Al-Shabaab yaungana rasmi na al-Qaeda

Kundi la Waislam wenye itikadi kali nchini Somalia, al-Shabaab, limetangaza kuwa linaungana na kundi la al-Qaeda.

Mpiganaji wa al-Shabaab akisimamia ugawaji chakula Somalia

Tamko hilo limetolewa katika picha ya video iliyotolewa na makundi hayo mawili.

Yusuf Garaad wa Idhaa ya Kisomali ya BBC ambaye ameitazama video hiyo amesema kundi hilo ambalo jina lake kamili ni Harakat al Mujahiddin al Shabaab, limetangaza rasmi kuungana na al-Qaeda.

Madai ya muungano huo yametolewa na kiongozi wa al-Shabaab, Ahmed Godane, au maarufu kama Abu Zubair.

Mkuu wa al-Qaeda, Ayman al-zawahiri

Akizungumza kwa lugha ya Kiarabu,Abu Zubair amesema sasa watatii maelekezo kutoka kwa kiongozi wa al-Qaeda, Ayman al-Zawahiri.

Akizungumzia Marekani, Ahmed Godane amesema wakati wa dola pekee duniani- Marekani - sasa umefikia mwisho na kuwa utawala wa Uislam ndio utachukua mamlaka.

Kiongozi wa al-Qaaeda, Ayman al-Zawahiri, ambaye pia ameonekana katika video hiyo, ameisifia al-Shabaab na kukiri na kukubali kwa kundi hilo kuungana na al-Qaeda.

Amesema hizo ni habari njema kwa wafuasi wake.

Wapiganaji

Al-Zawahiri amesema Somalia itakuwa ngome ya Jihad katika pembe ya Afrika na kuongeza kuwa watateketeza kile alichotaja kuwa ni kiburi cha majeshi ya Kikristo kutoka Marekani, Ethiopia na Kenya dhidi ya Wasomali.

Ametoa wito kwa al-Shabaab kulinda watu wake hasa wale ambao ni dhaifu, na pia kutaka kwa wananchi wa Somalia kuunga mkono uamuzi wa vijana wao, akimaanisha al-Shabaab.

Al-Shabaab ni kundi lenye wapiganaji maelfu kadhaa, wengi wao wakiwa ni Wasomali. Hata hivyo wanao pia wapiganaji wa kigeni kutoka katika nchi zinazoizunguka Somalia na hata sehemu nyingine duniani.

Mitindo yao ya upiganaji ni pamoja na mabomu ya kujitoa mhanga na pia ya kutegwa ndani ya magari.

Mwenendo

Al-Shabaab kwa sasa inadhibiti maeneo kadhaa ya kusini na kati ya Somalia.

Katika miezi kadhaa iliyopita wamekuwa wakibanwa kutoka pande kadhaa. Mjini Mogadishu wanapambana na majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika, Amisom, yenye wanajeshi kutoka Uganda, Burundi na Djibouti. Majeshi hayo yanadhibiti zaidi mji mkuu, Mogadishu.

Upande wa kusini, majeshi ya Kenya yameshambulia ngome za al-Shabaab ardhini, baharini na angani. Majeshi ya Ethiopia pia yanashambulia kundi hilo kwa upande wa kaskazini na tayari wameteka mji wa Beled Weyne, mji muhimu katikati mwa Somalia.

Kuungana kwa al-Shabaab na al-Qaeda huenda kukabadili mwenendo mzima wa mzozo wa Somalia.

chanzo na bbc swahili

Views: 531

Tags: Al-Shabaab, al-Qaeda, na, rasmi, yaungana

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by Arab Boy on February 12, 2012 at 1:25pm

Dr Simba. Wewe hauna ufahamu kuhusu mambo ya utumwa au biashara ya utumwa. Tazama link hii ili upate kufungua akili yako na ujue biashara hii ilikuaje.

http://en.wikipedia.org/wiki/History_of_slavery

Comment by samora rajab albert on February 11, 2012 at 7:36pm

hawa nao sijui wanafanya kazi sa ngapi?

Comment by bongo on February 11, 2012 at 3:02am

Dr Sambi...Utumwa ulianza karne 15 iliyopita wakati mwingereza alivoanza kutawala dunia.Mwingereza alivoitawala dunia aliweza kuichukua Spain ,Scotland, Irland na mpaka huko Amerika,Canada mpaka Australia na nyingi ambazo hatuwezi kuzitaja.Na walisaidiana wajerumani, wafaransa na wapotugizi kuzitawala mpaka nchi za Afrika.Na biashara ya utumwa iliwasababisha waafrika kupelekwa amerika kwenda kuijenga nchi.Hao waarabu unaowazungumzia hapo Zanzibar walifanya biashara ya utumwa chini ya utawala wa kingereza.Kwasababu Mfalme aliekuwapo hapo alikuwa analindwa na waingereza na amri yote inatoka kwa wazungu yeye ni kama picha tu.Sasa wewe hufai kulalamikia waarabu kwasababu hawajakutawala hata kidogo.Waarabu kuja kwao huku Afrika ni kibiashara zaidi.Na historia tuliosoma mashuleni ni potofu kwakuwa waingereza bado wametawala mpaka hivi leo.Kwahiyo ni muhimu kuijua historia bila kujali Dini wala Kabila ili tufaidishe jamii yetu ijayo kwasababu watatudharau baadae kama hatujisahihishi kwa kile tulichoambiwa uongo.Waarabu hawajakutawala wewe wala hawajakunyonya na wale waliowanyanyasa mababu zetu na kuwatumia hutaki kuwasema Why????Na mpaka leo hii bado tunawatumikia kisaikologia na mpaka rasilimali zetu bado wanazitumia huku wananchi masikini.Wake up Dr Sambi!!!! 

