CD ZA KUMMALIZA KAKOBE HIZI HAPA

Na Haruni Sanchawa
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship , Askofu Zachary Kakobe (pichani) yupo hatarini kutokana na mbinu mbalimbali  za kimafia zinazodaiwa kufanywa na wabaya wake ambapo amebamba CD zilizobeba mpango wa kummaliza.

Habari kutoka katika chanzo chetu zinasema kundi hilo la wabaya wa Kakobe limepanga  njama za kumsambaratisha kiongozi huyo kwa kupandikiza chuki miongoni mwa waumini wa kanisa hilo ambalo lina matawi nchi nzima.

Habari zinasema tayari kundi hilo la watu watano (majina tunayo), limefanya mikutano mbalimbali na mmoja wa wanakikundi hicho ni mwanasiasa ambaye anaendesha taasisi moja ya kiraia na wawili ni wachungaji wa kanisa.

Mchungaji mmoja ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini alilithibitishia gazeti hili kuwa  mkutano muhimu wa kundi hilo ulifanyika Desemba 10, mwaka jana,  na kilichojadiliwa kimenaswa na Kakobe kikiwa kwenye CD.

Hata hivyo, alisema kuwa wanakikundi hicho walivurugana baada ya mhudhuriaji mmoja kutaka apewe fedha za kazi ili ‘awashe moto’ kwa waumini wa Kakobe kupitia vyombo vya habari kwa kuandaa mkutano na waandishi wa habari.

“Mhudhuriaji huyo ambaye ni mchungaji alitaka apewe fungu kubwa la fedha la kufanyia kazi hiyo lakini alipokataliwa akaanza kumkaripia mchungaji mwingine ambaye ana uwezo wa kifedha kuwa anaharibu mpango.

“Mchungaji aliyeambiwa kuwa anaharibu mpango wa kumsambaratisha Kakobe  alibaini kuwa njama zinazopangwa siyo za kulijenga kanisa, hivyo alipinga, lakini wenzake walikubaliana kuwa abambikiwe kashfa chafu,” alisema  mchungaji huyo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa mtoa habari wetu, mchungaji mwingine alisema mipango hiyo ikifanikiwa watachagua magazeti ambayo hayaogopi na yana ujasiri wa‘kuanika maovu’ na moja ya magazeti hayo ni hili.

Habari zinasema kutokana na wachungaji hao kuvurugana, habari zilimfikia Askofu Kakobe ambaye alipewa mkanda  ambao ulikuwa umerekodi mazungumzo yote ya njama hizo chafu.
Alipopigiwa simu juzi (Jumapili) na mwandishi wetu, Askofu Kakobe na kuulizwa kama madai hayo ameyasikia  alikiri kumfikia.
“Ni kweli kabisa nimepata mkanda wa mazungumzo yao na ni kweli huu ni mpango wa kimafia. Leo (Jumapili) nitachezesha CD ya mazungumzo hayo kwa waumini wangu,” alisema Kakobe.

Aliongeza kuwa hiyo ni vita ya shetani ambayo anaamini atashinda kwa kuwa Mungu yupo na hana upendeleo.

Mwandishi wetu alihudhuria ibada ya Jumapili katika Kanisa la Kakobe na kushuhudia CD hiyo ikichezeshwa ambao zilisikika sauti za watu wakijadili mpango huo wa kumsambaratisha.

Wakati huo huo, kuna madai kuwa  Askofu Kakobe amefunguliwa kesi Mahakama Kuu yenye namba 79/2011  na  wachungaji watatu,  Dezidelius Patric, Angelo Mutasingwa na Benedict Kaduma inayotarajia kutajwa Julai 1, mwaka huu lakini katika mahubiri yake kanisani hapo Kakobe alisema anasikia tu kupitia vyombo vya habari kwani hajapata hati yoyote ya kisheria.

“Wawili kati ya hao wanaodaiwa kunifungulia kesi walishafukuzwa na kanisa letu  kutokana na kukiuka maadili ya kanisa, wakaanzisha kanisa lao, moja linaitwa  Ukombozi na lingine ni Victory,” alisema Kakobe alipoulizwa baadaye na mwandishi wetu.

