‘BETHDEI’ YA KAJALA GEREZANI VILIO TUPU

Na Gladness Mallya
JUMAPILI ya Julai 22, mwaka huu ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa msanii wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja (pichani), staa huyo alisheherekea siku yake hiyo kwa majonzi akiwa katika Gereza la Segerea jijini Dar  huku vilio vikitawala Rasasi Mchanganyiko linakudondoshea habari kamili.
‘Bethdei’ hiyo ilifanyika Jumapili ambapo baadhi ya wasanii walifika katika gerezani  kwa ajili ya kumpelekea zawadi mbalimbali huku wakimwimbia Kajala wimbo maarufu wa ‘Happy Birthday’  wakati staa huyo akiwa nyuma ya nondo.
Baadhi ya watu waliofika gerezani hapo kwa ajili ya kuungana naye katika kusheherekea ni pamoja na mtoto wake Paula, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Bilaly Mashauzi pamoja na Jeniffer Pemba.
JENIFFER AKABIDHI KEKI
Dada huyo ambaye ni rafiki wa karibu na Kajala ambaye pia ndiye mwenye jukumu la kumpelekea chakula kila siku, Jumapili iliyopita aliandaa keki ya nguvu pamoja na zawadi nyingine kwa ajili ya sherehe ya Kajala, bitu hivyo vilipokelewa na askari wa magereza na kukaguliwa kisha kufikishwa kwa mlengwa.
LULU AJUMUIKA
Baada ya muda mfupi staa mwingine anayetajwa kwenye kifo Steven Kanumba Elizabeth Michael ‘Lulu’ naye alijumuika na Kajala kusimama nyuma ya nondo kwa ajili ya kusheherekea bethdei hiyo pamoja na kuwasalimia watu waliofika ambapo wote walionekana kufarijika na ujio wao.
VILIO VYATAWALA
Hata hivyo, tofauti na ilivyotegemewa  kwani vilio vilichukua nafasi gerezani hapo kutokana hali ilivyokuwa kwani Kajala na Lulu hawakuweza kuungana na wapendwa wao kusheherekea pamoja kutokana na sheria za Jeshi la Magereza kutoruhusu tendo hilo.
SHILOLE ALALAMA
Kwa upande wake, Shilole mbali na kushiriki kuangusha kilio lakini alikuwa akilalamika kwamba yupo katika wakati mgumu na haoni raha ya  mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa kuwa mwaka jana aliwaalika Kajala na Lulu wakala futari pamoja nyumbani kwake.
 “Sina budi kuwaombe dua katika mfungo huu wa Ramadhan ili Mungu awajalie waweze kutoka na tuungane tena kama zamani,” alisema.

Views: 4145

Tags: mchanganyiko11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by daudi charles mponda on July 31, 2012 at 12:50am

TUBUNI KWA KUWA UFALME WA MUNGU UMEKARIBIA

Comment by meggie impostra on July 26, 2012 at 11:43am

mhmmmm mungu wasaidie hawa watoto jmniii kama mafundisho wameishayapataaaa

Comment by Nassir S Buheti on July 26, 2012 at 1:44am

Mungu yupo pa1 nanyi

Comment by mammy on July 25, 2012 at 11:40am

inatia moyo sana!

Comment by Dr joseph kingo on July 25, 2012 at 11:15am

si vizuri kulalamika wakati tatizo lishatokea.kajala ninaamini kuwa uchungu na machozi yako ya kila siku ni ishara tosha kabisa kuwa hapo ulipo umefikishwa na mumeo Tapeli na muhalifu sugu.watu husema binadamu hujifunza kutokana na makosa lakini ni muhimu kuepuka makosa na kujifunza kwa mifano.ulikimbilia sana fedha na ngoa ya haraka bila kufahamu huyo mume wako ni lukumba lukumba.

Comment by raphael Joram on July 25, 2012 at 9:55am
safi shilole kwa kukumbuka watu wenye taabu wakati huu mfungo wa ramadhani
UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }