Musa Mateja na Issa Mnally
Zomea zomea iliyoambatana na miluzi mingi, ilichukua nafasi wakati wa shoo ya fainali ya Shindano la Bongo Star Search 2010 (BSS), sehemu kubwa ya hadhira ikilalamikia mchezo mchafu a.k.a uchakachuaji wa kura.

Watu hao, walilalamikia matamshi ya majaji kuwa yalionesha dhahiri kwamba mshindi walikuwa naye, hivyo siku hiyo walikuwa wanajaribu kupambana na ‘presha’ ya wengi waliyetaka Joseph Pyne ‘Mzungu’ ashinde.
‘The Biggest IQ’, Ijumaa Wikienda lilikuwepo kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam ambako shindano hilo lilifanyika Ijumaa iliyopita na kushuhudia mchakato mzima ambao ulilalamikiwa kwa kuingia kwa kauli za ubaguzi wa rangi.
MSHINDI
‘Super Vocalist’, Mariam Mohamed Uwesu ndiye aliyeibuka kidedea na kwa ushindi wake, alikabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi milioni 30 ambazo ndizo zawadi yake.

Mariam ambaye ni yatima asiye na baba, akiwa na umri wa miaka 20, alifanikiwa kushinda taji hilo kutokana na mtaji wake mkubwa wa nyimbo za Taarabu na kipawa cha sauti alichonacho.

Baada ya ushindi huo, Mariam a.k.a Mama wa Kujishebedua ambaye ni mkazi wa Mabibo, Dar es Salaam alisema kuwa zawadi hiyo itamsaidia kumtunza mtoto wake, Shamsa mwenye umri wa miaka mitatu.

“Nadhiri yangu ni kumlea mwanangu katika mazingira bora. Nitahakikisha natumia pesa nilizopata kumlea mwanangu,” alisema Mariam.

Akaongeza: “Nawashukuru Watanzania kwa ushindi huu, nawashukuru majaji na familia yangu kwa sapoti waliyonipa.”
UBAGUZI WA RANGI
Majaji wa Shindano la BSS hasa Rita Paulsen ‘Madam’ na Joachim Kimaryo ‘Master Jay’, walitupiwa lawama na watu wengi kwamba kauli zao zilikosa staha, hivyo kujikuta wakizungumza kibaguzi dhidi ya Joseph Pyne.

Maneno yaliyolalamikiwa ni “oneni wanamuziki, siyo Mzungu watu wanababaika na Mzungu, angalieni vipaji,” ambayo yalitamkwa na Madam Rita, mengine yakiwa “watu waache ushamba wa kubabaikia Wazungu,” yaliyosemwa na Master Jay.

Pamoja na kulalamikiwa na wengi, watu wawili kati ya wachache wenye asili ya Bara la Ulaya walisema kuwa Tanzania ni nchi safi isiyo na  ubaguzi lakini walisikitishwa na Majaji wa BSS hasa Rita na Jay.

“Tulikuja kuona shindano na tulifarijika kuona kuna mtu ambaye hana asili ya nchi hii lakini amefika fainali. Tulikuja hapa kushangilia uungwana wa Watanzania lakini kauli za majaji zimetufanya tuumie sana,” alisema Vanessa Holler, raia wa Uholanzi.

Hata hivyo, akitetea hilo, Madam Rita alisema kuwa majaji hawakuwa wabaguzi ila Watanzania ndiyo walioingiza ubaguzi kwa kumshangilia Mzungu asiyeweza na kuwaacha wazawa wenye vipaji.

“Haikuwa nzuri, Watanzania walikosea wakafurahi kuona Mzungu anaimba Kiswahili wakasahau pale tunataka vipaji. Watanzania ndiyo wabaguzi kwasababu waliwabagua wenzao wenye vipaji na kumng’ang’ania Mzungu asiyejua.”
MATOKEO YALIKUWA ‘FEA’
Pamoja na kelele nyingi ukumbini kutaka Pyne ashinde, watu wengi waliozungumza na gazeti hili walisema kuwa matokeo yaliyompa Mariam taji yalikuwa sahihi kwasababu ana kipaji kikubwa.