Views: 2614

Tags: uwazi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by Elimringi moshi on April 4, 2012 at 7:47am
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa! Guys Open your eyes the world is almost Over, and this the time for feck prophets! Read your Bible everything is clearly stated!
Comment by Elimringi moshi on April 4, 2012 at 7:44am
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa! Guys Open your eyes the world is almost Over, and this the time for feck prophets! Read your Bible everything is clearly stated!
Comment by samora rajab albert on July 3, 2011 at 12:47am
makubwa
Comment by magdalena cathbert on June 29, 2011 at 7:50pm
HATA CKU MOJA USIMHUKUMU MTUMISHI WA MUNGU ,MUNGU MWENYEWE NDIO ATAMSHUHULIKIA.
Comment by richardngeze on June 28, 2011 at 6:18pm
Yafaa kuvuana magamba na hata ikibidi kwa nguvu.
Comment by Baraka Busima on June 28, 2011 at 5:45pm
kila mtu ashike alicho nacho hizi ni siku za mwisho mi siwezi kushangaa kwa sababu yanakuja zaidi ya haya
Comment by Gratious Kimberly(TKN) on June 28, 2011 at 3:54pm

You People...eti mtumishi wa mungu....Kakobe.   Inamaana zamani wakati wa missionaries hawajaja na kutuletea vitabu vya Yesu...Mungu...Hakuwepo?.....Duniani Hakuna Mtumishi wa Mungu!1...Wote sisi ni viumbe tusiojua hata nini maana ya dini wala faida yake.  Hakuna Fisadi kama kakobe...." eti tuliwafukuza wachungaji kwa utovu wa nidhamu"...Kama kweli wewe unamwamini Mungu unaweza kumfukuza mtu kwenye imani au kanisa?.....Sisi tutakufa masikini tu...maana vitabu vya Kikristo walileta Missionaries...na vya Kiislamu walileta waharabu...tukapewa kwa nguvu na kulazimishwa na utumwa juu yake.  Na walipoacha hivyo vitabu  Zamani kulikua na dini chache sana  2 za kikristo na 1 ya kiislamu....sasa  angalia kuna Dini na makanisa zaidi ya 30 tofauti kila mtu na Biblia yake.   Kwanini Biblia haikutokea Rwanda?...kwanini Quraan Hakutokea kilwa?...Vyote vimeletwa na wageni nasisi tunafuata kama mbuzi...ndo maana tukaitwa kondoo!! Kabla wapumbavu hawajaja  tuliishi na amani na tamaduni zetu...sasa angalia siku hizi...wapi kuna amani????.....Mzungu aliyekuletea vitabu vya dini....yuko Kahama na mwadui anaiba madini yetu ......na mwarabu  yuko anadai pesa zake za Dowans ...sisi tunagombana makanisani na misikitini....wao wenyewe  hata dini sio muhimu tena!!....

NYIE MNAFIKIRI WAZUNGU   AU WAHARABU WALIVYOKUA NA TAMAA NA UBINAFSI; WANGEKUA WANAJUA NJIA YA KWENDA KWA MUNGU, KWELI WANGEKUJA AFRIKA NA KUTUBEBA SISI NGEDERE?????

Visa tu ya kwenda kwao wanatunyima!...na sisi bado tumeshikilia vitabu walivyoleta wao na kutulazimisha kuvisoma..eti tuna viiita vitabu vitakatifu....kitabu kimeandikwa kwa mkono wa binadamu na mawazo yake??

yesu....mweupe, malaika mweupe, mtume mweupe...?ß....ebu chora picha ya malaika mweusi kama mmasai alafu ipeleke church Arusha kama hujafukuzwa huko na hao ha wamasai kanisani!!!

Tuamke jamani!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!...Ende

Comment by Yuda Thadei on June 28, 2011 at 2:23pm
fedha! fedha! fedha! kweli ni sabuni ya roho!!
Comment by Miriam John Mndolanga on June 28, 2011 at 1:59pm

HAYA NDIO YALE ALIYOYASEMA MWOKOZI WETU YESU KRISTO 'WENGI WATAKUJA KWA JINA LANGU, WATAVUTA WENGI NA KUWADANGANYA. MTAWAJUA KWA MATUNDA YAO' NA MATUNDA YA WACHUNGAJI HAO WATATU NI HUO UONGO NA UOVU JUU YA KABOBE.

Comment by julius manning on June 28, 2011 at 1:42pm
Kakobe amepoteza mwerekeo, mara awabebe wanasiasa mara tusikie anawavua watu dhahabu
UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }