Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania (CKHT) Chakanusha Taarifa za Wizi

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (CKHT) kinakanusha taarifa zilizotolewana gazeti la Kiswahili la kila Jumatano, Mwanahalisi, ambazo zinadai kupitia toleo lake namba 301 la Julai 4- 10, 2012 kwamba kuna ufisadi mkubwa unaodaiwa kufikia Shilingi Bilioni Mbili.
Katika taarifa hiyo isiyokuwa na chembe ya ukweli gazeti hilo linadai fedha hizo ziliibwa kati ya mwaka 2008 na 2012. Kumekuwa na mlolongo wa taarifa za uzushi na uongo kwenye baadhi ya magazeti, likiwemo Mwanahalisi, zenye nia ya kukichafua Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (CKHT) na viongozi wake wa ngazi za juu. Taarifa hizo,kwa kiasi kikubwa, zimekuwa zikishabikia watu wanaoshukiwa kuhusika na upotevu wa rasilimali za Chuo, ikiwemo fedha. 
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (CKHT) hutumia njia mbalimbali zilizoainishwa katika Hati Idhini ya Chuo ya 2007 na kadiri ya sheria husika za nchi kuhusu kutoa taarifa rasmi za mahesabu yake ambayo kila mwaka hukaguliwa na CAG na taarifa ya ukaguzi wa mahesabu ya chuo ya mwaka 2010/11 imeishatolewa na Chuo kimepata hati safi. Taarifa hizo zitapelekwa Bungeni hivi karibuni na hakuna sababu ya mtu mwingine au gazeti kama Mwanahalisi kutengeneza mahesabu ya Chuo nje ya utaratibuhuo rasmi ambao ndio unatumika na Baraza la Chuo kusimamia matumizi ya fedha na raslimali zote za Chuo kama msingi wa utawala bora.
Mtindo huu wa gazeti la Mwanahalisi kutengeneza mahesabu yake ya Chuo ni uvunjaji wa sheria za nchi nani Kinyume kabisa na matarajio ya uandishi adilifu na una nia ya kuupotosha umma na kushirikiana na mafisadi. Ni matumaini ya chuo kwamba vyombo husika vitachukua hatua mbalimbali kulizuia gazeti hili kuendeleza kuandika uzushi.
Chuo Kikuu Huria Tanzania kinasema kuwa mlolongo wa taarifa zinazochapishwa katika magazeti haya ni za uongo, uzushi na zenye lengo la kuchafua jina zuri la chuo chetu chenye kutoa elimu nafuu na bora ya masafa kwa jamii. Ni ushauri wetu kwa uongozi wa magazeti husika kuwa endapo watahitajitaarifa sahihi kuhusu uendeshaji wa chuo ni bora kuwasiliana na wasemaji wa chuo katika njia muafaka.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano na Masoko,
CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA
 Kwa Mawasiliano Zaidi;
Albert Z. Memba, 
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko, Chuo Kikuu Huria
cha Tanzania S.L.P 23409, Dar es Salaam,Tanzania.
 Tel. + 255 222668445; Fax. + 255 22 2668779; E‐Mail: dcm@out.ac.tz

Views: 175

Tags: OPEN

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by julius manning on July 18, 2012 at 12:45pm
tumekusikia kaini tutamtuma CAG amalize utata

NI SUPERMARKET GANI BORA KULIKO ZOTE KATI YA HIZI? NA KWA NINI? TOA MAONI YAKO!
  

Forum

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by cantonna Mar 18. 2 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by penina mwailunda Mar 26. 2 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by 278l80orb0i39 Mar 4. 1 Reply

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by 278l80orb0i39 Mar 4. 1 Reply

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by 278l80orb0i39 Mar 4. 5 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by 278l80orb0i39 Mar 4. 18 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by 278l80orb0i39 Mar 4. 32 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

JUAN MATA KUTUA MANCHESTER UNITED ATASIADIA KULETA MATOKEO BORA BAADA YA TIMU KUSUASUA?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by 278l80orb0i39 Mar 4. 90 Replies

Juan Mata anataraji kutua Manchester United akitokea klabu ya Chelsea ya…

TOP NEWS WEEK HII

Latest Activity

readulislam posted a status
5 minutes ago
readulislam posted a status
6 minutes ago
readulislam posted a status
9 minutes ago
readulislam posted a status
15 minutes ago
readulislam posted a status
16 minutes ago
MIM ZIM posted a status
19 minutes ago
readulislam posted a status
19 minutes ago
GLOBAL's 15 blog posts were featured
20 minutes ago
GLOBAL posted blog posts
21 minutes ago
readulislam posted a status
23 minutes ago
sukanta sarkar posted a status
""
26 minutes ago
sukanta sarkar posted a status
""
26 minutes ago

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }