Hemed Kisanda na Jelard Lucas
Kwa muda mrefu alisubiriwa kutoa tamko hili, tangu mwaka 2006 ilikuwa ikivumishwa na kuripotiwa katika vyombo mbalimbali vya habari lakini akawa mzuri wa kukanusha lakini Jumamosi iliyopita, Mfalme Commercial Rap, Ambwene Yesaya ‘AY’ alizungumzia kwa kina siri yake na Staa wa Kenya, Cecilia Wairimu ‘Amani’.

The 5star Paper, Risasi Mchanganyiko, lilifanya ‘straight talk’ na AY kwenye mgahawa wa Steers, Millenium Tower, Kijitonyama, Dar ambapo alikiri kuwahi kutoka kimapenzi na Amani lakini akaeleza kwa sasa ni zilipendwa.

Ambwene Yesaya ‘AY’
AY, alisema kuwa hivi karibuni kuna vyombo vya habari vilitangaza kuwa amerudiana na Amani kitu ambacho alikikanusha vikali.

Baada ya kukanusha taarifa hizo za Amani, AY alisema kuwa hivi sasa ana mpenzi mpya ambaye ni mtumishi wa wizara moja nchini.

Hata hivyo, AY alimtaja mrembo wake kwa jina moja la Jamie na kugoma kumuelezea zaidi wala wizara anayofanyia kazi kwa maelezo kuwa ni mapema mno kutangaza vitu hivyo.

“Nimesikia tetesi za watu wakisema nimerudiaana na Amani, huo siyo ukweli hata kidogo sijawahi kulifikiria hilo, mimi nilikwenda Kenya kwa ajili ya kazi tu, hata hivyo kwa sasa nina ‘jiko’ jipya na mapenzi yangu na Amani yalikwisha siku nyingi,” alisema AY.

Alisema, kuondoka kwa Amani na kujiweka kwa Jamie, isiwe sababu ya jamii kumchukulia ni kiwembe kwa sababu hiyo ni hali ya kawaida kwa mtu kubadilisha mpenzi baada ya kubaini kwamba aliyenaye siyo mwenzi sahihi.

Cecilia Wairimu ‘Amani’
“Najua baada ya kuweka wazi uhusiano wangu na Jamie kuna watu wataanza kunifuatilia kwa mabaya na mazuri, au kunifanyia fitina lakini nimejipanga kuhakikisha naulinda uhusiano wangu mpya usivurugwe na mtu yeyote,” alisema AY na kuongeza:

“Lengo langu hasa ni kufunga pingu za maisha, watu wataanza kutufuatilia kwa sasa wakitaka kujua huyo Jamie yupoje. Nimejipanga sana.”

Mbali na hilo, AY alisema siku chache zijazo atakwea pipa kuelekea Miami, Marekani kwa ajili ya kufanya ‘kolabo’ na mkali wa Pop na Reggae duniani, Sean Kingston.

Views: 1401

Tags: mchanganyiko11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by hamza salum on April 11, 2011 at 6:13pm
safi sana kaka tunakutakia kila lakheri
Comment by mwanaid shaban on January 20, 2011 at 1:34pm
good
Comment by Isaya Ibrahimu on January 19, 2011 at 5:54pm
FUNGA PINGU YA MISHA,OL DA BEST
Comment by shola ama on January 14, 2011 at 3:03pm
i knew they wont last some kenyan women?mmh,no word!!!
Comment by Sarah on January 13, 2011 at 11:45pm
MUNGU AKUJALIYE KILA LA KHERI. NI KWELI UKIWA NA NEW REALATIOSHIP WATU WANATAKA KUJUA EVEN YOR FANS, SASA WEWE UNATAKIWA BE COOL AND OPEN MIND KWAMBA ITAKUJA MAMBO MENGI ZA NZURI NA MABAYA. 
Comment by loveness natai on January 13, 2011 at 2:50pm

kila la heri kaka..........i like you

 

Comment by lilian ernest bitegeko on September 22, 2010 at 9:45am
ALL THE LACK AY
Comment by mcmillan andrew laiza on September 2, 2010 at 9:23am
safi sana kijana wewe ndiyo unafaha kuwa msani kama kioo cha jamii
Comment by Easther on September 1, 2010 at 8:56pm
mimi siku zote ni mshabiki wako ay,ni star bt huna kashfa za pombe ulimbukeni wala madem,umetulia kaka wanaokuponda waulize mpaka sasa hv hao wameshakuwa na uhusiano na wangapi mpaka sasa hv,jibu hapo hesabu kuanzia thelathine kwenda mbele,big up kaka,inaelekea huyo bibie jamie kakukuna hasa mpak umemweka hadharani,ulivyokuwa msiri wewe,kila la heri kaka
Comment by hussein hassan hussein on September 1, 2010 at 2:51pm
jokate je nae zilipendwa au kinyemela?

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by hiepelines Jul 4. 6 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Aug 15. 7 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Aug 15. 6 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by Joe reggan Apr 24. 2 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }