tanzanian boy on April 23, 2011 at 5:25pm
mambo mengine bwana. tumerudi enzi za ujima. hii ndiyo tz
Comment by Lutchiana Robert on April 9, 2011 at 12:39pm
kwa taarifa yako hata sisi tunaosoma hii blog ni madaktari pia kumbuka hii ni internet hivyo pia kwa wale ambao hawana elimu ya magonjwa wanauwezo wa kutafuta humu humu wakapata ufumbuzi, aina hizo za kisukari ulizotuambia ni uwongo mtupu hazipo kisayansi zimekaa kienyeji zaidi, ungezungumzia mechanism ya insuli na failure of pancrease to work properly as well as in heritage characters ukarelate na kisukari chako hicho, jamani tafuteni njia nyingine za kumponda Babu otherwise tujikaliage kimya tu time will tell na ushahidi utatoka tena kwa wingi kama unavyoona foleni kula samunge ndivyo watu watakuwawengi wakitoa shuhuda mimi na wewe hatujui zitakuwa chanya au hasi juu ya hiyo dawa lets wait and see.
Comment by juan son miguel on April 8, 2011 at 10:11pm
TUWE MACHO SIJUI LAKINI TUWENI MACHO,,,,,,BALI HEBU TUMWACHIE MUNGU,,,LAKINI VIPI HAO WENGINE KAMA MBEYA,MWANZA,,,,,,,,,AU TUSEME TANZANIA IMEBARIKIWA    MAANA KILA KITU TANZANIA,,,,HAYA TANZANITE TANZANIA,VYURA WANAONYONYESHA TZ,,,,,LAANA TANZANIA UCHUNAJI WA NGOZI TZ,,OOOOH TANZANIA HIVI KWELI?AU    SIJUI'''''''
Comment by Nurudin Iddi Kassim on April 8, 2011 at 5:06pm

kilam2afanye afikirie swala babu baade utapaata chakufany ni nn kwa mtazamo wako

 

Comment by Herieth leonard on April 8, 2011 at 3:16pm
Me nataka kwenda,nilipieni nauli aaahaaäæå!natania
Comment by YONAH MAGNUS MGONGOLWA on April 8, 2011 at 10:08am
uongo wako upo wazi,ungekuwa ulikuwa unaongea sauti inasikika ningesema umeropoka,kwanza daktari uliyemhoji huyo wa mhimbili kakataa kutaja jina,je huyo daktari ksomea udaktari msituni?wewe na daktari uliye mhoji mnaonekana mnaushetani ndani yake,kama daktari kathibitisha anaogopa nini kuweka hadharani?kwanini yeye hakuteuliwa katika wale madaktari waliotumwa loliondo?inaonesha ni kilaza.wewe uliyeandika hii makala ni mchawi au?nani uliyemuona amepukutika.acha umbeya wewe cku zako zakuishi zitakuwa chache kwaajiri yauropokaji wako.
Comment by Ashagrace on April 8, 2011 at 10:02am
Jamani ,kikombe cha babu kinazingatia zaidi suala la IMANI, ieleweke hivyo sasa kama ww unaenda kwa kusema ngoja nikajaribu utaula wa chuya huponi ng'o!!! na hajalazimisha m2 kama hutaki ww si uache na uonye na familia yako , kwanza ww unayechonga hujawahi umwa wewe, BIG UP KIKOMBE CHA BABU.
Comment by benny tungaraza on April 7, 2011 at 11:54am
acheni uzushi..watu waliopona ni wengi kuliko wasiopona na kumbuka hata malaria huua pamoja na watu kutibiwa hospitalini...tuna ushuhuda wa wengi waliopona kisukari miongoni mwetu wala hilo si jambo la kificho..usifikiri msongamano wa watu kwa babu ni kwa kusikia tu, watu wameona miujiza wazwaz ndo  maana wanajazana kule...tutakwenda na hatutaacha.
Comment by tanzanian boy on April 6, 2011 at 5:19pm
inasikitisha, inabidi watu wamgeukie Mungu, na kuachana na huu uchafu . Mungu inusuru tanzania na mtego huu


ADVERTISEMENT


TANGAZA HAPA

ADVERTISEMENTS

Latest Activity

GUNZ TRUVADA posted a status
"KUMPA ASIYE KUPA NI SAWA SAWA NA KUTUPA"
3 minutes ago
othman Ochu posted a status
"SCENE 1 WAHUSIKA: AMIDU , SHARIFA MAHALI: ZANZIBAR MUDA : JIONI ( WAKIWA WANASHUKA TOKA KATKA BOTI YA JION KUINGIA KATKA MJI WA ZANZI"
9 hours ago
Priscus Adelard shared GLOBAL's blog post on Facebook
9 hours ago
mrembo commented on julius manning's photo
Thumbnail

Mtanzania huru

"pole sana usijali iko siku mungu atakujaalia mungu hamtupi mja wake"
10 hours ago
mrembo commented on Sili Silali's photo
Thumbnail

Duh!

"mama mzima hayawani mavazi gani hayo takupa mfano chungwa likiwa halijamenywa unatamani ulile…"
10 hours ago
kaka commented on Ali Amur Ali's video
Thumbnail

AZIMIO LA KUANGAMIZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE

"hapo ni kina dada kutua comment zao"
10 hours ago
Gaston Kayombo commented on Ali Amur Ali's video
12 hours ago
roylicious and Jackson Jacob are now friends
12 hours ago
babu wa loliondo (cup) updated their profile
12 hours ago
julius manning commented on julius manning's photo
Thumbnail

vijana 2016 itakuwa hivi

"@furaha mimi ni kikongwe hayo ni kazi kwako."
13 hours ago
Masalu Mayeji Many'hasimha shared GLOBAL's blog post on Facebook
13 hours ago
kheri zewe commented on Sili Silali's photo
Thumbnail

Duh!

"minyama uzembe"
13 hours ago

© 2012  

Designed & Developed by
G5 CLICK COMPANY.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

How to make a Website