Muelimishaji rika na masuala ya VVU, Taji Liundi akitoa elimu kwa wasanii na wadau wa sanaa waliofika kwenye program maalum iliyoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwenye Ukumbi wake kupitia Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila wiki.
Msanii maarufu wa Sanaa ya Uchoraji Mohamed Raza akiuliza na kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimabali kuhusu VVU.
Na Mwandishi Wetu
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kupitia programu yake ya kila wiki ya Jukwaa la Sanaa limetoa elimu kwa wadau wa sanaa kuhusu virusi vinavyosababisha UKIMWI na jinsi vinavyoweza kuathiri mwili wa binadamu.
Akizungumza kwenye program hiyo, muelimishaji rika na kamishna mstaafu wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI nchini, Taji Liundi alisema kwamba,wasanii ni kada inayoathirika sana na janga hili hivyo elimu hiyo ni muhimu kwa wao kujikinga na kuwakinga mashabiki wao.
“Umaarufu wa wasanii unaletwa na mashabiki na kazi yao ni ya muingiliano mkubwa kiasi kwamba wanatakiwa kuwa makini ili mwisho wa siku wasipukutuke na janga hili. Wanapaswa kuzingatia elimu kama hizi na hata kubuni kazi zenye kuzingatia haya” alisema Taji Liundi.
Awali akitoa elimu kwa wadau wa sanaa Taji alisema kwamba,wasanii wengi wamekuwa wakijikuta kwenye vishawishi vya kufanya vitendo vya ngono na watu wasiyowafahamu na waliokutana nao kwa mara ya kwanza kwenye maonyesho hali ambayo inahatarisha afya zao.
Aliongeza kwamba, umaarufu, matamanio na kuamini bila kutumia vipimo ndivyo vimekuwa vikiwaweka watu wengi hususan wasanii wenye muingiliano mkubwa na jamii katika mazingira hatari ya kuambukizwa VVU.
Alizidi kueleza kwamba, kwa sasa hakuna kampeni zinazolenga kupambana na janga hili kama ilivyokuwa zamani ambapo kampeni kama za ISHI zilisaidia kutoa elimu pana kwa jamii hivyo kutoa wito kwa wasanii kutumia fursa kama za Jukwaa la Sanaa katika kupata elimu hii muhimu.
Baraza la Sanaa limekuwa likiendesha program maalum ya Afya kwa wadau wa Sanaa hususan wasanii kila baada ya miezi mitatu na tayari wasanii na wadau wapatao 200 wameshapewa elimu ya VVU na kupima afya zao.
Captions
1. Muelimishaji rika na masuala ya VVU, Taji Liundi akitoa elimu kwa wasanii na wadau wa sanaa waliofika kwenye program maalum iliyoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwenye Ukumbi wake kupitia Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila wiki.
2. Taji Liundi akiwaonesha Wasanii na wadau wa Sanaa jinsi Virusi vya UKIMWI vinavyopenya kwenye damu na kusababisha mtu kudhoofu. Kulia kwake ni Kaimu Mratibu wa Programu ya Jukwaa la Sanaa, Bi.Agnes Kimwaga.
3. Msanii maarufu wa Sanaa ya Uchoraji Mohamed Raza akiuliza na kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimabali kuhusu VVU.
4. Mdau akimuuliza muelimishaji rika juu ya matumizi ya Kinga na nafasi yake katika kukinga maambukizi ya VVU.
5. Sehemu ya Wadau wakimsikiliza muelimishaji rika Taji Lindi.
Comment
Comment by Janeth Jr on July 20, 2011 at 12:26am
Comment by William Jotham on July 19, 2011 at 5:51pm | 1 |
GLOBAL |
| 2 |
NDAUKA the GREAT |
| 3 |
julius manning |
| 4 |
LJH_3 |
| 5 |
hope |
| 6 |
Tatu Majaliwa |
| 7 |
mayalilwa |
| 8 |
steven emmanuel |
| 9 |
Matilanga Lukingita |
| 10 |
Mishy chunga |
Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Mohammed Mar 26. 6 Replies 0 Likes
JE, NI KWELI KWAMBA KIPIGO CHA BAO 2-1 ILICHOKIPATA MAN UTD KUTOKA KWA REAL MADRID USIKU WA KUAMKIA LEO LAWAMA ZOTE ZIMWENDEE MWAMUZI WA MCHEZO AU MAN UTD WAJILAUMU WENYEWE? TUPE MAONI YAKO!!!
Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Ali Abdalla Ali Apr 22. 20 Replies 8 Likes
Tumeshuhudia kwa siku za hivi karibuni hali halisi iliyokuwa inatokea katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, kwa hali hii ni ishara kuwa Spika na Naibu wake washindwa kuliongoza bunge hilo?
Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Phinehas Rishiansia Kileo May 3. 6 Replies 3 Likes
Wafuasi wa CCM wakimshambulia mfuasi wa Chadema mkoani Dodoma…
Tags: BENDERA, WA, DODOMA, NANI, KULAUMIWA?
Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by NELSON UVAMBE yesterday. 27 Replies 5 Likes
HIVI KARIBUNI KUMEKUWEPO UPOTEVU WA AMANI HAPA NCHINI PAMOJA NA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI. MKOANI KAGERA WANANCHI WENYE HASIRA WALIWAUA POLISI, IJUMAA ILIYOPITA WAKULIMA NA WAFUGAJI HUKO WILAYANI KILOSA WALIZUA VURUGU NA KUFUNGA BARABARA,…
Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Domino Bagambisa Jan 21. 17 Replies 4 Likes
Kiungo hatari wa Azam FC, Mrisho Ngassa leo amepelekwa Simba SC kwa mkopo na timu yake…
Tags: SOKA
Started by GLOBAL in Habari. Last reply by Billy Frank Irungu Apr 26. 118 Replies 21 Likes
Tags: NCHINI, HAPA, UNAFURAHIA, HUDUMA, ZAKE?
Started by Gysper in Siasa. Last reply by Jamal amor May 9. 24 Replies 4 Likes
hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?
Started by Kulikoni Ughaibuni in Siasa. Last reply by richardngeze Feb 12. 12 Replies 9 Likes
Tanzania tuna tatizo kubwa.Hakuna haja ya kunyoosheana vidole as to nani amechangia tatizo hilo bali cha muhimu na haraka ni namna tutakavyoweza kutatua tatizo hili.Nisimung'unye maneno: tatizo kubwa linaloikabili ni kuwa na Rais ambaye takriban…
© 2013 Created by Global Publishers.




You need to be a member of Global Publishers to add comments!
Join Global Publishers