“Hayo mambo ya majaji watajua wenyewe, kuna ustaarabu kidogo ulikosekana. Tunaangalia ukweli hapa, Mariam alistahili kushinda na yule Pyne hajui kuimba,” alisema George Hamdan wa Sinza.

Ramla Sabah alisema: “Niwapongeze majaji kwa ujasiri wao, wangeweza kushangaza kama wangempa ushindi Pyne, yule hana lolote hata nafasi ya tatu haikumfaa.”

PYNE ALITIBUA
Habari zinasema kuwa Pyne alitibua majaji akiwa ndani ya Jumba la BSS lakini alivuruga zaidi alipochombeza maneno jukwaani aliposema: “Watanzania inukeni tukomeshe ubabaishaji.”

Maneno hayo, yalitajwa kuwa ni dongo kwenda kwa majaji kwa kile kilichodaiwa kwamba tayari alikwishanasa ‘data’ kuwa hatashinda.

Ni kutokana na maneno hayo, mmoja wa majaji wa shindano hilo, Salama Jabir alisema kuwa Pyne hawezi kushinda, vinginevyo angejipiga risasi.
Pyne alipozungumza na gazeti hili alisema:

“Sikuzungumza vile kuwapiga dongo majaji, nilikuwa nasema tu, ila kusema ukweli kwa kura naamini mimi ndiye mshindi, mengine sijui.”
WASHINDI KWA JUMLA
Mbali na Mariam, aliyetoka wa pili ni James Martin, Pyne alishika namba tatu, Bella Kombo alibaki wa nne ingawa alitisha jukwaani mpaka Madam Rita akambatiza jina la Madonna mdogo wakati Waziri Salum heshima yake ni Tano Bora.

Martin alipata shilingi milioni 10, Pyne milioni tano, Bella aliambulia 1,500,000 na Salum akibaki na 1,000,000.

WASHINDI NYIMBO ZA UKIMWI
Martin aliongoza hivyo akanyakua shilingi 1,500,000, Mariam alitoka wa pili akazawadiwa shilingi 1,200,000 wakati Salum alishika nafasi ya tatu na kupewa shilingi 700,000.

Views: 425

Tags: ijumaawikienda11

Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers

Comment by big1 on December 26, 2010 at 8:23pm
WEWE @vita Umeshakaa abroad?kama bado basi ungeishi uku usingeongea uliyoyaongea hapo!!!UBAGUZI upo UK,upo USA upo all over europe!!!mpaka keshokutwa,unalijua hilo? jinsi awo mnaoita wazungu wanavyowatesa dada zetu weusi uku??!!!!bora niashie hapa !!hilo msiyoyajua bora waachieni wausika Master J ndoo muhusika ,kama ubabaishaji bongo ndoo asili yetu bana sasa cha ajabu nini??!!! !!!!!GPL next1 pls
Comment by vita wilbards on December 20, 2010 at 7:16pm

KWA KWELI NILIKERWA NA HISIA ZA KIBAGUZI ZA MASTER J NA MADAME RITA

KAMA HAMKUTAKA WAZUNGU SI MNGEMBWAGA CHINI KATIKA HATUA ZA USAILI NI UBABAISHAJI NA KUKOSA WELEDI WA ART INDUSTRY

MIMI NI MWEUSI LAKINI NINGEKUWA UK NA WAINGEREZA WAKANITOLEA KAULI KAMA HIZO SIKU HIYO HIYO NINGERUDI BONGO SINA MCHEZO NA UBAGUZI KWA KWELI

HALAFU WE MADAMME RITA ULIKOSA NIDHAMU KWA KULEWA SIKU NYETI KAMA ILE, KAMA HUWEZI POMBE SI KUACHA MANAKE KUJISHEBEDUA SI KUJISHEBEDUA MPAKA KICHEFUCHEFU KWA WATIZAMAJI EBO JIREKEBISHE MAMA WALA HUKUPENDEZA

NAKUPONGEZA KWA UBUNIFU WAKO ILA NIDHAMU NI MUHIMU

Comment by ramadhani hamis athuman on December 20, 2010 at 6:23pm

all in all big up master j and rita...nyie ndio wazalendo wakweli...kwa upeo wenu inaonekana kabisa mshakaa nje nakuona wenzetu wanavyopendelea uzawa...wabongo tunababaika sana ndiyo maana tupo nyuma,mama rita ningekuepo karibu ningekukis,mzalendo ulie tukuka...wabongo always mbeleeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!

