AJALI YA MV BUKOBA TUMESHINDWA KUJIFUNZA?

NI mfano wa sinema ya kutisha iliyojaa kila aina ya ukatili. Abiria wachache walionusurika katika ajali ya kuzama kwa meli ya Mv Bukoba Mei 21, mwaka 1996 bado wanaamini walipona kwa muujiza.

Miaka kumi na sita baada ya tukio hilo, leo hisia zinaturudisha katika kumbukumbu za ajali hiyo ambayo ilipima uwezo na udhaifu wetu wa kukabiliana na maafa ambayo tumeendelea kuyashuhudia kwa vipindi tofauti.

Wanafunzi wa sekondari za Bwiru wavulana na wasichana wanaikumbuka sana siku hii hasa waliozoea kuoga ziwani asubuhi, kwa mbali waliona harakati za mitumbwi na meli eneo la tukio. Wengi walitoroka na kujikuta uwanja wa mpira Nyamagana wakishangaa kuwasili kwa miili ya marehemu.

Tangu kuzama kwa meli ya Mv Bukoba limebaki kuwa tukio la kihistoria ambalo athari zake ziko wazi kwa mamia ya familia waliopoteza ndugu na wategemezi wao. Inakadiliwa zaidi ya watu 800 walikufa ingawa katika nchi isiyo na mfumo mzuri wa ukusanyaji wa takwimu kwa vyovyote vile idadi hiyo haiwezi kuwa sahihi.

Kwamba meli hiyo ilikuwa imejaza kuzidi uwezo wake sio habari mpya, kwani tangu wakati huo mamia ya wasafiri wa majini wameendelea kupoteza maisha kwa tatizo lile lile la kuruhusu vyombo vilivyochoka kuzidisha abiria.

Familia zilizokuwa na uwezo ziligeuka masikini, yatima, na wajane wakishindwa kudai mali za ndugu zao. Wenye tamaa walitumia udhaifu wa marehemu kutoandika wosia kupora mali na kujitajirisha na hata familia za wahanga kubebeshwa mzigo wa madeni.

Tulitakiwa kujifunza kutokana na ajali hiyo kuliko kuendelea kuficha udhaifu wa vyombo hivyo kwa kuvipaka rangi mpya huku tukijua havina uwezo au vimepoteza sifa ya kusafirisha abiria na mizigo yao.

WASEMAVYO WAHANGA WA MEI 21, 1996
David Mutensa mfanyabiashara wa mjini Bukoba ni miongoni mwa abiria walionusurika ambaye hajui sehemu ya kuanzia simulizi baada ya kuelea majini kwa muda wa saa tano akisubiri kuokolewa.

Anaanza hivi:

Akiwa ni abiria wa daraja la kwanza aliona hali imekuwa mbaya mapema alfajili na meli ilipoanza kupinduka na kuzama alichukua boya dogo na kujirusha majini huku kila abiria akipigania roho yake.

“Sijui pa kuanzia kwani lilikuwa ni tukio la ghafla, meli kupinduka haijawahi kutokea duniani nilivaa boya dogo na kumwambia mwanamke aliyekuwa jirani yangu twende, akasema twende wapi mwanangu” anaeleza

Anasema alifahamu matumizi ya maboya (life jacket) baada ya kusafiri mara nyingi na meli na wakati mmoja mabaharia waliwahi kufanya mazoezi ndani ya meli jinsi ya kujiokoa kwa kutumia vifaa hivyo.

Maana yake ni kuwa wapo abiria wengi ambao hawakuwahi kuona vifaa hivyo achilia mbali kufahamu matumizi yake na kwa kuikosa elimu hiyo walishindwa kujiokoa hata kama vifaa hivyo vilikuwa mbele yao.

Huyu ni miongoni mwa abiria wengi waliolazimika kuanza upya shughuli zao za biashara na kuwa kifuta machozi cha shilingi laki moja kwa aliyenusurika na laki tano kwa waliopoteza ndugu hakikuwa kipimo sahihi ikilinganishwa na madhara waliyopata.

