Na Mwandishi Wetu
Ofisa Mwandamizi Uchukuzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Makao Makuu jijini Dar, Kitengo cha Makontena, Leslie Milanzi (54) amejikuta ndani ya aibu nzito kufuatia madai kwamba, amekutwa akiwa na mke wa mtu kwenye nyumba ya kulala wageni ‘gesti hausi’, Ijumaa Wikienda linashuka na ‘diteilzi’.

Tukio hilo lililoacha historia, lilijiri Desemba Mosi, 2010 (Siku ya Ukimwi Duniani) majira ya alasiri kwenye chumba namba tano cha hoteli moja (jina tunalo), Buguruni, Dar.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, mume aliyejitambulisha kwa jina la Shaha Juma alidai kumbamba Milanzi akiwa na mkewe wa ndoa aitwaye Salia.

Chanzo hicho kikaongeza kudai kuwa, kabla ya fumanizi hilo lililokusanya mashuhuda kibao, mume wa mwanamke huyo alikuwa na kibarua kizito cha kufuatilia nyendo za ‘wezi’ hao mpaka ndani ya chumba hicho.

“Unajua jamaa kabla hajawabamba, alifuatilia kwa karibu mno nyendo zao za siku hiyo mpaka wanaingia hapa gesti, pia akahakikisha anakijua na chumba,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kiliendelea kuanika kweupe kwamba, baada ya mwanaume huyo kujiridhisha kwamba, mkewe Salia na mzee huyo wamo ndani ya chumba hicho, aliita mashahidi ambao hawakutajwa majina ili kushuhudia tukio hilo.

Inadaiwa kuwa, mlango uligongwa na mume wa mwanamke huyo alizama ndani sanjari na mashahidi wake na kuanza kumhoji Bw. Milanzi kisa cha kuingia gesti na mke wa mtu ambapo alibabaika katika utetezi.

Lakini kwa upande wa pili, habari zilizopatikana kutoka kwa wahudumu wa gesti hiyo zinadai kwamba, Milanzi alijitetea kwa kusema kuwa, kama ni lawama basi mwanamke huyo ndiye anayetakiwa kubebeshwa, kwani hakuwahi kumwambia mzee huyo kuwa yeye ni mke wa mtu.

Aidha, ilisemekana kuwa, mbali na mwanamke huyo kutosema ni mke wa mtu, lakini pia hakuwa na dalili zozote zinazoonesha kuwa ameolewa, kama vile pete au hofu ya muda.
Ijumaa Wikienda lilimsaka Shaha na kumuuliza kama kuna ukweli wa madai hayo ambapo alikiri.

“Ni kweli, mke wangu nimemkuta chumba cha gesti na mwanaume, lakini nimeshawahi kumuonya kwa simu mara kadhaa huyu mzee aache kumchukua mke wangu, hakutaka kusikia,” alisema mume huyo.

Akaongeza: “Taarifa za tukio zipo Buguruni Polisi lakini RB ipo nyumbani (hakusema ni wapi) na kwa wakati huu siwezi kurudi kwa sababu nipo kazini.”

Wikienda lilipofika Kituo cha Polisi Buguruni, lilikosa ushirikiano kutoka kwa askari waliokuwa zamu siku ya Ijumaa baada ya kudai kuwa wao si wasemaji wa jeshi hilo.

Kwa upande wake, mzee Milanzi alipopatikana kwa simu yake ya mkononi siku ya Ijumaa alikiri kutokewa na tukio hilo, lakini akasema ‘amechoreshewa’.

“Ni kweli mkasa umenikuta, lakini umechezeshwa tu na watu. Yule mwanamke hajasema ameolewa,” alisema.

Mzee huyo aliongeza kuwa alipenda kufika kwenye ofisi za gazeti hili, Bamaga- Mwenge ili kuweka wazi kila kitu lakini akasema kwa bahati mbaya alikuwa safarini Morogoro.

Hata hivyo, katika hali isiyokuwa ya kawaida, dakika chache baada ya ‘mtuhumiwa’ huyo kumaliza kuongea utetezi wake, simu yake iliingia kwa mwandishi wetu ambapo sauti ya mtu mwingine ilisikika ikivurumisha matusi huku ikidai kama habari hii itatoka gazetini watu wataoneshana kazi mjini.

“Ninyi ni matepeli tu, hamna lolote, mnaunganisha unganisha picha halafu mnawasingizia watu, ala…(tusi), nakwambia hivi, ninyi…(tusi) kama hii habari itatoka basi hapa mjini (Dar) tutaoneshana kazi, si mnajifanya watoto wa mjini,” ilisema sauti hiyo na kukata simu.