Comment by Mawazo Katota on February 11, 2012 at 12:25am

Mmmmmmh ni rahisi kusema. kweli mambo ni magumu sana nchini somalia. Nawapa pole sana wananchi wa nchi hiyo.

Comment by Richard Laurent on February 10, 2012 at 7:55pm

Jamaa wana msimamo wa Kinyama, hawana ubin adamu hata kidogo

Comment by bongo on February 10, 2012 at 7:36pm

Mh!! Dr Sambi mimi nadhani wewe ndio mgumu kuelewa dunia hii ilipotokea na tunakokwenda.Nadhani rudi uangalie upya historia ya dunia hii ili ujue mbaya wako ni nani.Mbona mambo siku hizi yapo waziwazi tu lakini bado watu kumbe mme lala hebu amkeni jamani msipende kutawaliwa hivo.Ni muhimu kwa vizazi vyetu ili wasije fanya makosa tuliyoyafanya kwakweli itakuwa ni aibu na sijui tutawaeleza nini.Hebu tafuta mtu wa kutoka West Africa akupe historia yao.Tusisubiri mpaka yakafika kwetu inabidi tuwe makini ili tuinusuru nchi yetu.Wakija huku kutuchanganya vichwa vyetu kama wewe unavojichanganya basi ujue tutakufa kwa mafungu na mali asili zetu zitachotwa zote na watafanya nchi yao na kujitia kuja kutupa usalama huku wanatuua taratibu.Nadhani watanzania sasa umefika wakati tuache hizi starehe za kupitiliza kiasi na kufanya ibada kwa wingi kwasababu vita kila kona.Maana Dar siku hizi kila siku kunafunguliwa sehemu za starehe na kuwapumbaza wananchi mpaka tunajisahau na kuona hatufi.

Comment by julius manning on February 10, 2012 at 4:45pm

hiyo ni propoganda yao baada ya kuona wamebanwa vilivyo na hawana pa kupumilia, hao wahaini sharti waangamizwe tumechoka na unyanyasaji wao wa kuwanyima wenzao Elimu ambao ni ufunguo mhimu katika maisha ya binadamu

Comment by kaka on February 10, 2012 at 2:27pm

MAMBO YA MAJAMBAZI HAO YOTE NI BIASHARA YA MAREKANI KUNA BIASHARA HAPO

Comment by Dr Sambi on February 10, 2012 at 2:06pm

wee thabit unaelekeaa ulikuaa unakuaa wa mwisho darasani kila siku maana sasa ujui duniaa inakwenda vp wee marekani tuu basi uwoni kwamba kuna vita ya siri kati ya waislamu na wakrito auu unateteaa ilii umwagaji damu utokeee wee kwelii mslamuu hawo al shababi al quida wote mashetani wakubwa ujuii kuwa mwarabu ndioo aliyoo anzishaa utumwa afrika na kufanya mpaka wazungu kutufanya na sisi watumwa yani kwa kifupi yeye ndio alianzisha wizi africa mpaka wameichukuaa nusu ya afrika leoo hii unaona nnchi kama tunisia libya egypt algeria na morocoo zote hizi zilikuaa arthii ya watu weusi na sioo waarabu mwarabu ndioo aliaanzisha kumzarau mtuu mweusi na kumfanya kama mtumishi mambo ambayo mpaka leoo yanatokeaaa kwenye jamii ya watu weusi kwaiyo wacha ulimbukeni hao wanatakiwa kumwagiwa asidi watokomee wote.

Comment by thabit .. on February 10, 2012 at 12:23pm

hayo ni makundi ya wamarekani yenye nia ya kuangamiza Afrika, hakuna cha al-shabaab wala al-qaida. hizo ni propaganda tu.


ADVERTISEMENT


TANGAZA HAPA

ADVERTISEMENTS

Latest Activity

GUNZ TRUVADA posted a status
"KUMPA ASIYE KUPA NI SAWA SAWA NA KUTUPA"
1 minute ago
othman Ochu posted a status
"SCENE 1 WAHUSIKA: AMIDU , SHARIFA MAHALI: ZANZIBAR MUDA : JIONI ( WAKIWA WANASHUKA TOKA KATKA BOTI YA JION KUINGIA KATKA MJI WA ZANZI"
9 hours ago
Priscus Adelard shared GLOBAL's blog post on Facebook
9 hours ago
mrembo commented on julius manning's photo
Thumbnail

Mtanzania huru

"pole sana usijali iko siku mungu atakujaalia mungu hamtupi mja wake"
10 hours ago
mrembo commented on Sili Silali's photo
Thumbnail

Duh!

"mama mzima hayawani mavazi gani hayo takupa mfano chungwa likiwa halijamenywa unatamani ulile…"
10 hours ago
kaka commented on Ali Amur Ali's video
Thumbnail

AZIMIO LA KUANGAMIZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE

"hapo ni kina dada kutua comment zao"
10 hours ago
Gaston Kayombo commented on Ali Amur Ali's video
12 hours ago
roylicious and Jackson Jacob are now friends
12 hours ago
babu wa loliondo (cup) updated their profile
12 hours ago
julius manning commented on julius manning's photo
Thumbnail

vijana 2016 itakuwa hivi

"@furaha mimi ni kikongwe hayo ni kazi kwako."
13 hours ago
Masalu Mayeji Many'hasimha shared GLOBAL's blog post on Facebook
13 hours ago
kheri zewe commented on Sili Silali's photo
Thumbnail

Duh!

"minyama uzembe"
13 hours ago

© 2012  

Designed & Developed by
G5 CLICK COMPANY.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

How to make a Website