Simulizi ya Benezeti Benedict (46) mkazi wa kijiji cha Kashaba wilayani Missenyi inasikitisha. Ilikuwa mara yake ya kwanza kupanda meli akielekea Dar es Salaam na kuwa ana kumbukumbu mbaya za tukio hilo na hakuwahi kutamani kupanda tena meli.

Anasema akiwa ni abiria wa daraja la tatu pamoja na ugeni wake kwenye meli majira ya saa tisa usiku meli ilionekana kuwa na tatizo hali iliyomfanya asilale na kupakata begi kwa hofu.

Anachokumbuka ni kuwa ililala upande wa kushoto na baadaye upande wa kulia majira ya alfajili na kujikuta ameshikilia boya moja watu saba akiwemo mwanamke mmoja.

“Sikuwahi kupanda meli, usiku nilikuwa na wasiwasi na ilizama taratibu kwa kulalia upande wa kulia nilikimbilia upande wa nyuma ya meli na kuona watu wakielea majini” anasema

Ni tukio analosema lilikuwa mwanzo wake wa kuwa na ugonjwa washinikizo la damu mpaka leo, anapokumbuka picha mbaya ya ajali hiyo.

Huyu naye alipona kimiujiza. Geofrey Francis mkazi wa kijiji cha Buhembe nje ya mji wa Bukoba alikwenda bandarini amechelewa na matokeo yake aliambulia virungu vya polisi waliokuwa wanawazuia abiria wasiendelee kujipenyeza na kupanda meli hiyo.

Anadai juhudi za kutoa kiasi kidogo cha fedha kwa askali ili aruhusiwe hazikufanikiwa na aliungana na abiria wengine watatu ambapo walichukua uamuzi wa kukodi tax na kuifuata meli hiyo bandari ya Kemondo.

Katikati ya safari ya kuelekea Kemondo yalitokea mabishano kama kweli wataiwahi meli hiyo, tofauti iliyomfanya kila mmoja kutafuta sehemu ya kulala bila shaka kujipanga kutoa maelezo kwenye familia juu ya kisa cha kuachwa na meli.

Ni baadhi ya maelezo ya walionusurika, na wakati tukikumbuka miaka kumi na sita tangu kuzama kwa meli ya Mv Bukoba yameendelea kuwepo maafa mengi kama ushahidi kuwa uwezo wa kukabiliana na majanga bado haujaimarika.

Pamoja na ukubwa wa tukio hili taifa limeshindwa kutenga hata dakika moja ya kukaa kimya kuwakumbuka wahanga waliopoteza maisha. Dakika ya kutafakari tulipokosea na kujutia uzembe wetu ambao ni chanzo cha machozi, jasho na damu.

Wakizungumzia hali ya usafiri wa majini ilivyo sasa na wakati uliopita baadhi ya wananchi wameshauri kufanyika kwa ukaguzi wa mara kwa mara na kuongeza udhibiti wa ajali za majini.

Mmojwa wa wananchi hao John Lwekanika alilalamikia ubovu wa vyombo vinavyosafiri na kuwa Mv Bukoba isingezama kama viongozi wangekuwa makini tangu ununuzi wake hadi kuruhusu matumizi.

Anadai kuwepo kwa taarifa za muda mrefu kuwa meli hiyo ilikuwa na mapungufu ambayo yalifumbiwa macho na hatimaye kusababisha maafa makubwa.

Naye mshindi wa tuzo ya uandishi wa masuala ya majanga kwa mwaka 2010 Salome Gregory, anasema taifa halina mipango bayana ya kukabiliana na majanga na kuwa matukio mengi yanaweza kukabiliwa endapo viongozi watakuwa na dhamira ya kweli.

Ni mshindi kutoka gazeti la The Citizen ambaye anaamini elimu ya majanga ikitolewa mashuleni na katika ngazi ya familia utakuwa ni msingi wa kuzalisha viongozi watakaoibuka na mikakati ya kuyakabili majanga.

MAJANGA NA USIRI WA TAARIFA
Kama ilivyo ada matukio mengi ya maafa huundiwa tume za uchunguzi na hatimaye matokeo yake huwa siri ya waliochunguza na wale waliopelekewa taarifa.

Mapendekezo ya tume hufungiwa kabatini na wananchi huendelea kuongozwa na hisia wakati wa kujadili utata wa tukio.