Baada ya dakika tano, simu ya Milanzi iliingia tena kwa mwandishi na alipoipokea, sauti ya Milanzi ilisikika ikisema:

“Unajua bwana haya mambo yana utata mkubwa, mimi nimeonewa, hapa nilipo imebidi niwasiliane na watu wa Ikulu ili kuona tunafanyaje.”

Mwandishi wetu alimpa ‘kibali’ mzee huyo cha kuendelea kuwasiliana na watu wa Ikulu kama alivyodai lakini alimpa angalizo kuhusu watu wanaotumia simu yake kutukana na kukejeli.

...mpango mzima ulifanyika hapa..!

Views: 2941

Tags: ijumaawikienda11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by Mumewangu NAKUPENDA on December 12, 2010 at 5:04pm

yani huyo adhabu yake ni kumwachia uhuru ili afanye umalaya wake vizuri na kuangalia ustaaharabu mwinge mwanaume unasahauuuuuuuuuuuuuuuuuu

Comment by Habibu Kissio on December 12, 2010 at 12:32am

Huyo siye mke tena ni jamvi la wgeni,mie na mshauri huyo bwana mwenye wala asipoteza muda kupambana na mgoni wake wala kumfungulia jalada polisi kufanya hivyo ni kupoteza muda na pesa bure,yeye ni kumfungulia milanago mwana mama milango na kumtupia virago vyake akaendeleze ukware wake na tafundishwa na Mwailmu Mkuu wa wazinzI UKIMWI,kwani hata akimsmehe na akaendelea nae hawezi kuwa mke mwema na hawezi kufahamu kama ameshaathirika,na tunapashwa kuelewa kwamba si kila mwana mke anaweza kuwa mke wengine ni makeke na si kila mwana ume anaweza kuwa mume wengine ni magumegume,

Comment by Nehemia Mukunzi on December 9, 2010 at 8:28pm
Duh! Wera werraaaaaaaaa! mimi sina cha kuongezea maana watu wamenena kweli kweli humu!
Comment by levina nestory on December 7, 2010 at 3:13pm
ACHA WALI RAHA ZAO
Comment by D-MOVIC-PRINCE DILEN_DEMBA BA on December 7, 2010 at 2:23pm
DU KWANZA NAKILANI HIKI KITENDO CHA HUYU SIO BOSS BALI NI MMBWAAAA MKUBWA KWA KUFANYA HII KITU 2 SHAHA KWELI WEWE UNAHULUMA SANA POLE KWA HILO KAMA INGEKUA NI MIMI BASI HUYU BOSS WA BANDALI LAZIMA NA YEYE NIMTAFUNDE SIWEZI KUBALI ONA MKE WANGU KAMTAFUNA NA MIMI NIMUANGALIE TU LAZIMA NA YEYE NIMGEUZE BANA SIWEZI MUACHA HV HV TU LZM NIKUCHAKACHUE SANA BANA 3 KWANZA LAZIMA HATUA KALI ZICHUKULIWE KWA KUWATISHA WATU HATI UNAPIGA SIMU IKULU SIO UTAZANI WATU WATAKUOGOPA UKITAJA IKULU NDEZIIIIIIIIII WEWE NA 4 KUOMBA IKULU MSAMAHA KWA KUIZALILISHA IKULU KUWA DANGULO LAZIMA AAZIBIWE HUYU KENGE
Comment by Mushi Isaac on December 7, 2010 at 12:26pm
Hizi ni misheni za mjini tu,njaa kali kuna watu wanatapeli kwa njia hizi mjini hivi sasa aangalie sana hata huyo dada anahusika katika hilo kwanini hakumjulisha toka awali kuwa na mume?
Comment by Anselm on December 7, 2010 at 10:59am
Siku ya Ukimwi Duniani wao wanachakachuana pengine bila kinga,haya!!!
Comment by Anita Msuya on December 7, 2010 at 9:14am
Hela za rushwa hadi wake za watu. Limekuchwea. TRA hii ndo kazi yao kubwa.
Comment by Agnes Francis on December 7, 2010 at 8:59am
hapo hata kama ni kuunganisha picha kama asemavyo mbona ni dhahiri kabisa kwamba alikuwa gesti jamani jamani, wanawake tuangalie sana hili wewe mke wa mtu haijalishi umevishwa pete au laa ukiwekwa ndani tayari wewe ni mke, leo hii unaenda kuumbuka kiasi hicho dada mzuri.
Comment by gibson gilberty on December 7, 2010 at 8:15am
ya ngoso muachie ngoso na ya keisali muachie keisali
UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 ZIMEBAKI:

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 7 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 8 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by ages agae Sep 5. 3 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }