ARV’S BANDIA: WANAUME WAOTA MATITI, WANAWAKE NDEVU

Na Mwandishi Wetu
IMEDAIWA kuwa madhara makubwa ya zile ARV’s za bandia ni kuvurugika kwa mfumo wa homoni za mwili zikiwemo zile zinazotofautisha jinsi ya kike na kiume.

Kwa mujibu wa watu waliopata madhara kufuatia matumizi ya dawa hizo zinazoendelea kuzua gumzo nchini, dalili za miili kubadili mfumo huonekana na hivyo kutishia jinsi kuonekana katika mtazamo mwingine.
Baadhi ya wanaume wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (V.V.U) ambao wamekuwa wakitumia dawa za kurefusha maisha, wamejikuta wakivimba matiti na kuwa makubwa kama wanawake.  
Vilevile, wanawake wanaotumia dawa hizo wanalalamika kukutwa na matatizo kadhaa likiwemo la kuota ndevu.
Mwanaume tunayemtaja kwa jina moja la Mkanta (45), yeye amekumbana na tatizo la dawa hizo ambapo mbali na matatizo mengine alivimba matiti.
Anasema awali alijua ni hali ya kawaida na itaisha lakini baadaye akabaini kwamba dawa anazotumia ndiyo zinazompa aibu hiyo ya mwaka.

Mwanamke Mwanahamisi wa Kigoma (37), yeye anasema kwamba amekuwa akitumia ARV’s za kurefusha maisha yake kwa muda mrefu sasa tangu alipogundua kuwa ni mwathirika, mwaka 2008 lakini katikati ya mwaka huu, alianza kuhisi kuota vinyweleo mfano wa ndevu kwenye kidevu na mashavuni.
“Sikujua sababu lakini ilipotangazwa kwamba kuna ARV’s bandia ndiyo nikahisi sababu ni hiyo.
Daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambaye aliomba hifadhi ya jina lake, alikiri kuwa kutumia madawa bandia kunachangia homoni za mwili kuvurugika.
“Si ARV’s bandia tu, mtu yeyote anaweza kutumia dawa nyingine bandia au za kweli zisimpende na homoni za mwili zikavurugika, matokeo yake ni mtu huyo kuota ndevu kama ni mwanamke au kama ni mwanaume kuvimba matiti na makalio kuwa makubwa,” alisema daktari huyo alipoongea na paparazi wetu, juzi Jumanne.

Views: 720

Tags: amani11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

ADVERTISEMENT


Advertisement

 

Forum

KIPIGO CHA BAO 2-1 KWA MAN UTD, KOSA LA MWAMUZI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Mohammed Mar 26. 6 Replies

JE, NI KWELI KWAMBA KIPIGO CHA BAO 2-1 ILICHOKIPATA MAN UTD KUTOKA KWA REAL MADRID USIKU WA KUAMKIA LEO LAWAMA ZOTE ZIMWENDEE MWAMUZI WA MCHEZO AU MAN UTD WAJILAUMU WENYEWE? TUPE MAONI YAKO!!!

HALI INAYOENDELEA BUNGENI, SPIKA NA NAIBU WAKE WAMESHINDWA KUONGOZA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Ali Abdalla Ali Apr 22. 20 Replies

Tumeshuhudia kwa siku za hivi karibuni hali halisi iliyokuwa inatokea katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, kwa hali hii ni ishara kuwa Spika na Naibu wake washindwa kuliongoza bunge hilo?

VURUGU ZA CCM NA CHADEMA KUGOMBEA MLINGOTI WA BENDERA DODOMA, NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by Phinehas Rishiansia Kileo May 3. 6 Replies

Wafuasi wa CCM wakimshambulia mfuasi wa Chadema mkoani Dodoma…

Tags: BENDERA, WA, DODOMA, NANI, KULAUMIWA?

VURUGU ZINAZOENDELEA HAPA NCHINI NANI WA KULAUMIWA?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by mayalilwa Mar 8. 26 Replies

HIVI KARIBUNI KUMEKUWEPO UPOTEVU WA AMANI HAPA NCHINI PAMOJA NA WANANCHI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI. MKOANI KAGERA WANANCHI WENYE HASIRA WALIWAUA POLISI, IJUMAA ILIYOPITA WAKULIMA NA WAFUGAJI HUKO WILAYANI KILOSA WALIZUA VURUGU NA KUFUNGA BARABARA,…

MRISHO NGASSA KUPELEKWA SIMBA SC BILA RIDHAA YAKE, JE NI HALALI?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by Domino Bagambisa Jan 21. 17 Replies

Kiungo hatari wa Azam FC, Mrisho Ngassa leo amepelekwa Simba SC kwa mkopo na timu yake…

Tags: SOKA

hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Started by Gysper in Siasa. Last reply by Jamal amor May 9. 24 Replies

 hivi ni nani yuko sahihi kuhusu uchaguzi wa UMEYA arusha CCM au CHADEMA?

Kauli Ya JK kuwa Mauaji ya Arusha ni "Bahati Mbaya"

Started by Kulikoni Ughaibuni in Siasa. Last reply by richardngeze Feb 12. 12 Replies

Tanzania tuna tatizo kubwa.Hakuna haja ya kunyoosheana vidole as to nani amechangia tatizo hilo bali cha muhimu na haraka ni namna tutakavyoweza kutatua tatizo hili.Nisimung'unye maneno: tatizo kubwa linaloikabili ni kuwa na Rais ambaye takriban…

© 2013   Created by Global Publishers.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service