Katika nchi ambayo watendaji hugoma kuwajibika kwa kujiudhuru hata kama maafa yanahusishwa na uzembe, taarifa hizi ni muhimu kwani zinatoa mwanga kwa walioathirika kufungua malalamiko ya kulipwa fidia wakitegemea ushahidi wa tume.

Tangu kuzama kwa meli ya Mv Bukoba yamefuata maafa mengi yaliyohusisha kuzama kwa meli ya MV Spice na Mv Nyamageni, mitumbwi, treni, kufukiwa migodini achilia mbali maafa ya hivi karibuni katika kambi za jeshi Mbagala na Gongo la Mboto.

Tulitakiwa kujifunza kutokana na makosa na haikutegemewa kuwa baada ya miaka michache meli ya Mv Nyamageni ingezama katika ziwa lile lile na kuua abiria 28, na mpaka leo taarifa ya uchunguzi wa ajali hiyo haiko wazi.

Hakuna kiongozi aliyewajibika kama ambavyo hawafikirii, pale walipokufa abiria 281 tarehe 24, Juni 2002 baada ya treni kugongana na 73 kuzikwa makaburi ya maili mbili kule Dodoma baada ya kutotambuliwa kama wale wa Mv Bukoba waliozikwa kule Igoma jijini Mwanza.

Kama somo lingekolea ajali ya Agosti 5, ya wanafunzi 18 kufa maji kwa mtumbwi ziwa Victoria wilayani Sengerema wakienda shuleni isingetokea.Tukio hilo lilitanguliwa na vifo vya wanafunzi tisa waliozama mto Rufiji mkoani Pwani. Hatuwezi kukwepa ukweli kuwa ajali nyingi hazirekodiwi.

Tumeshuhudia juhudi za kujikosha kama ilivyokuwa baada ya wanafunzi 48 wa sekondari ya Shauritanga kuungua mabwenini. Shule zilipewa vifaa vya kuzima moto na kufundishwa matumizi yake. Hakuna anayejua kama ilikuwa hujuma, uzembe au vinginevyo. Mwaka juzi Shule ya wasichana Rugambwa mabweni yaliungua mara tatu na wanafunzi kunusurika kifo na hakuna kifaa chochote cha kuzima moto.

RAIS KIKWETE NA UJIO WA MELI MPYA
Miongoni mwa ahadi lukuki za rais Jakaya Kikwete kwa wakazi wa mkoa wa Kagera wakati akisaka muhura wa pili wa uongozi ni meli mpya kama mbadala wa Mv Bukoba. Ni kauli yenye matumaini na hakuna sababu ya kuitilia shaka kwamba ilificha hila za wanasiasa hasa pale uchaguzi usipotabilika.

Pamoja na kuimarika kwa miundombinu ya barabara kati ya Bukoba na Mwanza bado uhakika wa usafiri wa majini ni muhimu kwa ajili ya shughuli za kiuchumi. Wananchi watachagua aina ya usafiri waupendao na kuongeza ushindani katika upangaji wa bei.

Hata meli kongwe ya Mv Victoria ambayo inafanya safari zake kati ya Bukoba na Mwanza imeendelea kuwatia abiria wake majaribuni na imekuwa ikifanyiwa matengenezo ya mara kwa mara ambapo katika kipindi hicho meli ya mizigo ya Mv Serengeti huziba nafasi hiyo kwa muda.

Mwaka 2004, meli ya Mv Victoria iligonga mwamba eneo la Mubembe ikitoka Mwanza kuelekea Kemondo. Katika hotuba ya mpango wa maendeleo na makadirio ya matumizi ya fedha 2004/2005 aliyekuwa Waziri wa Mawasilinao na Uchukuzi Profesa Mark Mwandosya alidai ajali hiyo ilisababishwa na uzembe wa wafanyakazi.

Alisema uchakavu wa meli na changamoto nyingine vilisababisha lengo la makusanyo lisifikiwe kwa asilimia sita. Hata hivyo kosa moja la uzembe linaweza kuteketeza maisha ya maelfu ya watu na hali hiyo haiwezi kudhibitiwa kwa kushushwa vyeo au uhamisho.

Kumbukumbu ya kuzama kwa meli ya Mv Bukoba iturudishe kwenye umuhimu wa kuwa na viongozi wanaowajibika kwa kauli na vitendo. Ni dakika moja ya kujuta na kutafakari.

Makala hii iliandikwa na Phinias Bashaya akiwa Bukoba, Kagera.

Views: 707

Tags: BUKOBA, MV

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by msichoke mlugu on May 22, 2012 at 6:54pm

du  sijui lini?

Comment by lumi mwandelile on May 21, 2012 at 3:12pm

LABDA SIKU AKIZALIWA NYERERE MWINGINE, NDO SERIKALI ITAKUWA MAKINI NA MAJANGA

Comment by gaddafi on May 21, 2012 at 3:08pm

INASIKITISHA

NI SUPERMARKET GANI BORA KULIKO ZOTE KATI YA HIZI? NA KWA NINI? TOA MAONI YAKO!
  

Forum

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by cantonna Mar 18. 2 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by penina mwailunda on Thursday. 2 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by 278l80orb0i39 Mar 4. 1 Reply

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by 278l80orb0i39 Mar 4. 1 Reply

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by 278l80orb0i39 Mar 4. 5 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by 278l80orb0i39 Mar 4. 18 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by 278l80orb0i39 Mar 4. 32 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

JUAN MATA KUTUA MANCHESTER UNITED ATASIADIA KULETA MATOKEO BORA BAADA YA TIMU KUSUASUA?

Started by GLOBAL in Burudani. Last reply by 278l80orb0i39 Mar 4. 90 Replies

Juan Mata anataraji kutua Manchester United akitokea klabu ya Chelsea ya…

TOP NEWS WEEK HII

Latest Activity

dorah fredy commented on GLOBAL's blog post JINI ALINIGEUZA MWANAUME ILI NIMUOE - 14
"mmmmh"
7 minutes ago
ludger nyagali commented on GLOBAL's blog post THE BLOOD STAINED DRAFT - 93
"Haya sasa!!!!!!!!!!!!!!!1"
7 minutes ago
FURAHA TAUSI commented on GLOBAL's blog post WEMA, IDRIS MAHABA NIUE!
"hivi mnafikiri hivyo vinywaji vilivyopo hapo mezani ni chai au gahawa?"
7 minutes ago
dorah fredy commented on GLOBAL's blog post BASI TOROKA UJE - 17
"Makubwa sasa hapo sasa Zambi mtu mzima eeeeeeeeehhhhh"
7 minutes ago
ellymtima commented on GLOBAL's blog post Wakala wa Shetani - 32
"Hii story imeniboa yan uongo live ilo jibaba la miaka 50 liko wap???"
7 minutes ago
Suzaney Jackson commented on GLOBAL's blog post MWOKOTA CHUPA ZA MAJI - 17
"Duuuh lindaa"
7 minutes ago
Lisa Balou commented on GLOBAL's blog post WEMA, IDRIS MAHABA NIUE!
"Idris remember what your mama warned you about when you were in the bba house!"
7 minutes ago
Suzaney Jackson commented on GLOBAL's blog post BASI TOROKA UJE - 18
"Ujing uo judi akakufie uko"
7 minutes ago
Lisa Balou commented on GLOBAL's blog post ASKOFU GWAJIMA ATOLEWA POLISI KWA DHAMANA
"Vanesa umenena yote na mimi najiuliza hivyo hivyo, hasa la waumini kumshangilia askofu wao…"
7 minutes ago
ludger nyagali commented on GLOBAL's blog post Golden Tears (Machozi ya Dhahabu) - 54
"Jonathan unataka kuua!!!!!!!!!!!!!!!!"
7 minutes ago
FURAHA TAUSI commented on GLOBAL's blog post JINI ALINIGEUZA MWANAUME ILI NIMUOE - 14
"duh hatare"
7 minutes ago
penina mwailunda commented on GLOBAL's blog post ASKOFU GWAJIMA ATOLEWA POLISI KWA DHAMANA
"Ha ha ha Vanesa wewe!!!, hapo akili zako inatakiwa uzichanganye,  unakumbuka fungu fln hv…"
7 minutes ago

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }