ASALI: KIBOKO YA UNENE UNAOWAKERA WANAWAKE-3 & 4

Karibuni tena katika sehemu ya tatu ya makala yetu ya leo kuhusu kupunguza unene, mada ambayo imeonekana kuvuta hisia za wasomaji wengi. Katika sehemu hii ya tatu ya mfululizo wa mada hii tunaendelea kutazama namna asali inavyoweza kupunguza na kumaliza tatizo la unene. Endelea...

Baada ya hapo unaweza kuchuja na kupata kinywaji kisicho na vipande wala ungaunga. Kunywa nusu kikombe kabla ya kula kitu chochote asubuhi. Nusu kikombe kinachobaki, kihifadhi kwenye friji au sehemu safi na salama na uimalizie kunywa usiku wakati ukienda kulala.

Jambo la kuzingatia hapa ni kuepuka kuchanganya asali kwenye maji ya moto kabla hayajapoa, kwa kufanya hivyo utaua virubisho muhimu vilivyomo kwenye asali. Tengeneza na kutumia mchanganyiko huo kila siku na uangalie matokeo yake. Baadhi ya watumiaji wameweza kupunguza hadi kilo 3 kwa wiki moja.

Tahadhari inatolewa kwamba hakikisha unatumia mdalasini halisi kama ilivyo kwa asali. Aidha, mchanganyiko huo uutumie kwa kipindi ambacho utatimiza lengo lako la kupunguza uzito, lakini usitumie kwa muda mrefu sana na isizidi miezi minne mfululizo.

ASALI NA MDALASINI HUTIBU MAGONJWA MENGI
Imedhihirika kuwa asali na mdalasini vina uwezo wa kutibu magonjwa mengi. Nchi nyingi duniani zinazalisha asali na zimekuwa zikiitumia katika aina mbalimbali za madawa. Hata wanasayansi wa sasa wamekubali kwamba asali inasaidia katika kutibu magonjwa mengi.

Aidha, wanasayansi wamethibitisha ubora na maajabu ya asali kwa kusema kuwa ingawa asali ni tamu kama sukari, lakini ikitumiwa kwa kiwango kinachotakiwa kama dawa, haiwezi kumdhuru hata mgonjwa wa kisukari.

Katika toleo lake la Januari 17, 1995, jarida moja la nchini Canada liitwalo Weekly World News, lilichapisha orodha ifuatayo ya magonjwa yanayoweza kutibiwa na asali, kama ilivyothibitishwa na Wanasayansi wa Magharibi:

MAGONJWA YA MOYO:
Tengeneza ‘pesti’ ya asali na mdalasini (kama tulivyokwisha eleza), kisha tumia kama jamu kulia mkate, chapati, n.k na uwe unakula mara kwa mara wakati wa kufungua kinywa asubuhi.

Mchangayiko huu huondoa lehemu kwenye mishipa ya damu na hivyo kumuepushia mtu uwezekano wa kupatwa na mshituko wa moyo au kiharusi.

Na kwa wale ambao wameshapatwa na kiharusi kwa mara ya kwanza, watajiepusha na kupatwa kwa mara ya pili.

Utumiaji wa mara kwa mara wa mchanganyiko huu wa asali na mdalasini, huondoa tatizo la kupumua kwa shida na kuimarisha mapigo ya moyo.

Nchini Marekani na Kanada, wakunga wa majumbani wamegundua kwamba kadri mtu anavyozeeka, njia ya kupitishia damu nayo hudhoofika, lakini kwa kutumia asali na mdalasini mishipa huendelea kuimarika.

KUUMWA NA MDUDU
Mbali ya kukinga magonjwa ya moyo, asali na mdalasini pia ni dawa ya vidonda vitokanavyo na kuumwa na wadudu wa aina mbalimbali.

Ili kupata dawa hiyo, chukua kiasi kidogo cha asali na maji ya uvuguvugu (kijiko kimoja cha asali na vijiko viwili vya maji) kisha changanya na kijiko kimoja kidogo cha unga wa mdalasini na uwe kama ‘pesti’.

Upakae mchanganyiko huo katika sehemu inayouma kwa kuchua. Imeelezwa kuwa mara baada ya kupakaa mchanganyiko huo , nafuu huweza kuanza kuonekana ndani ya dakika moja hadi mbili, ikimaanisha utendaji kazi wake ni wa mara moja.

UGONJWA WA BARIDI YABISI
Mtu anayesumbuliwa na ugonjwa wa baridi yabisi (Arthritis) huweza kupata nafuu iwapo atatutumia mchanganyiko wa asali vijiko viwili na kuchanganya na glasi moja ya maji ya uvuguvugu pamoja na unga wa mdalasini. Mchanganyiko huu utumiwe kila siku asubuhi na jioni.

Katika utafiti mmoja wa hivi karibuni, uliofanywa na Chuo Kikuu cha Copenhagen nchini Denmark, uligundua kwamba wagonjwa 200 wa baridi yabisi au viungo vya mwili (arthritis) waliotibiwa kwa kupewa vijiko viwili vidogo vya asali na mdalasini kabla ya kufungua kinywa asubuhi, 73 waliacha kusikia maumivu ndani ya wiki moja.


ASALI: KIBOKO YA UNENE UNAOWAKERA WANAWAKE-4


Karibu tena katika sehemu ya nne na ya mwisho ya makala yetu kuhusu kupunguza unene na faida zingine za asali na mdalasini kiafya. Sasa endelea...

Baada ya mwezi mmoja, wagonjwa hao waliweza kuanza kutembea bila msaada wa mtu na bila kusikia maumivu kama waliyokuwa wakiyasikia kabla ya kuanza kutumia tiba hiyo.

KUTOOTA NYWELE/UPARA
Ni habari njema pia kwa watu wenye matatizo ya kutoota nywele utosini au kuwa na kipara. Changanya ‘Olive Oil’ ya moto na kijiko kimoja kikubwa cha asali na kijiko kidogo cha unga wa mdalasini. Kisha pakaa sehemu isiyoota nywele na uache kwa dakika 15 kabla ya kwenda kuoga. Dawa hii imeonekana kusaidia sana hata kwa kuweka kwa dakika 5 tu.

KUSAFISHA KIBOFU CHA MKOJO
Chukua vijiko viwili vikubwa vya unga wa mdalasini, changanya na kijiko kimoja kidogo cha asali, tia ndani ya maji ya uvuguvugu kisha kunywa, mchanganyiko huo huua wadudu wote na kuacha kibofu cha mkojo safi.

ASALI DAWA YA JINO
Ili kutengeneza mdalasini na asali kama dawa ya jino, chukua kijiko kimoja kidogo cha mdalasini na vijiko vitano vidogo vya asali. Changanya asali na mdalasini ili kupata mnato maalumu (paste). Pakaa mnato huo katika sehemu ya jino inayouma, mara tatu kwa siku hadi maumivu yatakapoondoka.

ASALI DAWA YA KUONDOA LEHEMU (CHOLESTROL)
Changanya vijiko vikubwa viwili vya asali na vijiko vitatu vidogo vya mdalasini kisha weka kwenye kikombe cha maji yenye moto kiasi kama ya chai na changanya. mchangaynyiko huo anapopewa mgonjwa wa lehemu, utafiti umeonesha kuwa kiwango cha lehemu katika damu hupungua kwa asilimia 10 ndani ya saa mbili tu.

Aidha, utafiti zaidi umeonesha kama mchanganyiko huo ukitumiwa mara tatu kwa siku kwa muda fulani, tatizo la lehemu huweza kutibiwa kabisa. Kwa mtu ambaye hana tatizo hilo kwa sasa, akiwa na mazoea ya kulamba asali kila siku vijiko viwili au kimoja baada ya mlo usiku, hatapatwa na tatizo la lehemu katika maisha yake. kama mnavyojua, lehemu ndiyo chanzo cha magonjwa ya moyo pia.

MATATIZO YA MAFUA
Kwa wale wenye matatizo ya mafua sugu au ya muda mrefu, wanaweza kupata nafuu au kupona kabisa kwa kutengeneza na kutumia mchanayiko wa asali na mdalasini . Changanya asali kijiko kimoja cha chakula na robo kijiko cha unga wa mdalasini, tumia mara tatu kwa siku.

ASALI HUWEZA KUTIBU TATIZO LA UZAZI
Kuna utafiti umeonesha kuwa asali huweza kuimarisha mbegu za uzazi kwa akina baba na kuondoa tatizo la kutoshika mimba kwa akinamama. Akina baba wenye tatizo la upungufu wa mbegu za kiume, walipoanza kutumia asali kwa kulamba vijiko vikubwa viwili vya asali kila siku kabla ya kulala, waliondokewa na tatizo hilo baada ya kipindi kifupi.