Comment by Sina dem on December 20, 2010 at 5:05pm

madam Rita ndiyo nini kulewa hivyo, singizia ulikula kungu sana, nawasubiri comedy wakutoe maana unavyoongea kipombe kabisa, masanja mgandamizaji wapi joti?

Comment by HASSAN119 on December 20, 2010 at 4:25pm

hongera mariam ulistahili ushindi mkubwa sana na mzungu alistahili kuwa nafasi ya tatu kwanza tukubali vipaji ni vya watanzania vinavyoenuliwa ili walete ajira mwetu nchini ila tulionesha kutokuwa na ubaguzi wa rangi na majaji nawapongeza sababu kura zaweza  mpa ushindi mtu yoyote asie na kipaji au mtu aweza nunua kura hapo majaji wanajukumu la kuchakachuwa hizo kura na kuangalia nani astahili na bella kombo wewe hata hustahili kufika final kipaji unacho ila kashfa nyingi tangu kwenye nyumba ya kili hse kwa hivyo ulisave kwa kipaji chako lakini miaka ya nyuma watu walitemwa mapema sana kwa utovu wa nidhamu kwa hivyo shukuru mungu wako hapo ulipofika alistahili waziri nafasi ya nne

Comment by saad almas on December 20, 2010 at 3:26pm

rita na majaji wako jifunzeni kwa tusker project fame mnatia aibu

Comment by saad almas on December 20, 2010 at 3:24pm

rita

Comment by Jirani Mwema on December 20, 2010 at 2:50pm
  • Hongera mama shemsa kwa ushindi mnono ulioupata.Ssa jaribu kutumia vizuri hiyo rizki uliopewa na mola wako.Hakikisha mtoto anapata bima ya elimu,na hakikisha unakuwa na bima ya afya.Huo ni mtaji mkubwaa
Comment by yeyoooooooo on December 20, 2010 at 2:15pm

hongera saaana dadaaetu rita kwa ujasili uloonyesha kwa kumchagua mshindi anaestahili. big up saana.na jay pia hongera. huyo vanessa holler mholanzi anashoboka tu hana lolote waholanzi wabaguzi kichizi .makaburu kwaombeni wa south msamaa kwa yale mlowatendea huna lolote.africa kwa waafrica tu.

 

mungu ibariki bongo

mungu ibariki africa

Comment by KUU LA MAADUI on December 20, 2010 at 1:46pm

THANK you maria victima pua zako zinanusha mbali.

Forum

MIEZI MITANO IMEBAKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TOVUTI YA TUME YA UCHAGUZI HAIPO HEWANI

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by hiepelines Jul 4. 6 Replies

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.IKIWA imebaki miezi…

Tags: NEC

ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?

Started by sebastian yordan luhanga in Maisha. Last reply by ages agae Aug 15. 7 Replies

naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?

Started by daniel paul in Siasa. Last reply by ages agae Aug 15. 6 Replies

JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri KUTOA…

MIUNDO MBINU TANZANIA

Started by Elibahati DAVID AKYOO in Siasa. Last reply by Joe reggan Apr 24. 2 Replies

Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je, hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…

OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU

Started by Erick Angelo in Soka. Last reply by ages agae Aug 15. 5 Replies

Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…

Tags: Okwi

TETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 6 Replies

Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji.  Waliotupwa…

Tags: SIASA

POLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?

Started by GLOBAL in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 21 Replies

Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…

Tags: VURUGU

KIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?

Started by Global Publishers Ltd in Siasa. Last reply by ages agae Aug 16. 33 Replies

Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya, Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!

Tags: katiba, siasa

© 2015   Created by Global Publishers Ltd.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

.fb-wrap { width:50%; margin: 0 auto; } .fb-like-box, .fb-like-box span, .fb-like-box span iframe[style] { width: 100% !important; }