Wanawake wa China na Japani wenye matatizo ya kutoshika mimba wamekuwa wakitumia mdalasini kuondoa tatizo hilo. Kuondoa tatizo hilo, wanawake hao huwa wanaweka mchanganyiko wa nusu kijiko kidogo cha asali na kiasi kidogo cha unga wa mdalasini na kuupaka mara kwa mara kwenye fisi mchana kutwa.

Utaratibu huo huwezesha mchangayiko huo kuingia mwilini taratibu kwa njia ya mate kwa siku nzima. Kuna ushuhuda uliwahi kutolewa wa mama mmoja nchini Marekani ambaye alikuwa na tatizo la kutokuzaa kwa muda mrefu, lakini baada ya kutumia asali na mdalasini waliweza kupata watoto mapacha.

Orodha ya matatizo ya kiafya yanayotibiwa na asali na mdalasini ni ndefu. Baadhi ya matizo hayo ni pamoja na kujaa gesi tumboni, upungufu wa kinga ya mwili, ukosefu wa choo, vipele, magonjwa ya ngozi, saratani ya tumbo na mifupa, uchovu, harufu mbaya mdomoni na kutosikia vizuri.

Kwa ujumla, asali na mdalasini inafaa kutumiwa katika milo yetu ya kila siku, kwani faida zake kiafya ni nyingi na ni kinga ya mataizo mengi ya kiafya, makubwa na madogo.
Kwa makala za zilizopita, fungua www.abdallahmrisho.blogspot.com

Views: 7941

Tags: asali, uwazi11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by Gervas Daniel Nyalusi on October 1, 2011 at 2:39pm
nyuki ni kiboko wameletwa makusudi na mungu kututengenea dawabure hata Yohana mbatizaji alikuwa anatumia asali na nzige kama chakula chake
Comment by ELIUT PAUL on October 1, 2011 at 1:20pm
Asanteni kwa kutujuza na ntaanza kuitumia kuanzia sasa..
Comment by Sarah on January 1, 2011 at 2:50pm
KWANZA AMNA DAWA YA KUNYWA AMBAYO INAPUNGUZA UNENE . MIMI NIME JARIBU KILA NJIA KULA VIDONGE , NA NIMEKUNYWA SLIM DIEAT, NA NIMEJARIBU KUNYWA SUPU YA KABECHI MMWEZI MMOJA. HAJANISADIA KITU.... Kitu iliyo nisadia kupunguza unene ni change my lifestyle na mazoezi, within 2years nimepunguza kilo 60kilos.. HII NDIO  DAWA..
Comment by Mbilinyi, Mario on December 14, 2010 at 8:46am

Ni kweli tunawashukuru kwa kutujuza dawa mbadala.

Comment by lion on December 8, 2010 at 5:10am
RAHA YA ASALI ULAMBISHWE UNA WA KUKULAMBISHA WEWE
Comment by kokusima on December 8, 2010 at 2:04am
asante kaka, ila mi nimeanza kunywa tangu tarehe moja nimeongezeka kilo mbili au nakunywa mdarasini wa kichina ahahaha! Asante Mrisho mwaya. Niligoogle nikapata kama unavyoeleza ila uzito wangu ni baada ya uzazi labda zangu hiziitaji mdalasini ukizingatia ninanyonyesha ila asante sana bado naendeleza dozi.
Comment by Angela Mushumbusi on December 6, 2010 at 11:32am
BORA TUPATE MBADALA, MAKE DUH HATARI SANA!!!!! ASANTEN KWA KUTUJUZA
Comment by lion on December 1, 2010 at 1:54pm
haha 3kg per week?
Comment by vita wilbards on November 30, 2010 at 7:48pm
KUMBE DAWA TUNAZO SASA INAKUWAJE WATU WANAHUSUDU MIDAWA YA MCHINA

ONGEZENI UTAFITI INAWEZEKANA HATA DAWA ZA ZA ASILI ZA KUONGEZA MAKALIO NAZO TUNAZO KULIKO HIZI ZA MCHINA ZENYE MADHARA
Comment by vita wilbards on November 30, 2010 at 7:47pm
HII NAYO NI KALI KWA KUWA NI YA ASILI

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by hiepelines Jul 4. 6 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Aug 15. 7 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Aug 15. 6 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by Joe reggan Apr 24. 2 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }